Kristo akiwa nje ya Kanisa.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Wakati wa Kanisa la Laodikia.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Laodikia.

Ufunuo 3:20-22,
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti Yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, Nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja Nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja Nami katika kiti Changu cha enzi, kama Mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba Yangu katika kiti Chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Sasa kuna utata mkubwa sana juu ya aya hii kwa sababu wengi sana wanaotenda kazi kibinafsi katika uinjilisti wa kibinafsi wanautumia kana kwamba Yesu alikuwa kwenye mlango wa moyo wa kila mwenye dhambi akipiga hodi apate kuruhusiwa kuingia. Ingesemwa basi ya kwamba kama mwenye dhambi angefungua mlango, Bwana angeingia. Lakini aya hii haizungumzi na wenye dhambi binafsi. Ujumbe huu wote una muhtasari kama ilivyo kila ujumbe katika kila wakati. Katika aya ya 22 inasema, “Yeye aliye na sikio, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia MAKANISA.” Kwa hiyo huu ndio ujumbe kwa kanisa la wakati wa mwisho. Hii ndiyo hali ya kanisa la Laodikia wakati mwisho wake unapokaribia. Si ujumbe wa kibinafsi kwa mtu mmoja; ni Roho akituambia mahali Yesu alipo. KRISTO AMELIACHA KANISA.

Je! hayo siyo matokeo dhahiri ama mwisho kama Neno likiwekwa kando badala ya kanuni ya imani kuweka kando, Roho Mtakatifu akiondolewa na mapapa, maaskofu, marais, washauri, nk. kuchukua mahali Pake, na Mwokozi akiwekwa kando na badala Yake nafasi ichukuliwe na utaratibu wa shughuli za kidini, ama kujiunga na kanisa, ama namna fulani ya kupatana na utaratibu wa kanisa? Kuna nini zaidi linaloweza kufanywa dhidi Yake? Huu ni ukengeufu! Huku ni kuanguka! Huu ni mlango uliofunguliwa kwa mpinga-Kristo, kwa maana kama Mmoja alikuja katika Jina la Baba Yake (Yesu) wala hakupokewa, lakini akakataliwa, basi atakuja mwingine aliye na jina lake mwenyewe (mwongo, mnafiki) naye huyo wao watampokea, Yohana 5:43. Mtu wa dhambi, huyo mwana wa upotevu atachukua mamlaka.

Mathayo 24, inataja ishara mbinguni kuhusu siku hii ya mwisho kabla tu ya kuja kwa Yesu. Sijui kama uliona ishara kama hiyo hivi majuzi ikitimizwa ipate kuonyesha kweli ile ile tuliyokuwa tukinena habari zake. Kweli hiyo ni kwamba Yesu amekuwa akisukumwa pole pole kando mpaka katika wakati wa mwisho amesukumwa nje ya kanisa. Kumbuka ya kwamba katika wakati wa kwanza kanisa lilikuwa karibu ni mviringo mzima wa kweli. Walakini kulikuweko na kosa dogo lililoitwa matendo ya wanikolai lililoifanya duara hiyo kutojaa. Ndipo katika wakati uliofuata giza zaidi lilipenya mpaka ile duara ya nuru ikapunguza mwangaza wake, ndipo giza likafunika sehemu kubwa zaidi ya ile duara. Katika wakati wa tatu ilifunikwa hata na zaidi, na katika wakati wa nne ambao ulikuwa ndio zile Zama za Giza, nuru ilikuwa karibu yote imekwisha.

Sasa fikiria juu ya jambo hili. Kanisa linaangaza katika nuru iliyotoka kwa Kristo. Yeye ndiye JUA. Kanisa ni MWEZI. Kwa hiyo mviringo huu wa nuru ni mwezi. Ulikuwa umepungua kutoka karibu mwezi mzima katika wakati wa kwanza, kufikia kipande chembamba katika wakati wa nne. Lakini katika wakati wa tano ulianza kukua. Katika wakati wa sita ukapiga hatua kubwa sana ya kukua kuendelea mbele. Katika sehemu ya wakati wa saba ulikuwa ungali unakua, ndipo mara moja ukakoma, na ukafifia karibu kabisa, hivi kwamba badala ya nuru ilikuwa ni giza la ukengeufu, na katika mwisho wa wakati ulikuwa umeacha kuangaza kwa maana giza lilikuwa limeshinda. Kristo sasa alikuwa nje ya kanisa.

Hii hapa ile ishara mbinguni. Kule kupatwa kwa mwisho kwa mwezi kulikuwa kupatwa kwa mwezi wote. Ulififia ukawa giza tupu katika hatua saba. Katika hatua ya saba, giza tupu liliingia wakati Papa wa Roma (Paulo wa Sita) alipoenda huko Palestina kufanya ziara takatifu ya Yerusalemu. Alikuwa ndiye papa wa kwanza aliyepata kwenda Yerusalemu. Huyo papa anaitwa Paulo wa Sita. Paulo alikuwa ni mjumbe wa kwanza na mtu huyu anaitwa kwa jina hilo. Angalia kwamba ni wa sita, ama hesabu ya mwanadamu. Hii ni zaidi ya kubahatisha. Na hapo alipokwenda Yerusalemu, mwezi ama kanisa likawa giza tupu. Mambo ndiyo hayo. Huu ndio ule mwisho. Kizazi hiki hakitapita mpaka yote yatakapotimizwa. Naam Bwana Yesu, njoo upesi!

Sasa tunaweza kuona ni kwa nini kulikuweko na mizabibu miwili, mmoja wa kweli na mmoja wa uongo. Sasa tunaweza kuona ni kwa nini Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja wa kimwili (aliyemtesa Isaka) na mmoja wa ahadi. Sasa tunaweza kuona ni kwa nini kwamba kutoka kwa wazazi wale wale wavulana wawili walitokea kama mapacha, mmoja akipenda na kuyajua mambo ya Mungu, na yule mwingine akijua mengi ya kweli hiyo hiyo, lakini hakuwa wa Roho yule yule, na kwa hiyo akamtesa mtoto aliyekuwa ameteuliwa. Mungu hakukataa vivi hivi tu kwa ajili tu ya kukataa. Yeye alikataa kwa ajili ya wateule. MTEULE HAWEZI kumtesa mteule. MTEULE HAWEZI kumdhuru mteule. Waliokataliwa ndio wanaowatesa na kuwaangamiza wateule. Loo, hao waliokataliwa ni wa kidini. Wao ni werevu. Wao ni wa ukoo wa Kaini, uzao wa nyoka. Wanajenga Babeli zao, wanajenga miji yao, wanajenga milki zao, na wakati wote wanamwita Mungu. Wanachukia uzao wa kweli, nao watafanya yote wawezayo, (hata katika Jina la Bwana) kuwaangamiza wateule wa Mungu. Lakini wanahitajika. “Makapi yana faida gani kwa ngano?” Bila makapi, hakuna ngano. Lakini mwishoni, inakuwaje kwa makapi? Yanateketezwa kwa moto usiozimika. Na hiyo ngano? Iko wapi? Imekusanywa katika ghala Lake. Ni mahali Yeye alipo.

Enyi wateule wa Mungu, jihadharini. Chunguzeni kwa makini. Kuweni waangalifu. Utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka. Mtegemeeni Mungu na mwe hodari katika uweza Wake. Adui yenu, ibilisi, hata sasa anazunguka-zunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze. Kesheni katika maombi na mwe imara. Huu ni wakati wa mwisho. Mizabibu yote miwili wa kweli na wa uongo inafikia kukomaa, lakini kabla ngano haijakomaa, magugu hayo yaliyoiva hayana budi kufungwa yapate kuteketezwa. Mnaona, yote yanajiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Huko ndiko kule kufungwa. Hivi karibuni utafika wakati wa ngano kuwekwa ghalani. Bali sasa hivi zile roho mbili zinatenda kazi katika ile mizabibu miwili. Tokeni kati ya hayo magugu. Anzeni kushinda mpate kuhesabiwa wanaostahili sifa kwa ajili ya Bwana wenu, na wanaostahili kumiliki na kutawala pamoja Naye.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Laodikia.



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
Mihuri Saba.


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Mihuri Saba.

 

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.



 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.

Kumbukumbu la Torati 6:4