Kitendawili.
<< uliopita
ijayo >>
Kitu lisilosadikika, bali ni kweli.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kitendawili.Sasa somo alasiri ya leo: Kitendawili. Sasa, neno kitendawili, kwa kuwa nimekuwa nikilitazama na kuwa na hakika ya kwamba nilikuwa sahihi, neno kitendawili linamaanisha, kulingana na Webster, kwamba ni “kitu lisilosadikika, bali ni kweli.” Sasa, mwajua, tumesikia ule msemo wa kale, kwamba, “Ukweli unaninii zaidi” (wanausemaje huo?) “ni wa kigeni zaidi kuliko hekaya,” ndivyo ukweli ulivyo. Kwa sababu, wakati mtu anaposema kweli, wakati mwingine ni wa kigeni sana.
-----
Yoshua hapa ni Kitabu, kwa kweli, ni Kitabu cha ukombozi, cha Agano la Kale. Yoshua, ingetupasa kukihesabu kuwa hivyo, Kitabu cha ukombozi. Kwa kuwa, ni, ukombozi una sehemu mbili. Ukombozi, mahali popote, una sehemu mbili. Hizo ni, “kutoka” na “kuingia.” Inahitaji sehemu mbili kufanya ukombozi, “kutoka,” “kuingia.”
Musa aliwakilisha torati iliyowatoa Misri, na, ambapo, Yoshua aliwakilisha neema iliyowapeleka katika nchi ya ahadi. Njia nyingine, ilikuwa, ile— torati na neema zilikuwa ni sehemu mbili mbalimbali za amri ya Mungu. Sasa, torati iliwatoa, Musa, na Yoshua akawaingiza.
Pia inawakilisha kitu fulani kwa siku yetu. Sasa inawakilisha, walivyokuwa safarini, wakitoka Misri kuingia kwenye nchi ya ahadi, vivyo hivyo nasi tumetoka ulimwengu wa Misri, machafuko, tukielekea kwenye Nchi ya ahadi. “Nyumbani mwa Baba Yangu mna makao mengi; kama isingalikuwa hivyo, ningewaambia,” Yohana 14. Kutoka “nje ya,” kuingia “ndani ya.”Torati ndiyo inayotufanya tujue tumekosea, bali neema ndiyo inayotusamehe. Torati haina matumaini ya ukombozi, kwa sababu... na kuikamilisha. Haina neema ndani yake, kwa sababu torati inaonyesha tu kwamba wewe ni mwenye dhambi, bali neema inakuambia jinsi ya kutoka humo. Sheria ni polisi aliyekuweka gerezani, bali ukombozi ndio uliokuja ukalipia faini yako; na “kutoka,” na “kuingia,” kuingia katika neema.
Waefeso. Sasa tunaona jambo lile lile, Agano la Kale, nafikiri Kitabu hiki cha Yoshua kinafaa. Neno linalofaa kwake, lingekuwa, Kitabu cha Efeso cha Agano la Kale. Kitabu cha Waefeso cha Agano la Kale, lingekuwa ni jambo zuri kukipa kitabu hiki Kitabu cha Yoshua, kwa sababu hakika kinafaa kwa hili.
Sasa tunaona Yoshua akiwakilisha neema, ama upatanisho, kwamba haingekuwepo kwenye wakati ule ule torati ilipokuwepo. Wala ujumbe wowote, unaowapeleka watu mbele, kamwe haupatani na ujumbe uliopita. Hautapatana. Hautapatana. Hapo ndipo mlipo na shida leo hii. Yesu alisema, “Hivi mtu yeyote huchukua kiraka kipya cha nguo na kukitia kwenye vazi kuukuu? Ama kuweka divai mpya kwenye viriba vikuukuu? Huharibika. Huvipasua.” Haviwezi kuistahimili hilo.
Naye Yoshua hangeweza kamwe kuingia katika huduma yake mpaka baada ya Musa kuondoka. Kwa hiyo unaona aya ya kwanza kabisa hapa, “Musa mtumishi Wangu amekufa; sasa inuka na uwapeleke watu hawa kwenye nchi ya ahadi.” Musa, akiwakilisha torati, alikuwa ametumikia wakati wake. Ni, sheria ilikuwa imetumika wakati wake.
Walianza kutoka, kweli, kwa neema, kwanza. Kabla hawajapata sheria, walipata neema. Wakati wakiwa Misri, pasipo na torati; hakukuwako na mtu huko chini, ni makuhani tu, na kadhalika, bali hawakuwa na torati yoyote. Torati ilikuwa bado haijatolewa. Neema iliwapa nabii. Na, pia, neema ilitoa upatanisho, mwana-kondoo wa sadaka. Tutaingilia jambo hilo juma hili, juu ya sadaka, damu, kwa maana hapo ndipo penye uponyaji wenu. Kwa hiyo kwenye... Upatanisho ulikuwa umetolewa kabla hapajakuwapo na torati yoyote. Neema ilikuwepo kabla ya torati, wakati wa torati, na baada ya torati. Kwa hiyo huyo hapo Yoshua, akiiwakilisha neema, alikuwepo moja kwa moja pamoja na torati, bali isingeweza kutumika mradi tu torati iko mahali pake hasa.
Na vivyo hivyo ulimwengu wa kanisa katika siku hii ya mwisho! Umekuja, umetumika mahali pake, bali wakati unakuja ambapo hauna budi kwisha. Haina budi kufanya hivyo. Hapana budi kuwepo na Waefeso, pia, ya safari hii, kama tu kulivyokuwa na ya safari zingine. Waefeso haina budi kuja, Waefeso, Waefeso ya safari hii. Angalia.
Ambapo sheria hiyo haingeweza kumwokoa mwenye dhambi, kama nilivyoeleza. Isingeweza. Kwa hiyo nchi ya ahadi iliwakilisha siku ya neema. Mnaona, asingeweza kuwaingiza, katika safari hiyo.Na kama mliona, katika safari hiyo, walikuwa na hatua tatu za safari yao. Kwanza ilikuwa ni maandalizi kwa imani, huko Misri, chini ya mwana-kondoo wa sadaka. Ndipo wakavuka Bahari ya Shamu, wakaingia nyikani, utengano, ambao uliwakilisha hatua nyingine ya safari. Maana, chini ya maandalizi, wakati wote walipokuwa tayari, basi walipofika kwenye Bahari ya Shamu, palikuwapo na kushindwa tena. Watu hawakuamini, baada ya kuona mambo mengi ambayo Mungu alikuwa amefanya. Bado hawakuamini. Na Mungu akaifungua Bahari ya Shamu na kuwatoa, ambayo tunafundishwa ya kwamba watu wote walibatizwa kwa Musa, chini ya lile Wingu na bahari.
Sasa wao walibatizwa, wakatubu na kubatizwa, na wakaja kutembea katika maisha mapya, katika nchi mpya, katika safari mpya, miongoni mwa watu wapya, na mkono wa Mungu juu yao. Lakini hatimaye ilifikia mahali, katika mwendo huu waliokuwa nao, ambapo hawakuridhika na mwendo wao wa neema. Iliwabidi wafikie kitu fulani ambacho wangeweza kufanya wao wenyewe. Sasa hapo ndipo watu wanapowazia, leo, juu ya uponyaji wa Kiungu, ama kazi nyingine yo yote ya neema, ya Mungu, ya kwamba kuna jambo fulani unalopaswa kufanya. Wewe, hakuna kitu unachopaswa kufanya ila kuamini, mwamini tu Mungu.
Na, wao, kama wangaliendelea! Ahadi hawakupewa chini ya torati. Ahadi ilitolewa kabla ya torati, pasipo na masharti yoyote kwake, “Nimewapa nchi hii, nendeni kule!” Lakini kabla hawajafikia ahadi hiyo, waliamua kulikuwa na jambo fulani walilopaswa kufanya wenyewe. Na, kwamba, bado tunaona hilo miongoni mwa wanadamu. Tunapenda kuwa hivyo, “Kuna jambo ambalo hatuna budi kufanya.” Tunajisikia hivyo, kwamba tuna sehemu mle pia.
Kweli una sehemu mle, hiyo ni kuyasalimisha mapenzi yako, mawazo yako, kwa mapenzi na wazo la Mwenyezi Mungu, na imekwisha. Hakuna lingine. Chukua tu ahadi Yake, usifikirie kitu kingine. Tembea na Hilo, na Mungu hufanya hayo mengine.
Ndipo walitaka sheria. Na Mungu daima hukupa shauku ya moyo wako; Yeye aliahidi kufanya hivyo. Ila tunaona, walipopiga hatua moja kutoka kwenye upande wa yale Mungu aliyowaahidi awali, basi huo ulikuwa mwiba katika mwili mpaka torati ilipoondolewa, mpaka Yesu Kristo alipokuja na kusulibishwa kuiondoa torati. Ulikuwa ni mwiba mwilini. Na chochote unachojaribu kufanya kwa nafsi yako, daima kitakuletea aibu. Kitakuletea matokeo mabaya. Mwamini tu Mungu tu, na hilo latosha. Kile Mungu alichoahidi, “Mimi ni Bwana Mungu Wako Ambaye huponya magonjwa yako yote.” Mnaona? “Kama kuna ye yote miongoni mwenu, mgonjwa, na awaite wazee wa kanisa.” Yeye aliahidi, “Kazi alizofanya, zingefanywa katika kanisa Lake.”
Ni kwa nini inatubidi kuyakubali madhehebu, na kadhalika, ambayo yatafutilia hayo mbali kutoka kwenye Kitabu? Mnaona, inakuwa mwiba katika mwili. Na hapa kwenye wakati wa mwisho, tunakabiliana na jambo hilo tena, uso kwa uso, ni juu ya Wamethodisti, Wabaptisti, Wapresbiteri, na wowote wale, mnaona. Wewe, huwezi kuendelea; huna budi kurudi kwenye Injili yote kamili. Ilifanywa kwa ajili ya mtu mkamilifu, na Mungu mkamilifu aliyefanyika mwili na kukaa miongoni mwetu. Nasi tunajua ya kwamba mambo hayo ni kweli.
Sasa kama tukiangalia, basi, safari yao nyikani ndipo walipofanya kosa lao lililo kuu mno ambalo Israeli ilipata kufanya, mpaka Kalvari, lilikuwa wakati (katika Kutoka 19) waliikubali torati badala ya neema. Walikuwa na neema. Walikuwa na nabii. Walikuwa na mwana-kondoo wa sadaka. Walikuwa na ukombozi. Walikuwa wamepitishwa kwenye Bahari ya Shamu. Walikuwa wameponywa magonjwa yao. Walikuwa wamepata maji kutoka kwenye mwamba uliopigwa. Walikuwa na mana kutoka mbinguni. Kila kitu walichohitaji walikuwa wamepewa, na bado walitaka kitu kingine.
Sasa huo ni mfano mkamilifu wa Waefeso wetu leo, hasa. Tulitoka chini ya Luther; tulipitia utakaso, chini ya Methodisti; kisha akaingia kwenye kule kurudishwa, chini ya Pentekoste. Kama vile ilivyokuwa hasa, safari ya jangwani. Na wakati Mungu alipotutoa, tulifanya vizuri sana. Lakini tulifanya nini? Nilitaka kuwa kama hao wengine. Sasa tunaona ya kwamba neema ndicho kitu pekee kinachotufanikisha, kamwe si torati.
Yoshua hapa ni mfano wa huduma ya siku za mwisho. Mnaona? Sasa kumbukeni hizo hatua tatu za safari. Zote zilikoma, kwanza ilibidi torati na kila kitu kukoma, kusudi Yoshua... Nalo Yoshua ni neno lile lile kama Yesu, “Yehova-mwokozi,” aliyewatoa kutoka nyikani mwao akawaingiza kwenye nchi ya ahadi. Sasa najua wengi hushikilia...
Nami sitaki kupingana na wasomi, bali wengi wanashikilia ya kwamba nchi ya ahadi inawakilisha Mbinguni. Isingeweza kuwakilisha Mbingu. Isingeweza, kwa kuwa walikuwa na vita, na matatizo, na vurugu, na kila kitu, kwenye nchi ya ahadi. Haiwakilishi Nchi ya ahadi.Lakini mnaona, kabla tu hawajaingia kwenye nchi ya ahadi, tofauti zote ambazo zilikuwa zimeibuka miongoni mwao. Wao... Moja ya mambo makuu ilikuwa ni Kora. Hakutaka uongozi huu wa mtu mmoja. Dathani, na jinsi walivyojitokeza mbele ya Musa na kujaribu kumwambia ya kwamba “ilibidi ujumbe umaanishe hili,” na kuweka tafsiri tofauti kwake, mawazo yao wenyewe ya kile lilichokuwa. Nao kila mmoja wao aliangamia! Kila mmoja!
Yesu alisema, “Wote waliangamia.”
Walisema, “Baba zetu walikula mana jangwani, kwa muda wa miaka arobaini,” Yohana Mtakatifu 6. Yesu alisema, “Na kila mmoja wao amekufa.”
Mauti maana yake ni “Kutengwa Milele.” Wote wamekufa, hata hivyo walifurahia kusikia ujumbe, hata hivyo walifurahia mana iliyoanguka. Si mana nyingine; ile mana halisi!-----
Sasa tunafundishwa, katika Ufunuo sura ya 6, ninaamini, naam, sura ya 6, ya ile Mihuri Saba. Hilo linapaswa... Kitabu hicho kufungwa kwa siri saba, ama Mihuri Saba, Ufunuo 6. Na katika siku ya mwisho, Ufunuo 10, katika Ufunuo 10, tunaona ya kwamba Laodikia, mjumbe wa mwisho wa wakati wa mwisho, na kwenye wakati wa unabii wake, ya kwamba Mihuri Saba ingefunguliwa, zile siri saba, siri zenye sehemu saba zilizokuwa zimeachwa.
Katika kila wakati kulikuwako na sehemu Yake iliyoachwa. Mtengenezaji hakuwa na wakati wa kuishughulikia. Katika siku za Luther, yeye alihubiri tu kuhesabiwa haki kwa imani. Alikuwa ameondoka, wakafanya kanisa. Baada ya hapo akaja Wesley, alihubiri utakaso. Huo hapo. Na halafu wakaja Wapentekoste.Lakini tumeahidiwa, kulingana na Ufunuo 10, na kulingana na Malaki 4, na Luka Mtakatifu 22:17, na kadhalika, ya kwamba hatuna budi kuja Waefeso kwa jambo hili. Kuna jambo lililoahidiwa, enyi marafiki. Lazima Waefeso waje, kwamba hizi siri saba za Neno la Mungu hazina budi kufunuliwa. Na ni katika wakati wa Laodikia ambapo hili linatukia. Ninaamini ya kwamba tuko pale. Ninaamini tuko moja kwa moja katika vivuli vya Kuja kwa Mwana wa Mungu. Na kama vile Yoshua, kabla tu ya Waefeso kuinuka, vivyo hivyo Yohana Mbatizaji alisimama kabla tu ya Waefeso wa pili. Nasi tumeahidiwa mwingine, Waefeso mwingine. Imebashiriwa hapa katika Maandiko, kwa hiyo nafikiri ya kwamba tunaishi katika Waefeso tena. Rudi tena kwenye... Tumeahidiwa kwamba yale yaliyosalia katika zile nyakati saba.
Sasa huwezi kuongeza chochote kwenye Kitabu, wala kuondoa chochote kutoka Kwake. Ufunuo 22:18 yasema hivyo, “Atakayethubutu, atakayeongeza neno moja, au kuondoa Neno moja, ataondolewa sehemu yake katika Kitabu cha Uzima.” Sasa hatuwezi kuongeza wala kuondoa. Kwa hiyo basi tunajua ya kwamba Luther asingeweza kulifikia; Wesley, na kadhalika, wale watengenezaji, Knox, Finney, Calvin, na kuendelea, na kadhalika, hawakulipata lote, bali waliyokuwa nayo ilikuwa ni Kweli ya Injili. Lakini sasa katika siku za mwisho, tumefahamishwa, na Neno, ya kwamba tutalifahamu, kwa kuwa utakuja wakati wa Waefeso kwake. Nasi tuko hapa! Kitendawili!
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kitendawili.