Uzao wa Nyoka.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Mwerevu Nyoka.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Uzao wa Nyoka.

Mwanzo 3:1-7,
1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.

Angalia sasa, hili ndilo lililotukia. Ninaamini, na ninaweza kuliunga mkono kwa Biblia, ya kwamba nyoka ndiye aliyefanya jambo hilo. Nyoka ni yule mtu aliyepotea kati ya sokwe na mwanadamu. Maana, sikilizeni, angalieni jambo hili sasa, ya kwamba nyoka hakuwa kiumbe kinachotambaa. Alikuwa “mwerevu” kuliko wanyama wote wa kondeni.
Naam, nilienda nikachukua kamusi, leo, kutoka kila mahali, kuchunguza neno hili, maana ya neno mwerevu. Linamaanisha “kuwa na akili, kuwa mjanja,” na, tafsiri nzuri sana ya Kiebrania (kutoka m-a-h-a-h, mahah) linamaanisha “kuwa na maarifa halisi ya kanuni za uhai.”

Sasa hebu na tuangalie jambo hili kwa dakika moja. Yeye ni mwerevu, mjanja, hata hivyo anaitwa “nyoka.” Lakini, kumbukeni, alikuwa ndiye mwerevu sana aliyekuwako, na alifanana zaidi na mwanadamu kuliko kitu cho chote kilichokuweko kondeni; aliyekuwa anafanana sana na mwanadamu. Yeye hakuwa kiumbe kinachotambaa. Ile laana ndiyo iliyomfanya kiumbe kinachotambaa. Naye alikuwa … Biblia ilisema yeye ndiye aliyekuwa na sura nzuri sana kuliko wote. Wala hata ile laana haikuondoa urembo wake wote; hata sasa rangi nzuri sana za nyoka zinapendeza, na madaha yake na ujanja wake. Hata ile laana haikuyaondoa. Lakini, kumbukeni, Mungu alimwambia ya kwamba miguu yake ingetoka naye angetambaa kwa tumbo lake. Nawe huwezi kuona mfupa mmoja katika nyoka unaofanana na wa binadamu, na hiyo ndiyo sababu sayansi imepotea. Lakini huyo hapo.

Mungu alificha jambo hilo kutoka kwenye macho ya wenye akili na werevu, na akaahidi kulifunulia wana wa Mungu, katika siku za mwisho wakati wana wa Mungu watakapodhihirishwa, wakati, “Wana wa Mungu waliofurahi hata kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.” Wakati ule ufunuo mkuu wa Uungu na kadhalika vingeshushwa katika siku za mwisho, Yeye angedhihirisha mambo haya kupitia wana wa Mungu. Mnajua Maandiko yanafundisha jambo hilo. Na tuko hapa. Hiyo ndiyo sababu Mungu anatufunulia mambo haya. Mungu anawaleta wanawe katika kudhihirishwa. Yeye anaenda na kuvuka vikomo vya maarifa yo yote ya mwanadamu, moja kwa moja hadi kwenye funuo za kiroho, na kuushusha chini. Je! hatukuwa tunafundisha, katika Biblia hii, “Hili ni kwa yeye aliye na hekima”? Si yale amesomea katika seminari fulani; bali kile alichojifunza akiwa magotini mwake mbele za Mungu, na yale yaliyompendeza Mungu kumpa. Wana wa Mungu, wakidhihirishwa!

Huyu hapa nyoka, sasa hivi ndivyo alivyokuwa yule nyoka; mimi nitawapa maelezo yangu kumhusu yeye. Tuna ile… tunashuka, kutoka chura, kuendelea hadi kwa kile kiluwiluwi, na kuendelea chini na kuendelea, na kadhalika na kadhalika, hata hatimaye unafikia kwenye tumbili, kwenye sokwe mtu. Na toka sokwe mtu, sasa tunaruka toka sokwe mtu mpaka kwa mwanadamu, nasi tunashangaa kwa nini. “Vema,” sayansi inasema, “sasa ngojeni! Tunaweza kumzalisha mwanamke kwa tumbili na kwa sokwe, halafu vinginevyo, mwanamume azae kwa sokwe.” Haitawezekana. Mzalishe na mnyama mwingine ye yote; haitawezekana. Damu haitachanganyana; chukua damu yako, ni damu tofauti kabisa, kabisa.

Kuna damu katikati hapa, nao hawawezi kumpata mnyama huyo. Loo, Haleluya, ninajisikia wa kidini sasa hivi. Angalia. Kwa nini? Mungu aliwaficha wao jambo hilo. Hamna mfupa ndani ya nyoka unaofanana na mfupa wa binadamu. Yeye aliweka jambo hilo mbali sana hata lisingegunduliwa na mtu mwerevu. Nami nitawaonesha mahali anapotoka mtu huyo mwerevu, aliko, hata hivyo. Mnaona, yeye hawezi kuja kupitia jambo hilo.

Halina budi kuja kwa ufunuo, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa...” “Juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa Langu; na milango ya kuzimu haitalishinda,” ufunuo wa kiroho. Hivi Habili alijuaje kumtoa mwana-kondoo, badala ya Kaini kutoa matunda ya kondeni? Lilifunuliwa kwake kiroho. Huupati kwa seminari. Huupati kupitia madhehebu. Unaupata kutoka Mbinguni.

Sasa mwangalie yule nyoka, huyu nyoka aliyekuwa kwanza. Hebu na tuchukue picha yake sasa. Yeye ni jamaa mkubwa mno. Yeye yuko kati ya sokwe na mwanadamu. Na, yule nyoka; ibilisi, Lusifa, alijua ya kwamba hiyo ndiyo damu tu ambayo ingechanganyikana na damu hii ya mwanadamu, mtu pekee angeliweza kushughulika naye. Yeye asingeweza kujishughulisha na sokwe mtu, damu hiyo isingechanganyikana. Asingejishughulisha na vitu tofauti. Asingejishughulisha na kondoo. Asingejishulisha na tofauti. Asingejishughulisha na mnyama ye yote; ilimbidi kujishughulisha na huyu nyoka.

Hebu tumchukue sasa tuone anafanana na nini. Yeye ni mtu mkubwa mno, jitu la zamani za kale sana. Huko ndiko wanakopata mifupa hii mikubwa, nami nitawaonesha jambo hili katika Biblia. Sasa angalia kwa makini. Vema. Mtu huyu mkubwa mno, hebu tuseme yeye alikuwa na urefu wa futi kumi, mabega makubwa mno; alifanana tu kabisa na mwanadamu. Nayo damu yake; baada ya yeye kushuka akaja, kulinganisha mnyama mmoja na mwingine.

Unaweza kuwazalisha wanyama. Na iliendelea kuwa damu ya hali ya juu, maisha ya hali ya juu, hali ya juu, mpaka yanapanda mpaka kwenye milki ya mwanadamu. Bali kiungo cha mwisho hapa, katikati hapa, kilikatwa kikaondolewa. Ni wangapi wanaojua ya kwamba sayansi haiwezi kupata kile kiungo kichilopotea? Ninyi nyote mnajua jambo hilo. Kwa nini? Huyu hapa, yule nyoka. Huyu hapa, jamaa mkubwa mno. Ndipo ibilisi anashuka, sasa, anasema, “Ninaweza kuvuvia.”
Sasa wakati unaanza kuwaangalia wanawake, na kucheza pamoja na wanawake, kumbuka, una upako wa ibilisi (na si mke wako mwenyewe). Angalia, sasa, ibilisi alishuka na akaingia katika yule nyoka. Kisha akamwona Hawa katika bustani ya Edeni, uchi, naye akazungumza juu ya lile tunda la katikati. Katikati inamaanisha “sehemu ya katikati,” na kadhalika; mnaelewa, katika kusanyiko lililochanganyikana. Ndipo akasema, “Naam, ni zuri. Ni zuri kwa macho.”

Alifanya nini? Akaanza kufanya mapenzi na Hawa, halafu akamjua kimwili, kama mume. Basi mwanamke akaona lilikuwa zuri, kwa hiyo akaondoka akaenda akamwambia mumewe, bali tayari alikuwa ametiwa mimba na Shetani. Ndipo akamzaa mwanawe wa kwanza, ambaye jina lake lilikuwa ni Kaini, mwana wa Shetani. “Sasa,” mnasema, “huo ni uongo.”
Vema, tutaona tu kama ni uongo ama ni kweli. “Nami nitaweka uadui kati ya Uzao wako na uzao wa nyoka.” Nini? Uzao wa nyoka! Mwanamke alikuwa na Uzao, naye nyoka alikuwa na uzao. “Huo utakuponda kichwa chako, na wewe utamponda Yeye kisigino.” Nako kuponda, hapo, kunamaanisha “kufanya Upatanisho.” Basi huo hapo “uzao” wako wa nyoka.

Sasa, angalia, hawa hapa wanatokea watu hawa wawili. Sasa, huyu nyoka, aliposimama pale, jitu hili kubwa mno likasimama pale, lilikuwa na hatia ya kufanya uzinzi na mke wa Adamu. Dhambi inakaa wapi leo? Kitu gani kinayafanya mambo yawe jinsi yalivyo leo? (Sasa, mimi... Hakika mnaweza kufahamu ninalosema. Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa.)

Basi alipofanya jambo hilo, Mungu akasema, akaanza kuwaita Hawa na Adamu.
Naye akasema, “Nilikuwa uchi.”
Naye akasema, “Ni nani aliyekwambia ulikuwa uchi?”
Ndipo wakaanza, kwa mtindo wa kijeshi, kulaumiana. Kasema, “Vema, mwanamke uliyenipa Wewe, alifanya jambo hilo. Ndiye aliyenishawishi.”
Ati naye akasema, “Nyoka ndiye aliyenipa tofaa”? Vema, mhubiri, jichunguze.
Mwanamke akasema, “Nyoka alinidanganya.” Mnajua maana ya kudanganya? Linamaanisha “kunajisi.”
Naye alinajisiwa. Ibilisi hakumpa tofaa kamwe. “Nyoka amenidanganya.”
Na ndipo laana ikaja.

Yeye akasema, “Kwa sababu ulimsikiliza nyoka badala ya mumeo, umeuondoa Uhai ulimwenguni. Nawe utazidisha uchungu wako; na kuzaa kwako kutakuwa kwa mumeo,” na kadhalika.
“Na kwa kuwa ulimsikiliza mke wako, badala ya Mimi (nimekutoa mavumbini; kiumbe kilicho cha hali ya juu sana), utarudi mavumbini.”
“Na, nyoka, kwa kuwa umefanya jambo hilo, miguu yako itatoka. Kwa tumbo lako utakwenda, siku zote za maisha yako. Nawe utachukiwa. Na mavumbi yatakuwa chakula chako.” Haya basi. Hicho hapo kiungo kile kilichopotea.

Sasa huyu hapa Kaini anakuja. Hebu na tuangalie tabia. Huyu hapa Kaini anakuja. Yeye ni kitu nini? Yeye ni mfanyabiashara mwerevu. Yeye hulima mashamba. Mwerevu, mwenye akili; wa kidini, wa kidini sana; angalia sifa zake sasa. Nenda tu pamoja nami kwa dakika chache zaidi. Huyu hapa anakuja. Yeye anajua yeye ni mwadilifu. Anataka kwenda kanisani. Yeye humjengea kanisa, humfanyia sadaka. Analeta madhabahu, na kadhalika. Alijenga madhabahu, akaweka maua yake juu yake. Akaweka shamba, matunda ya kondeni, akamtolea Mungu. Kasema, “Haya basi, Bwana. Ninajua tunakula matofaa, hilo ndilo lililosababisha.” Baadhi ya watoto wake wana wazo la namna ile ile. Inaonyesha hilo linatoka wapi. Akaleta matofaa yake, kutoka kondeni, akayaweka pale, kasema, “Haya yatafanya upatanisho.”
Mungu alisema, “Haikuwa matofaa.”
Lakini, kwa ufunuo wa kiroho, Habili alijua ilikuwa ni damu. Kwa hiyo akamleta mwana-kondoo, akamkata koo, naye akafa.
Ndipo Mungu akasema, “Hiyo ni kweli. Hilo ndilo lililosababisha jambo hilo. Ilikuwa ni damu.” Mnajua ni damu gani ninayonena habari zake. Vema. “Damu ndiyo iliyosababisha jambo hilo.”

Sasa angalia. Na basi Kaini alipomwona ndugu yake mtakatifu anayejiviringisha amekubalika mbele za Mungu, na ishara na maajabu zilikuwa zikitendeka kule, alimwonea wivu. Akasema, “Tutakomesha upuuzi huu sasa hivi.” Waangalie ndugu zake, waangalie watoto wake, siku hizi. “Naam, mimi ni mwerevu kuliko alivyo yeye,” kwa hiyo akakasirika. Hasira ilitoka wapi? Ungeweza kusema ya kwamba hasira ...? Alimwua ndugu yake. Yeye alikuwa muuaji.
Ungeweza kumwita Mungu muuaji? Na Adamu alikuwa mwana wa Mungu. Biblia ilisema, ya kwamba, “Adamu alikuwa mwana wa Mungu,” ule mwanzo msafi kule nyuma. Adamu alikuwa mwana wa Mungu. Na ule wivu na husuda, na kila kitu, visingeweza kutoka kwenye mkondo ule msafi.
Ulipaswa kuja kupitia mahali pengine... Nao ulikuja kupitia kwa Shetani, aliyekuwa mwuaji, kwanza. Biblia ilisema, “Yeye alikuwa mdanganyifu na mwuaji, kwanza.” Na ndiyo hilo hapo. Naye akamwua ndugu yake.
Basi huo ulikuwa ni mfano wa mauti ya Kristo. Halafu, kutokana na jambo hilo, bila shaka, Yeye alimwinua Sethi kuchukua mahali pake. Mauti, kuzikwa, na kufufuka kwa Kristo.

Angalia, basi, hawa hapa wanefili wako wanakuja. Ndipo Kaini akaenda katika nchi ya Nodi. Kama baba yake alikuwa jitu kubwa mno, Kaini angekuwa kama nani? Baba yake. Naye akaenda kwenye nchi ya Nodi, na kumchukua mmoja wa dada zake.
Njia pekee angeweza kufanya. Hakuna mahali pengine wanawake wangetokea, ila tu kupitia kwa Hawa. Wanadai wao walikuwa na wana na binti sabini. Kama hakukuweko na wanawake... Biblia haiwaandiki wanawake wanapozaliwa, ni wanaume tu. Basi wakati, kama hakukuweko na wanawake wengine ila Hawa, wakati alipokufa, jamii ya binadamu ilikoma kuweko. Ilimbidi kuwa na binti. Na ilimbidi amwoe dada yake mwenyewe.
Alienda katika nchi ya Nodi akampata mkewe. Basi alipokwisha kumwoa huko, huko ndiko walikowapata wale majitu wakubwa mno, ambao walikuwa ni wana wa Mungu walioanguka; waliokuja kupitia kwa baba yao, ibilisi, kupitia kwa Kaini. Hicho hapo kiungo chako kilichopotea.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Uzao wa Nyoka.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.

Mithali 30:20


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Pillar of Fire.

(PDF Kiingereza)

Mungu Akijificha
Kwa Urahisi...
(PDF)

Ndoa Na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)