Utungu wa Kuzaa.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Mbingu mpya na Nchi mpya.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Utungu wa Kuzaa.

Sasa, nataka kuzungumza alasiri ya leo juu ya somo nililotangaza: Utungu wa Kuzaa. Sasa, hilo linasikika baya sana, bali liko katika Biblia. Ninaamini ya kwamba Yesu hapa alikuwa akinena habari zake, kama Yeye alivyosema, “Mtakuwa na huzuni, bali huzuni yenu itageuka kuwa furaha,” akizungumza na wanafunzi Wake hapa, akijua ya kwamba kuzaliwa kwa Ukristo kulikuwa kunakuja. Na sasa mambo ya kale hayana budi kufa, kusudi yaliyo mapya yapate kuzaliwa. Kuwa na cho chote kinachozaa, haina budi kuwa na maumivu ya taabu. Na bila shaka walikuwa watapitia katika uchungu wa dhiki na maumivu makuu, kutoka kwenye torati kuingia katika neema.

Kawaida, uzazi wa kawaida ni mfano wa uzazi wa kiroho. Mambo yote ya kawaida ni mfano wa yale ya kiroho. Nasi tunaona, kama tukiangalia hapa nje kwenye ardhi, na kuona mti katika nchi, ukikua, ukishindania uzima. Hiyo inaonyesha ya kwamba kuna mti, mahali fulani, ambao haufi, kwa sababu unalilia jambo fulani. Tunaona watu, haidhuru wao ni wakongwe namna gani, ni wagonjwa jinsi gani, wana hali gani, wanalia, wapate kuishi, kwa kuwa inaonyesha kuna uhai mahali fulani ambapo tunaishi milele. Angalia jinsi lilivyo kamilifu.

Sasa, katika Yohana wa Kwanza 5:7, ninaamini ndivyo ilivyo, kama sijakosea, ilisema, “Wako watatu washuhudiao Mbinguni: Baba, Neno, na Roho Mtakatifu; hawa watatu ni Mmoja. Kuna watatu washuhudiao duniani, ambao ni maji, Damu, na Roho, nao wanakubaliana katika mmoja.” Sasa angalia. Hao watatu wa kwanza ni Mmoja. Hao watatu wa pili ni wa duniani, ambao hupatana kwa habari moja. Huwezi kuwa na Baba bila Mwana; huwezi kuwa na Mwana bila kuwa na Roho Mtakatifu. Lakini unaweza kupata maji bila Damu, na Damu bila Roho.
Nafikiri, kote katika nyakati zetu, hii imethibitika kwamba ni kweli; maji, Damu, Roho; kuhesabiwa haki, utakaso, ubatizo wa Roho Mtakatifu. Hiyo hufananishwa au inafanya ninii... au, na kivuli, ambayo hondoa kutoka kwenye kuzaliwa kwa maumbile.

Angalia wakati mwanamke ama cho chote kile katika utungu wa kuzaa, kwa ajili ya kuzaa. Jambo la kwanza linalotukia, ni kutoka kwa maji, kuzaliwa kwa kawaida; jambo la pili ni damu; halafu uhai unatokea. Maji, damu, roho; na hiyo hufanya kuzaliwa kwa kawaida, kwa maumbile.

Na ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa kiroho. Ni maji; kuhesabiwa haki kwa imani, kumwamini Mungu, kumpokea kama Mwokozi wako binafsi, na kubatizwa. Pili, ni utakaso wa roho, kwamba Mungu husafisha roho kutoka kwenye vitu vyote vya ulimwengu, na tamaa ya ulimwengu. Na ndipo Roho Mtakatifu anaingia na kutoa Uzao mpya na kukijaza chombo hicho kilichotakaswa.

Kwa mfano, namna hii. Sasa, hilo, niliwaambia. Kile usichoamini, weka kando, kisha ule sambusa. Angalia. Sasa, glasi iko kwenye ua wa kuku. Huichukui tu hiyo na kuiweka mezani mwako na kuijaza na maji ama maziwa. La. Unapoichukua, ni kuhesabiwa haki. Ukiiosha, ni kuitakasa, maana neno la Kiyunani kutakasa ni neno lenye sehemu mbili, ambalo linamaanisha “kuoshwa, na kutengwa kwa ajili ya kutumika.” Si katika utumishi; kwa ajili ya huduma. Halafu unapoijaza, inawekwa katika huduma.

Samahani kwa jambo hili sasa, sio kuumiza. Hapo ndipo ninyi Wapilgim Holiness, Wanazarayo mlishindwa kupiga hatua mpaka kuingia kwenye Pentekoste. Mlisafishwa kwa kutakaswa; lakini mlipokuwa tayari kuwekwa katika huduma, kwa karama za kunena katika lugha na vitu vingine, mlizikataa hizo, mkarudi zizini tena. Mnaona? Sasa, hilo ndilo linalotukia. Daima hufanya hivyo. Sasa, si kuwalaumu ninyi sasa, lakini ninii—ninataka kutoa jambo hili moyoni mwangu. Na hilo limekuwa likinichoma tangu nilipokuwa hapa, kwa hiyo ni heri nilitoe. Ninii tu, kama neema ya Carl, na Demos na hao wengine, na yenu nyote, nitajaribu kukomboa nafsi yangu kutokana na jambo hilo, unaona, ndipo basi ni juu yenu.

Ya kawaida, yakiwa mfano wa ya kiroho.
Sasa, tunaona basi, na amezaliwa kikamilifu. Wakati mtoto mchanga, kwa kawaida... Sasa wakati maji yanapovuja, haikubidi kumsaidia sana. Na wakati damu inapotoka, haikubidi kumshughulikia sana. Lakini, ili uhai uingie ndani ya mtoto huyo mchanga, huna budi kumpiga kofi la matakoni, na kumfanya apige makelele. Na hiyo ni ninii... Sasa, bila elimu, kwa kuwa ndugu zangu hapa wamefunzwa vizuri sana kwao, kwao, lakini sina budi kuchukua maumbile kuifananisha. Na hivyo ndivyo ilivyo. Hilo ndilo lililotukia. Inatakiwa kupigwa kofi halisi, kuingiza hili ndani yao.

Sasa, hebu chukua kidogo, namna fulani ya mshtuko. Labda, haitakulazimu kumpiga kofi, lakini mshtue tu kidogo. Wazo lenyewe la Yeye kuzaliwa, wakati mwingine, litafanya jambo hilo. Mnyakue, mtikise. Asipoanza kupumua, mpige kofi kidogo, ndipo atapiga mayowe, katika lugha isiyojulikana, kwa nafsi yake, nadhani. Lakini, yeye, hata hivyo, naye anapiga makelele. Nami nafikiri kama mtoto akizaliwa tu akiwa kimya, hana sauti, hana msisimko, huyo ni mtoto mfu.

Hiyo ndiyo shida ya kanisa siku hizi, mfumo; tuna watoto wengi sana waliokufa. Hiyo ni kweli. Wanahitaji kupigwa kwa Injili, mnaona, na kwa hiyo kuwaamsha, kuwafanya wajirudie, ili kwamba Mungu aweze kuwapulizia pumzi ya Uzima. Na sasa tunaona ya kwamba hiyo ni kweli sana. Ni theolojia ghafi, bali ni Kweli, hata hivyo.

-----
Tunaambiwa na manabii wa Mungu kwamba tunapaswa kuwa na nchi mpya, Mbingu mpya na nchi mpya. Kama unataka Maandiko juu ya jambo hilo, ni Ufunuo 21. Ningeweza kunukuu kwa ajili yenu, ninalo hapa. Yohana alisema, “Niliona Mbingu mpya na nchi mpya: kwa kuwa mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zilikuwa zimepita.” Ilikuwa imeondoka. Sasa, kama tutakuwa na nchi mpya, nchi ya zamani na nchi mpya haviwezi kudumu kwa wakati ule ule. Ama, ulimwengu mpya na ulimwengu wa zamani hauwezi kuwepo kwa wakati mmoja. Hakuwezi kuwa na taratibu mbili za ulimwengu pamoja kwa wakati mmoja. Sasa, kusudi upate ile nchi mpya, ile ya kale haina budi kufa. Sasa, kama ile ya kale haina budi kufa, basi inapata utungu wa kuzaa kwa ajili ya ile mpya sasa.

Halafu basi kama daktari alienda kumchunguza mgonjwa aliyekuwa katika uchungu wa kuzaa sasa, ninii... moja ya mambo ambayo daktari angefanya. Ambapo, ninazungumza mbele ya wawili ama watatu, niwajuao, madaktari wazuri wa madawa hapa, madaktari Wakristo. Nami ningewauliza jambo hili. Moja ya mambo ambayo daktari hufanya, baada ya kuwa amempima mgonjwa, ni kupima muda wa utungu, utungu wa kuzaa. Yeye hupima muda wa utungu, jinsi mmoja unavyokaribia mwingine, jinsi kila mmoja unavyokuwa mchungu zaidi. Mmoja ni mkali zaidi kuvumilia kuliko huo mwingine. Unaofuata, mkali zaidi, unakaribia karibu zaidi na mwingine. Hivyo ndivyo anavyopima hali hiyo, kwa utungu wa kuzaa. Vema, kama ulimwengu hauna budi kuachilia ulimwengu mpya uzaliwe, hebu tuchunguze tu baadhi ya utungu wa kuzaa tulio nao duniani, na ndipo tutaona kuhusu ni siku gani na una umbali gani katika utungu wake.

Vita vya Kwanza vya Dunia vilionyesha utungu mkubwa wa kuzaa. Ilionyesha moja ya utungu wa kwanza wa kuzaa kwake ukipata utungu wa kuzaa. Kwa sababu ya wakati huo kwake, tulikuwa tumeleta mabomu, na tulikuwa na bunduki, na gesi ya sumu. Nanyi mnakumbuka. Labda wengi wenu hamwezi. Nilikuwa mvulana mdogo tu mwenye umri wa kama miaka minane, lakini ninakumbuka wakinena juu ya hizi za haradali na klorini, na kadhalika. “Jinsi ilivyoonekana tu kama ingeanza tu na,” wakasema, “ingeiteketeza dunia nzima. Ingeua kila mtu. Vema, huenda ikawa ni kuachiliwa kwa hiyo, upepo tu ukiivumisha kote duniani.” Na jinsi kila mtu alivyoogopa kufa kwa hiyo silaha kuu ya gesi ya sumu! Dunia ilipitia, ikawa na utungu wake wa kwanza wa kuzaa.

Nasi tunaona sasa, tumekuwa na vita vya pili, Vita vya Ulimwengu, na maumivu yake yalikuwa makubwa zaidi. Unakuwa wa kutisha zaidi wakati wote, utungu wa kuzaa wa dunia. Dunia ilikuwa karibu iachilie, wakati wa bomu la atomiki, kwa maana lingeangamiza mji mzima. Utungu ulikuwa ni mkubwa zaidi kuliko utungu wa Vita vya Kwanza vya Dunia, katika kuiharibu nchi.

Sasa, inajua ya kwamba wakati wake wa ukombozi umekaribia. Hiyo ndiyo sababu ina wasiwasi sana, imechanganyikiwa, kama ilivyo, ni kwa sababu kuna bomu la haidrojeni, na makombora ya angani ambayo yangeweza kuuangamiza ulimwengu mzima. Taifa moja linaogopa lingine, haidhuru ni dogo jinsi gani. Wana makombora hayo wanayodai yataninii tu... Moja ya hayo. Wanaweza kuyaongoza kwa nyota na kuyaangusha mahali po pote ulimwenguni wanapotaka.

Urusi, kama nilivyosikia kwenye taarifa ya habari, hivi majuzi, inadai ya kwamba inaweza kuliangamiza taifa hili, na kuzuia hizo atomi ama vitu hivyo kuangamiza taifa lake. Hatujui la kufanya kuhusu jambo hilo. Kila mtu anatoa madai haya, na ndivyo ilivyo. Sayansi ya watu imeingia katika maabara kuu ya Mungu, mpaka watajiangamiza wenyewe. Mungu huachilia, daima huacha hekima ijiangamize. Mungu haangamizi chochote. Mwanadamu hujiangamiza mwenyewe kwa hekima, kama alivyofanya hapo mwanzo, akichukua hekima ya Shetani badala ya Neno la Mungu.

-----
Kwa hiyo inajua haiwezi kustahimili jambo hilo. Watu wanajua haiwezi kustahimili jambo hilo. Na ulimwengu unajua ya kwamba watafanya, watafanya hivyo. Kwa kuwa, Mungu alisema ilikuwa hivyo. “Mbingu zote na nchi zitateketezwa kwa moto.” Itakuwa ni kukarabatiwa kwa kitu hicho chote, kusudi ulimwengu mpya uzaliwe. Mungu ametabiri jambo hilo. Imeoza, katika mifumo yake yote, nayo haina budi kufanya hivyo, ipate kuoza. Hiyo ndiyo sababu hiyo, nilisema, ina wasiwasi sana na imeiva usoni, na inafadhaika. Na matetemeko ya nchi, kila mahali, na huku na huko pwani. Na mawimbi makubwa huko Alaska, na kutetemeka huku na huko katika pwani, kwa matetemeko ya ardhi na kadhalika. Na watu wakiandika, “Je! tuhame? Je! tuhame?” Mnaona? Hawajui la kufanya. Hakuna mahali pa salama ila Pamoja, hapo ni katika Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Na kuna jambo moja tu ambalo ni mahali pa salama, na hilo ni Yeye. Wote walio nje ya Hapo wataangamia, kwa hakika tu kama Mungu alivyosema.

Sasa hebu na tuangalie kwenye Kitabu cha Daktari, kama iko katika hali ya namna hii, na tuone kama jambo hili linapaswa kutukia wakati nchi mpya itakapozaliwa. Mathayo 24, katika Kitabu cha Daktari, ambacho ni Biblia, na hebu tuone kile kilichotabiriwa, dalili zake zingekuwaje.

Sasa, kama daktari anajua dalili za kuzaliwa kwa mtoto... Na yapata wakati ambapo mtoto atakuja, yeye huandaa kila kitu, kwa sababu anajua ya kwamba huo ndio ule wakati mtoto atakapozaliwa. Kwa sababu, dalili zote zinaonyesha; maji yametoka, damu. Na sasa ninii... Ni wakati. Mtoto ameshuka, na ni wakati wa mtoto kuzaliwa. Na kwa hiyo yeye huandaa kila kitu kwa ajili yake. Sasa, Yesu alitwambia hasa yale hasa yangetukia wakati huu. Sasa, Yesu alitwambia vile hasa ingetukia kwenye wakati huu. Alitwambia, katika Mathayo 24, ya kwamba Kanisa, Kanisa la kweli, na kanisa hilo lingine, lingekuwa...na Kanisa la kawaida, Kanisa la kiroho, “Wangefanana sana, hao waigaji, mpaka ingewapoteza walio Wateule, kama yamkini.” Kama ambavyo ilikuwa katika siku za Nuhu, “walivyokuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakiolewa,” na uasherati huu wote wa ulimwengu tunaouona siku hizi. Biblia, kile Kitabu, Kitabu cha Daktari kilisema ingetukia. Kwa hiyo, tunapoona jambo hili likitukia, tunajua ya kwamba kuzaliwa kumekaribia. Haina budi kuwa. Naam, bwana. Sasa, tunaangalia jambo hilo, kama taifa; si kama taifa, bali ulimwengu.

-----
Nini? Kanisa hili linapitia katika utungu wa kuzaa. Hivi hutafanya chaguo lako sasa katika Uwepo Wake? Nimewaonyesha Neno hasa, yale aliyosema angefanya. Tafuteni kwenye jengo hili, mwulizeni mtu ye yote aliyewahi kuguswa, ama kuzungumziwa, ama cho chote kile kilichofanyika, na mwone kama nimewahi kuwaona, kuwajua, ama jambo lolote juu yao. Mnafikiri mwanadamu angeweza kufanya jambo hilo? Hilo haliwezekani kabisa kwa jambo hilo kutukia. Vema, ni Kitu gani? Mwana adamu. “Neno la Mungu ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili, likitambua roho, siri za mioyo.” Ni kama tu vile lilivyokuwa kabisa wakati lilipofanyika mwili hapa duniani, katika Mwana wa Mungu, sasa linafunuliwa na Mwana wa Mungu kwani Yeye amekuja kumwita Bibi-arusi kutoka kwenye mfumo huo. “Tokeni kwake. Mkatengwe, asema Mungu. Msiguse vitu vyao vichafu, na Mungu atawapokea.”

Je! Uko tayari kuyatoa maisha yako yote kwa Mungu? Kama uko tayari, simama kwa miguu yako, useme, “Nitalikubali, kwa neema ya Mungu, sasa hivi, kwa kila kitu kilicho ndani yangu.”

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Utungu wa Kuzaa.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.

Yohana 16:20-21


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Ndoa Na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)

As the Eagle
Stireth her nest.

(PDF Kiingereza)

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.