Yesu Kristo ni Mungu.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Siri kuu ya Utatu.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ufunuo wa Yesu Kristo.

Ufunuo 1:5,
“Tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,”

Ufunuo 1:8,
“Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”

Sasa maneno yote haya, 'Yeye Aliyeko', na 'Aliyekuwako', na 'Atakayekuja', na 'Shahidi Mwaminifu', na 'Mzaliwa wa Kwanza wa Waliokufa', na 'Mkuu wa Wafalme wa Dunia', na 'Alfa na Omega', na 'Mwenyezi', ni sifa na maelezo ya MTU YULE YULE MMOJA, Ambaye ni Bwana Yesu Kristo, Ambaye alituosha dhambi zetu katika damu Yake Mwenyewe.

Roho wa Mungu ndani ya Yohana ananena namna hii kusudi aonyeshe Uungu Mkuu wa Yesu Kristo na kumfunua Mungu kama ni MUNGU MMOJA. Leo kuna kosa kubwa. Ni kwamba kuna Miungu watatu badala ya mmoja. Ufunuo huu kama alivyopewa Yohana na Yesu, Mwenyewe, husahihisha kosa hilo. Si kwamba kuna Miungu watatu, bali ni Mungu mmoja aliye na ofisi tatu. Kuna Mungu Mmoja mwenye vyeo vitatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ufunuo huu mkuu ni ule uliokuwa na kanisa la mwanzoni, na hauna budi kurejeshwa katika siku hii ya mwisho pamoja na kanuni sahihi ya ubatizo wa maji.

Sasa wanatheolojia wa kisasa hawatakubaliana nami kwa kuwa hapa ndipo palipoandikwa katika gazeti kubwa la Kikristo. “Fundisho hilo (kuhusu Utatu) ndilo asili na kiini hasa cha Agano la Kale. Ni asili na kiini kabisa cha Agano Jipya. Agano Jipya linapinga tu kama Agano la Kale wazo kwamba kuna zaidi ya Mungu mmoja. Hata hivyo Agano Jipya kwa udhahiri ule ule linafundisha ya kwamba Baba ni Mungu, na Mwana ni Mungu, na Roho Mtakatifu ni Mungu, na ya kwamba hawa watatu SI sifa tatu za Mtu yule yule, bali ni watu watatu wakisimama kwa kweli katika uhusiano wa kibinafsi mmoja kwa mwingine. Hapo tuna lile fundisho kuu la Nafsi Tatu lakini ni Mungu mmoja.”

Wanasema pia, “Mungu, kulingana na Biblia, si mtu mmoja tu, bali Yeye ni nafsi tatu katika Mungu mmoja. Hiyo ndiyo siri kuu ya Utatu”.

Hakika ni kweli. Watu watatu wanawezaje kuwa katika Mungu mmoja? Si kwamba tu hakuna Biblia kwa ajili ya jambo hilo, lakini hata inaonyesha ukosefu wa kutumia akili. Watu watatu mbalimbali, ingawa wao wana maumbile sawa, wanafanya miungu watatu, la sivyo lugha imepoteza maana yake kabisa.

Hebu sikiliza maneno haya tena, “Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, asema Bwana, Aliyeko, na Aliyekuwako, na Atakayekuja, Mwenyezi”. Huu ni Uungu. Huyu si nabii tu, mwanadamu. Huyu ni Mungu. Na si ufunuo wa Miungu watatu, bali wa MUNGU MMOJA, Mwenyezi.

Hawakuamini katika Miungu watatu mwanzoni mwa kanisa. Huwezi kupata imani ya namna hiyo miongoni mwa mitume. Ilikuwa ni baada ya wakati wa mitume ndipo nadharia hii ilipoingia na kweli ikawa hoja na fundisho kuu kwenye Baraza la Nikea. Fundisho la Uungu lilisababisha migawanyiko miwili hapo Nikea. Na kutokana na mgawanyiko huo kukatokea pande mbili zilizopita mpaka. Upande mmoja kweli uliingia katika imani ya miungu mingi, ukiamini katika Miungu watatu, na hao wengine wakaingia katika imani ya umoja. Bila shaka hilo lilichukua muda kutukia, bali lilitukia, na tunalo leo ii hii Lakini Ufunuo kupitia kwa Yohana kwa Roho kwa makanisa ulikuwa, “Mimi ni Bwana Yesu Kristo, nami ndimi YOTE hayo. Hakuna Mungu mwingine ye yote”. Naye akaweka muhuri Wake juu ya Ufunuo huu.

Fikiria hili: Baba wa Yesu alikuwa nani? Mathayo 1:18 inasema, “Alionekana ana mimba kwa Roho Mtakatifu”. Lakini Yesu, Mwenyewe, alidai ya kwamba Mungu alikuwa ni Baba Yake. Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu, kama tunavyotumia maneno haya mara nyingi, yanamfanya Baba na Roho kuwa MMOJA. Kweli ndivyo walivyo, la sivyo Yesu alikuwa na Baba wawili. Lakini angalia kwamba Yesu alisema ya kwamba Yeye na Baba Yake walikuwa Mmoja-sio wawili. Hilo linamfanya Mungu MMOJA.

Kwa kuwa jambo hili ni kweli kihistoria na Kimaandiko, watu wanashangaa hao watatu walitoka wapi. Likawa fundisho la msingi katika Baraza la Nikea mnamo 325 A.D. Utatu huu (neno lisilo la kimaandiko kabisa) ulitokana na miungu mingi ya Rumi. Warumi walikuwa na miungu wengi ambayo waliitolea maombi. Pia waliomba kwa mababu kama wapatanishi. Ilikuwa ni hatua tu ya kuipa miungu ya kale majina mapya, kwa hiyo tuna watakatifu ili kulifanya la Kibiblia zaidi. Kwa hivyo, badala ya Jupiter, Venice, Mars, na kadhalika, tuna Paulo, Petro, Fatima, Christopher, na kadhalika. Hawakuweza kuifanya dini yao ya kipagani kufanya kazi na Mungu mmoja tu, kwa hiyo walimgawa sehemu tatu, nao wakawafanya watakatifu kuwa wapatanishi kama walivyokuwa wamefanya na mizimu yao.

Tangu wakati huo watu wameshindwa kutambua ya kwamba kuna Mungu mmoja tu aliye na ofisi tatu au madhihirisho. Wanajua kuna Mungu mmoja kulingana na Maandiko, bali wao wanajaribu kulifanya kuwa nadharia ya mazingaombwe kwamba Mungu ni kama kichala cha zabibu; nafsi tatu zote zikishiriki Uungu ule ule sawasawa. Lakini inasema dhahiri hapa katika Ufunuo ya kwamba Yesu ni “Yeye Aliyeko”, “Yeye Aliyekuweko”, na “Yeye Atakayekuja”. Yeye ni “Alfa na Omega”, ambalo linamaanisha ya kwamba Yeye ni “A mpaka Z” au HAYO YOTE. Yeye ni kila kitu-Mwenyezi. Yeye ni Ua la Uwandani, Nyinyoro ya Bondeni, Nyota Yenye Kung'aa ya Asubuhi, Chipukizi la Haki, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni Mungu, Mwenyezi Mungu. MUNGU MMOJA.

I Timotheo 3:16 inasema, “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu: Mungu alidhihirishwa katika mwili, akajulikana kuwa na haki katika Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa katika Mataifa, akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika Utukufu”. Hivi ndivyo Biblia inavyosema. Haisemi kitu juu ya nafsi ya kwanza ama ya pili ama ya tatu hapa. Inasema Mungu alidhihirishwa katika mwili. Mungu Mmoja. Huyo MUNGU Mmoja alidhihirishwa katika mwili. Hilo linapaswa kutosheleza. Mungu alikuja katika umbo la mwanadamu. Hilo halikumfanya Yeye kuwa MUNGU MWINGINE. Yeye alikuwa MUNGU, MUNGU YEYE YULE. Ulikuwa ni ufunuo wakati huo, na ni ufunuo sasa. Mungu Mmoja.

Hebu na turudi nyuma katika Biblia na tuone kile alichokuwa hapo mwanzo kulingana na ufunuo aliotoa juu Yake Mwenyewe. Yehova mkuu alimtokea Israeli katika nguzo ya moto. Kama Malaika wa Agano Yeye aliishi katika ile nguzo ya moto na kuwaongoza Israeli kila siku. Hekaluni Yeye alitangaza kuja Kwake kwa wingu kuu. Ndipo siku moja Yeye alidhihirishwa katika mwili uliozaliwa na bikira uliokuwa umeandaliwa kwa ajili Yake. Mungu yule aliyefanya maskani Yake juu ya hema za Israeli sasa alijitwalia Mwenyewe hema ya mwili na akafanya maskani Yake kama mwanadamu kati ya wanadamu. Lakini Yeye alikuwa MUNGU YEYE YULE.

Biblia inafundisha ya kwamba MUNGU ALIKUWA NDANI YA KRISTO. MWILI huo ulikuwa ni Yesu. Katika Yeye ulikaa utimilifu wote wa Uungu, KWA JINSI YA MWILI. Hakuna kitu kinachoweza kuwa dhahiri zaidi ya hicho. Siri, ndiyo. Lakini ukweli halisi-hauwezi kuwa dhahiri. Kwa hiyo kama Yeye hakuwa watu watatu wakati huo, Yeye hawezi kuwa watatu sasa. MUNGU Mmoja: Na Mungu huyu huyu alifanyika mwili.

Yesu alisema, “Nilitoka kwa Mungu na ninaenda (kurudi) kwa Mungu”. Yohana 16:27-28. Hilo ndilo hasa lililotukia. Yeye alitoweka duniani kwa njia ya mauti Yake, kuzikwa, kufufuka, na kupaa. Ndipo Paulo akakutana Naye njiani akienda Dameski na akasema na Paulo na kusema, “Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?” Paulo alisema, “U nani Wewe, Bwana?” Yeye alisema, “Mimi ni Yesu.” Yeye alikuwa nguzo ya moto, nuru inayopofusha. Yeye alikuwa amerudi tena kuwa, sawasawa tu na vile alivyosema angekuwa. Akarudi katika namna ile ile aliyokuwa kabla hajachukua maskani ya mwili. Hivyo ndivyo hasa Yohana alivyoliona. Yohana 1:18 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mwana wa pekee, aliye katika kifua cha Baba, Yeye amemfunua”. Angalia mahali Yohana anaposema ya kwamba Yesu YUKO. Yeye yuko NDANI ya kifua cha Baba.

Luka 2:11 inasema, “Kwa maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi, ambaye ni Kristo Bwana”. Alizaliwa Kristo, na siku nane baadaye alipotahiriwa aliitwa Yesu, hata kama malaika alivyowaambia. Nilizaliwa Branham. Nilipozaliwa walinipa jina la William. Yeye alikuwa ni Kristo bali alipewa jina hapa chini miongoni mwa wanadamu. Hiyo maskani ya nje ambayo watu wangeweza kuona ilikuwa inaitwa Yesu. Yeye alikuwa Bwana wa Utukufu, Mwenyezi akidhihirishwa katika mwili. Yeye ni Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni yote hayo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ufunuo wa Yesu Kristo.

Kushusha (PDF Kiingereza)   Godhead Explained



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Maono ya Patmo.)


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Two Babylons

by Rev Alexander Hislop.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.

Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.

Kumbukumbu la Torati 6:4



 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.