Neno lililo hai mfululizo.

  Neno lililo hai mfululizo.

Maono ya Bibi-arusi.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Utungu wa Kuzaa.

Biblia ilisema, “Mkewe amejifanya tayari,” mwishoni mwa wakati. Alijifanyaje tayari? Kufikia kuwa Mke Wake. Naye anafanya nini? Alikuwa amevaa vazi la namna gani? Neno Lake Mwenyewe. Alikuwa amevalia Haki Yake. Hivyo ndivyo ilivyo. Ni sahihi. Mnaona?

Maono! Angalia, tunafunga tu sasa. Ninataka kusema jambo hili moja kabla tu ya kufunga. Hilo ndilo lililonifanya niseme jambo hili. Sasa, ni BWANA ASEMA HIVI. Kama mtu angesema jambo hilo, bila, kuliweka katika mawazo yake mwenyewe, angekuwa mnafiki na anapaswa kwenda kuzimu kwa ajili yake. Hiyo ni kweli. Kama angejaribu kupata kundi la watu, watu wazuri kama hawa, na kuwadanganya, mbona, angekuwa ni ibilisi katika mwili wa kibinadamu. Mungu kamwe asingemheshimu. Unafikiri Mungu angemheshimu shetani ama uongo? Kamwe. Mnaona? Linapitia juu ya vichwa vyao, nao hawalipati. Yeye huwavuta Wateule.

Waangalie manabii wote katika nyakati, jinsi alivyowapata Wateule.
Angalia, tukishuka kupitia, hata kwenye yale matengenezo. Kama vile, kanisa Katoliki la Kirumi lilimchoma moto Joan wa Arc, kwa kuwa ni mchawi. Hiyo ni kweli. Baadaye waligundua hakuwa. Alikuwa ni mtakatifu. Bila shaka, walifanya vitubio, wakaichimbua miili ya hao mapadre na kuitupa mtoni. Lakini, mnajua, lakini hilo halikutatua mambo katika vitabu vya Mungu. La. Walimwita Mtakatifu Patrick hivyo, pia, mnaona, na basi kama mimi ni mchawi yeye naye ni mchawi pia. Kwa hiyo, tunaona, angalia watoto wake. Angalia mahali pake, juu, angalia ni wangapi waliouawa. Angalia kwenye elimu ya wafia imani uone ni wangapi waliouawa pale. Mnaona, sivyo ilivyo.
Lakini madai ya watu, hilo halilifanyi kuwa hivyo. Ni yale Mungu aliyosema na kuthibitisha, kwamba ni Kweli. “Thibitisha mambo yote. Shikilia sana yaliyo mema.”

Sasa tunaona, sasa, hapa yapata miezi michache iliyopita, asubuhi moja, nilikuwa nikitoka nje ya nyumba, na ono likaja. Nami ninatoa changamoto kwa mtu ye yote hapa, ambaye amejua miaka hii yote, akaseme wakati wo wote ambapo Bwana aliwahi kuniambia “BWANA ASEMA HIVI” ila jambo hilo lilitukia. Ni wangapi wanaojua ni Kweli, inua mkono wako. Sawa. Kuna mtu yeyote angeweza kunena kinyume? Ni kweli. Usimsikilize mjumbe. Angalia Ujumbe ulivyo. Hivyo ndivyo ilivyo. Mnaona? Si hivyo. Msichunguze maskini [Sehemu tupu kwenye kanda.] Mwenye upara, mwajua, mtu, maana ni-ni mwanadamu tu, wote, na sisi sote ni sawa tu. Lakini angalia kile kinachotendeka. Hilo ndilo linalotangaza jambo hilo. Nilichukuliwa...

Sasa, ninajua watu wanasema kila namna ya mambo, nasi tunajua ya kwamba mengi ya hayo si sahihi. Siwezi kujibu kwa yale mengine, mtu ye yote asemayo. Sina budi kujibu yale ninayosema. Ninaweza tu kusema kama ni Kweli, ama si Kweli. Na mimi-mimi-mimi ndiye ninayepaswa kuwajibika kwa jambo hilo, si yale mtu mwingine asemayo. Siwezi kumhukumu mtu ye yote. Sikutumwa kuhukumu, bali kuhubiri Ujumbe.

Angalia. Ilibidi nionyeshwe- nionyeshwe Kanisa. Nami nilichukuliwa na Mtu Ambaye sikuweza kumwona, nami niliwekwa juu, kama, stendi. Nami nikasikia muziki mtamu sana niliopata kusikia. Nami nikaangalia, likija, na kundi la mabibi wadogo, karibu, walionekana kuwa, loo, umri wa miaka kama ishirini, kumi na minane, ishirini. Nao wote walikuwa na nywele ndefu, na walikuwa wamevaa nguo mbalimbali, mfano, nguo. Nao walikuwa wakipiga hatua kwa hatua kamilifu, kwa muziki huo, kama ilivyoweza kuwa. Nao wakaenda kutoka kushoto kwangu, wakizunguka upande huu. Nami niliwaangalia. Ndipo nikaangalia basi kuona ni Nani aliyekuwa akizungumza nami, nami sikuweza kumwona mtu ye yote.

Ndipo nikasikia bendi ya roki ikija. Na wakati nilipotazama upande wangu wa kuume, nikija huku, nikirudi, haya hapa makanisa ya ulimwengu yanakuja. Na baadhi ya... Kila mmoja amebeba bendera yao, kutoka mahali walipotoka. Baadhi ya mambo yaliyo machafu sana niliyopata kuona maishani mwangu! Na wakati kanisa la Marekani lilipokuja, lilikuwa jambo baya sana nililopata kuona. Baba wa Mbinguni ndiye Hakimu wangu. Walikuwa wamevaa sketi hizi chafu sana za kijivu, kama mmoja wa hawa wasichana wa baa, zilizo tupu upande wa nyuma, hapa juu; wameshikilia kitu kinachoonekana kama kipande cha karatasi ya kijivu; na kama dansi la hula; wamejipaka rangi; wamevaa kaptura fupi, wamekata nywele; wanavuta sigara; na wakikatika viuno, huku wakitembea kwa mdundo wa roki.
Nami nikasema, “Hilo ni kanisa la Marekani?”
Nayo Sauti ikasema, “Naam, ndiyo.”

Nao walipopita, iliwabidi kukishikilia namna hii, na kuiweka ile karatasi nyuma yao walipopita. Ni-nilianza kulia. Ni-niliwazia tu, “Katika kazi yangu yote, na yote niliyofanya.” Na kila kitu ambacho sisi wahudumu tumefanya kazi pamoja ... Na, ndugu, si-sijui ni kiasi gani mngeamini juu ya maono haya; bali ni Kweli, kwangu mimi. Daima imethibitishwa kuwa ni kweli. Nilipoona jambo hilo, na nikijua kilichokuwa kikiendelea, moyo wangu ulikuwa karibu kupasuka ndani yangu. “Nimefanya nini? Nimelikosaje? Nimedumu moja kwa moja na Neno hilo, Bwana. Na ningewezaje kufanya jambo hilo?”

Niliwazia, “Ungewezaje Wewe kunipa ono, si muda mrefu uliopita, na kuniona Humo? Nami nikasema, 'Vema, je! Itawabidi kuhukumiwa?' Akasema, 'Kundi la Paulo, pia.' Nikasema, 'Nimehubiri Neno lile lile alilohubiri.'” Wafanyabiashara Wakristo walibeba makala yake. Nami nikasema, “Kwa nini? Kwa nini iwe hivi?”
Niliona lile kundi la malaya likipita namna hiyo, wote wamevalia namna hiyo, na kujiita, “Kanisa la Bi Marekani.” Nilizimia tu.

Ndipo, moja kwa moja, nikasikia ule mziki mtamu halisi ukija tena, na huyu hapa Bibi-arusi mdogo yuaja tena. Yeye alisema, “Hiki ndicho kinachotoka, hata hivyo.” Na wakati alipopita pale, Yeye ni kama yule yule kwanza, akitembea kwenye hatua ya muziki wa Neno la Mungu, akipita mbele. Na nilipoona jambo hilo, nilisimama pale huku nimeinua mikono yangu miwili, nikilia, namna hiyo. Nilipokuja, nilikuwa nimesimama kwenye ukumbi wangu huko nje, nikiangalia moja kwa moja kote uwanjani.

Nini? Yeye anapaswa kuwa Bibi-arusi yule yule, wa aina ile ile, aliyejengwa kwa nyenzo ile ile aliyokuwa nayo kwanza. Sasa soma Malaki 4 uone kama hatupaswi kuwa na Ujumbe katika siku za mwisho, ambao “utaigeuza mioyo ya watoto iwaelekee baba zao,” kurudi kwenye Ujumbe wa asili wa kipentekoste, Neno kwa Neno. Ndugu, tuko hapa.

Sasa, kanisa hili linapaswa kupata ishara, na ishara yake ya mwisho. Tunaona hapa, katika Maandiko, unaona sasa, unaona, utungu mkuu wa kuzaa ambao uko katika wakati huu wa Laodikia. Inachosha. Kanisa lao linazaliwa mara ya pili. Si...

Hakutakuwako na dhehebu lingine kamwe. Kila mtu anajua ya kwamba kila wakati ujumbe ulipotolewa... Waulizeni hawa wanahistoria. Baada ya ujumbe kutolewa, dhehebu lilitoka kwake; loo, Alexander Campbell, kila kitu kingine, Martin Luther, na kila kitu. Waliunda madhehebu kutoka kwake. Na kwa kawaida ujumbe huenda tu kwa miaka mitatu hivi, uamsho. Hili limekuwa likitendeka kwa miaka kumi na mitano, na hakuna dhehebu lililotoka kwake. Kwa nini? Kapi lilikuwa ndilo la mwisho. Tuko mwishoni. Mnaona utungu wa kuzaa? Mnaona kuna nini? Ni mabaki tu watakaotolewa. Ni mabaki tu watakaotolewa. Na hiyo ndiyo sababu ninalia, na kukazana, na kusukuma, na kuweka kando kila upendeleo wa mwanadamu duniani, kupata kibali kwa Mungu, na kuendelea tu katika Neno Lake. Linaumwa. Hiyo ndiyo shida. Litazaa. Halina budi kufanya chaguo lake. Maandiko hayo yako ukutani. Tunaona dunia iko karibu kabisa kuondoka. Hiyo ni kweli. Nasi tunaona kanisa, limeoza sana, liko tayari kwenda. Na utungu wa kuzaa uko juu ya hayo yote, juu ya ulimwengu na kanisa pia. Na kuna karibu kuzaliwa ulimwengu mpya, na Kanisa jipya kuzaliwa, kuuendea, kwa ajili ya ule Utawala wa Miaka Elfu. Tunajua jambo hilo.

Angalia. Mungu humpa ... Na sikilizeni kwa makini hili, ndipo ninafunga. Ishara yake ya mwisho; Ujumbe wake wa mwisho, ishara yake ya mwisho. Ishara yake ya mwisho, ni, hana budi kuingia katika hali kama ilivyokuwa hapo mwanzo; ulimwengu, kanisa.

Angalia jinsi ilivyokuwa hapo mwanzo, miaka hiyo yote, bila, tangu Malaki mpaka Yesu. Liangalie, miaka yote sasa. Liangalie, huko nyuma kote, walivyoingia kwenye upotovu. Angalia nchi, jinsi ilivyokuwa kila wakati, kama katika siku za Nuhu, na kadhalika. Haina budi kuwa katika namna ile ile ya mfano, nasi tunaona jambo hilo. “Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu.” Tunaona mambo haya yote yakifanana tu...

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Utungu wa Kuzaa.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.

Yohana 16:20-21


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Ndoa Na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)