Utangulizi wa Nyakati za Kanisa.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Makanisa Saba ya Asia.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Efeso.

Ili mpate kufahamu kabisa ujumbe wa Nyakati za Kanisa ningetaka kuelezea kanuni mbalimbali zilizoniruhusu kuyapata majina ya wale wajumbe, urefu wa nyakati, na mambo mengine yanayohusika humo.

Kwa kuwa somo hili lilipaswa kuwa zito kuliko yote niliyopata kuchukua hadi wakati huu, nilimwomba Mungu kwa siku nyingi anipe upako wa Roho Mtakatifu. Na hapo tu ndipo niliposoma Maandiko juu ya Nyakati za Kanisa na kuchunguza kwa makini sana historia kadha wa kadha za kanisa zilizoandikwa na wanahistoria nilioweza kupata wasiopendelea kabisa upande wo wote. Mungu hakuacha kuyajibu maombi yangu, kwa maana wakati nilipokuwa nikisoma Neno na historia kadha wa kadha, niliwezeshwa na Roho Mtakatifu kuona utaratibu ukijifunua ambao ulidumu katika zile karne na hata kufikia moja kwa moja katika siku hii ya leo, ya mwisho.

Ufunguo niliopewa na Bwana ambao kwa huo niliweza kuamua mjumbe kwa kila wakati ni wa Kimaandiko kabisa. Kwa kweli huenda ukaitwa Jiwe la Msingi la Biblia. Ni ule ufunuo ya kwamba Mungu habadiliki hata kidogo, na ya kwamba njia Zake hazibadiliki kama jinsi tu Yeye asivyobadilika. Katika Ebr. 13:8 inasema,

“Yesu Kristo yeye yule jana, na leo, na hata milele.”

Mhubiri 3:14-15,
“Najua ya kwamba, kila kazi aifanyayo Mungu, itadumu milele: haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu: nayo Mungu ameifanya, ili watu wamche Yeye.
Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; na Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.”

Hili hapa: Mungu asiyebadilika mwenye njia zisizobadilika. Yale aliyofanya mara ya KWANZA Yeye hana budi kuendelea kuyafanya mpaka yatakapofanywa kwa mara ya MWISHO. Hakutakuwa na badiliko kamwe. Weka hilo kwenye Nyakati za Kanisa. Aina ya mtu ambaye Mungu alimchagua kwa wakati wa kwanza, na jinsi ambavyo Mungu alijidhihirisha katika huduma ya mtu huyo, itakuwa ndio mfano kwa ajili ya nyakati nyingine zote. Kile Mungu alichofanya katika wakati wa kwanza wa kanisa ndicho anachotaka kufanya katika nyakati zingine zote.

Sasa tunajua kabisa kutokana na Neno ambalo liliandikwa na Roho Mtakatifu jinsi kanisa la kwanza, la asili, lilivyoanzishwa na jinsi Mungu alivyojidhihirisha Mwenyewe ndani Yake. Neno haliwezi kubadilika wala kubadilishwa kwa sababu Neno ni Mungu. Yohana 1:1,

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”

Kubadilisha Neno lake moja, kama alivyofanya Hawa, kunaleta dhambi na mauti, kama vile pia inenwavyo katika Ufunuo 22:18-19,

“...Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki:
Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika kile Kitabu cha Uzima, na katika ule mji mtakatifu, na kutoka katika mambo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.”

Hivyo basi, vile kanisa lilivyokuwa wakati wa Pentekoste ndicho kipimo. Hicho ndicho kielelezo. Hakuna kielelezo kingine. Haidhuru wasomi wanasema nini, Mungu HAJABADILISHA kielelezo hicho. Yale Mungu aliyofanya kwenye Pentekoste hana budi kuendelea kuyafanya mpaka nyakati za kanisa zitakapofungwa.

Ingawa wasomi wanaweza kukwambia wakati wa mitume umekwisha, usiamini jambo hilo. Tamshi hilo ni kosa kwa sababu mbili. Kwanza kabisa, ni makosa kudhani hakuna mitume wengine zaidi, kwa sababu tu wale kumi na wawili wa kwanzai wamekufa. Mtume maana yake ni 'yeye aliyetumwa'; na kuna wengi waliotumwa leo, lakini wanaitwa wamishenari. Mradi tu watu wanaitwa na kutumwa wakiwa na Neno la Uzima wakati wa mitume upo unaendelea. Pili, wao wanazungumzia siku za 'nguvu za Roho Mtakatifu zilizodhihirishwa' kuwa kwamba zimekwisha kwa kuwa Biblia imekamilishwa. Hilo si kweli. Hakuna hata Andiko moja linalodokeza jambo hilo, lakini mengi yanasema vinginevyo. Hili hapa thibitisho letu ya kwamba mashtaka hayo mawili ni ya uongo.

Matendo 2:38-39,
“Basi Petro akawaambia, Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa Jina Lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

Ahadi za nguvu ambazo mitume walipewa wakati wa Pentekoste ni “kwa ajili yenu (Wayahudi), na kwa watoto wenu (Wayahudi), na kwa watu wote walio mbali (Mataifa), na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie (Wayahudi na Mataifa pia)”. Mpaka atakapoacha kuita, ujumbe wa Pentekoste na nguvu zake HAVITAKOMA.

Kile kanisa lilikuwa nacho kwenye Pentekoste ni haki yake isiyoweza kuondolewa. Mwanzoni, lilikuwa na Neno safi la Mungu. Lilikuwa na nguvu za Roho zilizodhihirishwa katika ishara na maajabu mbalimbali na karama za Roho Mtakatifu.

Waebrania 2:1-4,
“Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije wakati wo wote tukayakosa.
Kwa maana ikiwa lile Neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi (kwa Neno) ulipata ujira wa haki;
Sisi je! tutapataje kupona, tusipojali waokovu mkuu namna hii; ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia Yeye;
Mungu naye akishuhudia pamoja nao, kwa ishara na maajabu, na nguvu za namna nyingi, na vipawa vya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda Mwenyewe?”

Hilo kanisa la asili halikuundwa na wanadamu. Iliongozwa na Roho Mtakatifu. Halikuwa kubwa sana. Ilichukiwa na kudharauliwa. Lilikandamizwa. Iliteswa hata kufa. Lakini lilikuwa aminifu kwa Mungu. Lilidumu na kile kielelezo cha asili cha Neno.

Sasa msipotoshwe hapa. Niliposema ya kwamba Mungu na njia Zake hazibadiliki, sikusema ya kwamba kanisa na wajumbe wake wasingeweza kubadilika. Kanisa si Mungu. Kwa hiyo linaweza kubadilika. Lakini nililosema ni kwamba kwa sababu ya Mungu asiyebadilika na njia zisizobadilika tunaweza tukarudi nyuma huko mwanzo na kuona tendo la kwanza na lililo kamilifu la Mungu halafu tuamue kwa kipimo hicho. Hivyo ndivyo inavyofanyika. Kanisa la Kweli daima litajaribu kuwa kama la asili huko Pentekoste. Kanisa la Kweli la siku hizi litajaribu kulingana na lile la kwanza la mwanzoni. Nao wajumbe kwa makanisa, wakiwa na Roho yule yule wa Mungu ndani yao, watajaribu kulingana na mtume Paulo. Hawatakuwa kama yeye kabisa; lakini wajumbe wa kweli watakuwa ni wale wanaomkaribia kabisa Paulo, aliyekuwa hakufungwa na mtu ye yote, aliyejitolea kabisa kwa Mungu, na kuhubiri Neno la Mungu peke yake tu, na kumdhihirisha Roho Mtakatifu katika nguvu. Hakuna mwingine angeweza kufanya hivyo. Huna budi kuanzia na lile la mwanzoni. Kama vile mbegu izaavyo kwa jinsi yake, Kanisa la Kweli daima litakuwa ni lile linalojaribu kufuata nyayo za waanzilishi wake wa Pentekoste na wajumbe wake watamfuata mtume Paulo, yule mjumbe wa kwanza wa wakati wa kwanza wa kanisa. Ni rahisi jinsi hiyo, na ni zuri namna hiyo.

Nikiwa na ufunguo huu, ulio rahisi sana, hata hivyo ulio mzuri sana, niliweza, kwa msaada wa Roho Mtakatifu, kukisoma Kitabu cha Ufunuo na historia kadha wa kadha na kupata humo kila wakati, kumpata kila mjumbe, kupata muda uliodumu kila wakati, na kazi kila mmoja aliyotenda katika kusudi la Mungu tangu Pentekoste hata ukamilifu wa nyakati hizo.

Kwa sababu sasa unafahamu jinsi tunavyoamua Kanisa la Kweli lilivyokuwa (jinsi lilivyokuwa wakati wa Pentekoste na jinsi lilivyokuwa katika nyakati za mitume kama ilivyoandikwa katika Neno katika Kitabu cha Matendo) tunaweza kutumia kanuni ile ile kutuonyesha jinsi kanisa lilivyoshindwa. Kosa la msingi, ama makosa, yaliyopenyeza katika kanisa la kwanza na yakafunuliwa katika Kitabu cha Matendo na Ufunuo na pia katika zile Nyaraka yatazidi kudhihirishwa dhahiri zaidi na zaidi katika kila wakati unaofuata, mpaka tutakapofikia kuondolewa kabisa kwa ile kweli katika wakati wa mwisho, au Wakati wa Laodikia.

Sasa kutoka kwenye ufunguo huu wa kwanza ambao tumepokea kutoka kwa Bwana, kunakuja ukweli mwingine na wa ajabu kidogo. Nilisema ya kwamba Kanisa la Kweli daima litajaribu kuwa kama lilivyokuwa katika Kitabu cha Matendo. Hiyo ni kweli kabisa. Lakini tumegundua ya kwamba Neno pia linafundisha kupenyeza kwa kosa mpaka kweli imeondolewa kabisa katika siku ya mwisho wakati Bwana yuko karibu kuonekana. Swali sasa linazuka mioyoni mwetu; je! Mungu huwaacha walio Wake na kuwaacha waingie katika hali ya udanganyifu kabisa? La hasha, kwa maana Maandiko yanasema dhahiri kabisa katika Mathayo 24:24, ya kwamba 'Walio Wateule HAWAWEZI' kupotezwa.

“Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; kiasi kwamba wapate kuwapoteza KAMA YAMKINI, hata walio wateule.”

Itakuwaje basi? Jibu liko wazi mbele zetu. Kuna Kanisa la Kweli na kanisa la uongo. Kuna Mzabibu wa Kweli na mzabibu wa uongo. Lakini bila shaka kanisa hilo la uongo, kundi hilo la mzabibu wa uongo, daima litajaribu kunyakua mahali pa Kanisa la Kweli na kudai ya kwamba lenyewe, wala si walio Wateule, ndio walio halisi na wa kweli. La uongo litajaribu kuliua la Kweli. Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika Kitabu cha Matendo, hivyo ndivyo ilivyofafanuliwa katika zile nyakati saba, na hivyo ndivyo ilivyonenwa kwa udhabiti katika Nyaraka mbalimbali. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Hivyo ndivyo ilivyo sasa. Hivyo ndivyo itakavyokuwa. Haiwezi kubadilika.

----
Makanisa haya saba yaliyoko Asia Ndogo yalikuwa na tabia fulani ndani yao, katika siku hizo za kale, ambazo zilikuja kuwa tunda lililokomaa la nyakati za baadaye. Zile Mbegu zilizopandwa kule nyuma zilitokea baadaye katika mavuno yaliyokomaa, kama vile Yesu alivyosema, “Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?” Luka 23:31.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Wakati wa Kanisa la Efeso.



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
Mihuri Saba.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

   Maandiko Anasema...

Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi;

lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru.

Zekaria 14:6-7


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Mungu Akijificha Kwa
Urahisi...
(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)