Mkataa.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Kristo Amefunuliwa katika Neno Lake Mwenyewe.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kristo Amefunuliwa katika Neno Lake Mwenyewe.

Sasa nitazungumza juu ya somo hili la: Kristo Akifunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe. Jinsi ambavyo, katika zile Sifa Heri, kuna picha ya Kristo, amesimama moja kwa moja, kama. Hapo ndipo nilipowazia juu ya somo hili.

Sasa, Kristo na Neno ni kitu kimoja. Mnaona?

Wanasema, “Biblia ilikuwaje...?” Watu wanasema. Nilikuwa nikiendesha gari na mtu fulani si muda mrefu uliopita. Akasema, “Wazia jambo hilo. Sisi hapa duniani, namna tulivyo, na tunajua tu ama tunaweza kusema tu kwamba tumeokolewa na hadithi fulani ya Kiyahudi inayoitwa Biblia.”
Nikasema, “Bwana, sijui jinsi unavyosema jambo hilo, bali siamini ni hadithi ya Kiyahudi,” nikasema. Akasema, “Vema, unaomba, unaomba kwa kitu gani? Niliomba kitu fulani na mambo fulani; Sikukipata.”

Nikasema, “Unaomba vibaya. Hatupaswi kamwe kuomba kubadilisha nia ya Mungu; tunapaswa kuomba kubadilisha nia yetu. Nia ya Mungu hahitaji kubadilika kwo kwote. Mnaona? Mnaona, ni kweli.” Nikasema, “Siyo kile ulichoomba...” Ninamjua mvulana mmoja Mkatoliki, wakati mmoja, alikuwa na kitabu cha sala, akikariri sala, na kwa kusudi mama yake apate kuishi. Naye akafa, naye akakitupa kitabu cha maombi motoni. Vema, mnaona, sikubaliani na kitabu cha sala; lakini, hata hivyo, mnaona, unachukua mtazamo mbaya. Unajaribu kumwambia Mungu la kufanya.

Maombi yanapaswa kuwa, “Bwana, nibadilishe nilingane na Neno Lako.” Si ati, “Badilika,” si, “hebu naomba nibadilishe nia Yako. Unabadilisha nia yangu.” Mnaona? “Unabadilisha nia yangu iwe mapenzi Yako. Na mapenzi Yako yameandikwa hapa katika Kitabu. Na, Bwana, usiniache niondoke mpaka umeifanya nia ya— nia yangu kuwa kama nia Yako. Na kisha nia yangu itakapokuwa kama nia Yako, ndipo nitaamini kila Neno uliloandika. Nawe ulisema, mle ndani, utafanya kila kitu 'kitende kazi kwa manufaa' kwa wao wakupendao Wewe. Nami nakupenda, Bwana. Yote ni kufanya kazi pamoja kwa manufaa.”

-----
Angalia sasa, tunarudi, hatuna budi kuwa na kitu kingine ambacho hatuna budi kushikilia. Kitu fulani hakina budi kuwa nguzo ya kushikilia, kwa maneno mengine, ni mkataa. Na kila mtu hana budi kuwa na mkataa ama yakini. Nilihubiri juu ya jambo hilo wakati mmoja, miaka mingi iliyopita, kuhusu yakini, mahali ambapo ni neno la mwisho.

Kama vile mwamuzi kwenye mchezo wa mpira, kama anasema ni goli, hivyo ndivyo ilivyo hasa.
Haidhuru umelionaje, mwamuzi alisema ni goli. Ulisema, “Mi—Mi—MiMI... Halikuwa goli. Lilienda ... Niliona ninii ...” Haidhuru ni nini, wakati aliposema, “goli,” hivyo ndivyo ilivyo, hilo latosha tu. Yeye, yeye ndiye mkataa. Na taa ya barabarani ni mkataa, kama inasema, “nenda.” Unasema, “Vema, mimi, nina haraka, nina...” La, la. Inasema, “Wewe simama kimya wakati jamaa huyo mwingine anapoondoka.” Mnaona? Ni mkataa.

Sasa, hapana budi kuwe na mkataa kwa kila kitu ufanyacho. Ilibidi kuwe na mkataa wakati ulipomchagua mke wako. Ilibidi kuwe na mwanamke uliyemchagua. Sasa, hapana budi kuwe na wakati ambapo, wakati utakaponunua gari, utafanya mkataa wa aina gani. Je, itakuwa Ford, Chevy, Plymouth, gari la kigeni, chochote kile, huna budi kuwa na mkataa. Na ndivyo ilivyo na maisha ya Kikristo. Hapana budi kuwe na mkataa.

-----
Vema, kila dhehebu ni mmataa kwa waamini wao. Lakini, kwangu mimi, na kwa wale ninaotumaini ya kwamba ninawaongoza kwa Kristo, na kwa Kristo, Biblia ndiyo mkataa wetu. Haidhuru... Maana, Mungu alisema, “Neno la kila mtu na liwe uongo, na Langu liwe Kweli.” Nami ninaamini ya kwamba Biblia ni mkataa wa Mungu. Haidhuru mtu mwingine yeyote anasema nini; Ni mkataa.

Biblia si kitabu cha mifumo. La, bwana. Si kitabu cha taratibu, wala kanuni za maadili. Biblia si kitabu cha taratibu, taratibu nyingi sana, na kadhalika. La, bwana. Si kitabu cha maadili. La, bwana. Sivyo. Wala si kitabu cha historia, kabisa. Ama, wala si kitabu cha theolojia. Kwa kuwa, ni ufunuo wa Yesu Kristo. Sasa kama mngetaka kusoma hayo, ninyi mlio na makaratasi yenu, mkiyaandika, huo ni Ufunuo 1:1 hadi 3, kama, Biblia ni “Ufunuo wa Yesu Kristo.”

-----
Sasa angalia Biblia hii. Baadhi yao walisema, “Loo, vema, imefanya hivi, imefanya vile.” Lakini hebu niwaambie jambo fulani, hebu tu...
Hebu na tuingie katika historia ya Biblia, kwa dakika moja tu, tuone mahali ilipotoka. Iliandikwa na waandishi arobaini mbalimbali. Watu arobaini waliandika Biblia, kwa muda wa miaka elfu moja mia sita, na katika nyakati mbalimbali, wakitabiri matukio muhimu sana yaliyowahi kutokea katika historia ya ulimwengu, na, mara nyingi, mamia ya miaka kabla haijatukia. Na hakuna hata kosa moja katika Vitabu vyote sitini na sita. Loo, jamani! Hakuna mwandishi ila Mungu Mwenyewe angeweza kuwa sahihi sana. Hakuna Neno moja linalopingana na lingine.

Kumbukeni, miaka elfu moja mia sita mbali mbali, Biblia iliandikwa, tangu Musa hadi— hadi kifo cha Yohana kwenye kile kisiwa, ama Kisiwa cha Patmo. Miaka elfu moja mia sita, na iliandikwa na waandishi arobaini mbalimbali; mmoja hata hakumjua huyo mwingine, nao kamwe hawakuwa nalo kama “Neno.” Wengine wao hata hawakuliona “Neno.” Lakini wakati walipoliandika Hilo, na ikafahamika kuwa ni manabii, basi, wakati walipounganisha unabii wao pamoja, kila moja ya hizo ilikubaliana na nyingine.

-----
Sasa, tuseme kwa mfano, kutoka... Vipi kama tungeenda sasa na kuchukua vitabu sitini na sita vya tiba vinavyohusika na mwili, vilivyoandikwa na shule arobaini mbalimbali za matibabu, miaka mia moja na kumi na sita ... ama miaka elfu moja mia sita? Sijui tungekuja na mwendelezo wa namna gani?... La, hakuna mwendeleo kwa jambo hilo.

Lakini hakuna Neno moja katika Biblia linalopingana na lingine. Hakuna nabii hata mmoja aliyempinga huyo mwingine. Walikuwa, kila mmoja, mkamilifu. Na wakati mtu alipoingia na kutoa unabii, na nabii huyo halisi aliinuka na kumwita aje, basi ilidhihirishwa. Mnaona? Mnaona? Kwa hiyo Biblia ni Neno la Mungu, kwa waamini wote wa kweli.

-----
Nao wataona, siku moja, ya kwamba hawaoni miaka milioni mia moja na hamsini ya anga la juu. Wanaenda moja kwa moja kwenye duara. Hiyo ni kweli kabisa. Utatambua, moja ya siku hizi, ya kwamba wakati utakapoenda Mbinguni, hutaruka kwenda mahali pengine. Ungali upo papa hapa, pia, katika kiwango kingine kinachoenda kasi zaidi ya hiki. Moja kwa moja kwenye chumba hiki kuna rangi inayokuja. Kila rangi, shati, mavazi, cho chote ulichovaa, ni cha Milele, kimewekwa moja kwa moja kwenye rekodi, kikizunguka na kuzunguka ulimwengu. Kila wakati unapofumbua macho yako, ni moja kwa moja kwenye rekodi. Angalia, televisheni itathibitisha jambo hilo.

-----
Sasa angalia, na hakuna kosa lo lote katika Maandiko. Yesu, Neno la Mungu, hutambua wazo lililo moyoni. “Neno la Mungu lina nguvu zaidi, ni kali,” Waebrania 4:12. “Neno la Mungu ni kali zaidi, lina nguvu zaidi kuliko upanga ukatao kuwili, hata huyatambua mawazo na makusudi ya nia.” Mnaona? Unaingia moja kwa moja ndani ya nia, na kuvuta, na kutambua. Utambuzi ni nini? “Kujulisha, kufunua.” Na hivyo ndivyo Neno la Mungu linavyofanya.
Leo tunasema, “Kanisa Katoliki ni Neno la Mungu; Wabaptisti, Wamethodisti, Wapentekoste, maskani.” Hilo ni kosa. Neno ni ufunuo; Mungu, akifunuliwa kwa Neno.

-----
Ni kamilifu sana, Neno la Mungu ni kamilifu sana, hata kwa Agano la Kale na Agano Jipya, ni nusu mbili na moja nzima. Hiyo ni kweli. Agano la Kale ni nusu Yake, na Agano Jipya ni nusu Yake; ukiliweka pamoja, una ufunuo wote wa Yesu Kristo. Hao hapo manabii wakinena, na huyu hapa katika Mwili; mnaona, nusu mbili na moja nzima.

Sasa, kumbukeni, Agano la Kale si kamili bila lile Jipya. Na lile Jipya lisingeweza kuwa kamilifu bila ya lile la Kale. Hiyo ndiyo sababu nilisema nusu mbili, moja nzima. Kwa kuwa, manabii walisema, “Atakuwa hapa! Atakuwa hapa! Atakuwa hapa; watamfanyia hivi. Watamfanyia hivi!” Naye ndiye huyu hapa, “Alikuwa hapa! Yeye alikuwa hapa, nao walimtendea hili, nao walimtendea hili.” Nilihubiri tu jambo hilo siku chache zilizopita usiku.

Sasa, kusudi tupate kusoma Maandiko, Paulo alimwambia Timotheo, “Jifunze, ukitumia kwa halali Neno la Mungu, ambalo ni Kweli.”
Hayo ni matakwa matatu katika Maandiko. Katika kutumia Neno la Mungu, kuna mambo matatu ambayo hupaswi kufanya. Sasa hebu na tusome hayo kwa dakika kumi zifuatazo; mambo matatu ambayo hupaswi kufanya. Na ninyi nyote mlio nchini, popote mlipo, kote nchini, hakikisheni mnaweka haya moyoni mwenu kama hamna penseli. Haikupasi kufanya mambo haya. Tunawaambia wakati wote jinsi mnavyopaswa kufanya, sasa nitawaambia yale msiyopaswa kufanya.

Sasa, hupaswi kulifasiri Neno vibaya. Unasema, “Vema, ninaamini inamaanisha hivi.” Linamaanisha vile tu linavyosema. Halihitaji mfasiri. Wala hupaswi kuliweka Neno mahali pasipo pake. Wala hupaswi kuliweka Neno mahali pasipo pake. Na kama tukifanya moja ya mambo katika haya, jambo hilo litatupa Biblia nzima katika mchafuko na ghasia.

Angalia. Kumfasiri vibaya Yesu, katika mfano wa Mungu katika mwanadamu, ungemfanya Yeye Mungu mmoja kutoka kwa watatu. Kumfasiri vibaya Yesu Kristo akiwa ni Neno, ungemfanya Yeye Mungu mmoja kati ya watatu, la sivyo ungemfanya Yeye Nafsi ya pili katika Uungu. Na kufanya hivyo, ungevuruga Maandiko yote. Usingeweza kufika po pote. Kwa hiyo halipaswi kufasiriwa vibaya. Na kama ukisema ya kwamba jambo fulani, ukiweka fasiri fulani juu Yake, na kulitumia Hilo kwa wakati mwingine; ama limekwisha kutumiwa kwa wakati mwingine, unafanya fasiri isiyo sahihi pia.

-----
Haya masharti matatu hayana budi kuwa. Haipaswi kufasiri vibaya, ama kulitumia vibaya, kulifasiri Hilo, ama ku— au kuliondoa kwenye sehemu Yake. Halina budi kuwekwa sawa kabisa jinsi Mungu alivyosema ilikuwa.

Kwa ulimwengu, ni Kitabu cha fumbo. Watu wanaamini ni Kitabu cha kimafumbo tu. Wakati mmoja nilikuwa nikizungumza na mtu mashuhuri sana hapa mjini, ambaye ana msimamo mkuu wa Ukristo, naye akasema, “Nilijaribu kusoma Kitabu cha Ufunuo usiku mmoja.” Kasema, “Yohana hapana budi alikuwa amekula masarufu ya pilipili kali kisha akapata jinamizi.” Mnaona, Kitabu cha siri.

Lakini, wakati kwa mwamini wa kweli, ni ufunuo wa Mungu akifunuliwa katika wakati tunaoishi. Yeye alisema, “Maneno Yangu ni Roho na ni Uzima.” Yesu alisema hivyo. Tena, “Neno ni Mbegu ambayo mpanzi alipanda.” Tunajua ya kwamba hiyo ni kweli. Ni Mungu katika umbo la Neno, na anaweza tu kufasiriwa na Yeye Mwenyewe.

Akili ya mwanadamu haiwezi kufasiri nia ya Mungu. Mtu mdogo— mwenye kikomo anawezaje kufasiri Akili isiyo na kikomo, wakati hatuwezi hata kufasiri mawazo ya mtu mwingine? Nanyi mnaona, Yeye Ndiye pekee anayeweza kulifasiri, Naye analifasiri kwa Yeye atakaye. Haikusema, “Wanadamu wa kale, walipokuwa wakizunguka-zunguka duniani katika nyakati nyingi na kwa namna nyingi.” “Mungu, katika nyakati nyingi na kwa njia mbalimbali alijifunua Mwenyewe kwa manabii Wake.” Mnaona?

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kristo Amefunuliwa katika Neno Lake Mwenyewe.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

  Maandiko Anasema...

Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

Waebrania 1:1-2


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)
Ambapo upanga ulionekana.

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)