Maono ya kuzimu.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Nafsi zilizo kifungoni sasa.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Nafsi zilizo kifungoni sasa..

Halafu basi nilikuwa huko nje nikiwinda wakati mmoja, ambayo inaonekana kuwa ni tabia ya pili kwangu, kupenda kuwinda. Nami nilikuwa huko nje nikiwinda na mvulana fulani, Jim Poole, mtoto mzuri. Nafikiri mvulana wake huja kanisani hapa, Jim mdogo, na familia nzuri ya watu. Ninawajua akina Poole. Mimi na Jimmy tulilala pamoja na kuishi pamoja tangu tulipokuwa wavulana wadogo shuleni. Tuna tofauti ya miezi sita, katika umri. Basi Jimmy aliachilia bunduki yake ikafyatuka, nayo ikanipiga risasi katika miguu yote miwili, akiwa karibu sana nami, kwa bunduki. Nilipelekwa hospitalini, na, kule, nikilala kule nikifa, hakukuwa na penicilini wala cho chote katika siku hizo. Naam, sasa, wao waliniwekea kitambaa cha mpira chini, nami najua usiku huo... Walikuwa wanifanyie upasuaji asubuhi yake.

Walichukua tu na kulisafisha lile jeraha, huku vipande vikubwa vya nyama vimelipuliwa, nao wangechukua mkasi na kuvikata, nami ilinibidi kushikilia mikono ya mwanamume fulani... Nao iliwabidi kushikilia, kukwatua mikono yangu kutoka kwenye viwiko vyake, walipo—walipomaliza. Nilipaza sauti na kulia, huku nimeshikilia namna hiyo, nao wakikatilia mbali sehemu hiyo ya mguu. Nilikuwa na umri wa miaka kumi na minne, mvulana tu.

Na usiku huo nilijaribu kulala, nao... Niliamka, kitu fulani kama maji kilianguka. Basi damu ikatoka, karibu nusu galani, nakisia, ilitoka kwenye hizo vena. Nao walikuwa na... walipiga X-ray, nao wakasema ile risasi ilikuwa imekaa karibu sana na mshipa wa damu, pande zote mbili, hata mkwaruzo mdogo tu ungeukata moja kwa moja sehemu mbili, nami ningeanza kutokwa na damu. “Vema,” nikawaza, “huu ndio mwisho wangu.” Ndipo nikaweka mikono yangu chini namna hii na kuuinua, huku damu inatiririkia mikononi mwangu, nilikuwa nimelalia damu yangu mwenyewe. Nikaita, nikapiga kengele. Nesi akaja, naye akaipanguza tu kwa taulo kwa maana wasingeweza kufanya kitu.

Basi asubuhi yake, katika hizo hali za kudhoofisha, hawakuwekea damu siku hizo, mwajua, kwa hiyo wao wakanifanyia upasuaji. Ndipo wakanipa nusukaputi. Na wakati mimi... Ile nusukaputi ya kale, nadhani mnakumbuka, ilikuwa nusukaputi ya kale. Basi nilikuwa kwenye nusukaputi hiyo, nilipopata fahamu, nilikuwa ninatoka kwenye nusukaputi hiyo baada ya masaa manane. Iliwabidi kunipa nyingi sana, walifikiri nisingeweza— nisingeweza kuamka. Wasingeweza kuniamsha.

-----
Ninakumbuka Bibi Roeder alisimama karibu nami, huko nje hospitalini... Nilipotoka kwenye nusukaputi hiyo, kuna jambo fulani lililonipata pale. Daima nimeamini kuwa ni ono. Maana, nilikuwa dhaifu sana, nami... Walidhani nilikuwa nakufa. Alikuwa analia. Nilipoyafungua macho yangu kuangalia, niliweza kumsikia akizungumza, ndipo nikarudi usingizini, kisha nikaamka, mara mbili tatu. Halafu basi nikapata ono wakati huo. Na ndipo nilikuwa...

Yapata miezi saba baadaye, ilinibidi kwenda na kutolewa pamba kwenye jeraha za risasi na nguo za kuwindia zenye grisi miguuni mwangu; yule daktari hakuzitoa. Na kwa hiyo damu ikapata sumu, miguu yote miwili ilikuwa imevimba na kukunjamana chini yangu, nao walitaka kuikata miguu yote miwili kwenye viweo vyangu. Nami ninaninii tu... Nikasema, “La, sogeeni juu zaidi mkaikatie hapa juu.” Singeweza kuvumilia jambo hilo, mnaona. Na kwa hiyo hatimaye, Daktari Reeder na Daktari Pirtle, kutoka Louisville, walinifanyia upasuaji, wakaikata mle ndani wakaitoa; na siku hizi nina miguu mizuri sana, kwa neema ya Mungu.

-----
Sasa katika wakati huu, kama nilivyokuwa na ono hili, na nikifikiri ya kwamba nilikuwa nimepita kutoka maisha haya nikaingia katika mateso. Na miezi saba baadaye, hapa katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Kaunti ya Clark, nilifanyiwa upasuaji wa pili. Na wakati huo, nilipotoka, nilifikiri nilikuwa nimesimama huko Magharibi. Nilikuwa na ono lingine. Na kulikuwa na msalaba mkubwa wa dhahabu angani, na Utukufu wa Bwana ukitiririka kutoka kwenye huo msalaba. Nami nilisimama nimeinua mikono yangu hivi, na huo Utukufu ulikuwa ukiangukia kifuani mwangu. Nami... Ono hilo liliniacha. Baba yangu alikuwa ameketi pale akiniangalia, wakati lile ono lilipokuja.

Daima nimejisikia, ninyi... Watu wote wanaonijua miaka hii yote, wanajua daima nimetaka kwenda Magharibi. Unajua jinsi ilivyo. Daima limekuwa jambo fulani kuelekea Magharibi. Lakini kwa sababu mtaalam wa nyota aliniambia wakati mmoja, jambo lile lile, ya kwamba ninapaswa kwenda magharibi... Nyota, wakati zinapovuka duara zao na kadhalika, nilizaliwa chini ya ishara hiyo, wala sitafanikiwa kamwe Mashariki; sina budi kwenda Magharibi. Basi mwaka uliopita nikaondoka nikaenda, Magharibi, kutimiza kile kimekuwa hamu yangu maishani, mnaona, kufanya jambo hilo.

-----
Basi baada ya hilo ono kunijia, nami nilikuwa mdhaifu sana, na nilikuwa nimepoteza damu hiyo yote, kisha nikaenda... Nilifikiri ninatumbukia katika Umilele usio na mwisho. Wengi wenu mmenisikia nikisimulia jambo hili hapo kabla, huku—huku ninatumbukia katika Umilele usio na mwisho. Kwanza, nilikuwa nikipitia kwenye kitu kama mawingu, kisha katika giza, halafu nikazama chini, chini, chini. Basi muda si muda, nikafikia kwenye nchi ya waliopotea, ndipo mle ndani nikalia kwa sauti kuu. Ndipo nikaangalia, na kule, kila kitu tu, hapakuwepo na msingi juu yake. Nisingeweza kamwe kuacha kuanguka. Ilivyoonekana, ningeendelea kuanguka Milele. Hapakuwepo na kikomo, mahali po pote.

Halafu basi ilikuwa ni tofauti jinsi gani na lile ono nililokuwa nimeona hapa, si muda mrefu uliopita, la kuwa Utukufuni pamoja na wale watu, [Kifo. Ni nini basi?] ile tofauti! Lakini katika jambo hili, nilipokuwa ninaanguka, hatimaye, nikamlilia baba yangu. Bila shaka, nikiwa mtoto tu, hivyo ndivyo ningefanya. Nikamwita baba yangu kwa nguvu, naye baba yangu hakuwa kule. Nami nikapaza sauti kwa ajili ya mama yangu, “Mtu fulani anishike!” Hakukuwa na mama pale. Nilikuwa tu nikienda. Nami nikamfokea Mungu kwa sauti kuu. Hakukuwako na Mungu pale. Hakukuwa na kitu pale.

Ndipo baada ya kitambo kidogo nikasikia sauti ya maombolezi sana niliyopata kusikia, nako kulikuwa ni kujisikia kubaya sana. Hakuna njia... Hata moto wenyewe unaowaka ungekuwa ni faraja ukilinganisha na jinsi hali hii ilivyokuwa. Sasa maono hayo hayajakosea kamwe. Nako kulikuwa kumoja kwa kujisikia kubaya sana nilikowahi kujisikia, na kile...

Nikasikia kelele fulani, ilisikika kama namna fulani ya hali ya kuzuriwa na pepo. Basi wakati iliposikika, nikatazama, wakija, na ilikuwa ni wanawake. Nao walikuwa wamejipaka rangi ya kijani kibichi, ningeweza tu kuona nyuso zao, nao walikuwa na vitu vyenye rangi ya kijani kibichi chini ya macho yao. Na macho yao yalionekana kana kwamba yamerudi nyuma, kama vile wanawake siku hizi wanavyoyapodoa macho yao, yakarudi nyuma namna hiyo, na ni macho yao tu na uso. Nao walikuwa wakisema “Uui, uui, uui, uui!” Loo, jamani!

Nikapaza sauti tu, “Ee Mungu, unirehemu. Kuwa na rehema, Ee Mungu! Uko wapi? Kama utaniruhusu tu kurudi na kuishi, ninakuahidi, kuwa mvulana mzuri.” Sasa, hilo ndilo jambo pekee ningeweza kusema. Sasa, Mungu anajua, na kwenye Siku ya Hukumu, Yeye atanihukumu kwa ajili ya tamshi hilo. Hivyo ndivyo nilivyosema, “Bwana Mungu, hebu nirudi, nami nitakuahidi nitakuwa mvulana mzuri.”

Basi nilipopigwa risasi, nilikuwa nimesema uongo, nilikuwa nimefanya karibu kila kitu kinachoweza kufanywa, ni jambo moja tu ninalosema... Afadhali niliseme wazi wakati niko papa hapa sasa. Basi nilipoangalia kule chini na kuona nilikuwa nimelipuliwa nusu vipande viwili, karibu vipande viwili, nilisema, “Mungu, nirehemu. Unajua kamwe sikufanya uzinzi.” Hilo ndilo jambo pekee nililoweza kumwambia Mungu. Sikuwa nimekubali msamaha Wake, na mambo haya yote. Ninasema tu, ningeweza kusema, “Sikufanya uzinzi kamwe.”

Na ndipo wakanipeleka kule. Halafu basi, katika jambo hilo, nililia, “Mungu, unirehemu. Nitakuwa mvulana mzuri, kama tu utaniruhusu kurudi,” kwa kuwa nilijua kulikuwa na Mungu mahali fulani. Na kwa hiyo nisaidie, hao viumbe wa kutaabisha walikuwa kila mahali, mimi nilikuwa mgeni aliyewasili hivi punde tu. Basi kujisikia kwenye kuchukiza kupindukia, kuogofya kupindukia, uovu mbaya kupindukia ambao... Ilionekana kama macho makubwa mno, kope kubwa zimetokeza namna hiyo, na zimerudi nyuma kama za paka, nyuma namna hii; na vitu vya rangi ya kijani kibichi, kama kwamba vilikuwa vimeoza ama cho chote kile. Nao walikuwa— walikuwa wanasema, “Uui, uui, uui!” Loo, ni kujisikia kulikoje! Sasa wakati mimi...

Basi katika dakika moja, nilikuwa nimerudi kwenye maisha ya kawaida. Kitu hicho kimenisumbua. Niliwaza, “Loo, hebu iwe kwamba sitaenda mahali kama hapo tena; pasitokee mwanadamu mwingine atakayelazimika kwenda mahali kama hapo.”

Miezi saba baadaye, nilipata ono la kusimama kule Magharibi, na kuona msalaba ule wa dhahabu ukinishukia. Nami nikajua ya kwamba kulikuwa na nchi ya waliolaaniwa mahali fulani.

Naam, sikuona jambo hilo sana mpaka yapata majuma manne yaliyopita. Mke wangu... Kamwe sikuwazia jambo hilo katika masharti haya. Yapata majuma manne yaliyopita, mimi na mke wangu tulishuka kwenda Tucson, kufanya manunuzi. Na tulipokuwa tumeketi... Mke wangu, tulishuka kuingia kwenye orofa ya chini, na kulikuweko na kundi la wavulana walioonekana kama dondoadume waliokuwa wamesokota nywele zao, mwajua, kama wanavyofanya wanawake, na kukatwa nywele mraba kwenye paji la uso, wamevalia hizi suruali ndefu walizopandisha juu sana, kwa namna fulani, nafikiri ni bitiniki, ama cho chote kile mnachoziita....

Kwa hiyo nikaenda kwenye orofa ya juu, na nikaketi chini. Basi nilipofanya hivyo, kulikuwa na kipandio, ilikuwa ni duka kubwa la J.C. Penny, nacho hicho kipandio kikiwapandisha watu. Vema, kweli nilichefuka tumboni mwangu, kuona hao wanawake wakipanda kuja kule; vijana, wazee, na wasiojali, wenye makunyanzi, vijana, na kwa kila njia, wamevalia vikaptura vidogo; miili yao najisi, na hao wanawake waliovalia kizinifu, wakiwa na nywele hizo kubwa mno namna hiyo, basi hawa hapa wanakuja. Basi mmoja anakuja moja kwa moja kutoka kwenye kipandio hicho, akija tu moja kwa moja namna hiyo, mahali nilipokuwa nimeketi kule nyuma kitini, nimeketi kule huku nimeinamisha kichwa changu.

Ndipo nikageuka na kuangalia. Na mmoja wao alipokuwa anakuja kwenye vile vipandio alikuwa anasema, “Uui,” akizungumza Kihispania, na mwanamke mwingine. Alikuwa mwanamke mweupe akinena na mwanamke wa Kihispaniola. Na nilipoangalia, [Ndugu Branham anadata kidole chake — Mh.] Mara nikabadilishwa. Hapo, nilikuwa nimeona jambo hilo hapo awali. Macho yake, mnajua vile ambavyo wanawake wanafanya siku hizi, kupodoa macho yao, hivi majuzi tu, kama paka, mnajua wanajipaka juu namna hii, huku wanavaa miwani ya paka na kila kitu, mnajua, huku macho yao yako hivi, na kitu kile cha kijani kibichi chini ya macho yao. Hicho hapo kile kitu nilichoona nilipokuwa mtoto. Huyo hapo yule mwanamke vile vile ilivyokuwa kabisa. Nami nikafa ganzi mwili mzima, kisha nikaanza kuangalia kila mahali, na palikuwepo na watu wale wakinong'oneza, mnajua, wakiongea juu ya bei na kadhalika katika lile jengo.

Ilionekana kana kwamba nilibadilika tu kwa muda kidogo. Nami nikaangalia, na nikawaza, “Hilo ndilo nililoona kuzimu.” Hao hapo, kuoza kule. Nilifikiri kilichowafanya wawe namna hiyo ni kwa kuwa walikuwa kuzimu, kitu fulani cha kijani kibichi na samawati chini ya macho yao. Na hapa kulikuwa na wanawake hawa waliopakwa rangi ya kijani kibichi, jinsi tu lile ono lilivyosema yapata miaka arobaini iliyopita.

Mnaona, yapata miaka arobaini iliyopita, ndivyo ilivyokuwa. Nina umri wa miaka hamsini na minne; Nilikuwa na umri wa miaka kumi na minne. Kwa hiyo yapata miaka arobaini iliyopita, mimi... Na hiyo ni ninii —ninii... Hiyo ndiyo namba, hata hivyo, ya hukumu, mnaona.

-----
Niliwaza wakati huo, nilipoyatazama hayo macho yanayoonekana yameoza ya wanawake hao. Kulikuweko na Wahispania, Wafaransa, na Wahindi, na watu weupe, na wote pamoja, lakini hizo nywele kubwa mno, mwajua, zilizochanuliwa, na vichanuo hivyo, jinsi wanavyozilaza kwa nyuma, kubwa mno, kisha zinatokeza nje. Mwajua, mnajua jinsi wanavyofanya jambo hilo, kuzitengeneza kama wanavyofanya. Halafu macho hayo yanayoonekana kana kwamba yameoza, na yale macho yaliyopodolewa, yanayorudi nyuma kama macho ya paka. Nao wakizungumza, nami huyo pale tena, nikisimama pale katika duka kubwa la J.C. Penney, nimerudi kuzimuni tena. Niliogopa sana. Nikawaza, “Bwana, hakika sijakufa, na Wewe umeniacha nije mahali hapa hata hivyo.”

Basi hao hapo, wakifanya... wanazunguka namna hiyo, kama vile katika ono lile, ilikuwa tu ni vigumu kusikia kwa maskio yako, mnajua. Kunong'ona tu na kuendelea, kwa watu, na hao wanawake wakipanda kwa kipandio hicho na kwenda kila mahali pale, na ile “Uui, uui!” Hayo hapo macho ya kijani kibichi, ya kuchekesha, na ya maombolezo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Nafsi zilizo kifungoni sasa..


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

Waebrania 9:27


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Pillar of Fire.

(PDF Kiingereza)

Mungu Akijificha
Kwa Urahisi...
(PDF)

Ndoa Na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.