Mungu aliye mwingi wa rehema.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mungu aliye mwingi wa rehema.

Sasa kama wengi wenu mnataka kuandika Maandiko ambayo mhudumu anasoma. Nami ningetaka ninyi, usiku wa leo, kama mkipenda, mfungue Waefeso. Nami nilikuwa nikizungumza Jumapili iliyopita juu ya Waefeso, jinsi ambavyo Kitabu cha Yoshua kilikuwa Waefeso wa Agano la Kale, na jinsi kilivyokuwa Kitabu cha ukombozi. Na ukombozi una sehemu mbili tofauti, “Kutoka nje ya” na “Kuingia ndani ya.” Kwanza, huna budi kutoka. Watu wengine wanataka kuingia pamoja na ulimwengu; bali huna budi kutoka ulimwenguni, kuingia katika Kristo. Huna budi kutoka katika kutokuamini, kuingia katika imani. Hakuwezi kuwa na kitu kimoja njiani mwako. Ili kweli uwe na imani halisi, huna budi kuacha kila kitu kilicho kinyume na Neno la Mungu, nyuma, kuingia katika imani. Na hicho kilikuwa ni Kitabu cha Waefeso wa Agano la Kale, Yoshua. Ambapo, Musa aliwakilisha torati, asingeweza kumwokoa mtu ye yote; bali neema ingeweza, na hapa Yoshua ni neno lile lile kama Yesu, “Yehova-mwokozi.”

Na sasa basi, tunaona ya kwamba tumekuja kwa Waefeso nyingine, Efeso nyingine sasa. Ambapo basi katika madhehebu yetu ya kiakili na mengineyo, na mipango yetu yote ya elimu, imekuja kwenye Yordani yake, ndipo inatupasa kuwa na Waefeso tena. Hatuna budi kuwa na kutoka, “kutoka” na “kuingia,” kwa ajili ya Kunyakuliwa.

Sasa tutasoma usiku wa leo kutoka sura ya 2 ya Waefeso. Nilikuwa nikisema hayo tu ili mfungue ma -mahali hapo, ama mfungue hiyo sura.

Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; Ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
[Waefeso 2:1-5]
Ninataka kuchukua kutoka hapo machache, ama sehemu ya kifungu hiki, “bali Mungu,” Mungu aliye mwingi wa rehema.

Nataka ninyi mwone hapa ambavyo nabii, mtume, namaanisha Paulo, ambaye- ambaye, alivyotaja hili, ambavyo, “Ninyi amewahuisha mliokuwa wafu. Ninyi amewahuisha ambao hapo kwanza mlikuwa wafu, wafu katika dhambi na makosa; mkifuata mambo ya ulimwengu, mapenzi ya mwili, na mkitimiza mapenzi ya nia. Ana...”

Ni kitu gani kilichosababisha badiliko hili, mnaona? Ni nini kilichosababisha hayo, “kutoka wakati mlipokuwa wafu”, hata kuhuishwa? Kuhuisha maana yake ni “kufanywa hai.” Kulikuwako na badiliko, kutoka mautini kuingia Uzimani. Hakuna mwingine, hakuna jambo lingine ambalo lingeweza kumpata mtu ye yote, mkuu sana, hata kumbadilisha kutoka mautini kuingia Uzimani. Mtu, kama alikuwa akifa, kimwili, na angeweza kuponywa kimwili, hilo lingekuwa ni jambo kuu, bali hakuna kitu kikubwa sana kama wakati amekufa kiroho na Mungu amemhuisha kwa Uzima.

“Ninyi zamani, katika nyakati zilizopita, mmekufa.” Ulikuwa umekufa. Hata wengi hapa usiku huu, wakati mmoja mnaweza kutazama nyuma na kuona kuwa mlikuwa wafu. Bali sasa mbona ninyi si wafu usiku huu, kama mlivyokuwa wakati huo? Unastahili kuwa hivyo, kwa sababu ulikuwa mwenye dhambi, “bali Mungu aliye mwingi wa rehema.” Hilo ndilo-hilo ndilo jambo lenyewe, “Mungu Ambaye alikuwa tajiri.” Mambo haya yote tuliyokuwa, “bali Mungu”! Hilo lilifanya badiliko papo hapo, “Mungu aliye mwingi wa rehema”!

Loo, nina furaha sana kwa ajili ya jambo hilo, ya kwamba Yeye ni mwingi wa rehema. Kama angalikuwa tu tajiri wa pesa, kama alikuwa tu tajiri wa vifaa, na hivyo ndivyo alivyo, lakini hata hivyo jambo kuu sana ni kuwa mwingi wa rehema. Loo, hilo ni neno kuu jinsi gani, jinsi ambavyo wakati mmoja tulikuwa tumekufa.

Nasi tulikuwa tukizungumza usiku wa juzijuzi juu ya jinsi ambavyo mbegu haina budi kufa. Na kila kitu karibu na chembechembe hiyo ya uhai haipaswi kufa tu, bali kuoza. Kama haiozi, haiwezi kuishi. Na kuoza ni, “kuharibiwa kabisa; imekwisha.” Na hata tutakapofikia mahali ambapo maoni yetu na mawazo yetu yamekwisha kabisa na kuoza kabisa kutoka ndani yetu, ndipo chembechembe ya uhai itaweza kuanza kuishi.

Sasa huenda tukaweza, huenda nikaingiza mafundisho machache tu hapa, ili nisije... Kama huamini, vema. Hilo ni sawa tu. Ninaamini jambo hilo. Naamini ya kwamba-kwamba binadamu anapozaliwa katika ulimwengu huu, anapokuwa mtoto mchanga, aliyezaliwa ulimwenguni, hungeweza kuwa hapa bila ya Mungu kujua tangu milele, kwa sababu Yeye hana mwisho, Yeye anajua mambo yote. Na wakati mtoto huyo mchanga anapozaliwa ulimwenguni, kuna kitu fulani katika mtoto huyo. Kama atapata Uzima, kuna kitu fulani kidogo mle ndani, ndani ya mtoto huyo basi, ambacho yeye atakifikia, mapema ama baadaye. Mbegu hiyo ndogo iko ndani yake. Sasa kama utachukua... Maandiko yanatangaza jambo hilo dhahiri.

Sasa kama una Uzima wa Milele usiku wa leo, kama tuna Uzima wa Milele, basi daima tulikuwako, kwa sababu kuna aina moja tu ya Uzima wa Milele. Daima tulikuwa hivyo. Na sababu ya sisi kuwa, kwa sababu sisi ni sehemu ya Mungu. Na Mungu ndiye kitu pekee kilicho cha Milele.
Na kama Melkizedeki alivyopokea sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu, na ilitolewa kwa mjukuu wake, Lawi, ambaye alikuwa bado katika viuno vya Ibrahimu; alitoa fungu la kumi, kwa maana alikuwa bado katika viuno vya Ibrahimu wakati alipokutana na Melkizedeki. Ninataka kuzungumza juu ya jambo hilo kule mahali pengine, asubuhi moja. Huyu Melkizedeki Ni Nani? Sasa angalia jambo hilo. Huko nyuma kabisa, Mungu alimjua mvulana huyu akishuka. Yeye alijua mambo yote.
Sasa sisi ni sehemu ya Mungu. Ulikuwa hivyo daima. Hukumbuki jambo hilo, kwa sababu ulikuwa tu sifa katika Mungu. Ulikuwa tu katika mawazo Yake. Jina lako lenyewe, kama liliwahi kuwa kwenye Kitabu cha Uzima, liliwekwa pale kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Yeye alijua ulivyokuwa.

Ninasema tu hili, si kuchanganya mafundisho, bali kulinyosha, ili kwamba tuondoke kwenye woga huu na hofu. Hujui wewe ni nani. Hamtakuwa, bali sasa ninyi ni wana wa Mungu. Mnaona, sikuzote mlikuwa wana wa Mungu. Mnaona?
Kwa maana wakati Mungu alipokuweka katika mawazo Yake hapo mwanzo, huna budi kuwa, sehemu fulani yako, Uhai wako ulio ndani yako sasa, ulipaswa kuwa pamoja na Mungu kabla ya hapo. Vema, wakati Yeye, kabla Yeye hata hajafanyika wa kimwili hapa duniani, kabla hakujakuwako na cho chote, bali Mungu, ulikuwa mmoja wa sifa Zake. Yeye alijua jina lako lingekuwa nani. Yeye alijua rangi ya nywele ambayo ungekuwa nayo. Yeye alijua yote kukuhusu. Jambo pekee lililotukia ni wakati wewe, ukiwa mwenye dhambi...

Wengi wenu mnaweza kushiriki pamoja nami juu ya wazo hili. Wakati ulipokuwa mvulana mdogo, ama msichana mdogo, ungetembea huku na huko na kungekuwa na mambo fulani ambayo yangekuwa tu, ambapo hayangewasumbua watoto wengine, ilionekana kana kwamba kulikuwa na kitu fulani ndani yako kilicholia. Kulikuwa na Mungu mahali fulani, hata hivyo ulikuwa mwenye dhambi. Mnakumbuka jambo hilo? Hakika. Sasa hiyo ilikuwa ni nini? Huo ulikuwa ndio huo Uhai mdogo ndani yako wakati huo.

Na halafu baada ya kitambo kidogo, mkaisikia Injili. Labda ulienda kanisani, ukachagua hiki na kile, kisha ukaondoka kutoka kwenye dhehebu moja hadi jingine. Lakini siku moja, wewe ukiwa sehemu ya Mungu, ilibidi uwe sehemu ya Neno. Na wakati uliposikia Neno, unajua mahali ulikotoka, ulijua Kweli ilikuwa ni nini. Ulikuwa daima, mbegu ilikuwa ndani yako daima. Neno liliona Neno lililokuwa ndani yako, lililokuwako kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, liliona Neno nawe ukaja Kwake.

Kama vile hadithi yangu ndogo ya tai, ya jinsi yule tai mdogo alivyoanguliwa chini ya kuku. Ndipo maskini jamaa huyo akatembea pamoja na hao kuku, yeye, yule kuku akalia, naye hakuelewa mlio wake. Na hao kuku wadogo, chakula chao walichokuwa nacho kwenye kitalu, yeye hakufahamu jambo hilo, jinsi walivyofanya jambo hilo. Lakini kulikuwa na kitu fulani ndani yake, kilionekana kuwa tofauti na vile kuku huyo alivyokuwa, kwa sababu hapo mwanzo alikuwa tai. Hiyo ni kweli. Siku moja mama yake alikuja akimwinda, na, wakati aliposikia mlio huo wa tai, ulikuwa tofauti na mlio wa kuku.

Na hivyo ndivyo ilivyo kwa kila mwamini aliyezaliwa mara ya pili. Unaweza kusikia theolojia yote unayotaka, na hitilafu yote ya kujibunia; bali wakati Neno hilo linapomulika huko nje, basi kuna kitu fulani kinachoshilia, unakuja Kwake. “Ninyi mliokuwa mmekufa katika dhambi (huo uhai) amewahuisha.” Lazima kuwe na Uhai pale wa kuhuisha, kwanza. Mungu, kwa kujua Kwake tangu asili, alijua mambo yote. Nasi tulichaguliwa tangu zamani kuwa wana na binti za Mungu. “Ninyi mlipokuwa mmekufa katika dhambi na makosa, ambayo katika sisi sote tulikuwa tumepita nyakati zetu, bali Yeye ametuhuisha.”

Mwangalie Paulo, wakati Paulo alipokuwa mwanatheolojia mashuhuri. Lakini alipokuja uso kwa uso na Neno hilo, Yesu, lilihuisha. Akawa hai upesi sana, kwa sababu yeye aliamriwa kuwa hivyo. Ninii ... Yeye alikuwa sehemu ya Neno; na wakati Neno lilipoliona Neno, ilikuwa ni tabia yake. Mlio wote wa kuku, katika makanisa halisi, haukuwa na matokeo kwake; alikuwa ameliona Neno. Lilikuwa ni sehemu yake. Alikuwa ni tai. Yeye hakuwa kuku; alikuwa tu kwenye kitalu pamoja nao. Lakini yeye alikuwa ni tai, kwanza.

Unaweza kuzungumza na watu wakati mwingine mitaani, kuzungumza nao juu ya Bwana, wanakucheka moja kwa moja. Vema, tunapaswa kufanya hivyo, hata hivyo. Lakini sikilizeni, “Hakuna mtu awezaye kuja Kwangu asipovutwa na Baba Yangu kwanza.” Inampasa Mungu kuvuta kwanza. Hapana budi kuwe na Uzima. “Na wote ambao amenipa Mimi, watakuja Kwangu.”

Yeye alifanya utaratibu kwa wale wanaotaka kukombolewa. Yeye alifanya utaratibu kwa wale wanaotaka kuponywa. Halafu basi kwa sababu kwamba alifanya jambo hili, linamfanya kuwa mwingi wa rehema, kama ambavyo daima amekuwa mwingi wa rehema. Haina budi kuwa, kama ukikataa Hili, hakuna kitu kilichosalia ila Hukumu, kwa sababu dhambi haina budi kuhukumiwa.

Farao, wakati alipoingia ba-baharini, kama mwigaji, akidhania kwamba angeweza kuingia kama Musa alivyoingia. Musa pamoja na jeshi lake, na Farao na jeshi lake wote pamoja walionekana iliwapasa kuangamia baharini. Bali Mungu, aliye mwingi wa rehema, akafanya mlango wa kutokea kwa ajili ya wana wa Waebrania, (kwa nini?) Kwa sababu walikuwa wakitekeleza wajibu wao, walikuwa wakifuata Neno. Sasa hiyo ndiyo njia pekee ya kupata rehema, ni kufuata maagizo ambayo Mungu ametupa tufuate. Hiyo ndiyo njia pekee anayoweza kuonyesha rehema, ni wakati tunapofuata yale aliyosema tufanye.

Kama vile mjadala mdogo si muda mrefu uliopita, pamoja na mhudumu aliyesema kwamba nilikuwa nikifundisha Fundisho la kimitume katika siku hii. Naamini nilieleza hayo siku moja au mbili zilizopita, au wakati fulani, jinsi alivyosema “Wewe unajaribu kuingiza fundisho la kimitume katika kizazi hiki.” Yeye alisema, “Wakati wa mitume ulikoma, pamoja na mitume.”
Nami nikamwuliza, “Vema, unaamini Neno?”
Akasema, “Naam.”
Nilisema, “Ufunuo 22:18 inasema, ya kwamba, 'Ye yote atakayeondoa Neno moja kutoka kwa Hili, ama kuongeza neno moja Kwake,' si maneno mawili tu; Neno moja, toa Neno moja.”
Kasema, “Ninaamini jambo hilo.”
Nilisema, “Basi ninaweza kuwaambia mahali ambapo wakati wa mitume ulitolewa, Baraka za kimitume zilitolewa kwa Kanisa; sasa wewe niambie ambapo Mungu aliziondoa Kanisani, kwa Neno. Huwezi kufanya jambo hilo; hakuna.” Nikasema, “Sasa kumbuka, ya kwamba Petro, kwenye Siku ya Pentekoste, yeye alikuwa ni-ndiye mwanzilishi wa wakati wa mitume. Naye akawaambia wote, 'Tubuni mkabatizwe katika Jina Lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.'”

Sasa kama unataka kusikiliza mlio wa kuku wa kimadhehebu, na kuishi huko nje katika mambo ya ulimwengu, basi inaonyesha ya kwamba kuna kasoro fulani. Kwa sababu, Hilo ni Neno. “Kila atakaye, na aje.” Na kama unayo nia, unapaswa kuja. Lakini kama huna nia, basi uko katika hali ya huzuni. Lakini kama una nia ya kuja, njoo ufuate kanuni ya Mungu! Wala Yeye hashindwi kutimiza yale aliyoahidi. Wakati mmoja nilikuwa kijana, na sasa mimi ni mzee, sijapata kumwona akishindwa katika Neno Lake. Kwa sababu, Yeye anaweza kufanya lolote bali hawezi kushindwa. Hawezi kushindwa. Mungu hawezi. Haiwezekani kwa Mungu kushindwa, na kubaki Mungu.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mungu aliye mwingi wa rehema.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Yohana 3:16-18


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet.

(PDFs Kiingereza)

Chapter 13
- God is Light

(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Kimo Cha Mtu
Mkamilifu.
(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.