Kutembea kwa Kikristo mfululizo Index.

Neno kwa kanisa.


  Neno lililo hai mfululizo.

Neno kwa kanisa.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
  Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa.


William Branham.

Pendaneni ninyi kwa ninyi zaidi ya yote. Pendaneni ninyi kwa ninyi Msi... Haidhuru kile shetani anachojaribu kusema! Sasa ninyi ni kundi moja kubwa tamu sasa, lakini kumbukeni onyo langu, unaona, Shetani hawezi kuachia hilo lidumu namna hiyo.

Hapana, bwana. Atatupia kila kitu mshale, ikiwa yeye angemleta mtu fulani ndani amfanye lengo lake. Atamleta ndani mtu mkosoaji au asiyeamini, na kumketisha chini, na kumfanya yeye kushiriki pamoja nanyi chini ya utulivu na mambo ya aina hiyo na ndipo atamtupia yule mtu aina fulani ya sumu, naye ataanza kuzunguka nayo kanisani. Msikae upande wake. Msiwe na chochote cha kufanya na kitu kingine chochote. Mdumu kupendana na wema na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi. Mwombeeni yule mtu, kwamba aokolewe vile vile, au yule mwanamke, au yeyote yule awaye, waombeeni tu. Na shikamaneni ninyi kwa ninyi
Na dumuni na mchungaji wenu. Unaona, Yeye ni mchunga kondoo, nanyi mpeni heshima. Yeye atawaongoza hadi mwisho na kwa sababu yeye ameamriwa na Mungu kufanya hivyo.

Sasa mnalikumbuka hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.” -Mh] Adui atakuja. Naye anapokuja. mshikamane tu pamoja kwa karibu zaidi. Na yule ambaye shetani anamtumia kama adui ama atatoka nje ama aingie ndani na kuwa mmoja wenu. Ni hilo tu.

Kamwe msifanye ukoo miongoni mwenu, au-au kuongea na kujifanyia mshikamano wa kiukoo. Sisi ni wamoja. Singesema “Mkono wa kushoto nimekukasirikia, nitakuondoa kwa sababu wewe si wa mkono wa kulia.” Yeye ni mkono wangu wa kushoto. Nataka akae pale. hata ncha ndogo ya kidole changu, nataka ikae pale pale tukae kila mmoja na mwingine, kila mmoja akae kabisa na mwingine.

Na sasa mnazo kanda juu ya hilo. Mnazo kanda juu ya kile tunachoamini. Mnazo kanda juu ya nidhamu kanisani, jinsi tunavyoenenda kwa kujiheshimu katika kanisa la Mungu, jinsi itupasavyo kuja hapa pamoja na kukaa pamoja katika makao ya Kimbinguni. Msikae nyumbani. Ikiwa Mungu yuko moyoni mwako huwezi kusubiri milango ifunguliwe pale, ili uingie hapa kushiriki pamoja na ndugu zako. Kama huwezi, hujisikii namna hiyo, ni wakati wa kwenda kwenye kuomba.

Bila shaka tuko katika siku za mwisho, pale Biblia ilipoinuka... au ilitufundisha kuku, “Zaidi tuonapo ile siku ikiwadia” kumpenda mwingine kwa upendo wa Kikristo na upendo wa Kiungu, 'kukusanyika wenyewe pamoja katika sehemu za Kimbinguni na-na Kristo Yesu,“ na pendaneni ninyi kwa ninyi. Kwa hili watu wote wajue ninyi ni wanafunzi Wangu, mtakapopendana ninyi kwa ninyi.” Hilo ni sahihi. Kaeni pamoja kila mmoja na mwingine.

Kama unafikiri ndugu amekosea kidogo, au dada, sema “Bwana usiniache kamwe shina la uchungu likachipuka kwa sababu ita-itamuathiri Yeye na itamtoa Kristo nje kutoka katika maisha yangu”. Ile sumu ya tindikali ya nia ya kudhuru wengine na wivu, na chuki, hayo yatamtoa tu Roho Mtakatifu atoke kwako. Itamwondoa Yeye hapa Hekaluni. itamuua Roho wa Mungu, au itamwondoa Yeye atoke hapa, kumsononesha mchungaji wenu. Itafanya kila kitu. Unaona? Msifanye hilo.

Mzidi zaidi kushikana tu karibu pamoja. Vuteni... Chukueni kishikizo kama ndugu alivyoshuhudia mhudumu hapa usiku ule, kuhusu kuwa na bakoli akiona kwenye ono. Tu... Hiyo inafunga pamoja silaha zote za Mungu. Hiyo inafunga pamoja tu, kaza, jongeeni karibu zaidi kila mmoja kwa mwingine, pendaneni ninyi kwa ninyi, kwa vyovyote... Zungumzeni mema kila mmoja juu ya mwingine. Semeni mambo mema kila mmoja kuhusu mwingine na ndipo Mungu atawabariki.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
  Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa.


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)
 

Kristo Ni Siri Ya
Mungu Iliyofunuliwa.

(PDF)

Kabla...

Baada ya...

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Neno lililo hai
mfululizo.

Jina la Mungu.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

  Maandiko Anasema...

Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.

Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.

Isaya 60:1-2