Mfululizo wa Wakati wa Mwisho.

  Mfululizo wa Wakati wa Mwisho.

Watiwa Mafuta Katika Wakati wa Mwisho.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Watiwa Mafuta Katika Wakati wa Mwisho.

Mathayo 24:23-24,
23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

Nawatakeni muone hapa katika Mathayo 24, Yesu alitumia neno “Makristo,” M-a-k-r-i-s-t-o, “Makristo.” Si Kristo, bali “Makristo,” wingi, si umoja. “Makristo.” Kwa hiyo, neno Kristo linamaanisha “aliyetiwa mafuta.” Na halafu kama ni “aliyepakwa mafuta,” hakutakuwa na mmoja tu, bali wengi, waliotiwa mafuta, “waliotiwa mafuta.” Mnaona?

La sivyo, kama Yeye angetaka kulichambua ili kwa namna fulani tupate kulifahamu vizuri zaidi, Yeye angesema, “Katika siku za mwisho watainuka watiwa mafuta wa uongo.” Sasa, hilo linaonekana karibu haliwezekani, mnaona, masharti ya “aliyetiwa mafuta.” Lakini angalia maneno yanayofuata, “na manabii wa uongo,” m-a-n-a-b-i-i, wingi.

Sasa, aliyetiwa mafuta, ni, “mmoja mwenye ujumbe.” Na njia pekee ambayo ujumbe unaweza kutolewa ni kwa yule aliyetiwa mafuta, na huyo angekuwa ni nabii, aliyetiwa mafuta. “Watatokea waalimu wa uongo, waliotiwa mafuta.” Nabii hufundisha ujumbe wake ni nini. Walimu waliotiwa mafuta, bali watu waliotiwa mafuta na mafundisho ya uongo. Waliotiwa mafuta, “Makristo,” wingi; “Manabii,” wingi. Na kama kuna kitu kama Ki-Kristo, umoja, basi hawa ingewabidi kuwa “waliotiwa mafuta,” kwamba unabii wao wa yale waliyokuwa wakifundisha ungekuwa tofauti, kwa sababu wao ni watiwa mafuta, waliotiwa mafuta.

Sasa, ni somo la shule ya Jumapili, tunataka ku-kujaribu kuleta hili kwenye shindano la kweli, kwa Maandiko, si kwa yale mtu mwingine amesema juu yake, bali ni kusoma tu Maandiko.
Mnaweza kusema, “Hili linawezekanaje? Hivi watiwa mafuta...”
Walikuwa nini? “Makristo,” M-a-k-r-i-t-o, watiwa mafuta. “Makristo, na manabii wa uongo.” Waliotiwa mafuta, bali manabii wa uongo!

Yesu alisema, ya kwamba, “Mvua huwanyeshea wenye haki na wasio haki.”
Sasa, mtu fulani anaweza kuniambia, “Je! Unaamini ya kwamba upako huo juu ya watu hao unamaanisha kwamba ni upako wa Roho Mtakatifu?” Naam, bwana, Roho Mtakatifu halisi wa Mungu juu ya mtu, na hata hivyo ni uongo.

Sasa sikilizeni kwa makini na mwone Yeye alivyosema. “Nao wataonyesha ishara na maajabu, hata ingewapoteza walio Wateule kama yamkini.” Nao wametiwa mafuta na Roho Mtakatifu halisi. Ninajua hili linasikika ni la kipumbavu sana, bali tutachukua wakati na kulielezea kwa Neno, ya kwamba hiyo ni HIVI BWANA ASEMA kabisa, ile Kweli.

-----
Mathayo 5:45,
45 Ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki;
(Mvua hujiliaa walio waovu sawasawa na walio wema.)

Waebrania 6:7-8,
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; 8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.

-----
Sasa linganisha hilo na Mathayo 5:24 tena. Angalia, Yesu alisema mvua na jua huja juu ya nchi, kwamba Mungu huituma kuandaa chakula na vitu kwa ajili ya watu wa duniani. Na mvua hutumwa kwa ajili ya chakula, mboga. Lakini magugu, kwekwe, vikiwa shambani, yanapokea kitu kile kile. Mvua ile ile inayoifanya ngano ikue ni mvua ile ile inayofanya magugu kukua.

-----
Naam, kwa hiyo, mvua ikishuka juu uoto wa asili wa nchi, ni mfano wa mvua ya Kiroho ambayo inatoa Uzima wa Milele, ikishuka juu ya Kanisa, kwa kuwa tunaiita mvua za masika na mvua za vuli. Na ni mvua, ikimwagika kutoka kwa Roho wa Mungu, juu ya Kanisa Lake.

Angalia, ni jambo la ajabu sana hapa. Mnaona? Wakati mbegu hizo zilipoingia ardhini, vyo vyote zilivyoingia pale, zilikuwa ni miiba kwanza. Lakini hapo ngano ile ambayo iliingia ardhini, na mboga, zilikuwa mboga kwanza. Na kila mimea ikijizaa, tena, ilionyesha ya kwamba ilikuwa katika mwanzo wa asili. Nao watawapoteza Walioteuliwa kama yamkini,“ maana wao wanapata mvua ile ile, baraka zile zile, wakionyesha ishara zile zile, maajabu yale yale Mnaona? ”Watawapoteza, ama watawadanganya walio Wateule kama yamkini.“ Sasa, mchongoma hauwezi kujizuia kuwa mchongoma, wala ngano haiwezi kujizuia kuwa ngano; ni kile Muumba wa kila kimoja alichokusudia hapo mwanzo. Hao ni Wateule. Mvua ile ile!

-----
Sasa jua huja na kuipevusha punje. Naam, haliwezi kuipevusha yote mara moja. Inapoendelea, ikikomaa, inaendelea kukomaa mpaka unapofikia kwenye suke kamili. Ndivyo ilivyo, leo, pamoja na Kanisa. Lilianza katika uchanga wake, huko nyuma katika wakati wa giza, ambapo lilikuwa chini ya ardhi. Limekua sasa hata kukomaa. Nasi tunaweza kuona jambo hilo, kikamilifu, namna ambavyo Mungu kwa maumbile daima...

Huwezi kuvuruga maumbile. Hiyo ndiyo shida ya siku hizi. Tunarusha mabomu, na huko nje katika bahari hiyo, tukivunja na kuvuruga kwa mabomu ya atomiki. Unaendelea tu kuvunjavunja zaidi na zaidi takataka hizo za wakati wote, unaziangusha mle ndani. Unakata miti; tufani zitakupata. Unauzuia mto kwa kujenga bwawa; utafurika. Huna budi kupata njia ya Mungu ya kufanya mambo na kukaa ndani yake. Tumewafanya watu madhehebu katika makanisa na mashirika; angalia tulichopata! Kaa katika njia iliyoandaliwa na Mungu.

Lakini, mnaona, “Yeye huituma mvua,” tukirudi kwenye somo letu, “juu ya wenye haki na wasio haki.” Yesu anakwambia hapa sasa, katika Mathayo 24, ingekuwa ni ishara katika wakati wa mwisho. Sasa, kama ishara hii itajulikana tu wakati wa mwisho, basi itabidi iwe ni baada ya kufunguliwa kwa Mihuri hiyo. Mnaona? Ni ishara ya mwisho. Hiyo ingekuwa, wakati mambo haya yatakapotukia, itakuwa katika wakati wa mwisho. Na itakuwa ni ishara, sasa, kwa hiyo Wateule hawatachanganyikiwa katika mambo haya. Mnaona jambo hilo? Halafu, halina budi kufunuliwa, kuwekwa wazi.

Angalia, ngano na magugu yote yanaishi kwa Upako ule ule kutoka Mbinguni. Wote wawili wanafurahia jambo Hilo. Ninakumbuka jambo hili, nikirejea kwenye tukio hili juu hapa siku ile kwenye Kinu cha Green. Ni- niliona ono hilo likitokea. Na kulikuwako na dunia kubwa, nayo yote ilikuwa imelimwa. Na hapo Mpanzi akatoka, kwanza. Ninataka kuweka hilo mbele yenu. Angalia kile kinachotoka kwanza, halafu kile kinachofuata. Na wakati Mtu huyu aliyevalia mavazi meupe alipokuja kote duniani, akipanda mbegu, ndipo nyuma Yake akaja mtu, amevaa nguo nyeusi, alionekana mjanja sana, akinyemelea nyuma Yake, akipanda magugu. Na wakati hili lilipotukia, ndipo nikaona mimea yote miwili ikikua. Na ilipokua, mmoja ulikuwa ni ngano na mwingine ulikuwa ni magugu.

Kisha kukatokea ukame, hapo ambapo, ilionekana kwamba, yote miwili ilikuwa imeviinamisha vichwa vyao ikililia mvua. Ndipo likatokea wingu kubwa juu ya nchi, nayo ikanyesha. Nayo ngano ikainuka na kusema, “Bwana asifiwe! Bwana asifiwe!” Na magugu yakainuka na kupiga makelele, “Bwana asifiwe! Bwana asifiwe!” Matokeo yale yale. Wote wawili wakiangamia, wote wawili wanaondoka. Na halafu ngano inainuka na kuona kiu. Na kwa sababu ilikuwa katika shamba lile lile, bustani ile ile, mahali pale pale, chini ya bubujiko lile lile la maji, ngano ikainuka kisha magugu yakainuka kwa kitu kile kile. Angalia, maji yale yale ya upako huzaa ngano, huzaa magugu.

Roho Mtakatifu yeye yule anayelitia mafuta Kanisa, ambaye huwapa shauku ya kuziokoa nafsi, ambaye huwapa nguvu za kufanya miujiza, Yeye huwashukia wasio haki kama wale wenye haki. Roho yeye yule! Sasa, huwezi kufanya jambo lingine na kuelewa Mathayo 24:24. Yeye alisema, “Watatokea Makristo wa uongo,” watiwa mafuta, wa uongo. Waliotiwa mafuta kwa Kitu kilicho halisi, bali wawe manabii wa uongo wa Kitu hicho, waalimu wa uongo wa Kitu hicho.
Ni kitu gani kingemfanya mtu atake kuwa mwalimu wa uongo wa kitu ambacho ni Kweli? Sasa tutafikia alama ya mnyama katika dakika chache, nanyi mtaona ni madhehebu. Mnaona? Walimu wa uongo; wa uongo, waliotiwa mafuta. Makristo waliotiwa mafuta, bali ni walimu wa uongo. Ndiyo njia pekee unayoweza kuona jambo hilo.

-----
Angalia, lakini kile wanachotoa ndicho kinachokuonyesha tofauti yake. “Kwa matunda yao,” Yesu alisema, “mtawatambua.” “Mtu hachumi zabibu katika miiba,” ingawa miiba kweli iko kwenye mzabibu. Hiyo ingewezekana, bali tunda litaonyesha. Tunda ni nini? Neno, kwa ajili ya tunda la wakati. Hivyo ndivyo ilivyo, mafundisho yao. Mafundisho ya nini? Mafundisho ya wakati, ni wakati gani. Mafundisho ya mwanadamu, mafundisho ya kimadhehebu, lakini, ama Neno la Mungu kwa huo wakati?
Sasa, wakati unaenda upesi sana, hata tungeshikilia jambo hilo kwa muda mrefu. Lakini nina hakika ya kwamba ninyi mliopo hapa, na nina hakika ninyi mlioko kote nchini, mnaweza kuona ninalojaribu kuwaambia, kwa kuwa hatuna muda mrefu zaidi wa kudumu katika jambo hilo.

Lakini ili kwamba muone ya kwamba Upako unakuja juu ya wasio haki, walimu wa uongo, na kuwafanya wafanye yale hasa Mungu aliyowaambia wasifanye; bali wao watalifanya, haidhuru. Kwa nini? Hawawezi kujizuia. Mwiba unawezaje kuwa kitu kingine ila mwiba? Haidhuru ni utanyunyiziwa mvua nzuri namna gani, hauna budi kuwa ni mwiba. Hiyo ndiyo sababu Yesu alisema, “Zitafanana sana zingewapoteza Walioteuliwa,” ambao ni mashina, “kama yamkini,” bali haiwezekani. Ngano haiwezi kufanya kitu ila kuzaa ngano; hivyo tu ndivyo inavyoweza kuvumilia.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Watiwa Mafuta Katika Wakati wa Mwisho.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.

Ufunuo 11:15


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Watiwa Mafuta Katika
Wakati wa Mwisho.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.