Mabirika Yavujayo.
<< uliopita
ijayo >>
Chemchemi ya Maji ya Uzima.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mabirika Yavujayo.Ninataka kuzungumza usiku wa leo juu ya somo hili, kwa muda mfupi tu juu ya: Mabirika Yavujayo. Israeli walikuwa wamefanya maovu mawili makubwa. Mungu alisema walikuwa wamemwacha Yeye, Chemchemi ya Uzima, nao walikuwa wamejichimbia mabirika ya kunywea. Sasa, hilo ni jambo fulani. Sababu ya mimi kufikiria juu ya somo hili ilikuwa ni kwa sababu ingeenda sambamba na yale niliyokuwa nikisema asubuhi ya leo, ya saa tunayoishi, na Sababu tunayoshindania.
Nasi tunawaangalia Israeli kama mfano, kwamba, kile Mungu alichokuwa, daima hana budi kubaki vile vile. Na kuna jambo moja tu ambalo Mungu aliwahi kuheshimu, hilo lilikuwa, njia Yake ambayo aliandaa kwa ajili ya watu. Na wakati walipotoka nje ya njia hiyo, basi Mungu alitahayarishwa, na Mungu akawafanya watu wateseke kwa ajili ya kuyaacha yale aliyokuwa amewaambia wafanye, haidhuru ilikuwa ni nini. Yeye hata aliwapa sheria, “Usiguse, usishike, usionje.” Si tu kwa sababu ya uovu wa kufanya jambo hilo, bali uovu wa kutotii yale Yeye aliyosema wafanye. Na daima hakuwezi kuwa na sheria bila adhabu kwa sheria. Kwa sababu, kama hakuna adhabu, basi, sheria si muhimu kwake isipokuwa iwe na adhabu. Torati!
Sasa, tunaona, yale waliyofanya katika siku hiyo yanaonekana sambamba na yale tunayofanya leo, yale watu wa kanisa wanafanya. Sasa tunaona jambo la ajabu hapa. Huenda likawa ni jambo geni kwa watu fulani, wakati Yeye aliposema, “Ninyi, wao, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo.” Sasa, labda baadhi yenu hamjui birika ni nini. Ni wangapi wanaojua birika ni nini? Vema, karibu ninyi nyote. Kama uliwahi kulelewa shambani, unajua birika ni nini. Ninakumbuka nimekunywa wadudu wa kutosha kutoka kwenye moja, kujua ninii birika. Nimehubiri nchini ambapo, kwenye miti ya vivuli, ambapo ungekuwa na mtungi mkubwa wa maji ya birika uliowekwa pale, nje ya mvua, mwajua, na kwa namna fulani yalikaa sana. Na halafu wadudu, wakati wa usiku, wangeingia mle. Na kwa hiyo ninajua maji ya birika ni nini.
Birika ni mahali, kitu kilichochimbwa ardhini, kuchukua mahali pa kisima. Ambapo watu hawana kisima, basi wanapata birika. Kwa maneno mengine, birika ni tangi la kujitengenezea ama kisima kilichotengenezwa na mwanadamu ardhini, ambacho mtu anachimba, kuchota maji, kuyatumia. Baadhi yao huyatumia kwa maji ya kuoshea, na wengine huyatumia kama maji ya kunywa, na kwa njia mbalimba, labda. Maji yote wakati mwingine, tuliyozoea kuyapata, yalikuwa kwenye birika. Tulikuwa na kitu cha kale ambacho ilikubidi kuzungusha, na kuzungusha, na kuzungusha, na kuzungusha, na kuzungusha, kuyavuta maji; kilifungiwa ndoo ndogo, kuyavuta maji hayo kutoka kwenye hilo birika.
Vema, tunaona jambo moja kuhusu birika ambalo ni tofauti na kisima. Sasa, birika litakuwa tupu. Birika haliwezi kujijaza lenyewe. Ni... Halitumainiki. Huwezi kutumainia birika. Halina budi kutumainia na kutegemea mvua zinazonyesha katika majira ya kiangazi ama katika majira ya kipupwe, vyovyote itakavyokuwa... Kwa kawaida, katika majira ya kipupwe wakati theluji na mvua zinapokuja, basi maji hutiririka kwenye birika. Na kama halipati maji hayo, basi huna maji yoyote. Yote... yanakauka. Wala haliwezi kujijaza lenyewe. Birika hilo la kale haliwezi kujijaza lenyewe. Linapata kujaa kwake kutokana na mvua zinazonyesha.
-----
Kwa hiyo, kweli ulikuwa na uchafu hapo ulipokuwa na birika chafu la kale. Ukiyaacha maji hayo yasimame kwenye birika, yanakuwa maji yaliyooza. Ndipo yanajaa vyura, na mijusi, na nyoka. Nasi tulizoea kuwaita “vifurukuta-mikia,” ninii wadogo... Sijui kama... Wao si kimelea, wao ni... Siwezi, sijui ungewaitaje. Bali vitu vidogo vinaingia majini, ambavyo tuliita vifurukuta-mikia. Mnajua ni kitu gani. Ni wangapi wanaojua ninachozungumzia? Loo, mbona, bila shaka, nyote mnaotoka mashambani mnajua. Mkiyafanya kuoza sana, na basi hawa wanaopenda maji yaliyooza wanaambatana nayo. Kwa kweli huja tu, kwa sababu maji yameoza. Na kwa sababu yameoza, yanawavutia wanyama mle wanaopenda vitu vilivyooza.Na hiyo ni kama makanisa yetu siku hizi. Nafikiri kwamba tumeacha... Moja ya dhambi kubwa mno ambazo makanisa yametenda leo, kama Israeli wakati huo, yalimwacha Yeye, Chemchemi ya Maji ya uzima, na kujichimbia mabirika ya kujitengenezea. Nayo yanakuwa makao ya kila kitu kinachopenda maji ya namna hiyo. Mijusi, vyura, na viini vichafu vya kila namna, vinaishi mle ndani, kwa maana ni tanki la kujitengenezea. Na katika tanki hili ambamo vitu hivi vinaishi, ni mfano mkamilifu wa madhehebu yetu leo.
“Sasa,” unasema, “Ndugu Branham, kwa nini unawashambulia sana watu hao?”
Inapaswa kuwashambulia. Haina budi kushambuliwa. Yatorokeni, kwa maana hatimaye yatafanyika ile alama ya mnyama. Kumbukeni, hiyo ni Kweli! Yatakuwa ni alama ya mnyama. Madhehebu yataongoza moja kwenye kitu hicho. Yamo njiani yakielekea kule sasa, kulazimisha, kwa kutumia nguvu. Angalia katika milki ya kale ya Kirumi. Jambo hilo ndilo hasa liliwaongoza kwenye ile alama ya ukengeufu. Mliona ya kwamba hakuna mtu angeweza kununua wala kuuza bila alama ya mnyama. Ilimbidi awe nayo.-----
Wanakiacha kisima kinachofoka maji, wakaziendea taratibu za kujitengenezea ama birika, ungeweza kuwazia mtu fulani akifanya hivyo? Ungewazia jinsi ilivyo akili ya mtu ambaye angekunywa maji matamu ya kisima kinachofoka maji, kisha ayaache hayo akanywe ya birika la kujitengenezea lenye vyura, na mijusi, na vifurukuta-mikia, na kila kitu ndani yake?
Haionekani kuwa ni jambo la busara kuwa sahihi, bali hivyo ndivyo hasa watu wamefanya. Wameacha Neno, Chemchemi ya kweli ya chanzo na Nguvu za Mungu, kunywa kutoka kwenye mabirika, na kujifanyia mabirika. Kama vile walivyofanya wakati huo, wamefanya hivyo sasa. Wanasema... Yeye alisema, “Wameniacha.” Hapa alisema, hapa katika Yeremia 2:14, ama 13, hasa.
Yeye alisema, “Wameniacha mimi, Niliye Chemchemi ya Maji ya uzima.”Sasa, tunaona birika ni nini. Tunaona kile inachokinga. Tunaona jinsi inavyotengenezwa. Ni kitu cha kujitengenezea ambacho kinatoka kwenye paa chafu. Yale maji yanayomwagika chini, hugonga kwenye paa lililo chafu, kisha yanatiririka tu kutoka kwenye paa, yanapitia kwenye kihori cha kujitengenezea, yanapitia kwenye mfuko wa kujutengenezea yakaingia katika tanki la kujitengenezea. Na uchafu wote unarundikana mle, na viini vya magonjwa, na mijusi, na vyura, na vitu vya ardhini, namna hiyo. Na, tazama, wao ni wanyama walio wachafu; vifurukuta-mikia, maji yaliyooza. Kifurukuta-mkia hakiwezi kuishi katika maji masafi. Kama kikiishi, yangekiua. Hakina budi kuwa katika maji yaliyooza.
Na hivyo ndivyo ilivyo na vimelea hivi vingi leo. Humwezi kuishi katika maji safi ya Roho Mtakatifu. Hiyo ndiyo sababu wao wanapinga Neno kwa nguvu, na kusema, “Linajinga Lenyewe. Hakuna kitu Kwake.” Ni kwa sababu hawana budi kuwa na namna fulani ya kidimbwi chenye maji yaliyooza kufurukutia mle. Sawa.
Hivyo ndivyo ilivyo na vyura, na kwa mijusi, na kwa viluwiluwi, na vitu kama hivyo. Hawana budi kusogea kwenye bwawa ama kidimbwi chenye maji yaliyooza, wapate kuishi, kwa maana asili yao ni kuishi mle. Wala huwezi kumbadilisha mnyama mpaka ubadilishe asili yake.
Wala huwezi kumfanya mtu alione Neno la Mungu mpaka asili yake imebadilishwa; na wakati asili yake imebadilishwa kutoka alivyo, akawa mwana wa Mungu, na Roho Mtakatifu anaingia ndani yake. Roho Mtakatifu aliandika Neno la Mungu!-----
Malalamiko yake yalikuwa, “Wameniacha Mimi, Neno; nao wamekubali birika livujalo, badala yake. Wamekubali... Wameniacha mimi, Niliye Chemchemi ya Uzima, Chemchemi ya Maji ya Uzima; nao wanatamani na wanaona afadhali kunywa kutoka kwenye birika lenye maji yaliyooza.” Ungeweza kuwazia jambo hilo?
Ungeweza kuwazia mtu sasa, ambaye, hapa kuna kisima kinachofoka maji kinachotoa tu maji hayo mazuri, yatokayo kwenye mawe ya chokaa, moja kwa moja kutoka katikati ya miamba, huko chini kwenye matuta ya mchanga, na kadhalika, baridi tu na nzuri kama iwezavyo kuwa; na anaona afadhali anywe kutoka kwenye birika kule, ambayo yametitririka kutoka juu ya ghala, na mabanda, na majengo yote ya nje kuzunguka mahali hapo? Na kuyaweka kwenye birika hilo pale, ambapo maji yanayopenya huchuruzikia mle, kutoka kwenye ghala ya nafaka, na maboma na mazizi, na kila kitu kikichuruzikia kwenye hilo birika, halafu tunataka kuku-... tungenywea hilo kabla hatujaenda kwenye hicho kisima kinachofoka maji? Kutakuwa na kasoro fulani kiakili kwa mtu huyo. Hiyo ni kweli.Na wakati mwanamume ama mwanamke atachukua msimamo wa madhehebu, yatakayoruhusu kukata nywele, kuvaa kaptura, vipodozi, kila namna ya hivi vitakataka vingine, na namna fulani ya mpango, na kufanya mambo haya yote yasiyofaa, na anaweza kwenda kwenye mchezo wa matufe, na upuzi huu wote kule, na anaweza kuvumilia mambo hayo; na kupenda hayo vizuri kuliko wanavyolipenda Neno la Mungu la mtindo wa kale ambalo hukata na kuchimba, na kuwafanya wanawake mabibi, na linawachukua na kuwafanya wavalie vizuri na kuenenda vizuri, linaondoa sigara na tumbaku, na kuapa na kulaani, na kudanganya na kuiba, mbali nawe, na ulimwengu wote kukutoka, na likakupa Kitu ambacho kinaridhisha kabisa. Kwa nini mwanamume ama mwanamke anaenda kwenye kitu kama hicho kwa ajili ya faraja? Unawezaje kupata faraja kutokana na jambo hilo?
-----
Watu wa siku hizi za mwisho wamemwacha, Neno la kweli, Maji ya Uzima; na wamejichimbia mabirika ya kimadhehebu; na, tena, wakachimba, walichimba!... Na sasa tunaona, wamekuwa na mabirika yaliyovunjika. Na ndipo birika hili limejazwa na vijidudu visivyoamini, majivuno yasiyoamini, mipango ya elimu, na kadhalika, ambayo ni kinyume cha ahadi za Mungu. Wao ni wanaoshuku Neno.Sasa, mabirika haya waliyo nayo, Biblia ilisema, yalikuwa “yanavuja.” Birika lililovunjika ni birika “linalovuja,” na linamwaga maji. Yanafanya nini? Yanaingia kwenye dimbwi la uchafu la kidini linaloitwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Na hapo ndipo birika linalovuja linapowaongoza, kwa sababu tu wamemwacha, na wame... Chemchemi ya Maji ya uzima; na kujifanyia mabirika haya. Wanachimba miradi mikubwa ya seminari ya masomo, elimu, na kadhalika. Hiyo ndiyo aina ya mabirika wanayochimba leo, ambapo mtu hana budi kuwa na Ph.D., ama LL.D., ama Shahada ya Sanaa, ama kitu fulani, kabla hata hajaenda kuhubiri. Mabirika ambayo yamejazwa na theolojia ya kujitengenezea. Wao wanawapeleka katika shule hizi kubwa mno za masomo, na humo wanawadunga kwa theolojia za kujitengenezea, na kuwatuma na hizo. Ni siku ya jinsi gani tunayoishi, mabirika ya kujitengenezea! Hakuna shida... Si ajabu kitu hicho kimekuwa ni ki— uvundo, loo, jamani, ni kwa sababu watu wananywea humo.
Na wakati watu wanapotaka furaha leo, wanafanya nini? Watu, badala ya kuikubali furaha ya Bwana, wanageukia dhambi, kwa furaha. Watu wanaokwenda kanisani na kudai kuwa ni watumishi wa Kristo, wanapopata wasiwasi sana watawasha sigara. Na wakati wao— wakati wao wanataka kujifurahisha, wanavaa nguo zao chafu na kutoka nje wakakate nyasi wakati wanaume wanapita, kusudi wawafanye wawapigie mruzi. Wanafanya kila kitu wapate kupendwa na watu. Wanataka kuonekana kama nyota wa sinema. Hiyo ndiyo furaha yao.
Wakati, Yesu alisema, “Mimi ndimi utoshelevu wao.”Sababu ya wao kwenda kwenye jambo hilo, ni kwa sababu hawataki kunywa kutoka kwenye Chemchemi hiyo. Wameikataa. Hawataki kuinywa. Wamejiunga na namna fulani ya taratibu za kujitengenezea, namna fulani ya birika iliyojaa namna zote za vitu vilivyooza, waweze kwenda hivyo.
-----
Sasa katika kufunga, huenda nikasema jambo hili. Kila kilicho tofauti na Hiki ni mabirika yavujayo, na hatimaye yatamwaga yale utakayotia ndani yake; kama unaweka matumaini yako yote, wakati wako wote, na kila kitu, katika moja ya hayo mabirika yaliyooza. Yesu alisema ya kwamba yalikuwa mabirika yavujayo. Mungu alisema, “Yanavuja, yatamwaga cho chote unachotia ndani mwao.” Huwezi kuendelea mbele zaidi nayo, kwa maana yatamwaga cho chote unachotia ndani. Kwa maana Yeye ndiye njia pekee ya kuelekea kwenye ile Kweli, kwenye Uzima, hata furaha ya Milele, na amani ya Milele. Yeye ndiye tu peke Yake na njia pekee ya kwenda Kule. Loo, jamani!Chemchemi isiyoisha ya Uzima ni Yesu Kristo. Kwa nini? Na Yeye ni nani? Neno, lile lile; Neno, Uzima, Chemchemi, “yeye yule jana, leo, na hata milele.” Mwamini wa kweli, ni furaha yake kuu, Uzima wake mkuu. Na kuridhika kwake ku kuu ni katika Kristo. Hakuna kusukuma, hakuna kuvuta, hakuna kujiunga, hakuna dhamana; kuamini tu na kupumzika. Hivyo ndivyo alivyo kwa waaminio.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mabirika Yavujayo.