Yehova-Yire #1.
<< uliopita
ijayo >>
Uzao wa Abrahamu.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Yehova-Yire #1.Mwanzo 22:14,
Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.Hebu turejee nyuma sasa kwenye Mwanzo 12. Mungu alimwita Abrahamu kwa njia ya neema. Siyo kwa sababu yeye alikuwa mtu tofauti; yeye alikuwa Abrahamu tu, mtu wa kawaida tu. Siyo kwa sababu yeye alikuwa kuhani au mtu mashuhuri; yeye alikuwa mkulima tu. Yeye alikuja chini kutokea mji wa Mnara wa Babeli, pamoja na baba yake, na walikuwa wamekwenda Ukaldayo, Uri ya Ukaldayo. Na, kule, alikuwa mkulima, labda alilima wakati wa mchana na kukuza chakula chake. Yeye alikuwa amemuoa binamu yake, Sara. Nao hawakuwa na watoto, na Abrahamu alikuwa na umri wa miaka sabini na tano Mungu alipomwita yeye, na Sara alikuwa na umri wa miaka sitini na tano.
Na Mungu alimwambia Abrahamu wakati Yeye alipomwita, Yeye alisema, “Nakwenda kukufanya wewe baba wa mataifa,” na kwenda kumpa yeye mtoto kwa njia ya Sara. Sasa, Abrahamu alikuwa ni mgumba. Na Sara alikuwa, vema, miaka sitini na tano, Sara alikuwa amekwishakupita kwa miaka kumi au kumi na tano umri wa kuweza kuzaa. Abrahamu alikuwa ameishi na Sara tangu akiwa na kama umri wa wa miaka kumi na sita au kumi na saba, binamu yake. Na, wao, yeye alikuwa amekuwa mume kwake miaka yote hii hadi yeye alipokuwa na umri wa miaka sabini na tano, na Sara alikuwa na umri wa miaka sitini na tano, na ndipo Mungu akaja chini na kusema, “Ninakwenda kukupa wewe mtoto, kwa njia ya Sara.” Na yeye hakuyumba kwenye hiyo ahadi ya Mungu, bali aliiamini hiyo!
Ungeweza kuwazia mwanamume mzee, mwenye umri wa miaka sabini na tano, na mwanamke, miaka sitini na tano, wakienda chini, wakitetemeka, chini kwenda kwa daktari, na kusema, “Daktari, nataka wewe uandae hospitali sasa. Sisi tunaweza kukuita usiku wowote, kwa sababu, unajua, tunakwenda kuwa na mtoto.”? Daktari angelisema, “Naam, ndiyo, bwana, ninyi ni... Lo, lo, lo!” Mara tu walipokuwa wakipiga simu, waseme, “Ni bora tumfuatilie, huyu ana tatizo fulani.” Na kila mtu anayemchukulia Mungu alivyo kwenye ahadi Yake anachukuliwa, na ulimwengu kuwa, “mwendawazimu.” Paulo alisema, “Katika njia inayoitwa ‘uzushi,’ hiyo ndiyo njia ninayomwabudu Mungu wa baba zetu.” Uzushi wa kidini ni “wendawazimu,” tunajua. Ni upuuzi kwa akili za kimwili. Imani ni wendawazimu kwa kila mtu isipokuwa Mungu na yule mwenye hiyo imani. Hilo ni sahihi.
Lakini Mungu alimwahidi Abrahamu, na Abrahamu aliamini hilo. Kamwe yeye hakusema, “Mungu, hilo litakuwaje?” Yeye alisema, “Sawa, Mungu, mimi naamini hilo.” Na naweza kumwona yeye akienda nyumbani, akisema, “Sara, hebu twende chini na tuwe na yadi kadhaa za nepi, na tuwe na pini kadha, na tuwe na viatu fulani. Tunakwenda kuwa na mtoto.” Loo, jamani!
----
Uzao wa Abrahamu leo, mbona, ule tunaoita Uzao wa Abrahamu, ni dhaifu kuliko mchuzi uliotengenezwa kutokana na kivuli cha kuku aliyedhoofika kwa njaa. Ndiyo, bwana.
Mungu anataka Wakristo walio imara wanaolichukua Neno la Mungu, waishi au wafe. Ni kitu kile kile. Amina. “Mungu alisema hivyo!” Huo ni Uzao wa Abrahamu, uliozaliwa kwa Roho na Neno la Mungu. Hilo ndilo linalosimama.“Mbingu na nchi zitapita, lakini Neno Langu halitapita kamwe.” Hilo ndilo jambo lenyewe. Kile Mungu alichoahidi, Mungu anaweza kufanya. Mungu hashindwi. Yeye hawezi kushindwa. Kuna kitu kimoja pekee ambacho Mungu hawezi kufanya, na hicho ni kushindwa. Yeye hawezi kushindwa, hicho ndicho kitu pekee Yeye hawezi kufanya. Lakini Yeye hawezi kushindwa. Mungu alipoahidi hilo, hiyo ni ile Kweli, Hilo linabaki pale daima. Hilo linakuwa limekwisha daima. Mungu anaponena Neno, hilo tayari limekamilika daima.
-----
Najisikia wa kidini ninapowazia juu ya Abrahamu, nikijua kuwa tunaweza kuwa Uzao wake, ule Uzao wa Abrahamu pamoja na hizi ahadi zote. Siyo tu kuifanya hiyo kuwa hakika, Mungu aliinua mkono Wake juu, akaapa kwa Yeye Mwenyewe, kuwa angelifanya hiyo. Kiapo ni, siku zote, agano linathibitishwa na kiapo, na Mungu aliapa kwa Nafsi Yake Mwenyewe kwa sababu hakuna wa juu zaidi wa kuapa kwa yeye. Yeye aliapa kwa Nafsi Yake Mwenyewe, kuwa angelifanya hilo.Sasa kile ulimwengu, jinsi, nini-tatizo letu ni nini? Ahadi kama hiyo! Imani iliyojengwa kwenye kitu fulani kama hicho, imani iliyojengwa! Neno lililoahidi haya mambo katika siku za mwisho, na hapa tunayaona yakitukia moja kwa moja mbele zetu, na bado tunajitweza. Uzao wa Abrahamu? Loo, jamani! Nataka ninyi mshikilie kwenye hilo, “Uzao wa Abrahamu.”
Mwanzo 12, kile Mungu alichohitaji kwa Abrahamu kilikuwa utenganisho kamili. Sasa, leo, wao wanataka wachanganyaji. “Ee, tunapomchagua mchungaji, inampasa yeye awe na nywele zilizosokotwa, na awe ametoka moja kwa moja Hollywood, unajua, na aweze kusema, ‘ah-mina’ kwa uzuri zaidi, na anayevaa nguo zilizo bora zaidi ya zote, na anayeendesha Cadillac lililo kuu, na-na kadhalika namna hiyo, na yeye awe mchanganyaji mzuri. Yeye hufanya hili. Na awe anakunywa pombe mara chache pamoja nasi, ili awe mtu mwenye kuweza kuchanganyika na watu wengine. Yeye ahudhurie kwenye karamu ya kadi ya akina bibiye wazee, na wao hushona na kufuma, na kufuma na kushona, na kuzungumza juu Binti Fulani na Fulani, na kadhalika, unajua, na yote namna hiyo. Na inapasa wao wawe namna ile ya wachanganyaji.”
Mungu alisema, “Nitengee Paulo na Barnaba!” Amina. Utenganisho! “Tokeni miongoni mwao na msishiriki vitu vyao vilivyo vichafu!” Mungu anataka utenganisho, kuangamiza dhambi kabisa. Jitenge! Hilo ndilo tatizo leo, sababu hatuwezi kuwa Uzao wa Abrahamu, hatuwezi kujitenga wenyewe na amri za sharti za kanisa na kanuni za imani za dini, na kadhalika, unaoitwa Ukristo, kwa Neno lililo hai. Jitenge mwenyewe na kutokuamini kwako, na uamini Neno la Mungu. Mungu atalifanya Hilo lidhihirike kwako. Sawa. Mwanzo 12, Mungu alisema, “Jitenge mwenyewe na jamaa yako na kila kitu kilichokuzunguka.”
----
Baada ya Abrahamu kujitenga mwenyewe na Lutu, kile tu hasa Mungu alichomwambia afanye. “Tenga kila dhambi inayotulemea sisi, toa nje kila kitu!” Pale, ndipo Mungu aliposema, “Abrahamu, sasa wewe ni mrithi wa vitu vyote. Tazama mashariki, tazama magharibi, tazama kaskazini, tazama kusini, tembea kote kwenye nchi, yote ni ya kwako!” Amina.Unatenga jambo lako, mwenyewe mbali na dhambi, kutokuamini. Kuna dhambi moja pekee, na hiyo ni kutokuamini. Kufanya uzinzi siyo dhambi, kunywa pombe siyo dhambi, kusema uongo siyo dhambi; hizo ni ishara zinazoashiria kutokuamini. Kama wewe uliamini, usingelifanya hayo mambo.Hakika. Yesu alisema katika Mtakatifu Yohana 5:24, “Yeye ayasikiaye Maneno Yangu na kumwamini Yeye aliyenituma Mimi, anao Uzima wa Milele na Milele,” ule Zoe, Roho Mtakatifu, kwa sababu yeye aliamini. Kwa usahihi. Sasa, hadi wewe umpokee Huyo, wewe ni mwamini wa kujifanya, huyo aliye katika hilo kundi. Lakini wao wanapoamini kwa uhalisi, wakijitenga wenyewe, basi wewe unapojitenga mwenyewe mbali na kutokuamini kwako kote, na ukamwamini Mungu, unaenenda kwa udhabiti, ukichukua zile Amri, ukifanya kila kitu kilicho sahihi, basi Mungu atasema, “Kila ahadi katika kile Kitabu ni yako.” Amina. “Zote ni zako! Fungua kwenye Hiyo, kutoka Mwanzo hadi Ufunuo, yote ni yako!” Amina. “Kama mkikaa ndani Yangu na Neno Langu ndani yenu, mnaweza kuomba kile mtakacho, kitafanyika.” Nini? Inakupasa ujitenge mwenyewe, kwanza, mbali na kutokuamini kwako.
Unasema, “Ndugu Branham, wewe unaliweka karibu mno.” Yesu alisema, “Katika siku za Nuhu kulikuweko na wanane waliookoka. Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika kuja kwa Mwana adamu.”
“Hao ni wangapi, Ndugu Branham?” Huenda ikawa elfu nane, labda milioni nane, mimi sijui itakuwa wangapi. Lakini itakuwa katika uchache. Mmoja kutoka kwenye kila elfu mia moja, au kitu fulani kama hicho, ningesema. Vema.----
Abrahamu alijua kuwa kila kitu kilikuwa chake, hivyo basi Lutu alipokuja ndani, yeye alisema, “Sasa subiri kidogo.” Lutu alichukuliwa na mikono mikatili ya adui. Abrahamu alisema, “Huyo ni ndugu yangu, na nitakwenda kumtafuta.” Sasa kumbuka, kulikuweko na takriban wafalme saba au wanane waliokwenda pamoja, na kuja chini na kuchukua kila kitu na kuondoka nacho. Nao walipotoka, Abrahamu aliwachukua watumishi wake na kwenda kumtafuta, ili kumrejesha ndugu yake aliyepotea. Huyo ni Mkristo halisi, alikwenda kumtafuta ndugu yake aliyepotea! Je, Abrahamu alifanya nini wakati alipompata? Yeye aliwaua hao wafalme; na kurudi, akimleta ndugu yake, baada ya mapambano.Tazama, kulikuweko na Mfalme mmoja aliyekuja kumlaki na Abrahamu, akiwa anarudi, Melkizedeki. Melkizedeki, Yeye alikuwa nani? Yeye hakuwa na baba, Yeye hakuwa na mama. Kamwe Yeye hakuzaliwa, kamwe Yeye hafi. Hana baba, hana mama, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa uhai. (Haikuwa Mwana wa Mungu; kwa sababu Yeye alikuwa na Baba na mama, wote wawili walizaliwa na kufa, na kufufuka tena.) Lakini huyu Mtu kamwe hakuwa na baba au mama, Yeye ni Mungu! Hakika, Hicho ndicho Kitu pekee kilicho cha Milele na Milele.
Na Yeye alikutana na Abrahamu baada ya vita kwisha, akionyesha hilo kwa Uzao wa Abrahamu; baada ya sisi kumwendea ndugu yetu aliyeanguka, na vita kwisha. Melkizedeki aliandaa chakula gani? Divai na mkate, ushirika. Amina. Vita vinapomalizika, ndugu! Aliporudi, akimleta ndugu yake aliyepotea arudi nyumbani tena, akimrejesha tena. Na vita vilipomalizika, Melkizedeki alimlaki na kumpa ushirika wa meza ya Bwana. Yesu alisema, “Mimi sitakula au kunywa tunda la mzabibu tena hadi nitakapokula mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba Yangu.” Ndiyo, bwana. Sasa vita vilikuwa vimemalizika, Abrahamu alikuwa amerejea, ile sura ya 14; na yule Mshindi alikutana naye, yeye alipokuwa akiingia ndani pamoja na yule Mshindi.
----
Subirini kwa kitambo kidogo, ndugu, juu ya Pentekoste. Wao walikuwa orofani... Kama wewe ungewahi kuwa pale na kuona mchoro halisi, jinsi ulivyochorwa, wao walikwenda kupita ngazi upande wa nje na kwenda juu orofani. Wao walikuwa na mishumaa midogo ya mafuta ya mzeituni ikiwaka. Wao walikuwa juu pale kwa siku kumi mchana na usiku, milango yote ikiwa imefungwa. “Kukaja ghafla kutoka Mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wenye nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Ndimi kama moto, ndimi zilizogawanyika za moto, ulikaa juu ya kila mmoja wao. Wote walijazwa Roho Mtakatifu, wakatoka wakaenda uani, wakinena kwa lugha nyingine.”Angalia, huu Moto uliogawanyika ulikuwa nini? Ulikuwa Nguzo ya Moto, Roho Mtakatifu, Mungu, yule Malaika aliyewaongoza wao kupita jangwani, Yule ambaye alidhihirishwa mbele zao. Mungu alikuwa amejikata vipande Mwenyewe na kujigawanya Mwenyewe miongoni mwa watu, Roho Mtakatifu, na kwa pamoja sisi tunakuwa Kanisa la Mungu aliye hai. Agano! “Abrahamu na Uzao wake baada ya yeye, ule Uzao wa kifalme.” Ule ule Uzima uliokuwa ndani ya Kristo, ndani ya Kanisa, ukitenda matendo yale yale ambayo Kristo aliyatenda. Amina. Ni kitu kizuri iliyoje, marafiki!
----
Baba Mungu, zungumza na mioyo hapa jioni hii. Wewe unajua kusudio la hili. Wewe unajua, Baba, inapa-inapasa ifikie wakati kwamba jambo fulani inabidi lifanyike. Sisi-sisi tunaona hiyo hali, na jinsi kadiri inavyokuwa mbaya zaidi wakati wote. Nasi tunatambua kuwa kipindi cha kanisa la Pentekoste, katika siku za mwisho, ni Kipindi cha Kanisa la Laodikia, kilicho pekee ambacho Kristo alitolewa nje ya kanisa, akisimama, akibisha hodi akijaribu kurejea ndani. Ee Mungu, turehemu.----
Na, Ewe Mungu, ni-ni wakati wa ukichaa. Ni wakati wa kuchanganyikiwa akili. Ni-ni wakati ambapo mwanadamu hatasimama na kusikiliza, na kuchunguza. Na chini ya misisimko, na kadhalika, wao bado hudai kuwa wewe ni Uzao wa Abrahamu. Mungu, jinsi Wewe ulivyosema hilo lingekuwa, maroho yatakuwa karibu mno katika siku za mwisho, pamoja na uigizaji, hadi karibia hilo lingewadanganya wateule, kama ingaliwezekana. Na hilo liko hapa. Mungu, usiruhusu hawa watu, usiruhusu mmoja afanye hilo. Tafadhali, Baba. Naomba kwa ajili yao, kila mmoja. Katika Jina la Bwana Yesu, tujalie hilo.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Yehova-Yire #1.