Kufunuliwa kwa Mungu.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Mungu alifunikwa na pazia ndani ya Musa.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufunuliwa kwa Mungu.

2 Wakorintho 3:13-15,
13 Nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika,
14 Ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo hukaa, yaani haikufunuliwa kwamba huondolwa katika Kristo;
15 Ila hata leo Torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.
16 Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

----
Musa alikuwa na Neno. Sasa kumbuka, baada ya Neno kudhihirishwa; Musa alikuwa Musa tena. Unaona? Lakini wakati lile Neno lilipokuwa ndani yake ili litolewe kwa watu, yeye alikuwa Mungu; kwani hakuwa Musa tena, alikuwa na Neno la Bwana kwa ajili ya kipindi kile. Hakukuwepo na kitu chochote ambacho kingemgusa, hadi hilo liishe, alikuwa na Neno la Mungu likiwa pamoja naye. Hivyo basi wakati alipokuja, watu waligeuza vichwa vyao, hawakuweza kuelewa. Yeye alikuwa amebadilishwa, alikuwa mtu wa tofauti, Yeye alikuja na lile Neno. “Na aliweka pazia”, Biblia ilisema, “juu ya paji la uso wake”, kwani alikuwa na lile Neno. Naye alikuwa mwenyewe Neno kwao.

Sas, tazama, kama Musa... Ee ndugu, hili linakwenda kuwa tusi. Lakini kama Musa... Kama Paulo alivyosema hapa katika 2Wakorintho sura ya 3, kama Musa ilibidi afunike paji la uso wake kwa pazia akiwa na utukufu wa aina ile juu yake... Unaona? Kwa sababu ule ulikuwa utukufu wa asili, ile ilikuwa ni torati ya asili. Na kama Musa... hali akijua kuwa torati ilipasa ife. Lakini ule utukufu ulikuwa mkuu mno hata ukawapofusha watu macho, hivyo ikawalazimu kuweka pazia juu ya uso wake. Je, ni zaidi kiasi gani huu utakavyokuwa? (Watu waliopofushwa macho kiroho! Loo.) Ule utukufu ulipasa kufifia, lakini Utukufu Huu hauwezi kufifia. Unaona? Musa alikuwa na torati ya mwilini, hukumu, hakuna neema, hakuna chochote, ili kuhukumu tu. Lakini tunayosema habari zake... Ile haikuwa na msamaha, ile ilikuambia tu kile ulichokuwa. Hii inakupa njia ya kutokea. Na wakati pazia lilipoondolewa juu ya Neno, ee, jamani, itakuwa imani ya jinsi gani? Itapasa ifunikwe na pazia. Itabidi ifichwe nyuma ya pazia. Sasa, tazama, hivyo Roho amefichwa nyuma ya pazia katika hekalu la kibinadamu, unaona, yeye anahubiri neno la asili akiwa nyuma ya pazia la asili.

Sasa, Paulo akizungumza hapa sasa na katika hii-hisia hii, Roho-Neno “sisi ni wahudumu, si wa andiko (torati) lakini wahudumu watoshelevu wa Roho”, kuwa Roho analichukua andiko na kulidhihirisha. Ile ilikuwa ni Sheria tu; ilibidi uende na kuitazama, useme, “Usizini, Usiibe, Usiseme uongo, Usifanye hili, lile au linginelo”. Unaona? Ilikubidi uitazame hiyo. Lakini huyu ni Roho anayekuja juu ya Neno lililoahidiwa kwa ajili ya kipindi hiki, na analeta na kudhihirisha, (siyo vipande viwili vya mawe) lakini uwepo wa Mungu aliye hai. Siyo wazo la kubuniwa ambalo mtu fulani aliliunda au mazingaombwe ya Hondini, ila ni ile ahadi halisi ya Mungu iliyofunuliwa na kudhihirishwa mbele yetu kabisa. Ni pazia la aina gani ambalo hilo latakiwa nyuma kule? Na ku- kupoteza hilo...

Unaona, hilo lilikuwa kuu mno hadi watu wakasema, walisema wakati watakapomwona Yehova akishuka chini katika hii Nguzo ya Moto na akaanza kuitingisha dunia, na- na mambo aliyoyafanya, na mlima ukiwaka moto. Na hata kama mtu yeyote alijaribu kuuendea huo mlima aliangamia. Lilikuwa kuu mno hata Musa aliogopa lile tetemeko. Ndipo Kama wakati ule alitetemesha mlima tu, wakati huu atatetemesha mbingu na nchi. Vipi kuhusu Huu Utukufu? Kama ule ulifunikwa na pazia la asili, huu umefunikwa na pazia la kiroho. Hivyo, usijaribu kutazama yale ya asili, ingia katika Roho na uone mahali tulipo, unaona, ile saa tunayoishi.

Je, hili linaeleweka kwako? Unaona? Ni pazia la kiroho lililoko juu ya watu, wanaposema, “Mimi ni Mmethodisti. Na mimi ni mwema kama yeyote yule. Mimi ni Mbabtisti na mimi ni Mpentekoste”. Je hutambui kuwa kitu hicho ni pazia la mapokeo? Lina mficha Mungu awe mbali na wewe. Hivyo ndivyo vitu vinavyokuzuia wewe kufurahia yote... Ee, unasema, “Ninapiga kelele na kuruka juu chini”.

Yeye alisema, “Kila Neno”. Hawa aliamini kila Neno isipokuwa moja. Unaona? Ni Neno lote la Mungu, ile ahadi ya saa hii ikidhihirishwa. Unaona? Tazama sasa tunapoendelea mbele. Ninayo mengi hapa ya kuyaelezea, lakini nina kama kurasa ishirini hivi, lakini ina... ya- ya dokezo kadha, lakini sita-sitahubiri juu yake kabisa. Unaona, nitaharakisha.

Anafunikwa na pazia la asili kabla hajaweza kuhubiri Neno kwa watu. Sasa, Mungu yapasa ajifunike Mwenyewe kwa pazia, katika mwili wa kibinadamu kama alivyoahidi. Mungu... Unalipata hilo? Mungu yapasa ajifunike Mwenyewe na mwili wa kibinadamu, na akaweka juu yao pazia la asili (mnasema “Vema, mimi ni hili, mimi ni lile”), ili apate kusema na watu. Wakati hilo pazia, ambalo ni pazia la mapokeo, linaporaruliwa vipande, ndipo... hapo kile wanachosema “Mbona siku za miujiza zimekwishapita”.

----
Sasa, lile pazia la asili. Mungu aliye Neno amefunikwa na pazia la mwili wa kibinadamu. Hiyo ilikuwa nini? Mungu alifunikwa na pazia ndani ya Musa. Mungu alikuwa ndani ya Musa, amefunikwa na pazia, na uwepo wa Mungu ulikuwa ndani yake. Alikuwa pamoja na lile Neno kikamilifu mno namna hiyo, hadi ilibidi aufunike uso wake kwa pazia. Na ni nabii aliyethibitishwa aliyelikunjua Neno na kuwaambia, “Usifanye! Fanya! Na usifanye! Unaona?

Kukipa kile kizazi Neno Lake, Yeye alijifunika na pazia ndani ya binadamu, au lile Neno lingekuwa limewapofusha hata wale walioitwa. Unaona? Hata wale watu waliokuwa nje pale, hawakuweza kuvumilia kuona lile katika- katika Kitabu cha Kutoka tunalikuta hilo, walisema, “Hebu Musa aseme, siyo Mungu”. Unaona kwa nini ile Nguzo ya Moto haitokei kupita kiasi? Unaona?

Mungu alisema, “Nita- Nita- Nitafanya hilo, Nitawainulia nabii”. Amina! “Nitawainulia mmoja”. Na Yeye akaja jinsi ile ile kabisa. Yeye... Nita... Na Yeye atakuwa... atakuwa lile Neno. Yeye alisema, “Kama wanataka kuona kile Neno lilicho”, akasema, “Sasa Musa nilikutokea nyuma kule katika kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto,” akasema, “Ninakwenda kushuka chini na kuwasha moto ule mlima”. Akasema, “Wataona kuwa umesema kweli. Nitaonekana hapa katika- katika ile-njia ile ile ya moto uwakao. Nitaonekana hapa na kuwathibitishia watu. Nitaithibitisha huduma yako”. Hayo ndiyo aliyomwambia Musa hapa kwa maneno mengi.

Tazama, na alisema, “Sasa ninakwenda ku-Ninakwenda kukutukuza wewe mbele ya watu”. Akasema, “Mimi nilikutana nawe pale katika kichaka kilichokuwa kikiwaka moto, sasa Ninakwenda kushuka chini, Moto ule ule, na ninakwenda kuwafanya watu waone kuwa hukuwahi kamwe kusema uongo kuhusu Hilo.” Na hata wathibitishe kisayansi, kama mnataka. Unaona? Ninakwenda kushuka chini kabisa na kufanya wajue.

Na wakati Yeye alipoanza kunguruma, wakati Yehova alipoanza kunguruma, watu walisema, “Hapana! Hapana! Hapana! Hebu Yehova asiseme, tuta- tutakufa.” Unaona, Yeye alipasa kufunikwa na pazia. Hivyo Mungu alijifunika Mwenyewe kwa pazia ndani ya Musa na kumpa Musa Neno. Na Musa akashuka chini na kuhubiri lile Neno la Bwana akiwa na pazia limefunika uso wake. Hilo ni sahihi? Yehova akiwa amefunikwa na pazia ndani ya umbo la nabii, kwani ingelikuwa kikamilifu... Na Mungu alisema kuwa asingenena nao tena namna ile. Yeye angenena nao tu kwa njia ya nabii. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo angenena nao kuanzia hapo na kuendelea. Hiyo ndiyo njia pekee aliyowahi kuitumia kunenea. Hiyo ni sahihi. Hakuna njia nyingine kamwe. Yeye hasemi uongo.

Tazama, ni Musa peke yake aliyekuwa na Neno. Sasa, hapakuwepo na-na kikundi fulani kilichoshuka pale, hapakuwepo hata Mafarisayo au Masadukayo, au haikuwa ni- ni dhehebu fulani au ukoo fulani. Ilikuwa ni Musa! Mungu alimpata mtu mmoja. Yeye hawezi kuwa na vichwa viwili au vitatu tofauti. Yeye anakuwa na mtu mmoja. Musa alikuwa na lile Neno, na Musa alikuwa pekee. Wala Joshua hakuwa na Hilo. Hakuwepo mwingine aliyekuwa Nalo. Amina! Joshua alikuwa ni-jemadari, Joshua alikuwa kamanda katika jeshi. Joshua alikuwa mwamini, Mkristo. Lakini Musa alikuwa ni nabii. Neno haliwezi kuja kwa Joshua, sharti lije kwa Musa. Yeye alikuwa nabii mkuu wa saa hiyo. Tazama, Neno kamwe halikumjia Joshua hadi Musa alipokuwa ameondoka. Unaona? Hapana, bwana, Mungu hushughulika na mtu mmoja. Unaona? Sasa ni Musa tu aliyekuwa na lile Neno, siyo kikundi fulani.

Tazama, Mungu alionya mtu yeyote asijaribu kumfuata Musa ndani ya lile pazia, waigizaji. Unaona? Wanawake, wanawake, padri, yeyote aliyekuwa, awe mcha Mungu namna gani, awe dume kiasi gani, awe alikuwa wa kiasi gani, Yeye alionya, “Hebu Musa aje peke yake! Na kama mtu yeyote, au mnyama, analigusa, sharti auawe pale pale” Usije ukaruka lile pazia, lile pazia lilikuwa la mtu mmoja tu. Huo ujumbe ni mmoja. Unaona? Kule Hekaluni, ni mmoja tu aliyeingia mara moja kwa mwaka, aliyepakwa mafuta na kuandaliwa kuingia mle, siyo kuleta Neno kutoka kule, bali kutoa dhabihu ya damu. Hata kule tu kupita karibu yake, ni mmoja tu. Mtu mwingine yeyote alikufa. Unaona?

Sasa wamekufa kiroho. Hili ni pazia la kiroho. Unaona? Lile lilikuwa pazia la asili. Hili ni pazia la kiroho. Unaona? Wao wanaendelea kupita na kuingia ndani mle, utaweza kuwatambua. “Ee, Ninajua! Ninajua hilo, lakini nina...” Endelea mbele, ni sawa tu, hii inanena tu... Unakumbuka pigo la mwisho kule Misri lilikuwa kifo, kabla ya kule kutoka. Pigo la mwisho duniani ni kifo kiroho, kabla ya kule kutoka. Ndipo watateketezwa na kurudia kuwa mavumbi, na wenye haki watatembea juu ya hayo majivu yao. Lakini jambo la mwisho ni kifo cha kiroho, kukataa Neno.

Sasa tazama, Mungu alionya mtu yeyote asijaribu kumfuata Musa kuvuka lile pazia la Moto. Musa ilipasa afunikwe na pazia, ilipasa aje kutokea pale. Na Musa aliingia mle kama Musa, aliingia ndani ya hii Nguzo ya Moto; na wakati aliporudi kutoka huko alikuwa amefunikwa na pazia, kwani aliingia ndani ya Hilo, akatoka kwenye mapokeo yake, mapokeo ya wazee. Yeye aliona ile Nguzo ya Moto, lakini sasa anaingia ndani ya Hiyo Nguzo ya Moto. Unaona? Amina. Na akatoka nje akiwa amefunikwa na pazia. Neno la Mungu ndani ya mtu, Amefunikwa na pazia. Hapa anatoka nje, ee, jamani, ninaliona hilo likitendeka. Alionya mtu yeyote asithubutu kufanya hilo, hakuna mtu atakayeweza kuigiza Hilo. Afadhali usijaribu. Unaona? Hata kuhani, au mtu mtakatifu, popote alipokuwa, kadinali, askofu, chochote kinginecho, kilipojaribu kuingia mle kwenye lile pazia kilikufa. Mungu aliwaonya. Hatutakuwa na uigizaji.

Lile Neno Lake hufunuliwa kwa mmoja. Ndivyo ambavyo imekuwa siku zote, nabii amekuwa akija na Neno la Bwana katika kila kipindi, kila wakati, ukipitia Maandiko yote. Unaona? Lile Neno huja kwa mmoja. Katika kila kipindi ni hivyo hivyo, hata katika vipindi vya kanisa, kuanzia kile cha kwanza hadi cha mwisho. Wengine wanazo nafasi zao, hiyo ni sahihi, tazama, lakini ukae mbali na Nguzo ya Moto. Unaona? Ni somo zuri jinsi gani tunajifunza hapa! Unaona, kila mtu anataka kuwa namna ya Musa, na ni kila mtu...

Mnakumbuka yale Dathani na wenzake waliyosema nje kule? Walisema, “Sasa Musa subiri hapa dakika moja, wewe unajitukuza kupita kiasi juu ya watu”. Unaona? Sasa wako watu wengine hapa ambao Mungu amewaita. Hiyo ni kweli. Wao... kila mmoja alikuwa anafuata vema hali wao walipoendelea na safari, lakini wakati mmoja alipojaribu kupanda juu na kuchukua nafasi ya Mungu ambayo alimpa Musa, ambayo ilikuwa imechaguliwa tangu asili na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi hiyo, ajaribu kuichukua, moto ulishuka na kufungua ardhi na wao wakamezwa ndani yake. Unaona? Uwe tu Mkristo mzuri, mtaua- mtaua unayeamini Neno la Mungu. Unaona? Kaa mbali na hiyo Nguzo! Ni somo kuu jinsi gani!

Mungu alikwishamtokea kwanza Musa katika kichaka kilichowaka moto, Mungu alikuwa amefunikwa na pazia la Nguzo ya Moto. Sasa, sikiliza kwa makini sana, sasa, kwa dakika moja. Mungu kwanza alikuja kwa Musa. Alikuwa amefunikwa na pazia. Mungu alikuwa ndani ya Nguzo ya Moto, amefichwa nyuma huko katika kichaka, unaona, kama chini ya ngozi, unaona, nyuma kando ya kiti cha rehema penye madhabahu-Unaona? Yeye amefunikwa na pazia. Siku zote amefunikwa na pazia. Na wakati alipokuja kwa Musa, Yeye alikuwa katika Nguzo ya Moto, amefunikwa na pazia katika Nguzo ya Moto. Lakini hapa mbele ya watu, Mungu alimthibitisha Yeye kwa ile ile Nguzo ya Moto. Unaona? Musa alisema...

Sasa angalia! Je, unasoma... Je unaruhusu akili zako kuiona njia ya kutokea? Unaweza ku... “Walio na masikio, hebu wasikie”. Unaona? Wakati Mungu alipomtokea Musa alikuwa katika Nguzo ya Moto, wakati Alipomwita yeye aingie katika huduma yake. Na Musa alikuja na kuwaambia watu kuhusu hilo. Wao hawakuweza kuamini hilo. Bado alitenda miujiza na mambo kama hayo, lakini wakati huu Mungu alitokea kwa uwazi kisayansi na kuthibitisha huduma ya Musa kuwa ndiye yule yule Mungu aliyesema naye, kwani Yeye alitokea katika umbo la Nguzo ya Moto na kuuwasha mlima moto. Na Yeye alikuja kwa Musa ndani ya kichaka, akazungumza naye. Vema.

Mungu kwanza amtokea Musa katika kichaka kilichowaka moto, pazia. Mbele ya watu, Mungu amefunikwa na pazia tena, na kumthibitisha Musa kwa hilo pazia, kwa kujifunika Mwenyewe kwa huo huo Moto, hiyo hiyo Nguzo ya Moto iliyoshuka kutoka- kutoka kwao- kutoka kwao, hivyo wao waliweza tu kusikia Neno la Mungu. Je unalipata hilo? Ni lile Neno tu, wao walisikia Sauti Yake. Kwani Musa alikuwa kwao, Neno lililo Hai. Musa! Unaona, Mungu alikuwa amethibitisha hilo Neno hivyo kwa njia ya Musa! Unaona, Musa alisema... Mungu alimwambia Musa, “Nenda chini pale, na nitakuwa pamoja nawe, hakuna chochote kitakachosimama mbele yako”. “MIMI NIKO AMBAYE NIKO”.

Musa alishuka chini na kusema, “Yawezekana usiamini hili, labda, lakini Mungu alinitokea mimi katika Nguzo ya Moto na kuniambia mambo haya”. “Ee, tunavyo vitu mbalimbali vinavyoendelea kufanyika”. Mbona mchungaji farao alisema, “Vema ninayo mazingaombwe ya kichawi ya hali ya ya chini. Mbona ninao wachawi hapa wanaoweza kumbadilisha nyoka kuwa... fimbo kuwa nyoka. Njooni hapa wachawi”. Na wao wakaja pale na kufanya mambo yale yale.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufunuliwa kwa Mungu.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.

1 Timotheo 3:16


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)
 

Chapter 11
- The Cloud

(PDF Kiingereza)
 

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.