Ukweli kuhusu dhambi ya asili.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Dhambi ya asili. Ilikuwa ni matofaa?
(Uzao wa Nyoka.)


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Efeso.

Ufunuo 2:7,
“...Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya Mti wa Uzima, Ulio katika bustani ya Mungu.”

“Mti Wa Uzima.” Huo si msemo unaopendeza? Umetajwa mara tatu katika Kitabu cha Mwanzo na mara tatu katika Kitabu cha Ufunuo. Katika sehemu zote sita ni mti ule ule na unaonesha kwa mfano kitu kile kile hasa.

Lakini mti wa Uzima ni nini? Vema, kwanza kabisa ingetupasa kujua mti wenyewe unawakilisha nini. Katika Hesabu 24:6, kama vile Balaamu alivyotoa sifa za Israeli, yeye alisema walikuwa “mfano wa mishubiri aliyoipanda Bwana.” Miti katika Biblia nzima inanena juu ya watu, kama vile katika Zaburi 1. Hivyo basi Mti wa Uzima hauna budi kuwa ni Mtu wa Uzima, na huyo ni Yesu.

Sasa katika Bustani ya Edeni kulikuwako na miti miwili iliyosimama katikati yake. Mmoja ulikuwa ni Mti wa Uzima, huo mwingine ulikuwa ni Mti wa Kujua Mema na Mabaya. Mwanadamu alipaswa kuishi kwa Mti wa Uzima; bali hakupaswa kugusa mti huo mwingine la sivyo angekufa. Lakini mwanadamu alikula mti huo mwingine, na wakati alipofanya jambo hilo, mauti ilimwingia kwa njia ya dhambi, naye akatenganishwa na Mungu.

Sasa huo mti kule nyuma katika Edeni, Mti ule ambao ulikuwa ndio chanzo cha uzima, ulikuwa ni Yesu. Katika Yohana, sura ya sita hadi ya nane, Yesu anajiweka Mwenyewe kama chanzo cha uzima wa milele. Yeye alijiita Mwenyewe Mkate kutoka mbinguni. Alinena juu ya kujitoa Mwenyewe na ya kwamba mtu akimla Yeye hatakufa kamwe. Alitangaza ya kwamba alimjua Ibrahimu, na ya kwamba Ibrahimu asijakuwepo, Yeye ALIKUWEKO. Alitabiri ya kwamba Yeye Mwenyewe angewapa maji yaliyo hai ambayo mtu akiyanywa hangeona kiu tena, bali angeishi milele. Alijionyesha Mwenyewe kama MIMI NIKO NILIYE MKUU. Yeye ni Chakula Cha Uzima, Kisima Cha Uzima, Aliye wa Milele, MTI WA UZIMA. Yeye alikuweko kule nyuma katika Edeni katikati ya bustani kama tu vile atakavyokuwa katikati ya bustani ya Mungu.

Wengine wana wazo ya kwamba ile miti miwili katika bustani ilikuwa tu ni miti mingine miwili kama ile mingine ambayo Mungu alikuwa ameiweka mle. Lakini wanafunzi makini wanajua ya kwamba sivyo ilivyo. Wakati Yohana Mbatizaji alipopaza sauti ya kwamba shoka limewekwa kwenye shina la miti yote, yeye hakuwa tu anazungumzia juu ya miti ya kawaida, lakini juu ya kanuni za kiroho. Sasa katika I Yohana 5:11 inasema,
“Na huu ndio USHUHUDA, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.”
Yesu alisema katika Yohana 5:40,
“Wala hamtaki kuja Kwangu mpate kuwa na uzima.”
Kwa hiyo ushuhuda, Neno la Mungu, linasema dhahiri na kwa wazi ya kwamba UZIMA, UZIMA WA MILELE, umo katika Mwana. Hauko mahali pengine po pote. I Yohana 5:12,
“Yeye aliye Naye Mwana anao huo UZIMA; asiye naye Mwana wa Mungu HANA huo Uzima.”
Sasa, kwa kuwa ushuhuda huo hauwezi kubadilika, kupunguzwa wala kuongezewa, basi huo ushuhuda unasimama ya kwamba UZIMA HUO UMO KATIKA MWANA... Kwa kuwa jambo hili ni kweli, ULE MTI KATIKA BUSTANI HAUNA BUDI KUWA NI YESU.

Sawa. Kama Mti wa Uzima ni mtu, basi Mti wa Kujua mema na mabaya ni mtu PIA. Haiwezi kuwa vinginevyo. Hivyo ndivyo Mwenye Haki na yule Mwovu walivyosimama pamoja pale katikati ya Bustani ya Edeni. Ezekieli 28:13a,
“Ulikuwa (Shetani) ndani ya Edeni, bustani ya MUNGU.”

Hapa ndipo tunapopokea ufunuo wa kweli wa Uzao wa Nyoka. Hivi ndivyo ilivyotukia hasa katika Bustani ya Edeni. Neno linasema ya kwamba Hawa alidanganywa na yule nyoka. Yeye kweli alidanganywa na yule nyoka. Inasema katika Mwanzo 3:1,
“Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.”

Mnyama huyu alikuwa anafanana sana na mwanadamu (na hata hivyo alikuwa mnyama halisi) hata angeweza kuhojiana na kunena. Alikuwa mnyama anayeweza kusimama wima na kwa namna fulani alikuwa kati ya sokwe mtu na mwanadamu, lakini anafanana zaidi na mwanadamu. Alikuwa anafanana sana na mwanadamu hivi kwamba mbegu yake ingeweza, na iliweza kuungana na ya mwanamke na kumfanya abebe mimba. Wakati jambo hili lilipotukia, Mungu alimlaani nyoka. Aligeuza kila mfupa katika mwili wa nyoka hivi kwamba ilimbidi kutambaa kama nyoka. Sayansi inaweza kujaribu iwezavyo, wala haitapata pengo lililopotea. Mungu alihakikisha hatalipata. Mwanadamu ana akili na anaweza kuona uhusiano wa mwanadamu na mnyama na anajaribu kuthibitisha jambo hilo kwa ivolusheni. Hakuna ivolusheni yo yote. Lakini mwanadamu na mnyama walichangamana. Hiyo ni moja ya siri za Mungu ambazo zilibaki zimefichwa, lakini hapa zimefunuliwa. Jambo hilo lilitukia moja kwa moja kule nyuma katikati ya Edeni wakati Hawa alipoacha Uzima akakubali Mauti.

Angalia yale Mungu aliyowaambia kule bustanini.
Mwanzo 3:15,
“Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na Uzao wake, na Huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.”
Kama tukikubaliana na Neno ya kwamba mwanamke kweli alikuwa na Uzao, basi nyoka naye bila shaka alikuwa na mzao. Kama Uzao wa mwanamke ulikuwa mtoto mwanamume asiyetokana na mwanamume, basi uzao wa nyoka utapaswa kuwa katika mtindo ule ule, na hiyo ni kusema mwanamume mwingine hana budi kuzaliwa mbali na njia ya mwanamume. Hakuna mwanafunzi asiyejua ya kwamba Uzao wa mwanamke alikuwa ni Kristo aliyekuja kwa njia ya Mungu, mbali na kujuana kimwili kwa binadamu. Inajulikana vizuri pia ya kwamba kule kupondwa kwa kichwa kwa nyoka kulikobashiriwa kwa kweli kulikuwa ni unabii kuhusu yale ambayo Kristo angetimiza dhidi ya Shetani msalabani. Pale msalabani Kristo angekiponda kichwa cha Shetani, naye Shetani angekiponda kisigino cha Bwana.

Sehemu hii ya Maandiko ni ufunuo wa jinsi ambavyo uzao halisi wa nyoka ulivyopandwa duniani, yaani kama vile tulivyo na taarifa ya Luka 1:26-35, ambapo imeandikwa taarifa halisi ya vile Uzao wa mwanamke ulivyodhihirishwa kimwili mbali na njia ya mwanamume.
“Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, Kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Na huyo malaika akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe: umebarikiwa kati ya wanawake. Naye alipomwona, akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa Mtoto Mwanamume; na jina lake utamwita YESU. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba Yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme Wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu Zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo Hicho Kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu.”

Kama vile Mzao wa mwanamke ulivyokuwa ni Mungu Mwenyewe kabisa akijizaa katika mwili wa mwanadamu, vivyo hivyo na uzao wa nyoka ni njia halisi ambayo Shetani aliona aliweza kujifungulia mlango wa kuingia katika jamii ya binadamu. Haingewezekana kwa Shetani (kwa maana ni kiumbe cha kiroho KILICHOUMBWA tu) kujizaa katika njia ambayo Mungu alijizaa, kwa hiyo taarifa ya Kitabu cha Mwanzo inasimulia ambavyo yeye alitoa mbegu yake na kuanzisha ama kujiingiza mwenyewe katika jamii ya binadamu. Pia kumbukeni ya kwamba Shetani anaitwa nyoka. Ni uzao wake au kuingizwa kwake katika jamii ya binadamu tunayonena habari zake.

Kabla ya Adamu kumjua Hawa kimwili, nyoka alitangulia kumjua. Na huyo aliyezaliwa kwake alikuwa Kaini. Kaini alikuwa wa (alizaliwa na, alitokana na) “Yule Mwovu.” I Yohana 3:12. Roho Mtakatifu ndani ya Yohana hangeweza mahali fulani amwite Adamu “Yule Mwovu” (kwa maana hivyo ndivyo ambavyo angekuwa kama yeye ndiye aliyemzaa Kaini) na katika mahali pengine amwite Adamu “Mwana wa Mungu” ambavyo ndivyo alivyokuwa kwa kuumbwa. Luka 3:38. Kaini aligeuka akawa na tabia kama ya baba yake, anayeleta kifo, mwuaji. Kumkaidi kwake Mungu kabisa wakati alipokabiliwa na Mwenyezi katika Mwanzo 4:5,9,13,14, kunamwonyesha yakini kuwa asiye na tabia kabisa ya binadamu, hata alionekana kama amezidi taarifa yo yote tuliyo nayo katika Maandiko ya kuhusu Shetani kukabiliana na Mungu.

“Bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso Wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.”

Angalia jinsi kumbukumbu ya Mungu inavyoandika taarifa halisi ya kuzaliwa kwa Kaini, Habili na Sethi. Mwanzo 4:1,
“Adamu akamjua Hawa mkewe, naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Akaongezea akamzaa ndugu yake, Habili.”
Mwanzo 4:25,
“Adamu akamjua mke wake tena; akamzaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi...”
Kuna wana WATATU waliozaliwa kutokana na vitendo VIWILI vya kujuana kimwili kwa Adamu. Kwa kuwa Biblia ni Neno halisi na kamilifu la Mungu, hili si kosa bali ni kumbukumbu la kutuangazia. Kwa kuwa wana WATATU walizaliwa kwa matendo MAWILI ya Adamu, unajua KWA KWELI ya kwamba MMOJA wa hao watatu HAKUWA mwana wa Adamu. Mungu aliandika kumbukumbu hili katika njia hii sahihi kutuonyesha jambo fulani. Ukweli wa mambo ni kwamba Hawa alikuwa na wana WAWILI tumboni mwake (mapacha) kutokana na kuchukua mimba zilizotungwa MBALIMBALI. Yeye alikuwa anabeba mapacha, huku ana mimba ya Kaini ikitangulia kwa kipindi cha muda fulani ile ya Habili.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Efeso.

Pia tazama... Uzao wa Nyoka.



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Fundisho la Wanikolai.)


Kama kula
matofaa
kunawafanya
wanawake watambue
wao ni uchi,
afadhali tuwape
matofaa tena.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi;

si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

1 Yohana 3:10-12


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Two Babylons

by Rev Alexander Hislop.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.