Yule Mwanamke Yezebeli.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Wakati wa Kanisa la Thiatira.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Thiatira.

Ufunuo 2:20-23,
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yao;
23 Nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa Mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.

Jambo la kwanza na lililo muhimu sana tunalojifunza juu ya Yezebeli ni kwamba yeye SI binti wa Ibrahimu, wala kuingizwa kwake katika makabila ya Israeli hakukuwa kuingizwa kwa kiroho kama kule kuingizwa kwake Ruthu, yule Mmoabi. La bwana. Mwanamke huyu alikuwa binti Wa Ethbaali, mfalme wa Sidoni (I Wafalme 16:31), ambaye alikuwa kuhani wa Astarte. Yeye alinyakua ufalme kwa kumwua Felesi, aliyemtangulia. Kwa hiyo tunaona mara moja ya kwamba yeye alikuwa binti wa mwuaji. (Hii hakika inatukumbusha juu ya Kaini.) Na namna alivyokuwa sehemu ya Israeli si kwa kupitia njia za kiroho ambazo Mungu alikuwa ameamuru kwa ajili ya kuwaingiza Mataifa; lakini aliingia kwa KUOLEWA na Ahabu, mfalme wa yale makabila kumi ya Israeli. Sasa muungano huu kama tulivyoona haukuwa wa Kiroho; ulikuwa wa kisiasa. Na hivyo mwanamke huyu aliyekuwa amezama katika ibada za sanamu hakuwa na shauku hata kidogo ya kuwa mwabudu wa Mungu Mmoja aliye wa Kweli, bali badala yake alikuja ameyakinia kuwageuza Israeli wamwache Bwana.

Sasa Israeli (yale makabila kumi,) tayari walikuwa wamejua ni nini kuabudu ndama wa dhahabu, bali walikuwa bado hawajajiuza kwa ibada za sanamu, kwa maana Mungu aliabudiwa na torati ya Musa ilikubaliwa. Bali tangu wakati wa Ahabu alipomwoa Yezebeli, ibada za sanamu ziliendelea katika mtindo wa kutisha mno. Ilikuwa ni wakati huu mwanamke huyu alipokuwa kuhani mwanamke katika mahekalu ambayo alimjengea Astarte (Vinasi) na Baali (mungu jua) ambapo Israeli walifikia upeo wa hatari sana katika maisha yao.

Tukiwa tumeshikilia jambo hili moyoni tunaweza sasa kuanza kuona kile ambacho Roho wa Mungu anaelezea katika wakati huu wa Thiatira. Hiki hapa.
Ahabu akamwoa Yezebeli naye alifanya jambo hilo kama werevu wa kisiasa kuimarisha ufalme wake na kuulinda. Hivyo ndivyo kanisa lilivyofanya kabisa wakati lilipoolewa chini ya Konstantino. Wote waliungana kwa sababu za kisiasa, ingawa waliingiza hali ya kiroho ndani yake. Sasa hakuna mtu anayeweza kunifanya nisadiki kwamba Konstantino alikuwa Mkristo. Yeye alikuwa mpagani mwenye yale yaliyoonekana kama mapambo ya Kikristo. Alichora misalaba myeupe kwenye ngao za askari. Alikuwa mwanzilishi wa Mashujaa wa Columba. Aliweka msalaba juu ya mnara uliochongoka wa Mt. Sofia na hapo akaanzisha mapokeo.

Wazo alilokuwa nalo Konstantino lilikuwa kuwaleta watu wote pamoja, wapagani, Wakristo wa jina na Wakristo wa kweli. Na kwa kitambo kidogo ilionekana kana kwamba angefanikiwa kwa maana waamini wa kweli walikuja kuona kama wangeweza kuwarudisha wale waliokuwa wameondoka kwenye Neno. Walipoona ya kwamba hawangeweza kuwarudisha kwenye ile kweli, walilazimika kutengana na hilo shirika la kisiasa. Ndipo walipofanya hivyo, waliitwa wazushi na wakateswa.

Hebu niseme papa hapa ya kwamba tunalo jambo lile lile likiendelea sasa hivi. Watu wote wanaungana pamoja. Wanaandika Biblia ambalo litamfaa kila mmoja iwe ni Myahudi, Mkatoliki, ama Mprotestanti. Wao wana Baraza lao wenyewe la Nikea bali wanaliita Baraza la Ekumeni. Na unajua haya mashirika yote yanawapiga vita akina nani? Yanawapiga vita Wapentekoste wa kweli. Simaanishi shirika linaloitwa Pentekoste. Ninamaanisha wale ambao ni Wapentekoste kwa sababu wamejazwa na Roho Mtakatifu nao wana ishara na karama miongoni mwao kwa maana wao wanatembea katika kweli.

Wakati Ahabu alipomwoa Yezebeli kwa sababu za kisiasa yeye aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Ukijiunga na shirika fulani basi unauza haki yako ya mzaliwa wa kwanza, ndugu, amini usiamini. Kila kundi la Kiprotestanti lililowahi kutoka kisha likarudi huko huko lilikotoka waliuza haki zao za mzaliwa wa kwanza, na unapouza haki yako ya mzaliwa wa kwanza, wewe ni kama tu Esau -unaweza kulia na kutubu utakavyo, bali haitakufaa kitu. Kuna jambo moja tu unaloweza kufanya na hilo ni, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, na mwache kuzishiriki dhambi zake!” Sasa kama hudhani ninasema kweli, hebu jibu tu swali hili moja. Kuna mtu ye yote aishiye anayeweza kuniambia ni kanisa gani ama ni tukio gani la Mungu lililopata kuwa na ufufuo na likapata kurudi baada ya kuunda shirika na kufanyika madhehebu? Someni historia zenu. Huwezi kupata moja -hata moja.

Ilikuwa ni saa ya usiku wa manane kwa Israeli wakati walipojiunga na ulimwengu na kuacha ya Kiroho kuendea yale ya kisiasa. Ilikuwa ni saa sita usiku huko Nikea wakati kanisa lilipofanya jambo lile lile. Ni saa sita usiku ambapo makanisa yanakusanyika.

Basi wakati Ahabu alipomwoa Yezebeli alimruhusu kuchukua fedha za serikali na kujenga majumba mawili makubwa sana ya kuabudia ya Astarte na Baali. Lile alilojengewa Baali lilikuwa kubwa vya kutosha kwa Israeli wote kuja na kuabudia hapo. Na wakati Konstantino na kanisa walipofanya arusi yeye alilipatia kanisa majengo, na kutengeneza madhabahu na sanamu, na akaunda serikali ya kanisa ambayo tayari ilikuwa inaumbika.

Basi wakati Ahabu alipomwoa Yezebeli alimruhusu kuchukua fedha za serikali na kujenga majumba mawili makubwa sana ya kuabudia ya Astarte na Baali. Lile alilojengewa Baali lilikuwa kubwa vya kutosha kwa Israeli wote kuja na kuabudia hapo. Na wakati Konstantino na kanisa walipofanya arusi yeye alilipatia kanisa majengo, na kutengeneza madhabahu na sanamu, na akaunda serikali ya kanisa ambayo tayari ilikuwa inaumbika.

Wakati Yezebeli alipoungwa mkono na nguvu za serikali aliwalazimisha watu dini yake na akawaua manabii na makuhani wa Mungu. Hali ilikuwa mbaya sana hata Eliya, mjumbe wa siku yake, alifikiria alikuwa ndiye peke yake aliyebakia; bali Mungu alikuwa na wengine 7,000 ambao walikuwa bado hawajampigia magoti Baali. Na sasa hivi kule nje kati ya hayo madhehebu ya Wabatisti, Wamethodisti, Wapresbiteri, nk., kuna baadhi yao watakaotoka na kumrudia Mungu. Nataka mjue mimi sipambani, sasa, na sijawahi kupambana na watu. Ni madhehebu -taratibu ya shirika ambayo ninapambana nayo. Mimi sina budi kuipinga kwa sababu Mungu anaichukia.

Sasa hebu na tusimame kwa dakika moja hapa turudie kuelezea kile tulichoelezea juu ya ibada kule Thiatira. Nilisema ya kwamba wao walimwabudu Apolo, (ambaye alikuwa mungu jua) pamoja na mfalme. Sasa huyu Apolo aliitwa 'mkinga maovu.' Aliwakingia watu maovu. Aliwabariki na alikuwa mungu halisi kwao. Alipaswa kuwafundisha watu. Alielezea habari za ibada, na taratibu za hekalu, ibada kwa miungu, juu ya kutoa dhabihu na kuhusu mauti na uzima baada ya kufa. Jinsi alivyotenda haya ilikuwa ni kwa kupitia kwa nabii wa kike aliyeketi amelala fofofo juu ya kiti cha miguu mitatu. Jamani! Mnaona jambo hilo? Huyu hapa nabii mke anayeitwa Yezebeli naye anawafundisha watu. Na mafundisho yake yanawapotosha watumishi wa Mungu na kuwafanya wafanye uasherati. Sasa uasherati maana yake ni “kuabudu sanamu.” Hiyo ndiyo maana yake ya kiroho. Ni muungano haramu. Muungano wa Ahabu na muungano wa Konstantino yote miwili ilikuwa haramu. Wote wawili walifanya uzinzi wa kiroho. Kila mzinzi ataishia kwenye ziwa la moto. Mungu alisema hivyo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Thiatira.

Kushusha (PDF Kiingereza)... Jezebel Religion.


   Maandiko Anasema...

Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo Yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama Mimi Nami nilivyopokea kwa Baba Yangu.

Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.

Ufunuo 2:26-28



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Nyakati Saba Za Kanisa.)


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Two Babylons

by Rev Alexander Hislop.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.

Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.