Ruthu, Mmoabu.
<< uliopita
ijayo >>
Mkombozi Alye Jamaa Wa Karibu.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mkombozi Alye Jamaa wa Karibu.Ninataka kuyaita mazungumzo haya madogo asubuhi ya leo, ninapoyafundisha, nikijaribu kuleta imani kwenu, ya ukombozi, na kwamba ni nini, na jinsi ya kuupokea. Ninataka kuyaita: Mkombozi Aliye Jamaa Wa Karibu.
Sasa, kukomboa chochote, ni “kukirudisha.” Kitu ambacho kimepotea, kama vile kuweka kwenye duka la rehani. Nawe unashuka uende kukikomboa hicho, kinakombolewa kwa gharama. Ndipo ni mali yako ya kibinafsi, ukiisha kukikomboa. Lakini sheria ya ukombozi, katika Israeli, ilibidi awe ni jamaa wa karibu, kuikomboa mali au kitu fulani kilichokuwa kimepotea.
Hadithi yetu inaanzia katika wakati wa watawala wa Israeli, ambao walikuwa ni waamuzi, baada ya kifo cha Yoshua. Na kupata picha nzuri sana ya jambo hili, soma kuhusu sura tano au sita za kwanza za Samweli wa Kwanza, nawe utapata hadithi yake halisi.
-----
Sasa, watu wengi wanaangalia Kitabu hiki cha Ruthu, kama wasemavyo, “Ni hadithi ya mapenzi ya Biblia.” Biblia ni hadithi ya mapenzi. Biblia nzima ni hadithi ya mapenzi. Sio tu kwamba ni hadithi ya mapenzi, bali ni nabii. Si kwamba ni nabii tu, bali pia ni historia. Sio kwamba tu ni hadithi ya mapenzi, historia, nabii, ni Mungu Mwenyewe. Kwa sababu, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Kwa hiyo, Neno ni Mungu katika maandishi. Hilo linapaswa kulitatua, ndugu; Mungu katika maandishi. Yehova, akichapishwa kwenye Kitabu. Na hakuna hata moja ya hayo ni namna fulani tu ya hadithi ya kubuni, bali yote ni Kweli kabisa. Kila sehemu Yake, iweke nafsi yako. Iko Hapo. Ni Ukweli, na Mungu atalitetea Neno Lake.Na hadithi hii iliandikwa, na hati zote za kale. Wakati walipokuwa wakiitenganisha Biblia, wale watu watakatifu, wakati walipokuwa wakijaribu kuiweka pamoja katika Agano la Kale, Kitabu hiki cha Ruthu kilikuwa kimoja cha Vitabu bora sana ambavyo walivikubali. Kwa nini? Ikiwa ni hadithi tu ya mapenzi, kwa nini waandishi na wahenga wa kale wakubali Kitabu hiki kuwa kimevuviwa? Kwa sababu, kuna ufunuo uliofichwa ndani Yake. Na katika ufunuo huu uliofichwa, unapata maana halisi. Utakuleta karibu sana na Mungu. Nami naomba, nafsi yangu yote, asubuhi ya leo, kwamba Mungu ataushika kila moyo, auduwaze kabisa, hata ajifunue Mwenyewe, kile tu alicho, katika hadithi hii; kile Yeye alicho kwako; jinsi ya kumkubali. Na mara ukiliona, ni rahisi sana, unashangaa jinsi gani ulivyopata kupita juu yake. Lakini inaweza tu kufunuliwa na Roho Mtakatifu.
-----
Sasa, hadithi hii inaanzisha kitu cha namna hiyo, kama mwanamke anayependeka, mzuri. Jina lake lilikuwa Naomi. Naomi maana yake ni “mwenye kupendeza.” Elimeleki alikuwa ni mumewe, maana yake ni “kuabudu.” “Ibada ya kupendeza” ilikuwa ni familia yake. Walikuwa na mtoto wa kiume, Maloni, ambalo linamaanisha “ugonjwa.” Na Kilioni, yule mwingine, alimaanisha “kuchoka, huzuni, majonzi.” Hiyo hapo hiyo familia.
Ndipo kukaja njaa katika nchi ya Israeli. Na kosa la kwanza ambalo Myahudi amewahi kufanya, ni, kuondoka katika nchi hiyo. Mungu aliwapa nchi hiyo. Wakati Ibrahimu alipopewa hiyo nchi, Mungu alimwambia asiondoke katika nchi hiyo. Naye alifanya kosa aliposhuka akaenda Gerari, akapata shida. Myahudi hapaswi kamwe kuondoka Palestina. Hapo ndipo alipopangiwa.-----
Sasa, ninataka kufananisha, asubuhi ya leo, Naomi, mama mkubwa, na kanisa la Othodoksi, kanisa la Othodoksi la Kiyahudi. Ruthu, Mmoabu, Mmataifa, akiwa ni Kanisa la Kikristo, Kanisa Jipya. Nami nataka kuliendea, kutoka katika awamu nne mbalimbali, Ruthu. Nimeziandika hapa. Ruthu, akiamua, akifanya uamuzi wake; Ruthu, akitumika; Ruthu, akipumzika; Ruthu, akizawadiwa. Tunaporudi: Ruthu, akifanya uamuzi; Ruthu, baada ya kufanya uamuzi wake, basi Ruthu anahudumu; ndipo Ruthu anapumzika; ndipo Ruthu anazawadiwa.-----
Ruthu, akifanya uamuzi. Sasa, Ruthu, akihudumu chini ya uamuzi wake. Sasa angalia kwa dakika moja tu. Sasa yeye anaenda kondeni, kuokota masazo. Sasa, mama yake alimwambia; ambapo, Agano la Kale likiliambia lile Jipya, mnajua. Mama yake alimwambia, kasema, “Tuna jamaa, na jina lake ni Boazi. Yeye ni tajiri. Naye ni jamaa wa karibu. Nenda kwenye shamba lake. Na labda … Usiende kwenye shamba jingine; nenda kwenye shamba lake.”
Jinsi Roho Mtakatifu anavyotuambia tusiende kando kwenye aina fulani ya kitabu cha kanisa, aina fulani ya katekismo, lakini twende Shambani mwa Mungu, Agano la Kale, Biblia. Usiseme, “Vema, tutasema hivi. Nasi tutasema hivi kwa ajili ya maombi. Tutakuwa na hili.” Kaa mumo humo Shambani. Nenda moja kwa moja ndani Yake, maana Yeye ndiye aliye Jamaa wa Karibu.Neno la Mungu, Agano la Kale, ni Jamaa wa Karibu wa lile Jipya. Kanisa la Kale ni mama wa Kanisa Jipya, mnaona, Mkristo, mwaminio. “Usiende kwenye shamba lingine. Kaa mumo humo katika shamba lake. Na labda, siku moja, huenda ukapata neema kwake.”
Na siku moja, alipokuwa huko kondeni, huyu kijana tajiri, jina lake Boazi, mtawala, mtu tajiri, alipita, naye akamwona. Loo, alipomwona, alimpenda. Alidhani alikuwa ni mwanamke mzuri sana. Alipenda tabia yake. Mnakumbuka, alisema, “Najua, halafu watu wanajua, ya kuwa wewe ni mwanamke mwadilifu.” Alifanya uamuzi wake, safi na dhahiri. Akarudi moja kwa moja kule, akaishi vile vile hasa alivyosema angefanya.Vinginevyo, leo, wao wanasema, “Tunajua ya kwamba wewe ni Mkristo. Tunajua ya kwamba wewe ni mtu wa Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii isipokuwa Mungu awe pamoja naye.” Hivyo ndivyo Nikodemo alivyomwambia Yesu, alisema, “Rabi, tunajua ya kwamba wewe u mwalimu aliyetoka kwa Mungu. Hakuna mtu awezaye kufanya mambo unayofanya isipokuwa Mungu awe pamoja naye.” Wakati, angeweza kumwona ameketi pale na kutambua mawazo ya moyo wao hasa.
Mwanamke aligusa vazi Lake. Akageuka, akasema, “Ni nani aliyenigusa?” Wote walikana. Akaangalia tena katika kusanyiko na kusema, “Wewe, unayetokwa na damu hapo, imani yako imekuponya.” Kasema, “Hakuna mtu anayeweza kufanya jambo hilo isipokuwa Mungu awe pamoja naye. Tunajua Wewe ulitoka kwa Mungu. Hatuwezi kukukubali, kwa sababu tutafukuzwa kanisani.” Mnaona? Huo mzabibu uliopandikizwa, Ndugu West, kama tulivyokuwa tukizungumza jana usiku, watakufukuza. “Lakini, chini moyoni mwetu, tunajua unatoka kwenye Mzabibu wa asili.” Kristo ndiye Mzabibu; sisi ni matawi. “Tunajua, kwa sababu tunaona Uhai ule ule ulio ndani ya Mungu, umo ndani Yako.” Huo ndio Boazi alikuwa ameona kwa Ruthu, uamuzi huo dhahiri, uadilifu huo wa mwanamke aliyesimama pale. Naye akampenda.
Sasa, ninawatakeni mwone. Naomi, kanisa la kale, alianza kumwelezea Ruthu sheria zote kuhusu dini yake, kama vile Agano la Kale ni kivuli cha Jipya. Sasa, ninawatakeni mpate hadithi hii papa hapa. Sasa, nataka kuonyesha vivuli. Agano la Kale linalielezea lile Jipya, kama tu utalisoma, kwa kuwa ni kivuli cha lile Jipya. Sasa, kama nilikuwa nikielekea kwenye ule ukuta, na sikuwa nimejiona mwenyewe, na nikione kivuli changu, ningejua, ningekuwa na dhana ya sura yangu. Na ikiwa (wewe) hujui Agano Jipya ni nini, soma la Kale nawe utaona kivuli chake. Mnaona? Na ndipo Agano Jipya linapoingia, unasema, “Mbona, hakika, hili ndilo.” Kitabu cha Waebrania, tukirudi nyuma, Paulo akikielezea.
Sasa, angalieni kwa makini sasa. Wakati Ruthu aliposema, ama… Naomi alipomwambia Ruthu, alisema, “Sasa, yeye ni jamaa yetu. Na kama unaweza kupata neema kwake, utapata raha.” Loo, jamani! “Kama unaweza kupata neema, utapata raha.” Boazi alimwakilisha Kristo, yule Tajiri, mrithi wa vitu vyote, Bwana wa mavuno. Loo, jamani! Jinsi ambavyo, wakati Boazi alipokuja amepanda farasi huko nje, katika lile gari, akiangalia kote mashambani, na macho yake yakamwangalia Ruthu! Alikuwa ni bwana. Yeye alikuwa bwana wa mavuno. Naye akapata neema machoni pake.
Hivyo ndivyo Kanisa linavyofanya, leo. Wakati Bwana wa mavuno akipita, Yeye haangalii jengo kubwa, minara mikubwa, kwaya zilizofunzwa vizuri. Anatafuta watu binafsi, wanaume na wanawake ambao wamejitolea na kufanya uamuzi dhahiri kwa Kristo, waliojiweka wakfu kwa utumishi Wake. “Mungu, ninaamini Hilo, kila Neno Lake. Wakati Neno Lako linaposema jambo lo lote, ninakaa moja kwa moja Nalo. Hilo ni Neno Lako. Ninaamini Hilo, kila Neno.” Hicho ndicho anachotafuta; Bwana wa mavuno. Hicho ndicho anachotaka kuwapa, Roho Mtakatifu, wale walio na njaa na kiu. “Heri ninyi wenye njaa na kiu, kwa maana mtashibishwa.” Yeye anajaribu kulipata Kanisa hilo, leo.
Sasa, basi, Ruthu aliombwa kufanya jambo ambalo lilikuwa la aibu, bali alikuwa tayari kwa sababu alikuwa ameamua. Ni mfano wa jinsi gani wa mwaminio! Ni mfano mkamilifu ulioje! Naomi, kanisa la kale, alisema, “Shuka uende, usiku wa leo. Ni msimu wa shayiri.” Loo, ni wazo zuri iliyoje tungeweza kutegemea hapo!
Naomi na Ruthu walikuja tu wakati wa shayiri. Msimu wa shayiri ulikuwa ni msimu wa mikate, ule wakati ambapo mkate mpya ulikuwa ukitolewa. Nalo Kanisa, katika siku hizi za mwisho, kupitia miaka elfu mbili ya mafundisho ya kipagani na kadhalika, limeingia katika msimu wa shayiri, na Maisha mapya, Mkate mpya, asali kutoka Mbinguni. (Russell, zungumza juu ya mkate wa ganda la asali!) Huu Ndio, Mkate kutoka Mbinguni. “Mimi Ndimi Mkate wa Uzima. Baba zenu walikula mana, nao wamekufa. Lakini Mimi Ndimi Mkate wa Uzima utokao kwa Mungu, kutoka Mbinguni. Mtu akila Mkate huu hatakufa kamwe.” Nalo Kanisa katika siku hizi za mwisho hapa, linaletwa, sasa hivi, kwenye msimu wa shayiri.
Ruthu, Mmataifa, aliyetengwa, akafukuzwa, ameingizwa ndani, ili akubaliwe kama Bibi-arusi. Kristo aliingia, kwenye msimu wa shayiri tu. Alisema, “Sasa jivike mavazi yako.” (Siyo, “Vua mavazi yako.”) Ni kinyume jinsi gani leo! “Jifunge mavazi yako, utakapokwenda kumlaki. Anaenda kupepeta shayiri, usiku wa leo. Shuka ujivike mavazi yako. Jifunike, ili kumlaki.”
Siku hizi, wanataka kujifunua. Jifunikeni. “Shuka, kwa sababu anapepeta shayiri. Na kisha uangalie mahali anapolala.” Ulifanya hivyo? Juu ya Golgotha. Miaka mingi iliyopita, niliweka moyoni mwangu mahali ambapo Yeye aliutoa uhai Wake, apate kunichukua. Paangalie mahali anapolala. Paangalie mahali alipolala. Hivyo ndivyo kila mwamini anavyopaswa kufanya. Angalia yale aliyokufanyia. Ujumbe wa Jumapili iliyopita, juu ya Ziara ya Kalvari, angalia yale aliyokufanyia.
Akasema, “Angalia mahali anapolala. Ndipo atakapojilaza chini kulala usingizi, kupumzika, nenda ujilaze miguuni pake.” Sio kichwani mwake; miguuni pake, kutostahili. “Kisha uchukue blanketi”
“aliyokuwa amejifunika nayo, ukajifunike nayo.” Loo! Mnaona jambo hilo? Loo, jamani! Ninajua huenda mkadhani mimi ni mshupavu wa dini. Lakini huyo ananifaa tu vizuri, huyo Roho wa Mungu. Angalia mahali alipolala, Kalvari; mahali alipolala kaburini; huko Gethsemane. Tia alama, na utambae mpaka miguuni Pake. Lala pale na ufe, wewe mwenyewe, kwa ninii yako... Haya basi. Jifunike, kabisa, na sketi Yake. Alisema, “Sketi,” ndivyo alivyoiita. Naye Ruthu akasema, “Usemayo, nitayafanya.”Loo, ni uamuzi dhahiri iliyoje kwa mwaminio! “Yale Biblia isemayo, hayo nitafanya. Anasema, 'Tubuni mkabatizwe, Jina la Yesu Kristo,' nitafanya hivyo. Kama ikisema, 'Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili,' nitafanya hivyo. Kama ikisema, cho chote ilichosema, 'Yesu Kristo yeye yule jana, hata milele.' Kile inachosema nifanye, nitakifanya.” Mnaona, Kanisa likichukua maagizo Yake kutoka kwenye Neno. Likajilaza chini.
Sasa, kumbukeni, hiyo ilikuwa ni fedheha kwa yule mjane mwanamke kulala karibu na mwanamume huyu, miguuni pake. Aibu, kwa ulimwengu wa nje. Loo, unaweza kustahimili jambo hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.” — Mh.] Hili hapa. Angalia. Angalia. Jambo ndilo hili. Kanisa, yule mwanamke kijana, mwanamume kijana, mzee au kijana, wanaombwa kujitenga na ulimwengu, na kuingia mahali, Ufalme wa Roho Mtakatifu, ambao ni aibu kwa ulimwengu. Moyoni mwao wanajua yote yanahusu nini. Lakini, kwa ulimwengu, wao wanakuwa washupavu wa dini. Wao wanakuwa mtakatifu anayejiviringisha ama kitu fulani juu ya wazo hilo, jina fulani la aibu. Lakini Kanisa linaombwa kufanya hivyo. Je! Uko tayari kuangalia mahali hapo, na kujilaza chini? [“Amina.”] Acha ulimwengu ukuite chochote wanachotaka.
Ule wimbo wa kale, tuliozoea kuimba.
Nimeanza kutembea na Yesu peke yake, mnaona,
Mto wangu, kama Yakobo, ni jiwe;
Nami nitachukua njia na wachache wa Bwana waliodharauliwa;
Nimeanza na Yesu. Ninapita.-----
Angalia mahali alipojilaza chini, nawe ujilaze chini hapo pamoja Naye. Je, uko tayari kwenda Kalvari, asubuhi ya leo, kama nilivyosema Jumapili iliyopita? Umepaangalia mahali hapo maishani mwako? Je! Umefika mwenyewe mahali ambapo Yesu alisulubiwa?Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mkombozi Alye Jamaa wa Karibu.