Fundisho la Balaamu.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Wakati wa Kanisa la Pergamo.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Pergamo.

Ufunuo 2:14,
“Unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwanzo mbele ya wana wa Israeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.”

Sasa, huwezi kuanzisha mpango wa Unikolai kanisani na ukose pia kujiingiza kwa fundisho hili jingine. Mnaona, ukiliondoa Neno la Mungu na kazi za Roho kama njia ya kuabudia (wao wanaoniabudu Mimi yawapasa waniabudu katika Roho na kweli) basi itakulazimu uwape watu aina nyingine ya ibada kuwa kibadala, na badilisho humaanisha Ubalaamu.

Endapo tutafahamu fundisho la Balaamu ni nini katika kanisa la Agano Jipya ni heri turudi nyuma tuone lilikuwa ni nini katika kanisa la Agano la Kale na kulitumia katika huo wakati wa tatu na halafu kulileta hadi siku hizi.

Hadithi hiyo inapatikana katika Hesabu Sura za 22 hadi 25. Sasa tunajua kwamba Israeli walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu. Walikuwa ndio Wapentekoste wa siku yao. Walikuwa wamekimbilia chini ya damu, wote walikuwa wamebatizwa katika Bahari ya Shamu nao wakatoka majini wakiimba katika Roho na kucheza kwa nguvu za Roho Mtakatifu, huku Miriamu, nabii mke, akipiga tari lake. Naam, baada ya wakati fulani wa kusafiri hawa wana wa Israeli walifika Moabu. Mnakumbuka Moabu alikuwa ni nani. Yeye alikuwa mwana wa Lutu kwa mmoja wa mabinti wake mwenyewe aliozaa, naye Lutu alikuwa mpwawe Ibrahimu, kwa hiyo Israeli na Moabu walikuwa ni wa ukoo mmoja. Ninawatakeni mwone jambo hilo. Wamoabu waliujua ukweli, kama waliuishi au la.

Kwa hiyo Israeli wakaja hadi mipakani mwa Moabu na wakatuma wajumbe kwa mfalme wakisema, “Sisi ni ndugu. Turuhusuni tupite katika nchi yenu. Kama watu wetu au wanyama wetu wakinywa ama wakila cho chote, tutakilipa kwa moyo mweupe.” Lakini Mfalme Balaki alihangaika sana. Kiongozi huyo wa kundi hilo la Wanikolai hakuwa tayari kuachilia kanisa lipite likiwa na ishara zake na maajabu na madhihirisho mabalimbali ya Roho Mtakatifu, huku nyuso zao ziking‟aa kwa utukufu wa Mungu. Ilikuwa ni hatari sana, kwa kuwa huenda angepoteza baadhi ya kundi lake. Kwa hiyo Balaki alikataa kuwaruhusu Israeli wapite. Kwa kweli, hofu yake ya watu hao ilikuwa ni kuu mno, hivi kwamba akamwendea nabii wa kukodisha aliyeitwa Balaamu na akamwomba awe mpatanishi kati yake na Mungu na amsihi Mwenyezi awalaani Israeli, na azivunje nguvu zao kabisa. Basi Balaamu, akiwa na shauku ya kushiriki katika mambo ya kisiasa na kuwa mtu mkuu, alifurahia tu sana kufanya hivyo. Lakini alipoona ya kwamba ilimlazimu amkaribie pia, asikilizwe na Mungu kusudi hao watu wapate kulaaniwa kwa kuwa hangeweza kufanya hivyo yeye mwenyewe, akaenda kumwuliza Mungu kama angeweza kumpa ruhusa aende. Sasa je! jambo hilo silo kama tu Wanikolai tulio nao siku hizi? Wao hulaani ye yote ambaye hangefuata njia zao.

Wakati Balaamu alipomwomba Mungu ruhusa ya kwenda, Mungu alimkatalia. Jamani liliuma! Lakini Balaki alisisitiza, akimwahidi hata zawadi kubwa zaidi na heshima. Kwa hiyo Balaamu akarudi kwa Mungu. Sasa jibu moja toka kwa Mungu lingetosha. Lakini sio kwa Balaam mkaidi. Mungu alipoona ukaidi wake, alimwambia asimame aende. Upesi akamtandika punda akaondoka akaenda zake. Yeye angepaswa kutambua ya kwamba haya yalikuwa tu mapenzi ya Mungu ya kuruhusu naye asingaliweza kuwalaani hata kama angeenda mara ishirini na kujaribu mara ishirini. Jinsi watu siku hizi walivyo kama Balaamu! Wanaamini katika Miungu mitatu, wanabatizwa katika vyeo vitatu badala ya JINA, na hata hivyo Mungu atamtuma Roho juu yao kama vile alivyofanya juu ya Balaamu, nao wataendelea kuamini kuwa wao wako sahihi kabisa, nao ndio hawa hapa akina Balaamu kwa kweli kabisa. Mnaona, fundisho la Balaamu. Endelea hata hivyo. Fanya upendavyo. Wao husema, “Naam, Mungu ametubariki. Lazima liwe ni sahihi.” Ninajua Yeye amewabariki. Sikatai hilo. Lakini ni njia ile ile ya kimadhehebu ambayo Balaamu alipitia. Ni ya kuasi Neno la Mungu. Ni fundisho la uongo.

Kwa hiyo Balaamu alishuka akaenda barabarani kwa ukaidi mpaka malaika aliyetoka kwa Mungu akasimama mbele zake. Lakini huyo nabii (askofu, kadinali, mwenye kiti, rais na msimamizi mkuu) alipofushwa mno katika mambo ya Kiroho kwa wazo la heshima na utukufu na pesa hata hakuweza kumwona malaika mwenye upanga uliochomolewa amesimama. Huyo hapo amesimama amzuie nabii mwenye kichaa. Maskini yule punda alimwona na akakwepa kwa nyuma na mbele hadi mwishowe akamseta Balaamu mguu wake kwenye ukuta wa mawe. Yule punda akasimama na hangeendelea kwenda. Hangeweza kwenda. Kwa hiyo Balaamu akaruka na kuanza kumpiga. Yule punda akaanza kuzungumza na Balaamu. Mungu alimwacha punda huyo anene kwa lugha. Punda huyo hakuwa chotara; yeye alikuwa ni mbegu asili. Akamwambia nabii aliyepofushwa, “Je! mimi si punda wako, nami, je! sijakubeba wewe kwa uaminifu?” Balaamu akamjibu, “Ndiyo, ndiyo, wewe u punda wangu nawe umenibeba kwa uaminifu hadi sasa; na ikiwa siwezi kukufanya utembee, nitakuua... masalale! ni kitu gani hiki, kuzungumza na punda? Ajabu hii, nadhani nilimsikia huyu punda akizungumza nami nilikuwa nikimjibu.”

Mungu daima amenena kwa lugha. Yeye alinena kwenye karamu ya Belshaza kisha kwenye Pentekoste. Yeye anafanya hivyo tena leo. Ni onyo la hukumu ijayo.

Ndipo yule malaika akaonekana na Balaamu. Naye akamwambia Balaamu kama si punda yeye angekuwa amekufa hata sasa hakika kwa kumjaribu Mungu. Lakini Balaamu alipoahidi kurudi, alitumwa aende na onyo la kusema yale tu Mungu aliyompa.

Kwa hiyo Balaamu akashuka akaenda akatengeneza madhabahu saba kwa ajili ya wanyama safi wa sadaka. Akachinja kondoo dume kuonyesha kuja kwa Masihi. Alijua la kufanya apate kumkaribia Mungu. Mitambo yake ilikuwa sawa; bali si nguvu za kuendesha; ndivyo iliyvo sasa. Hivi hamwezi kuona enyi Wanikolai? Kule chini bondeni walikuweko Israeli wakitoa dhabihu ile ile, wakifanya mambo yale yale lakini ni mmoja tu aliyekuwa na ishara zilizofuata. Ni mmoja tu aliyekuwa na Mungu kati yao. Desturi hazitakufikisha po pote. Haziwezi kupachukua mahali pa dhihirisho la Roho. Jambo hilo ndilo lililotukia kule Nikea. Waliyachukua mafundisho ya Balaamu, si mafundisho ya Mungu. Nao wakajikwaa; naam walianguka. Wakawa watu waliokufa.

Baada ya dhabihu kutolewa, Balaamu alikuwa tayari kutabiri. Lakini Mungu akaufunga ulimi wake naye hakuweza kuwalaani. Aliwabariki.

Balaki alikasirika sana, lakini hapakuwepo na chochote ambacho Balaamu angeweza kufanya kuhusu huo unabii. Ulikuwa umenenwa na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo Balaki akamwambia Balaamu ashuke chini, aende katika lile bonde, akaangalie upande wao wa nyuma aone kama kuna uwezekano wa kuweza kuwalaani kwa njia fulani. Mbinu alizotumia Balaki ni zile zile wanazotumia leo. Madhehebu makubwa hudharau vikundi vidogo, na cho chote wanachopata kati yao kiwezacho kusababisha kashifa wao wanakichukua na kukitangaza. Kama watu wa kisasa wakiishi katika dhambi, hakuna mtu anayesema neno juu yake; bali hebu mmoja wa wateule apatikane na shida na kila gazeti litalilipua kote nchini. Naam, Israeli alikuwa na sehemu zake dhaifu (kimwili). Walikuwa na upande wao usio mwema; bali licha ya kutokamilika kwao, kwa kusudi la Mungu ambalo hufanya kazi kwa uchaguzi, kwa neema wala si kwa matendo, WALIKUWA NA WINGU MCHANA NA NGUZO YA MOTO USIKU, WALIKUWA NA MWAMBA ULIOPIGWA, NYOKA WA SHABA NA ISHARA NA MAAJABU. Walithibitishwa— si kwa juhudi zao, bali katika Mungu.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Pergamo.


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Two Babylons

by Rev Alexander Hislop.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.


Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Yule Mwanamke Yezebeli.)


Mungu ana
sifa nyingi...
lakini ana jina
moja tu la
kibinadamu na
jina hilo ni
Yesu.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.

Kumbukumbu la Torati 6:4



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.