Simba ya Yuda.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

N'nani astahiliye?


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Pengo kati ya Nyakati Saba za Kanisa na Ile Mihuri Saba.

Ufunuo 5:2-4,
2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? 3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.

Sasa, “Na Malaika mwenye nguvu....” Sasa kifungu cha 2. ...Malaika mwenye nguvu kwa sauti kuu, akitangaza, N,nani astailiye...(Astailiye kwa kitu gani?) N,nani astailiye kukitwaa kitabu hicho.... Sasa, tunaona. Kile Kitabu kiko wapi sasa? Kwa mwenyewe wa asili, kwa maana kimepotezwa na mwana, mwana wa kwanza wa Mungu, katika jamii ya binadamu. Na wakati alipozipoteza haki zake, kumsikiliza Shetani, aliacha...Alifanya nini? Alikubali hekima ya Shetani badala ya Neno la Mungu.

-----
Wito wa yule Malaika ulikuwa wito wa Mkombozi aliye wa Jamaa wa Karibu kutokea. Mungu alisema, “Nina sheria; Mkombozi aliye wa Jamaa ya Karibu anaweza-anaweza kuwa kibadala. Mkombozi huyo aliye wa Jamaa wa Karibu yuko wapi? N’nani anayeweza kukitwaa? Nacho kilitoka kwa Adamu, kote kote kupitia kwa mitume wote na manabii, na kila kitu kingine, wala hakuna aliyepatikana. Sasa, na hilo je? “Hakuna mtu Mbinguni, hakuna mtu duniani, hakuna mtu aliyepata kuishi.” Eliya alikuwa amesimama pale. Musa alikuwa amesimama pale. Mitume wote walikuwa wamesimama pale, ama-ama wote waliokuwa wamekufa; watakatifu wote, Ayubu, wale wenye hekima. Kila mmoja alikuwa amesimama pale, wala hakuna mtu aliyestaili hata kukiangalia kile Kitabu, licha ya kukitwaa na kuivunja ile Mihuri. Sasa papa na hawa wengine wote wanaingilia wapi? Askofu wenu yuko wapi? Kustahili kwetu kuko wapi? Sisi si kitu. Hiyo ni kweli.

-----
Lakini, Yohana “alilia.” Hili hapa ndilo ninafikiri lilikuwa sababu ya kulia kwake. Kwa sababu, kama hakuna mtu aliyestaili na angeweza kukifungua Kitabu hiki cha Ukombozi, viumbe vyote vilikuwa vimepotea. Hiki hapa hicho Kitabu , hii hapa ile hati miliki, nayo itatolewa kwa Mkombozi aliye wa Jamaa wa Karibu ambaye anaweza kustaili. Hiyo ndiyo sheria ya Mungu Mwenyewe, na Yeye hawezi kuchafua sheria Yake, hawezi kukana sheria Yake, ndiyo namaanisha. Unaona? Mungu alihitaji Mkombozi aliye wa Jamaa wa Karibu aliyestaili, ambaye aliweza kufanya jambo hilo, ambaye alikuwa na mali ya kufanya jambo hilo.

Ndipo yule Malaika akasema, “Sasa hebu yule Mkombozi wa Jamaa wa Karibu na akaribie.” Na Yohana akaangalia. Na akaangalia kila mahali duniani. Akaangalia chini ya dunia. Na hapakuwapo na mtu. Viumbe na chochote kile vilikuwa vimepotea. Bila shaka, Yohana alilia. Kila kitu kilikuwa kimepotea. Kulia kwake hakukudumu ila dakika moja tu, hata hivyo. Ndipo akasimama mmoja wa wale wazee, kasema, “Usilie, Yohana.” Loo, jamani! Kulia kwake hakukudumu ila dakika moja tu. Yohana akawaza, “Loo, jamani, yuko wapi Mtu huyo? Manabii wako pale wamesimama; walizaliwa kama nilivyozaliwa mimi. Wenye hekima wako pale wamesimama...Loo, je! Hakuna mtu hapa?”

-----
Na Simba huyu wa kabila ya Yuda alishinda. Yeye alisema, “Usilie, Yohana. Kwa maana Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, ameshinda. Yeye ametiisha tayari. Yeye amefanya hivyo. Imekwisha, Yohana.” Whiu! Loo, loo jamani! Yeye alitoa kitakasaji ambacho kinarudisha dhambi kwenye mikono michafu ambayo ninii...kwa hekima yake, iliyomtia unajisi, mwanadamu. Naam.

Lakini wakati Yohana alipogeuka kuangalia, alimuona Mwana kondoo. Ni tofauti iliyoje na Simba! Yeye alisema “Simba ameshinda.” Mnaona, tena, ninaweza kutumia hilo hapo, Mungu akijificha katika urahisi. Yeye alisema, “Kuna Simba. Huyo ndiye yule mfalme wa wanyama. “Simba ameshinda.” Kitu chenye nguvu sana kuliko vyote vilivyoko ni simba. Nimelala huko katika misitu ya Afrika, nakusikia twi-twiga wakilia. Nana ndovu mkubwa, mwenye nguvu nyingi, huku ameinua mkonga wake hewani, “Whii,whii, whii.” Na kuwasikia watu wa-wa-wa wakatili waishio jangwani wakipiga kelele zao za kutisha na za kumwaga damu. Na me- mende, mpaka...Na mimi na Billy Paul tumelala katika kijibanda kichakavu kilichofunikwa kwa miti yenye miiba. Na kusikia, huko mbali kabisa, simba akinguruma, na kila kitu humo nyikani kinanyamaza. Hata mende wanaacha kupiga makelele. Mfalme anazungumza. Loo,loo,loo,loo,jamani! Ninawaambia, huo ndio wakati madhehebu na mashaka yanapoanguka ardhini. Kila kitu hunyamaza wakati Mfalme anapozungumza. Na Huyu ndiye huyo Mfalme, yaani Neno lake. Loo!

-----
Kwa nini atoke Yuda? “Ee Yuda, mfanya sheria hataitangulia, kati ya magoti yake, hata Shilo atakapokuja. Lakini atakuja kupitia kwa Yuda.” “Na yule Simba, alama ya kabila ya Yuda, ameshinda. Yeye ametiisha.” Na wakati alipoangalia pande zote kuona huyo Simba alipo, alimuona Mwanakondoo. Ajabu, anaangalia aone Simba na anamwona Mwanakondoo. Yule mzee alimtaja Yeye Simba. Lakini wakati Yohana alipotazama, aliona Mwanakondoo, “Mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Mwanakondoo aliyechinjwa. Ilikua ni nini? Huyo Mwanakondoo alikuwa nini? Alikuwa amelowa damu, amejeruhiwa. “Mwanakondoo aliyekuwa amechinjwa, bali alikuwa hai tena.” Naye alikuwa amelowa damu. Loo, jamani!

Mnawezaje kumwangalia Huyo, enyi watu, na ubaki mwenye dhambi? Mwanakondoo akatokea. Yule mzee akasema, “Simba ameshinda, Simba wa kabila ya Yuda.” Ndipo Yohana akaangalia amwone huyo Simba, na akaja Mwanakondoo, akatetemeka, amelowa damu, majeraha. Ameshinda tayari. Ungeweza kujua alikuwa vitani. Alikuwa amechinjwa, lakini alikuwa hai tena. Yohana hakuwa amemwona Mwanakondoo huyu hapo awali., unajua, hapa. Hakuwa ametajwa kabla. Hakuwa ametajwa mahali popote. Yohana hakumwona, kote Mbinguni alipokuwa akiangalia. Lakini huyu hapa anajitokeza.

Angalia mahali Yeye alipotokea. Alitoka wapi? Alitoka kwenye Kiti cha Enzi cha Baba, ambapo alikuwa ameketi tangu alipochinjwa na kufufuka tena. “Alifufuka na kuketi mkono wa kuume wa Mungu, akiwa hai siku zote ili atuombee.” Amina. Amesimama pale, leo, kama Mpatanishi, akiwa na Damu Yake Mwenyewe, kupatanisha juu ya ujinga wa watu. Sasa, huyo Ndiye ninayemtegemea. Bado Yeye alikuwa angali amefunikwa na kile kitakasaji, cha msamaha wa dhambi.

-----
Na, kumbukeni, jambo hili linakuja kwenye wakati wa saba wa kaniksa, wakati siri za Mungu zitakapofunguliwa. Sasa angalia kwa makini sana. Hili jambo unalopaswa kulipata. Sasa, Yeye amekuwa akifanya kazi Yake ya upatanisho, akimwombea mwamini. Kwa miaka elfu mbili aliyokuwa, Mwana-kondoo, huko nyuma. Sasa Yeye anatoka kuja kutoka katika Umilele, kukitwaa kile Kitabu cha hati miliki, na kuivunja ile Mihuri, na kuzifunua zile siri. Wakati gani? Kwenye wakati wa mwisho. Mnalipata? [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Vema, tutaendelea mbele basi. Sasa, kuvunja ile Mihuri na kuwafunulia siri zote, kumfunulia malaika wa saba, ambaye Ujumbe wake ni kufunua siri zote za Mungu. Siri za Mungu ziko kwenye hii Mihuri Saba. Unaona? Hivyo ndivyo Yeye alivyosema hapa. Siri zote ziko katika Mihuri Saba.

Naye Mwanakondoo anatokea sasa, anaacha kuwa Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu. Anakuwa Simba. Na wakati anapokuwa Simba, anakitwa kile Kitabu. Hizo ni haki Zake. Mungu alikishikilia, ile siri, lakini sasa yule Mwanakondoo anakuja. Hakuna mtu angeweza kukitwaa kile Kitabu. Kingali kiko katika mikono ya Mungu. Hakuna papa, kasisi, chochote kile, hawawezi kukitwaa (la) kile Kitabu. Ile Mihuri Saba haijafunuliwa. Unaona?

Lakini wakati, yule Mpatanishi, wakati kazi yake imekwishafanywa kama Mwombezi, anatokea. Na Yohana...Yule mzee alisema, “Yeye ni Simba.” Naye anajitokeza. Mwangalie. Loo, jamani! Unaona? Yeye anajitokeza kukitwaa kile Kitabu, sasa angalia, kuzifunua siri za Mungu, ambazo wengine wamezibuniabunia, katika nyakati hizi zote za kidhehebu.

Unaona, basi, yule malaika wa saba. Kama Kitabu hiki, siri, ni Neno la Mungu, yule malaika wa saba hana budi kuwa ni nabii, kujiwa na Neno la Mungu. Hakuna cha makasisi, mapapa, au chochote kile, kiwezacho kulipata; Neno haliwajilii watu kama hao. Neno la Mungu humjia nabii tu, daima.

Malaika 4 ilihaidi jambo hilo. Na wakati atakapotokea, atazichukua siri za Mungu, ambako kanisa lilikua limetatanikiwa kabisa katika madhebu haya yote, “Na kurudisha Imani ya watoto iwaelekee baba zao.” Na ndipo hukumu ya ulimwengu itashuka, na ulimwengu utachomwa moto. Halafu wenye haki watatembea juu ya majivu ya walio waovu, katika ule Utawala wa Miaka Elfu. 219 Mlipata jambo hilo sasa? Vema.

Wengine walikua wamelibunia jambo hilo, katika wakati wa kidhehebu. Lakini, unaona, hana budi kuwa ni mtu huyu, yule malaika wa saba wa...Ufunuo 10:1-4 ni nanii...Yule malaika wa saba amepewa siri za Mungu, na anamaliza siri zote ambazo ziliachwa, kote katika nyakati za kimadhehebu. Sasa unaweza ukaona ni kwa nini siwashambulii ndugu zangu walio katika madhehebu. Ni ule utaratibu wa kimadhehebu! Hawaninii, hawana haja ya kujitahidi kujua Hilo, kwa sababu halingeweza kufunuliwa. Hiyo ni kulingana na Neno. Walilidhania, na kuamini lilikuwapo, na kwa imani wakatembea Kwalo, lakini sasa limethibitishwa dhahiri. Amina. Loo, jamani, ni-ni Andiko la namna gani!

-----
Ni kitu gani? Sasa ni mali ya Mwanakondoo. Amina. Sheria za Mungu zilihitaji. Yeye ndiye anayekishikilia. Sheria ya Mungu ilihitaji Mkombozi aliye wa Jamaa wa Karibu. Ndipo Mwanakondoo akatokea, amekishika, “Mimi ni Jamaa yao wa Karibu. Mimi ni Mkombozi wao. Sasa mimi...Nimewafanyia upatanisho, na sasa niimekuja kudai haki zao kwa ajili yao.”Amina. Huyo ndiye peke yake. “Nimekuja kudai haki zao. Kwamba, wao wana haki ya kila kitu kilichopotea katika lile anguko, nami nimelipa ile gharama.” Loo, ndugu! Whiu! Hilo haliwafanyi kujisikia wa kiroho ndani? [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] “Si kwa kazi njema ambazo tumefanya, bali kwa neema Yake.” Loo, ngoja kidogo! Na hao wazee na kila kitu kinginecho wakaanza kutupa taji zao, na watu mashuhuri wakaanza kupomoka chini, unaona. Hakuna, hakuna mtu angeliweza kufanya jambo hilo.

Naye anakwenda moja kwa moja hadi kwenye mkono wa kuume wa Mungu, na kukitwaa kile Kitabu kutoka katika mkono Wake, na kudai haki Zake. “Nimewafia. Mimi ndiye Mkombozi aliye Jamaa yao wa Karibu. Ni mimi. Mimi ndimi Mpatanishi. Damu Yangu ilimwagwa. Nimefanyika Mtu. Nami nilifanya jambo hilo kusudi nilirudishe Kanisa hilo tena, lile nililoona kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Nimelikusudia. Nililinena, lingekuwako. Na hakuna mtu aliyeweza kukitwaa, bali nilishuka nikaenda nikafanya jambo hilo, Mimi Mwenyewe. Mimi ndiye Jamaa yao wa Karibu. Nilifanyika kuwa ndugu yao.” Ndipo anakitwaa kile Kitabu. Amina! Loo, Ni nani anayeningojea kule usiku wa leo? Ni nani Huyo, enyi kanisa, anayongojea Kule? Ni kitu gani kingine kingeweza kukungojea Kule? Yule Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu! Loo,jamani! Ni tamshi la fahari jinsi gani, ama tendo!.

Sasa yeye ana hati miliki ya ukombozi. Anayo katika mkono Wake. Upatanisho umekwisha. Anayo mkononi Mwake. Kumbukeni, ilikuwa imekuwa katika mkono wa Mungu, wakati wote, lakini sasa iko mkononi mwa Mwanakondoo. Sasa angalia. Hati miliki ya ukombozi, ya viumbe vyote, iko katika mkono Wake. Naye amekuja kuidai airudishe, pia, kwa ajili ya jamii ya binadamu. Si kuidai irudi kwa Malaika. Alidai iwarudie wanadamu, ambao walipewa hiyo, kuwafanya wana na binti za Mungu tena; kuwarudisha tena katika Bustani ya Edeni, kila kitu walichopoteza; viumbe vyote, miti, uhai wa wanyama, kila kitu kingine. Loo, jamani! Hilo haliwafanyi kujisikia wenye furaha?

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Pengo kati ya Nyakati Saba za Kanisa na Ile Mihuri Saba.



Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,

akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;

isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.

Ufunuo 10:5-7


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)
 

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)
Ambapo upanga ulionekana.

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.