Ubatizo wa Maji.
Ufunuo wa Yesu Kristo.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ufunuo wa Yesu Kristo.Ninakiri ya kwamba inatakiwa ufunuo wa kweli kutoka kwa Roho Mtakatifu kuona ukweli juu ya Uungu siku hizi wakati tuko katikati ya kupotoshwa kwa Maandiko mengi sana. Lakini kanisa lenye nguvu, lenye kushinda limejengwa juu ya ufunuo kwa hiyo tunaweza kumtarajia Mungu kufunua kweli Yake kwetu.
Hata hivyo, kwa kweli huhitaji ufunuo juu ya ubatizo wa maji. Uko papo hapo ukikukodolea macho usoni. Je! ingewezekana katika muda mfupi sana kwa mitume kuongozwa vibaya kutoka kwenye amri ya moja kwa moja ya Bwana kubatiza katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu na halafu uwakute katika kutotii makusudi? Wao walijua hilo Jina lilikuwa ni lipi, na hakuna hata mahali pamoja katika Maandiko ambapo wao walibatiza katika njia nyingine yo yote nje ya Jina la Bwana Yesu Kristo.
Akili ya kawaida ingekwambia ya kwamba Kitabu cha Matendo ni kanisa katika matendo, na kama wao walibatiza namna hiyo, basi hivyo ndivyo inavyopasa kubatiza. Sasa kama unafikiri hilo lina nguvu, unafikiri nini juu ya jambo hili? Mtu ye yote ambaye hakubatizwa katika Jina la Bwana Yesu ilibidi abatizwe tena.
Matendo 19:1-6,
“Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko, akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu tangu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawaambia, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana kweli alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini Yeye atayekuja nyuma yake, yaani, Kristo Yesu. Waliposikia jambo hili, walibatizwa katika Jina la Bwana Yesu. Na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia; nao wakanena kwa lugha na kutabiri.”Hivyo ndivyo ilivyo. Hawa watu wazuri huko Efeso walikuwa wamesikia juu ya Masihi ajaye. Yohana alikuwa amemhubiri. Wao walikuwa wamebatizwa wapate ondoleo la dhambi zao, wakitazamia MBELE wapate kuja kumwamini Yesu. Lakini sasa ilikuwa ni wakati wa kuangalia NYUMA kwa Yesu na kubatizwa ili kupata ONDOLEO la dhambi. Ulikuwa ni wakati wa kumpokea Roho Mtakatifu. Na walipobatizwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo, Paulo aliweka mikono yake juu yao na Roho Mtakatifu akaja juu yao.
Loo! hao watu wapendwa huko Efeso walikuwa ni watu wazuri; na kama mtu ye yote alikuwa na haki ya kujisikia salama, wao walijisikia. Angalia umbali waliokuwa wamekuja. Walikuwa wamesafiri wakafikia umbali wa kumkubali Masihi ajaye. Walikuwa tayari kwa ajili Yake. Lakini huoni ya kwamba ingawa walifanya hivyo walikuwa wamemkosa? Alikuwa amekuja na kuondoka. Walihitaji kubatizwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo. Walihitaji kujazwa na Roho Mtakatifu. Kama umebatizwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo, Mungu atakujaza na Roho Wake. Hilo ni Neno.
Matendo 19:6 ambayo tunasoma ilikuwa kutimizwa kwa Matendo 2:38,
“Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa Jina Lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”Mnaona, Paulo, kwa Roho Mtakatifu, alisema yale hasa Petro aliyosema kwa Roho Mtakatifu. Na lililosemwa HALIWEZI kubadilishwa. Halina budi kuwa vile vile tangu Pentekoste mpaka yule wa mwisho kabisa aliyeteuliwa amebatizwa.
Wagalatia 1:8,
“Lakini ijapokuwa sisi, au malaika wa mbinguni, atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.”Sasa baadhi yenu ninyi watu wa Umoja mnabatiza makosa. Mnabatiza kwa ajili ya kuzaliwa upya kama kwamba kuzamishwa majini huwaokoa. Kuzaliwa upya hakuji kwa njia ya maji; ni kazi ya Roho. Yule mtu ambaye kwa Roho Mtakatifu alitoa ile amri, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja wenu katika Jina la Bwana Yesu,” hakusema ya kwamba maji yalileta kuzaliwa upya. Yeye alisema ilikuwa tu ni ushuhuda wa “dhamiri safi mbele za Mungu.” Ilikuwa ni hayo tu.
1 Petro 3:21,
“Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaotuokoa sisi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu,) kwa kufufuka Kwake Yesu Kristo.”
Ninaamini jambo hilo.Kama mtu ye yote analo wazo lo lote la uongo ya kwamba historia inaweza kuthibitisha ubatizo wa maji katika njia nyingine yo yote mbali na Jina la Bwana Yesu Kristo, ningekushauri usome historia na ujionee mwenyewe. Ifuatayo ni kumbukumbu ya kweli ya Ubatizo uliofanyika huko Rumi 100 B.K. na ukatolewa tena katika Gazeti la TIME la tarehe 5 Disemba, 1955.
“Yule Shemasi akainua mkono wake, naye Publius Decius akaingia kwenye mlango wa mahali pa kubatizia. Marcus Vasca muuza kuni alikuwa amesimama katika kile kidimbwi maji yamemfikia kiunoni. Alikuwa anatabasamu wakati Publius alipokuwa akipita katika kidimbwi akaja akasimama karibu naye. 'Credis?' akauliza. 'Credo,' akajibu Publius. 'Ninaamini ya kwamba wokovu wangu unatoka kwa Yesu aliye Kristo, Ambaye alisulubishwa chini ya Pontio Pilato. Pamoja Naye nilikufa ili kwamba pamoja Naye nipate Uzima wa Milele. Ndipo akasikia mikono yenye nguvu ikimshikilia huku yeye akijiachilia kuanguka kinyumenyume katika kile kidimbwi, ndipo akasikia sauti ya Marcus kwenye sikio lake - 'Nakubatiza katika Jina la Bwana Yesu' - huku maji baridi yakimfunika.”
Hadi mpaka ile kweli ilipopotea (na haikurudi mpaka wakati huu wa mwisho - hii ni kutoka Nikea mpaka mwisho wa karne hii) walibatiza katika Jina la Bwana Yesu Kristo. Lakini umerudi. Shetani hawezi kuuzuia ufunuo wakati Roho anataka kuutoa.
Naam, kama kungalikuweko na Miungu watatu, ungaliweza kubatiza kweli kwa Baba fulani, na Mwana fulani, na Roho Mtakatifu fulani. Lakini ule UFUNUO ALIOPEWA YOHANA ulikuwa kwamba KUNA MUNGU MMOJA na Jina Lake ni BWANA YESU KRISTO, nawe unabatiza kwa Mungu MMOJA na mmoja tu. Hiyo ndiyo sababu Petro alibatiza jinsi alivyobatiza katika Pentekoste. Ilimbidi awe mwaminifu kwa ufunuo ambao ulikuwa, “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini, ya kwamba Mungu amemfanya YESU HUYO, mliyemsulibisha, kuwa BWANA NA KRISTO PIA.” Huyo hapo, “BWANA YESU KRISTO.”
Kama Yesu ni Bwana na Kristo 'PIA,' basi Yeye (Yesu) ni, na hawezi kuwa mwingine ila “Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” katika Nafsi MOJA aliyedhihirishwa katika mwili. SI “Mungu katika nafsi tatu, utatu uliobarikiwa,” bali ni MUNGU MMOJA, NAFSI MOJA yenye sifa tatu kuu, yenye afisi tatu zinazodhihirisha sifa hizo. Lisikieni mara nyingine tena. Yesu huyu huyu ni Bwana na Kristo “PIA.” Bwana (Baba) na Kristo (Roho Mtakatifu) ni Yesu, kwa sababu Yeye (Yesu) ni wote WAWILI (Bwana na Kristo).
Kama hilo halituonyeshi ufunuo wa kweli wa Uungu, hakuna kitakachotuonyesha. Bwana SI mwingine; Kristo SI mwingine. Huyu Yesu ni Bwana Yesu Kristo — MUNGU Mmoja. Filipo siku moja alimwambia Yesu, “Bwana, utuonyeshe Baba na itatutosha.” Yesu akamwambia, “Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote wewe usinijue? Aliyeniona Mimi amemwona Baba, basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Mimi na Baba Yangu ni Mmoja.”
----
Huwezi kumweka Mungu katika nafsi tatu ama sehemu tatu. Huwezi kumwambia Myahudi ya kwamba kuna Baba fulani, na Mwana fulani, na Roho Mtakatifu fulani. Yeye atakwambia upesi sana ambapo wazo hilo lilitoka. Wayahudi wanajua kanuni hii ya imani ilianzishwa kwenye Baraza la Nikea. Si ajabu wao wanatudhihaki kama makafiri.Tunazungumza juu ya Mungu asiyebadilika. Wayahudi wanaamini jambo hilo pia. Lakini kanisa lilimbadilisha Mungu wake asiyebadilika kutoka MMOJA kuwa WATATU. Lakini ile nuru inarudi wakati wa jioni. Ni ajabu iliyoje ya kwamba ukweli huu umekuja katika wakati ambapo Wayahudi wanarudi Palestina. Mungu na Kristo ni MMOJA. Yesu huyu ni BWANA NA KRISTO PIA. Yohana alikuwa na ufunuo, na YESU ndiye aliyekuwa Ufunuo huo, Naye amejionyesha Mwenyewe papa hapa katika Maandiko - “MIMI Ndiye Aliyekuwako, Aliyeko na Atakayekuja, Mwenyezi. Amina.”
Kama ufunuo umekupita, angalia juu na umtafute Mungu uupate. Hivyo ndivyo tu utakavyoupata. Ufunuo hauna budi kuja kutoka kwa Mungu. Hauji kamwe kwa majaliwa ya kibinadamu, ya kawaida, bali kwa uvumilivu wa Kiroho. Unaweza hata kukariri Maandiko, na ingawa hilo ni zuri sana, hilo halitafaa kitu. Haina budi kuwa ni ufunuo kutoka kwa Mungu. Inanenwa katika Neno ya kwamba hakuna mtu anayeweza kusema ya kwamba Yesu ndiye Kristo ila kwa Roho Mtakatifu. Huna budi kumpokea Roho Mtakatifu na ndipo, na ndipo tu, Roho anapoweza kukupa ufunuo ya kwamba Yesu ndiye Kristo: Mungu, Yule Mtiwa Mafuta.
Hakuna mtu anayejua mambo ya Mungu ila Roho wa Mungu na yeye ambaye Roho wa Mungu humfunulia hayo. Tunahitaji kumsihi Mungu kwa ajili ya ufunuo zaidi kuliko kitu kingine cho chote ulimwenguni. Tumeikubali Biblia, tumekubali zile kweli zake kuu, lakini ingali si halisi kwa watu walio wengi kwa sababu ufunuo wa Roho haupo. Neno halijahuishwa. Biblia inasema katika 2 Kor. 5:21 ya kwamba tumekuwa haki ya Mungu kwa muungano wetu na Yesu Kristo. Mlilipata? Inasema ya kwamba SISI NI HAKI YENYEWE YA MUNGU MWENYEWE kwa kuwa KATIKA KRISTO. Inasema ya kwamba Yeye (Yesu) alifanyika Dhambi kwa ajili yetu. Haisemi Yeye Mwenyewe akawa mwenye dhambi, lakini alifanyika DHAMBI kwa ajili yetu ili kwamba kwa kuungana kwetu na Yeye tuweze kufanyika HAKI ya Mungu.
Kama tukikubali kweli hiyo (na hatuna budi kuikubali) kwamba Yeye alifanyika DHAMBI kweli kabisa kwa ajili yetu kwa kupachukua mahali petu, basi hatuna budi kukubali ukweli kwamba sisi kwa kuungana kwetu Naye tumekuwa HAKI YENYEWE ya Mungu. Kukataa hilo moja ni kukataa hilo lingine. Kukubali hilo moja ni kukubali hilo lingine. Sasa tunajua Biblia inasema hivyo. Haliwezi kukanushwa. Lakini ufunuo wake haupo. Si halisi kwa wengi wa watoto wa Mungu. Ni aya nzuri tu katika Biblia. Lakini tunahitaji ifanywe HAI kwetu. Hilo litahitaji ufunuo.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ufunuo wa Yesu Kristo.
Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Matendo ya Mitume 2:36-39
Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Nyakati Saba Za Kanisa.)
Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.