Fundisho la Wanikolai.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Wakati wa Kanisa la Pergamo.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Pergamo.

Ufunuo 2:15,
“Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai, ambayo ninayachukia vile vile.”

Utakumbuka ya kwamba nilielezea katika Wakati wa Efeso kuwa lile neno, Nikolai, linatokana na maneno mawili ya Kiyunani: Nikao ambalo linamaanisha kutiisha, na Lao ambalo linamaanisha washirika. Nikolai maana yake ni, “kuwatiisha washiriki.” Sasa kwa nini hili ni jambo baya sana? Ni baya kwa sababu Mungu hajaliweka kamwe kanisa Lake mikononi mwa viongozi waliopigiwa kura wanaoongozwa na mawazo ya kisiasa. Ameliweka kanisa Lake katika ulinzi wa watu waliochaguliwa na Mungu, waliojazwa Roho, watu wanaoliishi Neno na kuwaongoza watu kwa kuwalisha Neno. Yeye hajawatenganisha watu katika madaraja hivi kwamba umati uongozwe na ukasisi mtakatifu. Ni kweli ya kwamba uongozi lazima uwe mtakatifu, lakini pamoja na hayo inapasa kusanyiko lote liwe takatifu. Isitoshe, hakuna mahali katika Neno ambapo makasisi ama wahudumu ama watu wa namna hiyo hupatanisha kati ya Mungu na watu, wala hakuna mahali ambapo wanatenganishwa katika kumwabudu kwao Bwana. Mungu anataka wote wampende na kumtumikia pamoja. Unikolai huharibu amri hizo na badala yake huwatenganisha wahudumu na watu na kuwafanya viongozi wawe mabwana-watawala badala ya kuwa watumishi. Sasa fundisho hili kweli lilianza kama tendo katika wakati wa kwanza. Yaonekana kwamba shida ilikuwa katika maneno mawili; “wazee wa kanisa” (makasisi) na “wachungaji” (maaskofu).

Ingawa Maandiko yanaonyesha kwamba kuna wazee kadha wa kadha katika kila kanisa, baadhi ya watu walianza (miongoni mwao akiwemo Ignatio) kufundisha kuwa wazo la askofu lilikuwa kwamba yeye ni mtu mwenye cheo kikubwa ama mwenye mamlaka na amri juu ya wazee. Sasa ukweli wa mambo ni kwamba neno “mzee” linaonyesha mtu huyo ni nani, ambapo neno “askofu” linaonyesha huduma ya mtu yuyo huyo. Mzee ni mtu mwenyewe. Mzee ni mtu mwenyewe. Askofu ni huduma ya huyo mtu. “Mzee” sikuzote limekuwa na kila mara litakuwa tu likimaanisha umri wa mtu katika Bwana. Yeye ni mzee, si kwa sababu amechaguliwa kwa kura ama amewekewa mikono, nk., bali ni kwa sababu yeye ana umri mkuu ZAIDI. Yeye amekolea zaidi, amefundishwa, si mwanafunzi, ni mtu anayetumainiwa kwa sababu ya ujuzi na uthabiti wa ujuzi wake wa Kikristo wa siku nyingi. Bali sivyo, maaskofu hawakushikilia nyaraka za Paulo, bali walipendelea kwenda kwenye taarifa ya Paulo ya wakati alipowaita wazee kutoka Efeso kwenda Mileto katika Matendo 20. Katika kifungu cha 17 taarifa hiyo inasema, “wazee” waliitwa na baadaye katika kifungu cha 28 wanaitwa waangalizi (maaskofu). Nao hawa maaskofu, (bila shaka wakiwa na mawazo ya kisiasa na wenye shauku ya kutaka madaraka) walisisitiza ya kwamba Paulo alikuwa akimaanisha kuwa “waangalizi” walikuwa ni zaidi ya mzee wa mtaa ambaye ana mamlaka rasmi katika kanisa lake mwenyewe tu. Kwao askofu alikuwa sasa mtu mwenye mamlaka juu ya viongozi wengi wa mitaa. Wazo kama hilo halikuwa la Kimaandiko wala la kihistoria, hata hivyo hata mtu wa hadhi kama ya Polikapu aliegemea kwenye mwongozo kama huo. Kwa hiyo, lile lililoanza kama tendo katika wakati wa kwanza lilifanywa fundisho la kweli na ndivyo lilivyo sasa. Maaskofu wangali wanadai mamlaka ya kuwaongoza watu na kuwatendea vile wapendavyo, wakiwaweka mahali wao wapendapo katika huduma. Jambo hili linakaidi uongozi wa Roho Mtakatifu aliyesema, “Nitengeeni Paulo na Barnaba kwa kazi ile niliyowaitia.” Hili ni pinga-Neno na ni pinga-Kristo. Mathayo 20:25-28, “Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; Na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; Kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi Yake iwe fidia ya wengi.“ Mathayo 23:8-9, “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana Mwalimu wenu ni Mmoja, yaani Kristo; nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni Mmoja, Aliye wa mbinguni.”

Ili kueleza jambo hili kwa wazi zaidi, hebu nielezee Unikolai kwa njia hii. Mnakumbuka ya kwamba katika Ufunuo 13:3 inasema, “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Sasa twajua kwamba kile kichwa kilichojeruhiwa kilikuwa ni Dola ya kipagani ya Kirumi, lile taifa kuu la dunia la kisiasa. Kichwa hiki kiliinuka tena kama “Dola ya kiroho ya Katoliki ya Kirumi.” Sasa angalia jambo hili kwa makini. Ni jambo gani ililofanya Rumi ya kipagani ya kisiasa ambalo lilikuwa ndilo msingi wa mafanikio yake? Hiyo, “iligawanya na kushinda.” Hiyo ndiyo iliyokuwa mbegu ya Rumi— tenganisha upate kushinda. Meno yake ya chuma yalirarua na kuangamiza. Yule aliyemrarua na kumwangamiza hangeweza kuinuka tena kama ule wakati alipoiangamiza Kathago na kutapanya chumvi humo. Mbegu zile zile za chuma zilibaki ndani yake wakati ilipoinuka kama kanisa la uongo, na mbinu zake zingali ni zile zile— tenganisha upate kushinda. Huo ni Unikolai na Mungu anauchukia.

Sasa ni jambo la kweli kihistoria linalojulikana sana kwamba wakati kosa hili lilipopenya likaingia kanisani, watu walianza kushindania huduma ya uaskofu na matokeo ikawa kwamba cheo hiki kilikuwa kikipewa wenye elimu zaidi na waliopiga hatua katika kupata mali na wenye mwelekeo wa kisiasa. Maarifa ya wanadamu na taratibu zake vikaanza kuchukua nafasi ya hekima ya Kiungu, na Roho Mtakatifu hakuwa tena anaongoza. Jambo hili bila shaka lilikuwa uovu wa kufisha, kwa kuwa maaskofu walianza kushikilia kuwa haikuhitaji tena tabia safi ya Ukristo kuhudumu aidha Neno au kuendeleza utaratibu wa dini kanisani kwa kuwa jambo muhimu ni sakramenti na taratibu zake. Jambo hili liliruhusu watu waovu (wadanganyifu) wawararue kondoo. Pamoja na mafundisho yaliyobuniwa na wanadamu ya kuwainua maaskofu hadi mahali ambapo hawakupewa katika Maandiko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa madaraja ambayo yaliunda serikali ya kidini; kwani muda si muda palikuwepo na maaskofu wakuu juu ya maaskofu na makadinali juu ya maaskofu wakuu na hata kufikia wakati wa Bonifasi wa tatu palikuwepo na papa juu ya wote, Kuhani Mkuu.

Huku yakiwemo mafundisho ya Wanikolai na muungano wa Ukristo na Ubabeli matokeo halisi kwa jumla hayana budi yalikuwa yale Ezekieli aliyoona katika Sura ya 8:10, “Basi nikaingia, nikaona; na tazama, kila namna ya wadudu, na wanyama wachukizao, na taswira za vinyago vyote vya nyumba ya Israeli, zimepigwa ukutani pande zote.” Ufunuo 18:2, “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza, kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Basi fundisho hili la Wanikolai, sheria hii iliyoanzishwa kanisani haikukubalika vizuri sana kwa watu wengi kwa kuwa waliweza kusoma waraka adimu au insha juu ya Neno lililoandikwa na mtu fulani mcha mungu. Kwa hiyo kanisa lilifanya nini? Liliwafukuza walimu wenye haki na kuyachoma moto magombo. Wakasema, “Inatakiwa elimu maalum kusoma na kulielewa Neno. Mbona hata Petro alisema kwamba mambo mengi aliyoandika Paulo yalikuwa magumu kuyaelewa.” Baada ya kuliondoa Neno kutoka kwa watu, muda si muda ilifikia mahali ambapo watu kusikiliza tu yale aliyosema kasisi, na kufanya aliyowaambia. Waliyaita hayo Mungu na Neno Lake takatifu. Waliyatwaa mawazo na maisha ya watu na kuwafanya wao watumwa wa ukasisi mdhalimu.

Basi kama ukitaka uhakika kuwa Kanisa Katoliki hudai maisha na mawazo ya watu, hebu sikiliza amri ya Theodosio wa X. Amri ya Kwanza ya Theodosio.

Amri hii ilitolewa mara tu baada ya yeye kubatizwa na Kanisa la Kwanza la Rumi. “Sisi watawala watatu wa dola tunaamuru ya kwamba raia wetu washike kwa uthabiti dini waliyofundishwa Warumi na Mt. Petro, ambayo imehifadhiwa kwa uaminifu kwa mapokeo na ambayo sasa inatangazwa na kuhani mkuu, Damasasi wa Rumi, na Petro, askofu wa Alekizandria, mtu mwenye utakatifu wa Kimitume kulingana na msingi wa Mitume, na mafundisho ya Injili; haya na tuamini katika Uungu mmoja wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wenye utukufu ulio sawa katika Utatu Mtakatifu. Tunaamuru ya kwamba wanaoishika imani hii waitwe Wakristo Wakatoliki; tunawabandika wafuasi wote wasio na akili wa dini nyingine jina lenye sifa mbaya la wazushi, na kukataza mikutano yao ya nyumbani kuitwa kwa majina ya makanisa. Mbali na hukumu ya haki ya kiungu, lazima wapatilizwe kwa adhabu kali ambayo serikali yetu, ikiongozwa na hekima ya mbinguni itaamua wanastahili kupewa...”

Zile sheria kumi na tano za adhabu ambazo mtawala huyu alizotoa katika miaka mingi kama hiyo ziliwanyang’anya wale wote wanaoamini katika wokovu haki zote za kuendeleza dini yao, ziliwaondoa kwenye kazi zote za serikali, na kuwatishia faini, kuwanyang’anya mali zao, kuhamishwa na hata katika matukio fulani, kifo.

Unajua nini? Tunaelekea kabisa upande huo leo.

Kanisa Katoliki la Kirumi hujiita kanisa Mama. Linajiita kanisa la kwanza ama kanisa la awali. Hilo ni sahihi kabisa. Lilikuwa ndilo Kanisa asili la Kwanza la Rumi lililoanguka na kuingia dhambini. Lilikuwa la kwanza ambalo liliunda madhehebu. Ndani yake mlionekana matendo na baadaye mafundisho ya Unikolai. Hakuna mtu atakayekana kuwa ndilo mama. Hilo ni mama na limezaa mabinti. Sasa binti hutokana na mwanamke. Mwanamke aliyevaa vazi la rangi nyekundu anaketi kwenye vilima saba vya Rumi. Yeye ni kahaba na amezaa mabinti. Mabinti hao ni makanisa ya Kiprotestanti yaliyotoka kwake na kisha yakarudi moja kwa moja kwenye madhehebu na Unikolai. Mama huyu wa makanisa binti anaitwa kahaba. Huyo ni mwanamke ambaye hakuwa mwaminifu kwa nadhiri zake za ndoa. Aliolewa na Mungu halafu akaenda kufanya uasherati na ibilisi na katika uasherati wake amezaa mabinti walio kama yeye kabisa. Muungano huu wa mama na binti ni upinga-Neno, upinga- Roho na kwa sababu hiyo ni upinga-Kristo. Naam, UPINGA- KRISTO.

Basi kabla sijaendelea mbali sana ninataka kusema kwamba hawa maaskofu wa mwanzoni walidhani ya kwamba wao walikuwa wako juu ya Neno. Waliwaambia watu kwamba wao waliweza kuwasamehe dhambi zao wakiziungama. Hilo halikuwa kweli kamwe. Walianza kuwabatiza watoto wachanga katika karne ya pili. Kwa kweli walibatiza kwa ajili ya kuzaliwa mara ya pili. Si ajabu watu leo hii wamechanganyikiwa. Ikiwa walikuwa wamechanganyikiwa namna hiyo wakati huo, karibu sana na Pentekoste, sasa wako katika hali mbaya zaidi kuliko nyakati zote zilizopita, wakiwa umbali wa yapata miaka 2,000 kutoka kwenye ile kweli ya asili.

Loo! Kanisa la Mungu, kuna tumaini moja tu. Rudi kwenye Neno na ukadumu nalo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Pergamo.



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Fundisho la Balaamu.)


Mungu ana
sifa nyingi...
lakini ana jina
moja tu la
kibinadamu na
jina hilo ni
Yesu.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

Waebrania 8:10


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Two Babylons

by Rev Alexander Hislop.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.