Kifo. Ni nini basi?
<< uliopita
ijayo >>
Ng’ambo Ya Pazia La Wakati.
William Branham.Asubuhi moja nilikuwa nimelala kwenye kitanda changu. Nilikuwa ndiyo tu nimeamka kutoka usingizini, na nikaweka mikono yangu nyuma ya kichwa changu na kutulia kichwa changu kikiwa juu ya mto. Ndipo nikaanza kujiuliza ule upande mwingine utakuwaje. Nilitambua kwamba nimeishi zaidi ya nusu ya maisha yangu kama nitaishi kuwa na umri kama watu wangu, na nilitaka kufanya zaidi kwa ajili ya Bwana kabla sijaondoka kwenye maisha haya.
Nikasikia Sauti ikisema: “Ndiyo tu unaanza! Endelea kupigana vita! Endelea kupigana!” Nilipokuwa nimelala pale nikitafakari yale maneno, nikawaza kwamba niliwazia tu kwamba nilikuwa nimesikia Sauti. Ile Sauti ikasema tena: “Endlea kupigana vita! Endelea kutembea! Endelea kutembea!” Bado nikiwa siamini, nikawaza kwamba inawezekana nimenena yale maneno mimi mwenyewe. Nikaweka midogo kati ya meno yangu na kuweka mkono wangu juu ya mdomo wangu na kusikiliza. Ile Sauti ikanena tena: “Endelea tu! Kama ungelijua kile kilichoko mwishoni mwa njia!” Nikasikia muziki na maneno ya wimbo wa zamani, uliozoeleka: “Natamani nyumbani na sina furaha, na nataka kumwona Yesu, Ningependa kusikia zile kengele za bandarini zikigonga mfululizo. Ingeng’arisha njia yangu na kuondoa woga wote. Bwana, hebu nitazame kupita pazia la wakati!”
Ndipo ile Sauti ikasema, “Je, ungependa kuona tu n’gambo ya lile pazia?” Nikajibu: “Hilo litanisaidia mno!”
Siwezi kusema kile kilichotukia. Kama nilikuwa katika mwili au nje au kama ilikuwa ni kubadilishwa, sijui, lakini haikuwa kama ono lolote nililowahi kuwa nalo. Niliweza kuona pale mahali nilikopelekwa na niliweza kujiona mwenyewe nikiwa nimelala nyuma kule juu ya kitanda changu. Nikasema: Hiki ni kitu kigeni!”
Kulikuweko na idadi kuu ya watu na walikuja wakikimbia kunisalimu, wakilia: “Loo, ndugu yetu wa thamani!” Kwanza walikuja wanawake vijana, walioonkena wakiwa katika umri wa miaka ya mwanzo ya ishirini, na walipokuwa wakinikumbatia walisema: “Ndugu yetu wa thamani!” Wanaume vijana, katika na mng’ao wa ujana, wakiwa na macho yaking’aa kama nyota kwenye usiku wa giza, wakiwa na meno kama lulu nyeupe, wakanikumbatia, wakisema, “”Ndugu yetu wa thamani!”
Ndipo nikaona kwamba mimi, pia, nilikuwa nimekuwa kijana tena. Nikajitazama mwenyewe pale na kugeuka na kutazama nyuma tena kwenye mwili wangu wa zamani ukiwa umelala kitandani mikono yangu ikiwa kisogoni mwangu. Nikasema: “Sielewi hili!”
Nilipoanza kujaribu kuelewa pale mahali nilikokuwa, nikaanza kutambua kwamba hapakuwepo na jana na hakuna kesho kule. Hakuna aliyeonekena kuchoka. Wakati umati wa wasichana walio wazuri zaidi ya wote niliowahi kuwaona waliponikumbatia, niligundua kulikuweko na upendo mkuu ulionizunguka na hakuna mvuto wa kimwili kama ulio katika tabia ya mwanadamu. Niliwaona hawa wasichana wote walivaa nywele zao hadi kiunoni mwao na sketi zao ziliteremka hadi kwenye nyayo zao.
Baada ya hili, Hope, mke wangu wa kwanza, akanikumbatia, na kusema: “Ndugu yangu wa thamani!” Ndipo mwanamke mwingine kijana akanikumbatia na Hope akageuka na kumkumbatia yule mwanamke kijana. Nikasema: “Silielewi hili. Hili ni jambo tofauti kabisa na upendo wetu wa kibinadamu. Sitaki kurudi kwenye ule mwili wa zamani kitandani.”
Ndipo Sauti ikanena na mimi: “Hiki ndicho ulichohubiri kwamba Roho Mtakatifu ni nini! Huu ni upendo mkamilifu. Hakuna chochote kitakachoingia hapa bila huo!”
Kilichofuata nilichukuliwa juu na kuketishwa mahali pa juu. Wote walionizunguka walikuwa idadi kuu ya wanaume na wanawake waking’aa kwa ujana. Walikuwa wakilia, kwa furaha: “Loo, ndugu yetu wa thamani, tuna furaha mno kukuona hapa!” Nikawaza: “Sioti ndoto, kwani naweza kuona hawa watu na naweza kuona mwili wangu ukiwa umelala nyuma kule kitandani.”
Ile Sauti ikanena na mimi: “Unajua imeandikwa katika Biblia kwamba manabii walikusanyika pamoja na watu wao.” Nikasema: “Ndiyo nakumbuka hilo katika Maandiko, lakini hakuna akina Branham wengi hivi.” Ile Sauti ikajibu: “Hawa siyo akina Branham. Hawa ni waongofu wako, wale uliowaongoza kuja kwa Bwana. Baadhi ya hawa wanawake unaofikiri ni vijana mno na wazuri walikuwa na umri wa zaidi ya miaka tisini ulipowaongoza kuja kwa Bwana. Si ajabu wanalia, ‘Ndugu yangu wa thamani!’” Ndipo ule umati ukalia kwa pamoja: “Kama hukuwa umekwenda na Injili, sisi tusingelikuwa hapa!”
Nikauliza: “Ee, Yesu yuko wapi? Nataka kumwona Yeye!” Wale watu wakajibu: “Yeye yuko juu zaidi kidogo. Siku fulani Yeye atakuja kwako. Wewe ulitumwa kama kiongozi, na Mungu atakapokuja, Yeye atakuhukumu wewe kulingana na fundisho lako.” Nikauliza: “Itawapasa Paulo na Petro kusimama kwenye hii hukumu pia?” Jibu lilikuwa: “Ndiyo!” Nikasema, “Nimehubiri kile wao walichohubiri. Sikupindisha kutoka Hilo kwenda upande mmoja au mwingine. Pale walipobatiza katika Jina la Yesu, nilifanya pia; pale walipofundisha Ubatizo wa Roho Mtakatifu, nilifanya pia. Chochote walichofundisha, nilifundisha, pia.”
Wale watu wakasema, “Tunajua hilo,” “na tunajua kwamba tutarudi duniani pamoja na wewe wakati fulani. Yesu atakuja na kukuhukumu kulingana na Neno ulilotuhubiria. Ndipo utatupeleka Kwake, na sote kwa pamoja tutarudi duniani kuishi milele.” Nikauliza: “Je, inanipasa kurudi duniani, sasa?” Wakajibu: “Ndiyo, lakini endelea kukazana!”
Nilipoanza kuondoka kwenye ile sehemu nzuri ya furaha, kadiri macho yangu yangeweza kuona, watu walikuwa wananijia ili kunikumbatia, wakilia: “Ndugu yangu wa thamani!”
Kwa ghafla nilikuwa nimerudi kwenye kitanda tena. Nikasema: “Ee, Mungu, nisaidie! Kamwe usiniruhusu niwe na suluhu na Neno. Hebu nidumu moja kwa moja kwenye Neno. Sijali kile mwingine yeyote anachofanya, Bwana, niruhusu nikazane kwenda kwenye ile sehemu nzuri, ya furaha!”
Nimeshawishika zaidi kuliko wakati wowote katika maisha yangu kwamba itahitaji upendo mkamilifu ili kuingia pale mahali. Hapakuwepo na wivu, hakuna kuchoka, hakuna ugonjwa, hakuna uzee, hakuna kifo. Uzuri mkuu na furaha.
Chochote unachofanya, weka pembeni kila kitu kingine hadi upate upendo mkamilifu! Fika mahali ambapo unaweza kumpenda kila mtu, hata kila adui. Haidhuru kama eropleni inatikisika, kimulimuli kinamulika, au bunduki za adui ziko juu yako, haya mambo hayajalishi: pata upendo mkamilifu!
Kama hujaokoka, mpokee Yesu Kristo kama Mwokozi wako sasa! Kama hujabatizwa katika maji, ubatizwe sasa! Kama hujapokea Ubatizo katika Roho Mtakatifu, upokee huo sasa! Kazana kuuendea huo upendo mkamilifu ambao utakupeleka kwenye ile sehemu nzuri na ya furaha ng’ambo ya pazia la wakati!
W. Branham.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ng’ambo Ya Pazia La Wakati.(PDF Kiingereza) The Rejected King.
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Waebrania 9:27,28
Bonyeza juu ya picha kushusha PDFs au ukubwa kamili picha.
Acts of the Prophet (PDFs Kiingereza) |
The Two Babylons by Rev Alexander Hislop. (PDF Kiingereza) |
Mteremko wa mlima na mwaridi katika theluji nchini China. |
Lilies ya Moto. |
Nguzo ya Moto. - Houston 1950. |
Mwanga juu ya mwamba piramidi. |
Hiki ndicho
ulichohubiri kwamba
Roho Mtakatifu
ni nini!
Huu ni upendo
mkamilifu.