Babeli ya Siri.
Wakati wa Kanisa la Pergamo.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Pergamo.Bebeli ndilo jina la asili la Babeli. Linamaanisha mchafuko. Ulianzishwa hasa na Kushi, mwana wa Hamu, lakini ulifanywa ufalme wenye nguvu na fahari chini ya mwanawe, Nimrodi, yule mwindaji hodari. Nimrodi, kulingana na maelezo ya sura ya kumi na moja ya Mwanzo na pia kulingana na historia ya kilimwengu, aliazimia kutimiza mambo matatu. Alitaka kujenga taifa lenye nguvu, na akalijenga. Alitaka kueneza dini yake mwenyewe, na akaieneza. Alitaka kujifanyia jina, nalo pia akafualu. Kufaulu kwake kulikuwa kukuu sana hivi kwamba ufalme wa Babeli uliitwa kichwa cha dhahabu kati ya serikali zote za ulimwengu. Kwamba dini yake ilipata umaarufu inathibitishwa kwa ukweli kwamba Maandiko yanaitambulisha kabisa na Shetani katika Isaya Sura ya 14 na Ufunuo Sura ya 17-18. Na kwa historia tunaweza kuthibitisha ya kwamba iliuvamia ulimwengu mzima na ndiyo msingi wa kila utaratibu wa dini ya ibada za sanamu, na kiini cha hadithi za miungu, ingawa majina ya miungu yanatofautiana katika sehemu mbali mbali za nchi kulingana na lugha ya watu. Kwamba alijifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe na kwa wafuasi wake ni wazi, kwa kuwa mradi wakati huu wa sasa unaendelea (hadi Yesu atakapojifunua kwa ndugu Zake) yeye ataabudiwa na kuheshimiwa, ingawa itakuwa chini ya jina jingine mbali na Nimrodi, na katika hekalu ambalo ni tofauti kidogo na lile aliloabudiwa hapo awali.
Kwa kuwa Biblia haishughuliki na historia za mataifa mengine kirefu, itakuwa ni muhimu kuchunguza kumbukumbu za kale za kilimwengu kupata jibu letu la jinsi Pergamo ulivyofanyika kiti cha enzi cha dini ya Kishetani ya Babeli. Chimbukko kubwa la taarifa hiyo itakuwa katika kumbukumbu za utamaduni wa Kimisri na wa Kiyunani. Sababu yake ni hii kwamba Misri ilipata sayansi yake na hisabati zake kutoka kwa Wakaldayo nayo Uyunani ulizipata kutoka Misri.
Sasa kwa kuwa makuhani ndio waliokuwa na jukumu la kufundisha sayansi hizi, na kwa kuwa sayansi hizi zilitumiwa kama sehemu ya dini, tayari tunajua ufunguo wa vile dini ya Babeli ilivyoimarika katika nchi hizi mbili. Ni kweli pia kwamba kila wakati taifa moja lilipoweza kulishinda taifa jingine, baada ya kitambo kidogo dini ya lililoshinda ilikuja kuwa dini ya lililoshindwa. Inajulikana vizuri sana ya kwamba Wayunani walikuwa na alama zile zile za Zodiaka kama za Wababeli; na imegunduliwa katika kumbukumbu za kale za Wamisri kwamba Wamisri waliwapa Wayunani elimu yao ya miungu mingi. Hivyo siri za Babeli zilisambaa kutoka taifa moja hadi jingine mpaka zikatokea huko Rumi, Uchina, India na hata katika Marekani zote mbili ya Kaskazini na ya Kusini tunaona jambo lile lile la msingi wa kuabudu.
Historia za kale zinakubaliana na Biblia ya kwamba dini hii ya Babeli hakika kabisa haikuwa dini ya awali ya watu wa kwanza duniani. Ilikuwa ni ya kwanza kuiacha imani ya asili; lakini yenyewe haikuwa ya asili. Wanahistoria kama Wilkinson na Mallet wamethibitisha kabisa kabisa kutoka kwenye maandishi ya kale ya kwamba wakati mmoja watu wote wa duniani walimwamini MUNGU MMOJA, mwenyezi, wa milele, asiyeonekana, Ambaye kwa Neno la kinywa Chake alinena vitu vyote vikawepo, na kwamba katika tabia Yake alikuwa mwenye upendo na mwema na mwenye haki. Lakini kwa kuwa Shetani daima atapotosha cho chote awezacho, tunamwona akipotosha nia na mioyo ya watu ili kwamba waikatae ile kweli. Kwa vile daima amejitahidi apate kuabudiwa kama kwamba yeye alikuwa ndiye Mungu wala si mtumishi na kiumbe cha Mungu, aliondoa ibada kutoka kwa Mungu kwa kusudi kwamba aweze kuileta kwake mwenyewe na kwa hiyo atukuzwe. Kwa kweli hakika alitimiza shauku yake ya kusambaza dini yake kote ulimwengu mzima. Jambo hili linathibitishwa na Mungu katika Kitabu cha Warumi, “Wakati walipomjua Mungu, hawakumtukuza kama ndiye Mungu, mpaka wakapotea katika uzushi wao, na kwa mioyo yenye giza wakakubali dini iliyopotoka mpaka waliabudu viumbe wala si Muumba.” Kumbukeni, Shetani alikuwa kiumbe cha Mungu (Mwana wa Asubuhi). Hivyo tunaona ya kwamba pale ambapo wakati mmoja ukweli ulisambazwa kati ya wanadamu, na wote wakaishikilia hiyo kweli moja, kulikuja siku baadaye wakati kundi kubwa lilipomwacha Mungu na likaeneza utaratibu wa ibada za kishetani kila mahali ulimwenguni. Historia inathibitisha ya kwamba wale wa kabila la Shemu waliosimama pamoja na ukweli usiobadilika walikuwa katika upinzani thabiti dhidi ya wale wa Hamu walioiacha kweli na kujiingiza kwenye uongo wa ibilisi. Hakuna wakati wa kujiingiza katika mjadala wa jambo hili; limeingizwa tu upate kuona kulikuweko na dini mbili na mbili peke yake, na ile ya yule mwovu ikaenea kote ulimwenguni.
Imani ya Mungu mmoja iligeuka ikawa imani ya miungu mingi huko Babeli. Uongo wa ibilisi na mafundisho ya siri za ibilisi ziliinuka dhidi ya kweli ya Mungu na siri za Mungu katika mji huo. Shetani kweli akawa mungu wa dunia hii na akawashurutisha kumwabudu wale aliokuwa amewadanganya, akiwafanya waamini ya kwamba yeye alikuwa ndiye Bwana kweli.
Dini ya miungu mingi ya yule adui ikaanza na fundisho la utatu. Ilikuwa ni huko nyuma kabisa katika zamani za kale sana ambako wazo la “Mungu mmoja katika nafsi tatu” lilizaliwa. Ni ajabu vipi ya kwamba wanatheolojia wetu wa kisasa hawakuona jambo hili; lakini kwa dhahiri kama vile baba zao walivyodanganywa na Shetani, wao wangali wanaamini katika nafsi tatu katika Uungu. Hebu na tuonyeshwe mahali pamoja tu katika Maandiko ambapo pana ushuhuda wo wote kwa fundisho hilo. Je! si ni jambo la ajabu kwamba wakati uzao wa Hamu ulipoenda zake katika ibada za Kishetani ambazo zilikuwa na wazo la kimisingi la miungu mitatu kwamba hakuna dalili hata moja ya uzao wa Shemu wanaoamini jambo kama hilo ama walio na desturi za ibada zinazohusika na hata mfano wake? Sio ajabu kwamba Waebrania waliamini, “Sikia, Enyi Israeli, Bwana Mungu wenu ni Mungu MMOJA”, kama kungalikuweko na nafsi tatu katika Uungu? Ibrahimu, wa mzao wa Shemu, katika Mwa. 18, aliona Mungu MMOJA tu na malaika wawili.
Sasa utatu huu ulioneshwaje? Ulioneshwa katika umbo la pembetatu zilizo sawa kama vile tu unavyooneshwa huko Rumi leo. Ajabu, Waebrania hawakuwa na wazo kama hilo. Sasa ni nani aliye sahihi? Je! Ni Waebrania au Wababeli? Huko Asia wazo la imani ya miungu mingi la miungu watatu katika mmoja lilitokea katika sanamu iliyokuwa na vichwa vitatu katika mwili mmoja. Yeye anaoneshwa kama watu watatu. Huko India, waliamua mioyoni mwao kumwonyesha kama mungu mmoja katika maumbo matatu. Sasa kwa kweli hiyo ni theolojia nzuri ya kisasa. Huko Japani kuna Budha mkuu mwenye vichwa vitatu kama yule tuliyekwisha kuelezea.
Lakini ya wazi sana kuliko zote ni ile inayoonyesha wazo la utatu wa Mungu katika hali tatu za: 1 Kichwa cha mzee kikionyesha Mungu Baba, 2 Duara ambayo katika zile siri ilimaanisha “Mzao” ambao nao unamaanisha Mwana. 3 Mabawa na mkia wa ndege (hua). Hapa ndipo palipokuwapo na fundisho la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nafsi tatu katika Uungu, utatu kweli-kweli. Unaweza kuona jambo lile lile huko Rumi. Sasa hebu niulize mara nyingine tena, je! hivi haishangazi kwamba ibilisi na watu wake wanaomwabudu kweli walifunuliwa ukweli mwingi zaidi ya baba wa imani (Ibrahimu) na uzao wake? Je! haistaajabishi ya kwamba waabudu Shetani, walijua mambo mengi zaidi kuhusu Mungu kuliko watoto wa Mungu? Sasa hivyo ndivyo wanatheolojia wa kisasa wanavyojaribu kutuambia wakati wanapozungumza juu ya utatu. Kumbuka tu jambo hili moja tangu sasa na kuendelea: kumbukumbu hizi ni kweli na jambo hili ni kweli_Shetani ni mwongo na baba wa uongo, na wakati wo wote anapokuja na nuru yo yote bado ingali ni uongo. Yeye ni muuaji. Na fundisho lake la utatu limeangamiza umati wa watu na litaangamiza mpaka Yesu atakapokuja.
Kulingana na historia haikuchukua muda mrefu kwa badiliko kufanywa katika wazo hili la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Shetani aliwachukua hatua kwa hatua kutoka kwenye ile kweli. Wazo la Uungu lililojitokeza sasa lilikuwa: 1 Baba wa milele, 2 Roho wa Mungu aliyefanyika mwili katika mama wa KIBINADAMU. (Je! hilo linawafanya mfikiri?) 3 Mwana fulani wa Kiungu, tunda la huko kufanyika mwili, (Mzao wa mwanamke).
Lakini ibilisi hajatosheka. Bado hajafaulu kuabudiwa, ila kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Kwa hiyo wanachukua watu mbali zaidi kutoka kwenye kweli. Kupitia mafundisho yake ya siri yeye anawafunulia watu ya kwamba kwa kuwa yule baba Mungu mkuu asiyeonekana hajishughulishi na mambo ya kibinadamu, lakini yeye anaendelea kuwanyamazia, basi kwa sababu hiyo anaweza kuabudiwa katika ukimya. Kwa kweli hiyo inamaanisha kutomjali sana iwezekanavyo, ama kabisa. Fundisho hili lilienea duniani pia, na hata leo huko India unaweza kuona ya kwamba mahekalu ya yule muumbaji mkuu, mungu mkimya, inashangaza idadi yake ni ndogo.
Kwa kuwa halikuwa jambo la lazima kumwabudu yule muumba-baba, basi lilikuwa tu ni jambo rahisi kwamba ibada zilibadilishwa zikawa ni “Mama na Mwana” kama vitu vya kusujudiwa. Huko Misri kulikuwako na muungano huo huo wa mama na mwana walioitwa Isiri na Osiri. Huko India ilikuwa ni Isi na Iswara. (Angalia jinsi hata majina yanavyofanana.) Huko Asia ilikuwa ni Sibele na Diusi. Huko Rumi na Uyunani ikawa ni vile vile tu. Na huko China. Vema, wazia mshangao wa baadhi ya wamishenari wa Katoliki ya Kirumi walipokuwa wanaingia Uchina wakakuta huko Madona na Mwana akiwa na miali ya nuru inayotoka kutoka kwenye kichwa cha huyo mtoto mchanga. Sanamu hiyo ingeweza vizuri kubadilishwa kwa urahisi na ile iliyoko Vatikani ila kwa tofauti iliyopo katika sura ya uso.
Inatubidi sasa kugundua asili ya mama na mwana. Yule mungu-mama asili wa Babeli alikuwa ni Semirami ambaye aliitwa Rea katika nchi za mashariki. Alimshika mwana mikononi mwake, ambaye ingawa alikuwa ni mtoto mchanga, alisemekana kwamba ni mrefu, mwenye nguvu, mwenye sura nzuri na hasa sana anayewavutia wanawake. Katika Ezekieli 8:14 aliitwa Tamuzi. Kati ya waandishi wa vitabu bora sana yeye aliitwa Bakusi. Kwa Wababeli alikuwa Ninasi. Sababu ya yeye kuwakilishwa kama mtoto mchanga aliyeshikwa mikononi na hata hivyo anatajwa kama mtu mkuu na mwenye nguvu mno ni kwamba yeye anajulikana kama “Mume- Mwana”. Moja ya jina lake la cheo lilikuwa ni “Mume wa Mama”, na huko India ambako hao wawili wanajulikana kama yule Iswara na Isi, yeye (mume) anawakilishwa kama yule mtoto mchanga kwenye titi la mke wake mwenyewe.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Pergamo.
Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
Mwanzo 10:8-10
Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.