Siku hiyo pale Kalvari.

<< uliopita

ijayo >>

  Ufufuo Mfululizo.

Ni siku muhimu sana!


William Branham.
 

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Siku hiyo pale Kalvari.

Luka 23:33,
Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto.

Ni siku muhimu sana! Ni moja ya siku muhimu sana katika siku zote ambazo Mungu aliwahi kupambazuka duniani. Na kama ni muhimu sana kwa jamii ya binadamu, Kalvari, nafikiri ni vema kwetu kurudi nyuma na kulichunguza, na tuone maana yake kwetu. Kwa maana, nina hakika, katika saa hii ya mwisho tunayoishi, tunatafuta kila umuhimu wa Mungu ambao tunaweza kujua. Na yote tuwezayo kujua, tuko hapa kujifunza habari zake, kuona yale yaliyo kwa ajili yetu, na yale ambayo Mungu ametufanyia, na kuona yale Yeye ameahidi kutufanyia. Na hiyo ndiyo sababu ya sisi kuja kanisani.

Hiyo ndiyo sababu mhubiri huhubiri, hiyo ndiyo sababu anajifunza na kutafakari Maandiko, na kutafuta uvuvio, ni kwa sababu yeye ni mtumishi wa umma kwa watu wa Mungu. Naye anajaribu kupata kitu ambacho kitaninii… ambacho Mungu angepaswa kuwaambia watu Wake, kitu ambacho kingewasaidia. Labda, huenda ikawa, kuwahukumu katika dhambi zao, bali ingekuwa msaada wa kuwainua, kusudi wapate kuziacha dhambi zao kisha wainuke ili wamtumikie Bwana. Na wahudumu wanapaswa kutafuta mambo haya.

Iwapo siku hii ni muhimu sana, moja ya siku zilizo kuu sana, hebu na tuangalie mambo matatu ambayo siku hiyo ilimaanisha kwetu. Tungeweza kuchukua mamia. Lakini, asubuhi ya leo, nimechagua tu mambo matatu mbalimbali, muhimu tunayotaka kuangalia, kwa dakika chache zijazo, ambayo Kalvari ilimaanisha kwetu. Nami naomba ya kwamba itamhukumu kila mwenye dhambi aliyeko, ya kwamba itamfanya kila mtakatifu kupiga magoti yake, ya kwamba itamfanya kila mgonjwa ainue imani yake kwa Mungu na aondoke ameponywa, kila mwenye dhambi aokolewe, kila aliyerudi nyuma arudi na ajionee aibu, na kila mtakatifu afurahi na apate kitu kipya cha kushikilia na tumaini jipya.

Jambo moja kuu muhimu ambalo Kalvari inamaanisha kwetu na ulimwengu ni, ilimaliza swali la dhambi mara moja tu. Mwanadamu alipatikana na hatia ya dhambi. Na dhambi ilikuwa ni adhabu ambayo hakuna mtu angeweza kulipa. Adhabu ilikuwa kubwa sana hata hapakuwapo na mtu ye yote ambaye angeweza kulipa adhabu hiyo. Kwa kweli ninaamini ya kwamba Mungu alilikusudia namna hiyo, ya kwamba adhabu ingekuwa kubwa sana hivi kwamba hakuna mtu angaliweza kuilipa, ili aweze kuifanya, Mwenyewe. Sasa, adhabu ya dhambi ilikuwa mauti. Nasi sote tulizaliwa katika dhambi, tukaumbwa katika uovu, tukaja ulimwenguni, tukisema uongo. Kwa hiyo hapakuwapo na mmoja wetu aliyestahili, ama, wasingeweza kumpata mtu yeyote duniani aliyestahili.

Na dhambi haikuanza duniani. Dhambi ilianza Mbinguni. Lusifa alikuwa... Lusifa, Ibilisi, alikuwa kiumbe kilichohukumiwa, kwa sababu ya kutotii kwake, kabla hajaipiga dunia. Dhambi ilianza Mbinguni, ambapo Mungu aliwaweka Malaika, na kadhalika, juu ya msingi ule ule aliowaweka wanadamu; maarifa, mti wa maarifa, mti wa Uzima na mti wa maarifa, ambapo mwanadamu angeweza kuchukua chaguo lake. Na Lusifa alipopewa mamlaka ya kuchagua, yeye alitaka kitu bora kuliko kile alichokuwa nacho Mungu. Hilo lilisababisha shida.

Na kulikuweko na deni la dhambi. Madai yake yalikuwa mauti. Adhabu ilikuwa mauti. Na, hiyo ni, tungeweza kuzungumzia hili kinaganaga, kwa maana siamini kuna mauti ila moja. Kuna Uzima mmoja. Ninaamini mtu aliye na Uzima wa Milele hawezi kamwe kufa. Nami ninaamini kuna kuangamizwa kabisa kwa mtu huyo anayetenda dhambi, kwa kuwa Biblia ilisema, “Nafsi itendayo dhambi, hakika itakufa.” Si mtu huyo; “Nafsi itendayo dhambi.” Kwa hiyo, hakika Shetani hana budi kufa, apate kuangamizwa kabisa. Jinsi ambavyo sikubaliani na walimwengu wote wanaosema ya kwamba Shetani ataokolewa! Alitenda dhambi, naye ndiye mwanzilishi wa dhambi. Na nafsi yake ilitenda dhambi; Naye alikuwa ni roho. Roho hiyo itaangamizwa kabisa, kusiwepo kitu cho chote kilichosalia.

Nayo dhambi ilipoingia duniani kule nyuma mwanzoni kama shuka nyeusi ikishuka kutoka mbinguni, ilipoozesha dunia. Ilikitupilia kila kiumbe duniani, na viumbe vyote vya Mungu, utumwani. Mwanadamu alikuwa chini ya utumwa wa mauti, magonjwa, shida, huzuni. Viumbe vyote vikaanguka pamoja naye. Dhambi ndiyo nusukaputi ambayo kweli iliipoozesha dunia. Na ndipo tukawekwa humu, tumekata tamaa, kwa sababu kila kiumbe duniani kilitiishwa chini yake. Na kila mmoja iliyezaliwa duniani alitiishwa chini yake. Kwa hiyo ilipaswa kuja kutoka mahali fulani ambako hakuna dhambi. Isingeweza kutoka duniani. Mmoja wetu asingeweza kumkomboa huyo mwingine. Ilipaswa kutoka kwa mwingine.

Kwa hivyo, mwanadamu alipotambua ya kwamba alikuwa ametenganishwa na Mungu wake, akawa mzururaji. Walilia. Walipaza sauti. Walitaabika. Wakazunguka-zunguka milimani, na katika jangwa, wakiutafuta mji ambao Mwenye Kuujenga na Mwenye Kuubuni ni Mungu. Kwa kuwa, yeye alijua ya kwamba kama angewahi kurudi katika Uwepo wa Mungu, angeweza kuzungumza jambo hilo pamoja Naye. Lakini hakukuwa na njia ya kurudi. Alipotea. Hakujua aelekee upande gani, kwa hiyo alitoka tu, akitangatanga, akijaribu kutafuta mahali fulani ambapo angeweza kupata njia ya kurudi Mahali hapo. Kitu fulani ndani yake kilimwambia ya kwamba alitoka kwenye— Mahali palipo kamili. Hakuna mtu hapa katika wasikizi hawa waliopo hapa asubuhi ya leo, ama katika wasikizi wa kanda za sumaku ambako zitasambazwa duniani kote, hakuna hata mmoja hapa ama po pote pale, ila yule anayeutafuta ule ukamilifu.

Unalipia bili zako, unafikiri, “Hilo litamaliza.” Unapolipia bili zako, ndipo kuna mtu mgonjwa katika familia yako. Magonjwa yanapokwisha, ndipo una bili nyingi zaidi za kulipa. Punde si punde nywele zako zinapata mvi, ndipo unataka kurudia ujana. Na kuna jambo fulani kila wakati, daima, kwa sababu ya hilo wimbi la dhambi. Lakini moyoni mwako, kwa kuwa unatafuta hilo, inaonyesha ya kwamba kuna ukamilifu mahali fulani. Kuna kitu mahali fulani.

-----
Hatimaye, siku moja, hiyo ni ile siku pale Kalvari, Mtu mmoja akashuka akaja kutoka Utukufuni. Mmoja, kwa Jina la Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, aliyetoka Utukufuni, na Kalvari ikatengenezwa. Hiyo ndiyo siku ambayo gharama ililipwa, na swali la dhambi likatatuliwa milele. Naye akafungua njia ya kitu hiki tunachokionea njaa na kukionea kiu. Ilileta mahali pa utoshelevu. Hakuna mtu aliyepata kutembelea Kalvari na kuona jinsi ilivyokuwa, anayeweza kubaki alivyokuwa. Kila alichoonea shauku au kutamani sana kinapatikana anapofika mahali hapo.

Ilikuwa ni siku muhimu sana, na jambo muhimu sana, liliutikisa ulimwengu. Iliitikisa ulimwengu jinsi ambavyo haujatikiswa hapo awali, Yesu alipokufa pale Kalvari naye akalilipia swali la dhambi, dunia hii yenye dhambi ilitiwa giza kabisa. Jua lilitua mchana nalo likazimia roho kwa wasiwasi. Miamba ikatikisika, milima ikapasuka, miili ya waliokufa ikafufuka ghafla kutoka kaburini.

Ilifanya nini? Mungu akalenga shabaha pale Kalvari. Alimjeruhi huyo mnyama, aitwaye Shetani, milele. Sasa yeye amekuwa mkali zaidi tangu wakati huo, kwa sababu ilileta Nuru kwa jamii ya binadamu. Na kila mtu anajua ya kwamba mnyama aliyejeruhiwa ndiye mkali sana, anayetambaa huku amevunjika mgongo. Sasa, Shetani alitupwa nje, pale Kalvari. Dunia ilithibitisha ya kwamba ilikuwa hivyo. Gharama kuu sana iliyopata kulipwa, na Mtu pekee ambaye angeilipia, alikuja na akafanya hivyo pale Kalvari. Hapo ndipo gharama kubwa ilipolipwa. Hilo ni moja ya mambo.

Mungu alihitaji hilo. Hakuna mtu aliyestahili. Hakuna mtu aliyeweza. Hakuna mtu angaliweza kufanya hivyo. Ndipo Mungu akaja, Mwenyewe, na akafanyika mwanadamu, na akaishi maisha ya kibinadamu, chini ya tamaa za kibinadamu, na akasulubiwa pale Kalvari. Na pale, wakati Shetani alipodhani kwamba Yeye asingelifanya hivyo, kwamba Yeye asingelistahimili, Yeye aliistahimili Gethsemane na kila jaribu lililowahi kumkabili mwanadamu. Yeye alipitia huko kama watu wote, lakini Yeye akalipa ile gharama.

Na hiyo ndiyo iliyoitia giza kabisa dunia nzima Kama ile nusukaputi ya kumtia ganzi mtu anapofanyiwa upasuaji. Daktari anapompa mtu hiyo nusukaputi, kwanza humfanya apoteze fahamu kabla hajafanya upasuaji. Naye Mungu alipolifanyia kanisa u-pasuaji, ulimwengu ulipata nusukaputi, maumbile yakapata mshtuko mkubwa sana. Si ajabu! Mungu, katika mwili wa kibinadamu, alikuwa akifa. Ilikuwa ndiyo saa ambayo ulimwengu ulikuwa umeitazamia, hata hivyo wengi wao hawakuijua.
Kama ilivyo siku hizi, watu wengi wanayatazamia mambo haya, hata hivyo hawayatambui. Hawatambui njia ya kutokea. Wao wangali wanajaribu kutafuta anasa na mambo ya ulimwengu, wakijaribu kutafuta njia ya kutokea.

Kumekuwa, na vibao vingi vilivyoelekeza kwenye siku hiyo, vivuli vingi vikuu. Ilikuwa ameoneshwa na kivuli cha mwana-kondoo, na fahali, na hua, na mambo haya yote, lakini hata hivyo yasingeweza kuivunja. Yasingaliweza kuvunja hiyo ngome ya mauti. Kwa kuwa Shetani aliitawala dunia. Miamba ile ile ambayo wakati mmoja alitembea, juu yake huku na huko duniani, kiberiti kilichowaka moto. Lusifa alikuwa mwana wa asubuhi, naye alitembea duniani wakati ilipokuwa volkeno inayowaka moto. Miamba hiyo hiyo iliyokuwa imepata baridi, wakati Yesu alipokufa Kalvari, ilibubujika toka ardhini.

Gharama iliyopwa, na utumwa wa Shetani ukavunjiliwa mbali. Mungu akairudisha mkononi mwa mwanadamu, njia ya kurudia kile alichokuwa akitafuta. Haikumpasa kulia tena. Akapiga, wakati Yeye alipouvunja uti wa mgongo wa Shetani, kule Kalvari, uti wa mgongo wa dhambi, wa magonjwa! Na hiyo ikamrudisha kila mwanadamu, duniani, katika uwepo wa Mungu, huku dhambi zimesamehewa. Haleluya! Dhambi zetu zimesamehewa. Shetani hawezi tena kututia giza akatuondoa kwa Mungu. Kuna njia kuu iliyotengenezwa. Kuna simu iliyowekwa pale. Kuna simu inayoelekea Utukufuni, inamleta kila mtu karibu na simu hiyo. Kama mtu amejaa dhambi, inamuunganisha na kituo chaa kati. Anaweza kusamehewa dhambi hiyo. Si hivyo tu, bali dhambi hiyo imelipiwa. Loo! Haikubidi kusema, “Mimi sistahili.” Hakika, haungeliweza, kamwe kustahili. Lakini Mtu anayestahili alichukua mahali pako. Wewe uko huru. Haikubidi kutangatanga tena. Si lazima uwe mtu wa kutafuta anasa hapa duniani. Kwa:

Kuwa damu imebubujika,
Ni ya Imanueli,
Ambapo wenye dhambi walioga chini ya kijito,
Husafiwa kweli.

Haikupasi kupotea. Kuna njia kuu, na Njia, nayo inaitwa Njia ya utakatifu. Mwenye taka haipitii. Kwa kuwa yeye huja kwenye chemchemi, kwanza, kisha anaingia katika njia kuu.

Alivunja nguvu za Shetani. Aliifungua milango ya gereza la kuzimu, kwa kila mtu aliyefungiwa, katika dunia hii, katika magereza, akiogopa wakati wa kufa, kile mauti yangefanya kwake. Pale Kalvari, Yeye aliifungua hiyo milango ya gereza, na kumwachilia huru kila mfungwa. Haikubidi tena kunyanyaswa na dhambi. Haikubidi tena kuvitoa viungo vyako kufanya dhambi, kunywa pombe, kuvuta sigara, kucheza kamari, kusema uongo. Unaweza kuwa mwaminifu, mwenye haki, na mnyofu. Wala Shetani hawezi kufanya lo lote kuhusu hilo, kwa kuwa umeshikilia kamba, kamba ya kuokolea, imetiwa nanga katika Mwamba Wenye Imara. Hakuna kitu kinachoweza kukutikisa kutoka Kwake. Hakuna upepo unaoweza kukutikisa kutoka Kwake. Hakuna kitu, hata mauti yenyewe, inayoweza kututenganisha na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu. Hivyo ndivyo Kalvari ilimaanisha.

Watu waliokuwa utumwani waliwekwa huru. Watu ambao wakati mmoja walikuwa chini ya hofu ya mauti hawawezi tena kuogopa mauti. Mtu anayeuonea shauku mji, ambao Mwenye Kuujenga na Mwenye Kuubuni, ni Mungu, anaweza kutembea katika njia iliyo kuu, na kuuelekeza uso wake Mbinguni, kwa sababu yuko huru. Haleluya! Yeye amekombolewa. Yeye hahitaji kutangatanga tena, kwa maana kuna njia ya kujua kama uko sahihi au la. Mungu hutupa Uzima. Dhambi zetu zimeondolewa. Siku hiyo pale Kalvari gharama ililipwa.

-----
Kwanza, inatupasa kutafuta kujua maana ya siku hiyo. Pili, inatupasa kuona yale hiyo siku iliyotufanyia, sasa vile ilivyotufanyia. Sasa, ya tatu, hebu na tuone yanayotupasa kuifanyia siku hiyo. Tunapaswa kufanya nini?
Kwanza, inatupasa kuichunguza, kwa kuwa ni siku kuu, siku iliyo kuu kuliko siku zote. Gharama ya dhambi ilimalizika. Nguvu za Shetani zilivunjwa.

Na sasa tunataka kuona kile tunachopaswa kufanya katika kurudi. Sasa mahali pake, Yesu alipokufa msalabani, pale Kalvari siku hiyo, Yeye hakulipa tu gharama ya dhambi zetu, bali alilipa gharama hiyo na pia akatufanyia njia tupate kumfuata Yeye; kwa maana sisi, kama Adamu aliyeanguka ambaye amekombolewa, Kama Roho alivyomwongoza Adamu (Adamu wa kwanza) kwa Roho, ambaye alikuwa na mamlaka juu ya maumbile yote, ndipo sisi (Adamu wa pili), ama watu wa duniani tumekombolewa na Kristo, tangu siku hiyo pale Kalvari, tunaweza kumfuata Yeye. Sasa, wakati alipokufa pale Kalvari, alifanya njia. Alitoa Roho, Roho Mtakatifu, ambaye alimtuma arudi duniani, kwa ajili yako na mimi tupate kuishi kwake. Hiyo ndiyo maana ya Kalvari kwetu, kumfuata Yeye.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Siku hiyo pale Kalvari.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

2 Wakorintho 5:17


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Chapter 9
- The Third Pull

(PDF Kiingereza)

Kabla...

Baada ya...

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.