Historia ya Kanisa.

<< uliopita

ijayo >>

  Mungu na Historia mfululizo.


William Branham.

Ili mpate kufahamu kabisa ujumbe wa Nyakati za Kanisa ningetaka kuelezea kanuni mbalimbali zilizoniruhusu kuyapata majina ya wale wajumbe, urefu wa nyakati, na mambo mengine yanayohusika humo.

Ufunguo niliopewa na Bwana ambao kwa huo niliweza kuamua mjumbe kwa kila wakati ni wa Kimaandiko kabisa. Kwa kweli huenda ukaitwa Jiwe la Msingi la Biblia. Ni ule ufunuo ya kwamba Mungu habadiliki hata kidogo, na ya kwamba njia Zake hazibadiliki kama jinsi tu Yeye asivyobadilika. Katika Ebr. 13:8 inasema, “Yesu Kristo yeye yule jana, na leo, na hata milele.”

Hili hapa: Mungu asiyebadilika mwenye njia zisizobadilika. Yale aliyofanya mara ya KWANZA Yeye hana budi kuendelea kuyafanya mpaka yatakapofanywa kwa mara ya MWISHO. Hakutakuwa na badiliko kamwe.

Sasa tunajua kabisa kutokana na Neno ambalo liliandikwa na Roho Mtakatifu jinsi kanisa la kwanza, la asili, lilivyoanzishwa na jinsi Mungu alivyojidhihirisha Mwenyewe ndani Yake.

Neno haliwezi kubadilika wala kubadilishwa kwa sababu Neno ni Mungu. Yohana 1:1, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”

Hivyo basi, vile kanisa lilivyokuwa wakati wa Pentekoste ndicho kipimo. Hicho ndicho kielelezo. Hakuna kielelezo kingine. Haidhuru wasomi wanasema nini, Mungu HAJABADILISHA kielelezo hicho. Yale Mungu aliyofanya kwenye Pentekoste hana budi kuendelea kuyafanya mpaka nyakati za kanisa zitakapofungwa.

Dondoo kutoka... Wakati wa Kanisa la Efeso.

  Mungu na Historia mfululizo.

Makanisa Saba ya Asia.

Efeso.

Mji wa Efeso ulikuwa mmoja wa miji mitatu mikubwa sana ya Asia. Mara nyingi uliitwa mji wa tatu wa imani ya Kikristo, Yerusalemu ukiwa wa kwanza, na Antiokia ya pili. Ulikuwa ni mji tajiri sana. Serikali ilikuwa ya Kirumi lakini lugha ilikuwa ni Kiyunani.

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Efeso.

Smirna.

Mji wa Smirna ulikuwa kaskazini kidogo ya Efeso kwenye mlango wa Ghuba ya Smirna. Kwa sababu ya bandari yake nzuri sana ilikuwa ni kituo cha biashara mashuhuri kwa mauzo yake ya nje. Pia ulisifika sana kwa shule zake za ufasaha wa kuongea, falsafa, udaktari, sayansi, na majengo mazuri.

Neno Smirna linamaanisha, “uchungu,” likitokana na neno, manemane. Manename ilitumiwa katika kuhifadhi maiti. Kwa hiyo tuna maana mbili zinazopatikana katika jina la wakati huu. Ulikuwa ni wakati wa uchungu uliojaa mauti.

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Smirna.

Pergamo.

Pergamum (jina la kale) lilikuwa Mysia, katika wilaya iliyotiwa maji na mito mitatu, ambapo mmoja wao uliwezesha kuwasiliana na bahari. Ulielezewa kama mji uliokuwa maarufu kuliko yote katika Asia. Ulikuwa mji wa utamaduni na wenye maktaba ya pili kwa ukubwa kutoka ile iliyokuwa Aleksadria. Hata hivyo ulikuwa ni mji wenye dhambi nyingi, uliopenda sana ibada za uasherati za Eskalpia, ambaye walimwabudu katika mfano wa nyoka aliye hai aliyewekwa na kulishwa hekaluni.

Kiti cha enzi cha Shetani na Makao Yake. Pergamo hapo mwanzo haukuwa mahali ambapo Shetani (kuhusu mambo ya kibinadamu) alikaa. Babeli ndio daima umekuwa makao yake makuu halisi na kwa mfano wa makao yake makuu. Ibada za Kishetani zilianzia katika jiji la Babeli.

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Pergamo.

Thiatira.

Kihistoria, mji wa Thiatira ulikuwa ndio mdogo wa yote kwa umashuhuri kati ya miji yote ile saba ya Ufunuo. Ulijengwa ndani ya mipaka ya Misia na Ionia. Ulizungukwa na mito mingi, lakini ilijaa wadudu wafyonza damu. Sifa yake moja uliosifika nayo sana ilikuwa kwamba ulijiweza kifedha kwa sababu ya vyama vya ushirika wa biashara ya wafinyanzi, watengenezaji ngozi, wafumaji, mafundi rangi, mafundi wa nguo, nk. Ni katika mji huu ambamo Lidia, yule mwenye kuuza rangi ya zambarau, alitoka. Yeye alikuwa Mzungu mwongofu wa kwanza wa Paulo.

Sasa sababu iliyomfanya Roho kuuchagua mji huu kama tayari uliokwisha kuwa na mambo ya kiroho kwa ajili ya wakati wa nne ilikuwa ni kwa sababu ya dini yake. Dini kuu ya Thiatira ilikuwa ni ibada ya kumwabudu Apolo Tirimnaio ambayo iliunganishwa na madhehebu ya kumwabudu mfalme. Apolo alikuwa mungu jua, na wa pili katika mamlaka kutoka kwa baba yake, Zeu.

Ni jambo linalostahili kuangaliwa sana ya kwamba jina lenyewe Thiatira linamaanisha, “Mtawala Mwanamke.”

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Thiatira.

Sardi.

Sardi ulikuwa mji mkuu wa Lidia ya kale. Ulitoka katika mikono ya wafalme wa Lidia ukawa wa Waajemi halafu ukatekwa na Alekzanda Mkuu. Ulitekwa na Antioka Mkuu. Ndipo Walfame wa Pergamo wakafaulu kuutawala mpaka wakati Warumi walipouteka. Katika wakati wa Tiberia ulikumbwa na matetemeko ya ardhi na tauni. Siku hizi ni lundo la magofu na haukaliwi na watu.

Dini ya mji huu ilikuwa ibada chafu ya kuabudu mungu wa kike Sibele. Magofu makubwa sana ya hekalu hilo yangali yanaweza kuonekana.

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Sardi.

Filadelfia.

Filadelfia ilikuwa maili sabini na tano kusini mashariki mwa Sardi. Ulikuwa ndio mji wa pili kwa ukubwa katika Lidia. Ulikuwa umejengwa juu ya vilima vingi katika wilaya iliyokuwa maarufu sana kwa kilimo cha divai. Sarafu zake zilikuwa na kichwa cha Bakasi na sanamu ya Bakante (kuhani mwanamke wa Bakusi).

Mji huo ulipatwa na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara, walakini muda wake wa kudumu ulikuwa ni mrefu zaidi kati ya ile miji saba ya Ufunuo. Kusema kweli mji huo ungali uko chini ya jina la Kituruki la Alasehir, ama Mji wa Mungu.

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Filadelfia.

Laodikia.

Jina hilo, Laodikia, ambalo maana yake ni, “haki za watu” lilitumiwa sana na lilipewa miji kadha kwa kuwaheshimu mabibi wa kifalme walioitwa hivyo. Mji huu ulikuwa mmoja wa miji iliyokuwa muhimu sana kisiasa na iliyostawi kibiashara sana katika Asia Ndogo. Mji huo ulipewa mali nyingi sana na wenyeji mashuhuri.

Ulikuwa ni kituo cha shule kuu ya uuguzi. Watu wake walijulikana katika sanaa na sayansi. Mara nyingi uliitwa „mji mkuu wa nchi” kwa kuwa ulikuwa makao makuu ya nchi kwa miji mingine ishirini na mitano. Mungu wa kipagani aliyeabudiwa hapo alikuwa ni Zeu. Kwa kweli mji huu wakati mmoja uliitwa Diopolisi (Mji wa Zeu) kwa heshima ya mungu wao. Katika karne ya nne mkutano muhimu wa baraza la kanisa ulifanyika hapo. Matetemeko ya mara kwa mara ya ardhi hatimaye yalisababisha uhamwe kabisa.

Kutoka... Wakati wa Kanisa la Laodikia.



 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Ufunuo 1:19-20


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Mungu Akijificha
Kwa Urahisi...
(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)