Maono ya Patmo.


  Kitabu cha Ufunuo mfululizo.

Yohana katika Patimo.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Maono ya Patmo.

Ufunuo 1:9-10,
9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo.
10 Nalikuwa katika Roho siku ya Bwana; na nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu.

Mfuatano huu wa maono ya Ufunuo wa Utu wa Yesu Kristo ulitolewa kwa Yohana wakati alipokuwa amepelekwa kwenye Kisiwa cha Patmo. Kisiwa hiki kidogo kiko maili thelathini kutoka pwani ya Asia Ndogo katika Bahari ya Aegean. Kwa kuwa kilikuwa na miamba na kimejaa nyoka, mijusi na nge, kilikuwa na thamani ndogo ya kibiashara, kwa hiyo kilitumiwa na Dola ya Kirumi kama koloni la adhabu ambapo waliwekwa majambazi sugu, wafungwa wa kisiasa, na kadhalika.

Mtaona ya kwamba Yohana amejielekeza kwa Wakristo kama ndugu katika dhiki. Ilikuwa ni wakati huu ambapo kanisa la mwanzoni lilikuwa likipitia katika mateso makuu. Dini yao haikuwa tu “imenenwa kila mahali” bali watu wenyewe walifungwa gerezani na kuuawa. Yohana, kama wengine wengi, sasa alikuwa akifungwa gerezani kwa ajili ya Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. Wakati alipokamatwa, wao walijaribu kumuwua kwa kumchemsha katika mafuta kwa masaa ishirini na manne bila kufanikiwa. Maafisa waliokasirika sana na wasiokuwa na la kufanya basi wakamhukumu kwenda Patmo kama mchawi. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye, naye aliachwa kuondoka katika kisiwa hicho na kurudi Efeso ambako aliendelea tena kama mchungaji mpaka wakati wa kifo chake.

Utukufu wenye sifa saba wa Utu Wake.

Ufunuo 1:14-16,
14 Kichwa Chake na nywele Zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho Yake kama mwali wa moto.
15 Na miguu Yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono Wake wa kuume; na upanga mkali wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa Chake; na uso Wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.

Jinsi kuonekana kwa Yesu kulivyomvutia na kumtia moyo Yohana, ambaye alikuwa uhamishoni kwa ajili ya Neno, na tazama, NENO Lililo Hai sasa linasimama mbele zake. Ni ono linalotia nuru namna gani, kwa maana kila wasifa wa sifa Zake una maana. Ni ufunuo mzuri ulioje wa Utu Wake mtukufu.

1.Nywele Zake Nyeupe kama Sufu.

Yohana kwanza anaona na kutaja weupe wa nywele Zake. Zilikuwa nyeupe, na zenye kung'aa kama theluji. Hii haikuwa ni kwa sababu ya umri Wake. Loo, la. Zile nywele nyeupe na zenye kung'aa sana hazionyeshi uzee bali ujuzi, kukomaa, na hekima. Yule wa Milele haazeeki. Wakati ni nini kwa Mungu? Wakati haumaanishi mengi kwa Mungu, lakini hekima inamaanisha mengi. Ni kama wakati ambapo Sulemani alipomwomba Mungu apewe hekima kuwahukumu watu wa Israeli. Sasa Yeye yuaja, Hakimu wa dunia yote. Atavikwa taji ya hekima. Hiyo ndiyo maana ya nywele nyeupe na zenye kung'aa sana.

Yeye alikuwa ni Hakimu akivifungua vitabu na kuhukumu kwavyo. Danieli alimwona akija katika mawingu. Hivyo ndivyo Yohana alivyoona hasa. Wote wawili walimwona Yeye sawa kabisa. Walimwona Hakimu akiwa na mshipi Wake wa hukumu juu ya mabega Yake, akisimama msafi na mtakatifu, amejaa hekima, amestahili kabisa kuuhukumu ulimwengu katika haki. Haleluya.

2.Macho Yake kama Moto.

Wazia jambo hilo. Hayo macho ambayo wakati mmoja yalififia kwa machozi ya huzuni na huruma. Hayo macho yaliyolia kwa huruma kwenye kaburi la Lazaro. Macho hayo ambayo hayakuona uovu wa wale wauaji waliomsulibisha Yeye msalabani lakini akalia kwa huzuni, “Baba wasamehe.” Sasa macho hayo ni mwali wa moto, macho ya Hakimu Ambaye atawapatiliza wale ambao walimkataa. Katika hisia zote za kibinadamu alizodhihirisha sana kuliko zote wakati alipotokea kama Mwana wa Adamu lilikuwa hili, Yeye alilia mara nyingi. Hata hivyo nyuma ya kulia huko na huzuni hiyo kulikuwa kungali kuna Mungu.

Macho hayo hayo yaliona maono. Yaliangalia ndani katika mioyo ya wanadamu na kujua mawazo yao na njia zao zote mbalimbali. Mungu alikuwa akiangalia kwa macho yawakayo ya kibinadamu, Ambaye aliwaambia wale wasiojua vile alivyokuwa Yeye, “...Msiposadiki ya kuwa Mimi Ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.” Yohana 8:24.
“Kama sizitendi kazi za Baba Yangu, msiniamini; lakini nikizitenda, (kazi za Baba Yangu), ijapokuwa hamniamini Mimi, ziaminini zile kazi...” Yohana 10:37,38.
Kama Yeremia wa zamani, Yeye alikuwa nabii aliaye, kwa maana watu hawakulipokea Neno la Mungu nao waliuwekea kando ufunuo.

Hayo macho yanayowaka moto ya Hakimu yanayowaka kama moto hata sasa yanarekodi maisha ya wanadamu wote. Yakienda mbio huko na huko duniani kote, hakuna kitu asichojua. Yeye anajua shauku za moyo na yale kila mmoja anayotaka kufanya. Hakuna jambo lililofichwa ambalo halitafunuliwa, kwa maana vitu vyote viko tupu machoni Pake Yeye aliye na mambo yetu. Wazia jambo hilo, Yeye anajua hata sasa yale unayowazia.

Naam, Huyo hapo anasimama kama Hakimu mwenye macho makali kama miali ya moto kutoa hukumu. Siku ya rehema imekwisha. Loo! laiti watu wangalitubu na kuutafuta uso Wake katika haki wakati kungali bado kuna wakati. Laiti wangalikifanya kifua Chake mto wa kulalia kabla ulimwengu haujateketea katika moto.

3.Miguu ya Shaba.

“Na miguu Yake ilikuwa kama shaba iliyosuguliwa, kana kwamba imesafishwa katika tanuru.” Shaba inajulikana kwa ugumu wake wa ajabu. Hakuna kitu kinachojulikana ambacho kuchanganya nayo ili kuichezea. Lakini shaba hii inayoeleza miguu Yake ingali ni ya ajabu zaidi kwa kuwa imestahimili moto wa tanuru, jaribio ambalo hakuna kitu kingine kimelipitia. Na hiyo ni kweli kabisa. Kwa maana shaba inaashiria Hukumu ya Kiungu: hukumu ambayo Mungu aliiamuru na kuitimiza.
Hesabu 21:8-9,
Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti: na itakuwa, kila mtu aliyeumwa, aitazamapo, ataishi.
Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikawa, nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Israeli walikuwa wametenda dhambi. Dhambi ilipaswa kuhukumiwa. Kwa hiyo Mungu akamwamuru Musa kuweka nyoka ya shaba juu ya mti, naye aliyeiangalia aliokolewa kutoka katika adhabu ya dhambi yake.

Lakini siku moja miguu hiyo ya shaba itasimama juu ya nchi. Naye atakuwa Hakimu wa dunia yote, Naye atawahukumu wanadamu kwa haki na ukamilifu. Wala hakutakuwako na kuepa hukumu hiyo. Hakuna kugeuza haki hiyo. Hakutakuwa na kuichezea. Mwenye kudhulumu atazidi kudhulumu; mwenye uchafu atazidi kuwa mchafu. Yeye asiyebadilika hatabadilika wakati huo, kwa maana Yeye kamwe hajabadilika wala hatabadilika. Hiyo miguu ya shaba itamponda adui. Itamwangamiza mpinga-Kristo, yule mnyama na ile sanamu na yote yale yaliyo maovu usoni Pake. Ataziangamiza taratibu za makanisa ambayo yamechukua Jina Lake ili tu kupotosha uzuri wake na kuwasagasaga pamoja na mpinga-Kristo. Waovu wote, makafiri, wasiosadiki kuna Mungu, watu wa kisasa, wana mapinduzi, wote watakuwa pale. Mauti, kuzimu, na kaburi vitakuwa pale. Naam vitakuwa pale. Kwa kuwa atakapokuja, vitabu vitafunguliwa. Hapo ndipo hata kanisa lenye uvuguvugu na wale wanawali watano wapumbavu watakapotokea. Atawabagua kondoo na mbuzi. Wakati atakapokuja Yeye atautwaa ufalme, kwa maana ni Wake, na pamoja Naye watakuwepo maelfu mara melfu kumi, Bibi-arusi Wake, anakayekuja kumtumikia. Utukufu! Loo, ni sasa hivi ama sivyo kamwe. Tubu kabla hujachelewa sana. Amka kutoka katika wafu na ukamtafute Mungu ujazwe na Roho Wake la sivyo utakosa uzima wa milele. Fanya hivyo sasa wakati kungali kuna wakati.

4.Sauti Yake Ilikuwa kama Sauti ya Maji mengi.

Sasa maji yanawakilisha nini? Lisikieni katika Ufunuo 17:15,
“...yale maji uliyoyaona,... ni jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha.”
Sauti yake ilikuwa kama sauti ya makutano yakinena. Ni kitu gani? Ni hukumu. Kwa maana hizi ni sauti za makutano ya mashahidi, ambao kwa Roho Mtakatifu katika nyakati zote wamemshuhudia Kristo na kuihubiri Injili Yake. Itakuwa ni sauti ya kila mtu ikisimama katika hukumu dhidi ya mwenye dhambi ambaye hangekubali kuonywa. Sauti za wale wajumbe saba zitasikika kwa sauti kuu na dhahiri. Hao wahubiri waaminifu waliohubiri nguvu za wokovu wa Yesu, waliohubiri ubatizo wa maji katika Jina la Yesu, waliohubiri kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu, waliosimama na Neno kuliko walivyosimama na maisha yao wenyewe; wote walikuwa ni sauti ya Yesu Kristo kwa Roho Mtakatifu katika zile nyakati zote. Yohana 17:20,
“Wala si hao tu ninaowaombea, lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya Neno lao.”

Loo! laiti tu ungaliliona jambo hilo. Maji ndiyo yaliyouangamiza ulimwengu, lakini yalikuwa ni maji yale yale ambayo yaliyomwokoa Nuhu na pia yakaiokoa dunia yote kwa ajili ya Nuhu. Isikilizeni sauti Yake, sauti ya watumishi Wake, inapowaita kwenye toba na uzima.

5.Katika mkono Wake wa kuume Kulikuwako Nyota Saba.

“Naye alikuwa na nyota saba katika mkono Wake wa kuume.”
Sasa bila shaka tayari tunajua kutoka kwenye kifungu cha ishirini nyota hizo saba ni nini hasa. “Na siri ya zile nyota saba ni malaika (wajumbe) wa yale makanisa saba.” Sasa tusingeweza kufanya kosa hapa kwa sababu yoyote, kwa kuwa Yeye hutufasiria jambo hilo. Hizi nyota saba ni wale wajumbe kwa zile nyakati saba za kanisa zinazofuatana. Hawatajwi kwa majina. Wao wameandikwa tu kama saba, mmoja kwa kila wakati. Tangu Wakati wa Efeso na kuendelea mpaka kwenye Wakati huu wa Laodikia kila mjumbe alileta ujumbe wa kweli kwa watu, bila kukosea kuliweka hilo Neno la Mungu katika wakati huo huo tu wa kanisa. Kila mmoja alishikilia hilo. Wao walikuwa thabiti katika uaminifu wao kwa ile nuru ya kwanza. Kwa kuwa kila wakati wa kanisa ulikuwa unawacha Mungu, mjumbe wake mwaminifu aliurudisha wakati huo kwenye Neno. Nguvu yao ilikuwa inatoka kwa Bwana la sivyo hawangeweza kamwe kuyastahimili mawimbi. Walikuwa salama wakiwa katika ulinzi Wake, kwa kuwa hakuna kitu kingaliweza kuwapokonya kutoka katika mkono Wake, na wala hakuna kitu kingaliweza kuwatenganisha na upendo wa Mungu, iwe ni maradhi, hatari, uchi, njaa, upanga, uzima au mauti. Walikuwa wamejisalimisha kwa dhati na kulindwa na nguvu Zake zote. Wao hawakuyajali mateso yaliyowakabili. Uchungu ama dhihaka hazikuwa ni kitu cho chote bali sababu ya kumpa Mungu utukufu ya kwamba walihesabiwa kwamba wanastahili kuteswa kwa ajili Yake. Na katika shukrani kwa ajili ya wokovu Wake waliangaza kwa nuru ya uhai Wake na wakadhihirisha mng'ao wa upendo Wake, subira, upole, kiasi, unyenyekevu, uaminifu. Na Mungu aliwaunga mkono kwa maajabu, ishara, na miujiza. Walishtakiwa kuwa washupavu wa dini, na watakatifu wanaojifingirisha. Walishutumiwa na madhehebu na kudhihakiwa, bali walidumu waaminifu kwa Neno.

Na faraja hii si kwa ajili ya wale wajumbe saba wa wakati wa kanisa. Kila mwamini wa kweli yumo katika mkono wa Mungu na anaweza kunywa katika upendo Wake na nguvu Zake, na kupata fadhili zote za yale yote Mungu aliyo kwa mwamini. Yale Mungu anayompa mjumbe huyo, na jinsi anavyombariki na kumtumia hayo mjumbe, ni mfano kwa waamini wote juu ya wema Wake na malezi Yake kwa washiriki WOTE wa mwili Wake. Amina.

6.Upanga wenye makali kuwili.

“Na katika kinywa Chake mlitoka upanga wenye makali kuwili.”
Katika Waebrania 4:12,
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”
Katika kinywa Chake kulitoka upanga mkali wenye makali kuwili ambao ni NENO LA MUNGU.

Sasa Paulo alisema ya kwamba Neno lilikuja katika nguvu na katika sauti. Neno lililohubiriwa kweli lilijidhihirisha. Kama upanga uwakao na kukata liliingia katika dhamira za watu, na kama kisu cha mpasuaji lilikata likaondoa magonjwa na kuwafungulia wafungwa. Kila mahali waamini hawa wa mwanzoni walipoenda, “Walienda wakihubiri Injili (Neno) na Mungu alithibitisha Neno hilo kwa ishara zilizofuata.” Wagonjwa waliponywa, pepo walitolewa, nao walinena kwa lugha mpya. Hilo lilikuwa Neno likitenda kazi. Neno hilo halijashindwa kamwe katika vinywa vya Wakristo wanaoamini. Na katika wakati huu wa mwisho liko hapa likiwa na nguvu zaidi na likiwa kuu zaidi kuliko lilivyowahi kuwa katika bibi-arusi Neno wa kweli. Loo! enyi kundi dogo, enyi kusanyiko dogo, shikilieni Neno, jaza kinywa chako na moyo kwalo, na siku moja Mungu atakupa ule ufalme.

7.Uso Wake kama Jua.

Katika Ufunuo 21:23,
“Na mji ule hauhitaji jua, wala mwezi, kuuangaza: kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.”
Huu ni Yerusalemu Mpya. Mwana-Kondoo atakuwa katika mji huo, na kwa sababu ya uwepo Wake, hakutahitajika nuru: Jua halitachomoza na kuwaka kwake, kwa kuwa Yeye ndiye Jua na Nuru yake, Yeye Mwenyewe. Mataifa watakaoingia ndani yake watatembea katika nuru Yake. Je! wewe hufurahi ya kwamba siku hiyo imetufikia? Yohana aliona siku hiyo ikija. Hata hivyo, Bwana Yesu, njoo upesi!

Malaki 4:1-3,
1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru: na watu wote wenye kiburi, naam, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi: na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa Majeshi, hata haitawaachia shina wala tawi.
2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha Jina Langu Jua la Haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa Zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu katika siku ile niifanyayo, asema Bwana wa Majeshi.

Hilo hapo tena. JUA likiangaza katika nguvu zake zote. Loo, nguvu za Mwana wa Mungu zikiangaza katikati ya vile vinara vya taa saba vya dhahabu. Huyo hapo amesimama, Hakimu, Yeye aliyeteseka na kufa kwa ajili yetu. Alichukua hasira ya hukumu ya Kiungu juu Yake Mwenyewe. Yeye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu peke Yake. Kama tulivyokwisha kusema, kwa mwenye dhambi sauti Yake ni kama sauti ya maporomoko ya maji ama mawimbi meupe yakitwanga katika mawimbi ya mauti kwenye ufuko wenye miamba. Lakini kwa mtakatifu, sauti Yake ni kama sauti ya kijito kinachoimba kwa utamu unapolala starehe, umeridhika katika Kristo. Akiangaza juu yetu kwa miali Yake ya upendo ya joto, Yeye anasema, “Usiogope, Mimi ndimi Niliyekuwako, Niliyeko, Ninayekuja; Mimi ni Mwenyezi. Hakuna mwingine ila Mimi. Mimi ni Alfa na Omega, ni YOTE.” Yeye ndiye Ua la Uwandani, Nyota Yenye Kung'aa ya Asubuhi. Yeye ndiye mzuri sana kuliko elfu kumi nafsini mwangu. Naam, siku hiyo kuu iko karibu kupambazuka na Jua la Haki litazuka lenye kuponya katika mbawa Zake.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Maono ya Patmo.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Nami nilipomwona, nalianguka miguuni Pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono Wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho,

Na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele, Amina; Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

Ufunuo 1:17-18.



Kitabu cha Ufunuo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Mti wa Uzima. Dhambi ya asili.)


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Yeye ni I kuwa
ni nani.

Kristo. Katika
dhahabu ya kinara.

Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

The Two Babylons

by Rev Alexander Hislop.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima
na mwaridi katika
theluji nchini China.

Lilies ya Moto.

 
 
 

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.