Huyu Melkizedeki ni nani?
<< uliopita
ijayo >>
Mtu huyu ni nani?
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Huyu Melkizedeki ni nani?Waebrania 7:1-3,
1 Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 Ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; 3 Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.Wazia juu ya Mtu huyu mkuu, jinsi Mtu huyu alivyo mkuu! Na sasa, swali ni, “Mtu huyu ni nani?” Wanatheolojia wamekuwa na mawazo mbalimbali. Lakini tangu kufunguliwa kwa ile Mihuri Saba, kile Kitabu cha siri ambacho kimekuwa cha siri kwetu... Kulingana na Ufunuo 10:1 hadi 7, siri zote zilizoandikwa katika Kitabu hiki, ambazo zimefichwa kote katika wakati wa watengenezaji, zinapaswa kuonyeshwa na malaika wa wakati wa mwisho wa kanisa. Ni wangapi wanaojua hiyo ni kweli? Hiyo ni kweli, inayopaswa kuletwa. Siri zote za Kitabu hicho cha siri zitafunuliwa kwa mjumbe wa Laodikia wa wakati huo.
Kuona kuna ubishi mwingi juu ya Mtu huyu na somo hili, nafikiri inatupasa kuliingilia, kuona kwamba Huyu ni nani. Sasa, kuna makundi mengi ya mawazo juu Yake.
Fundisho moja ni— hudai Yeye ni hadithi tu ya kubuniwa; “hakuwa mtu halisi. Kwa kweli hakuwa mtu.”
“Na hao wengine wanasema, ya kwamba, “Ulikuwa ni ukuhani. Huo ulikuwa ukuhani wa Melkizedeki.”
Hilo ndilo linalowezekana sana, linaloshikilia vizuri upande huo kuliko wanavyoshikilia ule mwingine, ni kwa sababu wanasema ulikuwa ni ukuhani.
Haiwezi kuwa hivyo, kwa kuwa katika kifungu cha 4 inasema Yeye alikuwa ni Mtu, “Mtu.” Kwa hiyo, kusudi awe Mtu, hana budi kuwa ni utu, “Mtu.” Si utaratibu; bali ni Mtu! Kwa hiyo Yeye hakuwa tu utaratibu wa ukuhani, wala hakuwa hadithi ya uongo. Yeye alikuwa ni Mtu.Na Mtu huyo ni wa Milele. Kama ukiangalia, “Hakuwa na baba. Hakuwa na mama. Hakuwa na mwanzo wa siku Zake. Na hakuwa na mwisho wa siku Zake.” Na ye yote ambaye alikuwa yungali hai usiku wa leo, kwa sababu Biblia ilisema hapa, ya kwamba, “Hakuwa na baba, wala mama, mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake.” Kwa hiyo hainabudi kuwa ni Mtu wa Milele. Hiyo ni kweli? Mtu wa Milele! Kwa hiyo ingeweza tu kuwa Mtu mmoja, huyo ni Mungu, maana Yeye Ndiye pekee aliye wa Milele. Mungu!
Sasa, katika I Timotheo 6:15 na 16, kama mngetaka kusoma hayo wakati mwingine, ningetaka msome hayo. Sasa, jambo ninaloshindania ni, ya kwamba, Yeye alikuwa ni Mungu, kwa sababu Yeye ndiye Mtu pekee anayeweza kuwa asiyepatikana na mauti. Na sasa, Mungu akijibadilisha Mwenyewe katika Nafsi; Hivyo ndivyo alivyokuwa, “Hakuna baba, hana mama, hana mwanzo wa uhai wake, hakuna mwisho wa siku zake.”
Sasa tunaona katika Maandiko ya kwamba watu wengi wanafundisha ya kwamba, “nafsi tatu katika Uungu.” Kwa hiyo, huwezi kuwa na utu bila kuwa mtu. Inahitaji mtu kufanya utu. Mhudumu Mbaptisti, majuma machache yaliyopita, alikuja, na akaja nyumbani kwangu, na kusema, “Ningetaka kukunyoosha juu ya Uungu wakati mwingine unapopata wakati.” Alinipigia simu, samahani. Nikasema, “Nina wakati sasa hivi, maana ninataka kuwa mnyofu, nasi tunaweka kando kila kitu kingine, kufanya jambo hilo.”
Ndipo akaja, akasema, “Ndugu Branham, unafundisha ya kwamba kuna Mungu mmoja tu.”
Nikasema, “Naam, bwana.”
Akasema, “Vema,” akasema, “Ninaamini kuna Mungu mmoja, bali Mungu mmoja katika Nafsi tatu.”
Nikasema, “Mabwana, rudia hilo tena.”
Yeye alisema, “Mungu mmoja, katika Nafsi tatu.”
Nikasema, “Ulisoma wapi?” Mnaona? Naye akaniambia chuo cha Biblia. Nikasema, “Ningeweza kuamini jambo hilo. Huwezi kuwa mtu bila ya kuwa utu. Na kama wewe ni utu, wewe ni nafsi moja kwako. Wewe ni mtu tofauti, binafsi.”
Naye akasema, “Vema, wanatheolojia hata hawawezi kuelezea jambo hilo.”
Nikasema, “Ni kwa ufunuo.”
Naye akasema, “Siwezi kukubali ufunuo.”
Nikasema, “Basi hamna njia kwa Mungu kuweza kukufikia kamwe, kwa sababu yamefichwa wenye hekima na akili, na kufunuliwa watoto wachanga— kufunuliwa, ufunuo kufunuliwa watoto wachanga walio tayari kuyapokea kujifunza.” Nami nikasema, “Hapangekuwepo njia kwa Mungu kukufikia, umejifungia mbali Naye.
Biblia nzima ni ufunuo wa Mungu. Kanisa lote limejengwa juu ya ufunuo wa Mungu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Mungu, ila tu kwa ufunuo. “Ambaye Mwana atamfunulia.” Ufunuo; kila kitu ni ufunuo. Kwa hiyo, kukubali... Si kukubali ufunuo, basi wewe ni mwanatheolojia baridi tu, wala hakuna tumaini kwako.Sasa, sasa, tunaona ya kwamba Mtu huyu “hakuwa na baba, hana mama, hana mwanzo wa siku zake wala mwisho wa uhai wake.” Ilikuwa ni Mungu, en morphe. Basi, ulimwengu— lile neno limetoka— kwa neno la Kiyunani maana yake “kubadilika,” lilitumika. Akijibadilisha, en morphe, kutoka Mtu mmoja hadi... Mtu mmoja; neno la Kiyunani hapo, en morphe, linamaanisha... Ilichukuliwa kutoka kwenye michezo ya kuigiza, ya kwamba mtu mmoja anabadilisha kinyago chake, kumfanya mtu mwingine.
Kama vile katika— shuleni, hivi majuzi tu, ninaamini, Rebeka, kabla tu hajamaliza, walikuwa na mchezo mmoja wa kuigiza wa Shakespeare. Na kijana mmoja ilimbidi abadilishe nguo zake mara kadhaa, kwa sababu alicheza sehemu mbili ama tatu mbalimbali; lakini, mtu yule yule. Akajitokeza, mara mmoja, yeye alikuwa jeuri; na wakati alipotoka mara nyingine, alikuwa ni mtu mwingine. Na sasa neno la Kiyunani, en morphe, linamaanisha kwamba yeye “alibadilisha kinyago chake.”
Na hivyo ndivyo Mungu alivyofanya. Ni Mungu yeye yule wakati wote. Mungu katika umbo la Baba, yule-yule Roho, Nguzo ya Moto. Mungu yeye yule alifanyika mwili na akakaa kwetu, en morphe, akatolewa apate kuonekana. Na sasa Mungu yeye yule ni Roho Mtakatifu. Baba, Mwana, Mtakatifu... si Miungu watatu; ofisi tatu, matendo matatu ya Mungu mmoja.
Biblia ilisema, “Kuna Mungu mmoja,” si watatu. Lakini hivyo ndivyo ambavyo wasingeweza... Huwezi kulinyoosha hili na kuwa na Miungu watatu. Usingeweza kumuuzia Myahudi hilo. Nitawaambia jambo hilo. Mtu anayejua vizuri zaidi, anajua kuna Mungu mmoja tu.Angalia, kama sanamu, yeye hujificha, akiwa na kinyago juu yake. Hivyo ndivyo Mungu alivyofanya kwa wakati huu. Imefichwa. Mambo haya yote yamefichwa, na yanapaswa kufunuliwa katika wakati huu. Sasa, Biblia inasema watafunuliwa katika nyakati za baadaye. Ni kama huyo fundi akifu— akifunika kazi yake hata wakati atakapoondoa kile kinyago kwake na ikaonekana wazi. Na hivyo ndivyo Biblia imekuwa. Imekuwa ni kazi ya Mungu iliyofunikwa. Nalo limefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, na siri Yake mara saba. Na Mungu aliahidi katika siku hii, katika wakati wa kanisa hili la Laodikia, Yeye angeondoa kifuniko hicho kote na tungeweza kuliona. Ni jambo la utukufu iliyoje!
Mungu, en morphe, amefunikwa katika Nguzo ya Moto. Mungu, en morphe, katika Mtu anayeitwa Yesu. Mungu, en morphe, katika Kanisa Lake. Mungu juu yetu, Mungu pamoja nasi, Mungu ndani yetu; kujidhili kwa Mungu.
Kule Juu, mtakatifu, hakuna mtu angaliweza kumgusa, Yeye alikaa mlimani; na hata kama mnyama aliugusa mlima, ilimbidi afe.
Na ndipo Mungu akashuka na kubadilisha hema Yake, kisha akashuka akaishi pamoja nasi, akawa mmoja wetu. “Nasi tukamshikilia,” Biblia ilisema. I Timotheo 3:16, “Bila shaka siri ya utauwa ni kuu; kwa maana Mungu alidhihirishwa katika mwili, akashikwa kwa mikono.” Mungu alikula nyama. Mungu alikunywa maji. Mungu alilala. Mungu alilia. Alikuwa mmoja wetu. Mzuri, amefananishwa katika Biblia!
Huyo alikuwa ni Mungu juu yetu; Mungu pamoja nasi; sasa ni Mungu ndani yetu, Roho Mtakatifu. Si Nafsi ya tatu; Mtu yule yule!Mungu alishuka na kufanyika mwili, na alikufa mauti, katika Kristo; kusudi apate kulisafisha Kanisa, apate kuingia ndani yake, kwa ajili ya ushirika. Mungu anapenda ushirika. Hicho ndicho alichomfanyia yule mtu mara ya kwanza, ilikuwa ni kwa ajili ya ushirika; Mungu huishi peke yake, pamoja na Makerubi. Na angalia sasa, Yeye alimfanya mwanadamu, naye mwanadamu alianguka. Kwa hiyo Yeye alishuka na kumkomboa mwanadamu, kwa sababu Mungu anapenda kuabudiwa. Neno lenyewe mungu linamaanisha “kitu cha kuabudiwa.” Na hii ambayo huja kwetu kama Nguzo ya Moto, ambayo wakati mwingine hugeuza mioyo yetu, huyo ni Mungu yule yule aliyesema, “Iwe nuru,” na ikawa nuru. Ni yeye yule jana, leo, na hata milele.
Sasa, hapo mwanzo Mungu aliishi peke yake, pamoja na sifa Zake, kama nilivyonena habari zake asubuhi ya leo. Hayo ni mawazo Yake. Hakukuwa na kitu, ni Mungu peke yake, bali Yeye alikuwa na mawazo. Kama tu vile mbunifu mashuhuri anavyoweza kuketi, mawazoni mwake, na kuchora kile anachofikiria ndicho atakachojenga. Kuumba, sasa, yeye hawezi kuumba. Anaweza kuchukua kitu ambacho kimeumbwa na kukifanya katika umbo tofauti; Maana Mungu ndiye njia pekee... Mmoja tu anaweza kuumba. Bali anawaza niani Mwake atakayotenda, na hayo ni mawazo Yake, hayo ni matakwa Yake. Sasa ni wazo, halafu analinena, na ni neno basi. Na ninii— neno ni... Wazo, linapotamkwa, ni neno. Wazo linapotamkwa ni neno, bali haina budi kuwa wazo kwanza. Kwa hiyo, ni sifa za Mungu; ndipo linakuwa wazo, halafu neno.
Angalia. Wale walio na uzima wa milele usiku wa leo, walikuwa pamoja Naye na ndani Yake, katika mawazo Yake, kabla hapajakuwepo malaika, nyota, kerubi, ama cho chote kile. Huo ni Umilele. Na kama una Uzima wa Milele, daima ulikuwa nao. Si kuweko kwako hapa, bali umbo na mfano ambao Mungu asiye kikomo...
Na kama Yeye si asiye na kikomo, Yeye si Mungu. Mungu hana budi kuwa asiye kikomo. Sisi tuna kikomo; Yeye hana kikomo. Naye alikuwa kila mahali, anajua yote, na ana nguvu zote. Kama sivyo, basi hawezi kuwa Mungu. Anajua mambo yote, mahali pote, kwa sababu ya kuenea Kwake kila mahali. Kujua yote kunamfanya Yeye awe kila mahali. Yeye ni Kiumbe; Yeye si kama upepo. Yeye ni Kiumbe; Yeye huishi katika nyumba. Lakini kwa kuwa anajua yote, akijua mambo yote, inamfanya Yeye awe kila mahali, kwa sababu Yeye anajua kila kitu kinachoendelea.
Hakuwezi kuwa na kiroboto kinachopepesa macho yake ila kile Yeye alichojua. Na alijua kabla ulimwengu haujakuwepo, ni mara ngapi kingefunga macho yake na kina shahamu kiasi gani ndani yake, kabla hapajakuwepo ulimwengu. Hilo halina kikomo. Hatuwezi kulielewa moyoni mwetu, bali huyo ni Mungu. Mungu, asiye na kikomo!
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Huyu Melkizedeki ni nani?
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Mathayo 1:21-23