Wakati wetu, Laodikia.
Wakati wa Kanisa la Laodikia.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Laodikia.Ufunuo 3:15-19,
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa Changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue Kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, na kwamba aibu ya uchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao Mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.Tulipokuwa tunasoma hili pamoja nina hakika ya kwamba umeona ya kwamba Roho hajasema jambo moja zuri kuhusu wakati huu. Yeye anatoa mashtaka mawili na kutoa hukumu Yake juu ya mashtaka hayo.
(1) Ufunuo 3:15-16, “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; Ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa Changu.”
Tutachunguza jambo hili kwa makini. Inasema ya kwamba kundi hili la wakati huu wa kanisa la Laodikia ni vuguvugu. Uvuguvugu huu unastahili hukumu kutoka kwa Mungu. Hukumu ni kwamba wao watatapikwa watoke katika kinywa Chake. Hapa ndipo hatutaki kukosea kama watu wengi wanavyofanya. Wao wanasema pasipo busara kabisa ya kwamba Mungu anaweza kukutapika utoke katika kinywa Chake na hilo linathibitisha ya kwamba hakuna kitu kama ukweli wo wote kwenye fundisho la uvumilivu wa Watakatifu. Ninataka kusahihisha mawazo yako sasa hivi. Aya hii haitolewi kwa mtu binafsi. Inapewa kanisa. Yeye analizungumzia kanisa. Isitoshe, kama utaliweka tu Neno niani utakumbuka ya kwamba hakuna mahali linaposema ya kwamba sisi tuko katika KINYWA cha Mungu. Tumechorwa kwenye vitanga vya mikono Yake. Tumebebwa moyoni Mwake. Huko nyuma kabisa katika nyakati zisizojulikana kabla ya wakati tulikuwa katika nia Yake. Tuko katika zizi Lake, na katika malisho Yake, lakini kamwe si katika kinywa Chake. Lakini ni kitu gani kilicho katika kinywa cha Bwana? Neno liko kinywani Mwake.
Mathayo 4:4, “Lakini akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”
Neno linapaswa kuwa vinywani mwetu, pia. Sasa tunajua ya kwamba kanisa ni mwili Wake. Liko hapa likipachukua mahali Pake. Ni kitu gani kitakachokuwa kinywani mwa kanisa? NENO. I Petro 4:11,
“Mtu akisema, na aseme kama mausia (Neno) ya Mungu.”
II Petro 1:21,
“Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali watu watakatifu wa Mungu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”
Basi watu hawa wa siku za mwisho wana shida gani? WAMEONDOKA KWENYE NENO. HAWANA MOTO TENA KUHUSU HILO. WAO NI VUGUVUGU KUHUSU HILO. Nitathibitisha jambo hilo sasa hivi.Wabatisti wana kanuni zao za imani na mafundisho ya sharti yaliyo na msingi wake katika Neno nawe huwezi kuwatikisa. Wao wanasema siku za miujiza za mitume zimekwisha na hakuna Ubatizo wa Roho Mtakatifu, baada ya kuamini. Wamethodisti wanasema (kwa kutumia Neno) hakuna ubatizo wa maji (kunyunyizia si ubatizo) na ya kwamba utakaso ndio Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kanisa la Kristo linashikilia sana ubatizo wa kuzaliwa mara ya pili na mara nyingi sana wanatumbukizwa wakiwa wenye dhambi wakavu na kutoka wakiwa wenye dhambi waliolowa maji. Hata hivyo wao wanadai ya kwamba mafundisho yao yana msingi wake katika Neno. Nenda moja kwa moja kwenye mstari na uwafikie Wapentekoste.
Wana Neno? Wape jaribio la Neno uone. Wao wataliuza Neno kwa jambo la kusisimua karibu kila wakati tu. Kama unaweza kutoa madhihirisho kama mafuta na damu na lugha na ishara nyinginezo, kama ziko kwenye Neno ama haziko, ama kama hayo yamefasiriwa vizuri kutoka kwenye Neno, walio wengi watalikimbilia. Lakini ni nini kimelipata Neno? Neno limewekwa kando, kwa hiyo Mungu anasema, “Mimi niko kinyume nanyi nyote. Nitawatapika mtoke katika kinywa Changu. Huu ndio mwisho. Kwa kuwa saba kati ya nyakati saba, sijaona kitu ila watu wakiliheshimu neno lao wenyewe kuliko Langu. Kwa hiyo mwishoni mwa wakati huu ninawatapika mtoke katika kinywa Changu. Yote yamekwisha. Nitazungumza basi. Naam, niko hapa katikati ya Kanisa. Amina wa Mungu, aliye mwaminifu na wa kweli atajifunua Mwenyewe na itakuwa KWA NJIA YA NABII WANGU.” Naam, hivyo ndivyo ilivyo. Ufunuo 10:7,
“Na katika siku za sauti ya mjumbe wa saba, atakapoanza kupiga baragumu, siri ya Mungu itatimizwa kama alivyowahubiri watumishi Wake manabii.”Hilo hapo. Yeye anamtuma nabii aliyethibitishwa. Anatuma nabii baada ya karibu miaka elfu mbili. Yeye anamtuma mtu fulani aliye mbali sana na madhehebu, elimu, na ulimwengu wa dini hivi kwamba kama vile Yohana Mbatizaji na Eliya wa kale, yeye atasikia tu kutoka kwa Mungu na atakuwa na “Bwana asema hivi” na kunena kwa niaba ya Mungu. Yeye atakuwa kinywa cha Mungu NAYE, KAMA INAVYOTANGAZWA KATIKA MAL. 4:6, ATAIGEUZA MIOYO WA WATOTO IWAELEKEE BABA ZAO. Atawarudisha wateule wa siku za mwisho nao watamsikiliza nabii aliyethibitishwa akitoa kweli halisi kama vile ilivyokuwa kwa Paulo. Atairudisha kweli kama walivyokuwa nayo. Na hao wateule walio pamoja naye katika siku hiyo watakuwa ndio wanaomdhihirisha Bwana kwa kweli na watakuwa ndio Mwili Wake na kuwa sauti Yake na kutenda kazi Zake. Haleluya! Mnaona jambo hilo?
Kuzingatiwa kwa muda mfupi kwa historia ya kanisa kutathibitisha jinsi wazo hili lilivyo sahihi. Katika Zama za Giza watu walikuwa karibu wamepotelewa na Neno. Lakini Mungu alimtuma Luther akiwa na NENO. Waluteri walikuwa ni kinywa cha Mungu kwa wakati huo. Lakini wao wakaunda madhehebu, na tena hilo Neno safi lilipotezwa kwa maana madhehebu huegemea kwenye mafundisho ya sharti na kanuni za imani, wala hawaegemei kwenye Neno lililo halisi. Wao hawakuweza tena kuwa kinywa cha Mungu. Ndipo Mungu akamtuma Wesley, naye alikuwa ndiye sauti iliyokuwa na Neno katika siku yake. Watu waliouchukua ufunuo wake kutoka kwa Mungu wakawa nyaraka zilizo hai zilizosomwa na kujulikana na watu wote kwa ajili ya kizazi chao. Wakati Wamethodisti waliposhindwa, Mungu aliwainua wengine na kwa hiyo jambo hilo limeendelea kwa miaka mingi mpaka katika wakati huu wa mwisho kuna watu wengine nchini, ambao chini ya mjumbe wao watakuwa ndio sauti ya mwisho kwa wakati wa mwisho.
Naam bwana. Kanisa si “kinywa” cha Mungu tena. Ni kinywa chake lenyewe. Kwa hiyo Mungu analiacha. Ataliangamiza kupitia kwa nabii na bibi-arusi, kwa kuwa sauti ya Mungu itakuwa ndani ya bibiarusi. Naam iko, kwa maana inasema katika sura ya mwisho ya Ufu. aya ya 17,
“Roho na bibi-arusi wasema, njoo.” Mara nyingine tena ulimwengu utasikia moja kwa moja kutoka kwa Mungu kama ilivyokuwa wakati wa Pentekoste; lakini bila shaka huyo Bibi-arusi Neno atakataliwa kama ilivyokuwa katika wakati wa kwanza.Sasa Yeye ameupigia kelele wakati huu wa mwisho, “Mnalo Neno. Mna Biblia nyingi kuliko mlivyowahi kuwa, lakini hamfanyi lo lote juu ya Neno ila kuligawanya na kulipasua vipande-vipande, mkichukua mnalotaka na kuacha yale msiyotaka. Hamtaki KULIISHI, ila kulibishania. Afadhali mngalikuwa baridi ama moto. Kama mngalikuwa baridi na mkalikataa, ningaliweza kuvumilia jambo hilo. Kama mngalikuwa moto kweli kweli kujua ni kweli na kuliishi, ningewasifu kwa ajili ya jambo hilo. Lakini wakati mnapolichukua tu Neno Langu wala hamliheshimu, Mimi Nami sina budi kukataa kuwaheshimu. Nitawatapika kwa maana mnanichefua moyo.”
Sasa mtu ye yote anajua ya kwamba maji yenye uvuguvugu ndiyo yanayokuchefua moyo. Kama unataka dawa ya kutapisha, maji yenye uvuguvugu ndiyo yanayofaa sana kunywa. Kanisa vuguvugu limemchosha Mungu Naye ametangaza atalitapika. Inatukumbusha jinsi alivyojisikia kabla tu ya ile gharika, sivyo?
Ee Mungu! laiti kanisa lingalikuwa baridi ama moto. Ni afadhali sana, lingekuwa na juhudi (moto). Lakini si moto. Hukumu imetolewa. Yeye si sauti ya Mungu tena kwa ulimwengu. Litashikilia kwamba ndivyo lilivyo, lakini Mungu anasema sivyo.
Loo! Mungu yungali ana sauti kwa ajili ya watu wa ulimwengu, kama vile tu aliyompa bibi-arusi sauti. Sauti hiyo imo ndani ya bibi-arusi kama tulivyosema na tutazungumza zaidi juu ya jambo hilo baadaye.
(2) Ufunuo 3:17-18, “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue Kwangu dhahabu iliyojaribiwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”
Sasa angalia fungu la kwanza la maneno ya aya hii, “kwa kuwa wasema.” Mnaona, wao walikuwa wananena. Walikuwa wakinena kama kinywa cha Mungu. Hili linathibitisha yale hasa niliyosema aya za 16-17 zilichomaanisha. Lakini ingawa wao wanasema hivyo, hilo halilifanyi kuwa ni sawa. Kanisa Katoliki linasema ya kwamba linanena kwa niaba ya Mungu, likisema ndilo sauti ya hakika ya Bwana. Jinsi watu wo wote wanavyoweza kuwa waovu kiroho jinsi hiyo ni zaidi ya nijuavyo mimi, lakini wao wanazaa kulingana na mbegu iliyo ndani yao, nasi tunajua mahali mbegu hiyo ilikotoka, sivyo?
Kanisa la Laodikia linasema, “Mimi ni tajiri na nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu.” Hivyo ndivyo lilivyojipima. Lilijiangalia na hilo ndilo lililoona. Likasema, “Mimi ni tajiri,” ambalo linamaanisha ni tajiri katika mambo ya ulimwengu huu.
Linajigamba mbele ya Yakobo 2:5-7,
“Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia hii wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? Hawalitukani Jina lile zuri mliloitwa?”
Sasa mimi SIDOKEZI ya kwamba tajiri hawezi kuwa wa Kiroho, bali sote tunajua ya kwamba Neno linasema ni wachache sana walio wa kiroho. Maskini ndio walio wengi katika mwili wa kanisa la kweli. Sasa basi, kama kanisa likijaa mali, tunajua jambo moja tu; “Ichabod” limeandikwa kwenye malango yake makubwa! Huwezi kukana hilo, kwa maana hilo ni Neno.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Laodikia.
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti Yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja Nami.
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti Changu cha enzi, kama Mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba Yangu katika kiti Chake cha enzi.
Yeye aliye na sikio, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ufunuo 3:20-22