Muhuri Wa Tano.

<< uliopita

ijayo >>

  Mihuri Saba mfululizo.

Roho zilizo chini ya madhabahu.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Tano.

Ufunuo 6:9-11,
9 Na alipoifungua muhuri ya tano nikaona chini ya madhabahu roho zaowaliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwanao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mwenye kweli,hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu yanchi?
11 Nao wakapewa kila mmojanguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado mu- muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao pia... ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.

Sasa, kwa namna fulani jambo hili ni la kisiri. Na sasa kwa ajili ya kanda, na makasisi na waalimu wanaoketi hapa, sasa, kama una maoni tofauti na Haya; nilikuwa nayo, mimi pia. Lakini ninayachukua tu kutokana na uvuvio, ambao ulibadilisha kabisa maoni yangu juu ya jambo Hilo. Unaona? Na ndipo ninaona, kama mtakavyoona hii ikifunuliwa, Hilo linarudi mojakwa moja huko nyuma na kuunganisha hizo nyakati za kanisa na Maandiko moja kwa moja pamoja, na kulifungamanisha. Unaona? Na hiyo ndiyo sababu kwamba ninaamini ya kwamba Hilo linatoka kwa Mungu.

-----
Angalia, hakuna kutajwa kwa Mnyama mwingine, ama Mwenye uhai-Mwenye uhai, kwenye huku kutangazwa kwa Muhuri wa Tano. Sasa kumbuka, alikuwako, kwenye Muhuri wa Nne. Alikuwako, kwenye Muhuri wa Kwanza, wa Pili, wa Tatu, na wa Nne, lakini hakuna ye yote hapa. Unaona? Sasa, kama ukiangalia, hebu na tusome tu nyuma, moja ya ile Mihuri. Hebu na turudi kwenye Muhuri wa Nne, unaona. Na hiyo ni aya ya 7. Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo uone! ...alipoi-... alipoifungua muhuri ya tatu, yule mwenye uhai wa tatu akisema, Njoo uone! nikasikia sauti ya-ya ...ya mwenye uhai wa pili,... Njoo uone! ...na mwenye uhai wa kwanza, Njoo uone!

Lakini tunapofikia Muhuri wa Tano, hakuna Mnyama. Sasa angalia tu. Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu... Upesi sana! Unaona, hakuna-hakuna Mwenye Uhai pale. Na Mnyama anawakilisha nguvu. Tunajua jambo hilo, unaona. Hakuna Mwenye Uhai. Sasa, mmoja wa hao Wenye Uhai, tunaona, katika kusoma ule-ule-ule ufunuo katika makanisa, ya kwamba mmoja wao alikuwa... alikuwa ni simba; na huyo mwingine-huyo mwingine alikuwa ni ndama; na huyo mwingine alikuwa ni mwanadamu; na huyo mwingine alikuwa ni tai. Tunaona, katika nyakati za kanisa, ya kwamba hao Wenye Uhai wanne, wakimaanisha nguvu nne, walikuwa wamekizunguka Matendo ya Mitume, jinsi tu vile ile-ile maskani jangwani.

-----
Angalia. Lakini, hapa, tunapokuja kwenye Muhuri huu wa Tano sasa, hakuna- hakuna- hakuna mpanda farasi anayetoka kwenda, wala hakuna Mwenye Uhai wa kuutangaza. Yohana alininii tu... Mwana- Kondoo aliufungua, na Yohana akauona. Hapakuwapo na mtu hapo wa kusema, “Sasa njoo, utazame. Njoo, uone.” Angalia, hapakuwapo na nguvu za huyo Mwenye Uhai. Ama hakuna... Na kwenye ule Muhuri waSita, hakuna Mwenye Uhai wa kuutangaza. Na kwenye Muhuri wa Saba, hakuna Mwenye Uhai wa kuutangaza. Hakuna nguvu za kuutangaza. Unaona, hakuna mtu anayeutangaza. Kwenye ninii... Angalia. Kwenye ninii... Baada ya Muhuri wa Nne, hakuna tangazo la nguvu zo zote za Mwenye Uhai, kutoka Muhuri wa Tano, Sita, ama wa Saba, hakuna kabisa.

Sasa angalia. Ninapenda jambo hili. Kama vile katika wakati wa yule mpanda farasi wa wale farasi wanne, yule mpanda farasi (umoja) wa wale farasi wa nne tofauti, kulikuwako na Mnyama ambaye alitangaza zile nguvu. Kila wakati huyo mpanda farasi alipomtandika farasi mwingine na akaja kumpanda, Mwenye Uhai wa aina nyingine alitokea na kutangaza jambo hilo, “Hiyo ni siri kuu.” Unaona?“ Hiyo ndiyo ile siri.” Kwa nini? Anatangaza siri.

Kwa nini hakuna mtu hapa kwenye Muhuri wa Tano, kuutangaza? Ni hivi, kulingana na ufunuo ambao Bwana Yesu alinipa leo, unaona, ama asubuhi ya leo, alfajiri. Hiyo ni, kwa sababu, ile siri ya nyakati za kanisa imekwisha tayari, kwenye wakati huu. Ile siri ya mpinga-Kristo imefunuliwa, kwenye wakati huu. Mpinga-Kristo aliendesha farasi mara yake ya mwisho, nasi tulimwona kwenye farasi wake wa kijivujivu, amechanganyika katika rangi zake nyingi, naye anaenda moja kwa moja mpaka upotevuni. Tutapata jambo hilo kwenye zile Baragumu, na kadhalika, tutakapofundisha jambo hilo. Ningeliliendea sasa, lakini tutaondoka kabisa kwenye somo hili tena.

-----
Sasa, kwa kuwa wao, wakati huu, kama ukiangalia, huu Muhuri wa Tano ukifunguliwa, unaona, Kanisa limekwisha ondoka. Haiwezekani tu kabisa, roho chini ya-lile Kanisa la mwanzoni. Sasa, sasa, tafadhali, kama ulipata kulisikiliza jambo hili kwa makini sasa, maana huu ndio ubish-... ubishi mkubwa, kwa hiyo nawatakeni msikilize kwa makini sana sasa. Na mna makaratasi yenu, na vitu vya kuandikia. Sasa, nawatekeni mwone.

Sasa, hizi haziwezi kuwa ni hizo roho. Maana, ro- roho za- za wenye haki, wafia imani, na watu wenye haki, Kanisa, Bibi-arusi,tayari zimenyakuliwa, kwa hiyo hawangekuwa chini ya madhabahu. Watakuwa Utukufuni, pamoja na Bibi-arusi. Sasa angalia. Kwa kuwa, wamekwenda katika uleUnyakuo, katika mlango wa nne wa Ufunuo. Walitwaliwa juu. Sasa, hizi roho ni akina nani, basi? Hilo ndilo jambo linalofuata. Ni akina nani, basi, kama wao si kile Kanisa la mwanzoni? Hawa ni Israeli ambao wataokolewa kama taifa, wote ambao wamechaguliwa tangu zamani. Hao ni Israeli. Hao ni Israeli, wenyewe. Unasema, “Loo! ngoja kidogo.” Unasema, “Haiwezekani kuwa ni wao....”

Loo! naam, wao wataokolewa. Hapa, hebu na tulitatue, dakika moja. Nina Maandiko manne ama matano. Nitachukua moja. Hebuna tuchukue Warumi, dakika moja, tuone kama ndio wao. Hebu tuchukue Kitabu cha Warumi, na twende kwenye-kwenye sura ya 11 ya Warumi, nasi tutaona. Ninii tu... Hebu na tulisome tu, na ndipo tutalipata sisi wenyewe binafsi. Warumi, sura ya 11, aya ya 25 na 26. Sasa msikilizeni Paulo hapa. Basi Paulo alisema, “Kama mtu mwingine ye yote, hata Malaika, akihubiri injili nyingine yo yote,” (ati nini?) “alikuwa alaaniwe.” Angalia. Kwa maana, ndugu zangu,sipendi msiijue siri hii, (a-ha), ili msijione kuwa wenye akili (naam); ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

-----
Angalia. Sasa ninawatakeni mwangalie jambo hili kwa makini sana. “Wakapewa nguo ndefu.” Wao hawakuwa nazo. Walipewa nguo ndefu, nguo ndefu nyeupe, kila mmoja wao. Sasa, watakatifu wanazo sasa, tayari wanazo; wanazipata hapa. Lakini, pale, “Wakapewa nguo ndefu.” Nao watakatifu tayari walikuwa na zao, na wameondoka. Unaona? Unaona? Wao walikuwa-hawakuwa... Wao, unaona, hawakuwa na nafasi, kwa maana walipofushwa na Mungu, Baba yao Mwenyewe; ili kwamba neema ya Mungu ingeweza kutimizwa, ili kwamba Bibi-arusi apate kuchukuliwa kutoka kwa Mataifa. Hiyo ni kweli?

-----
Sasa angalia. Wao walikuwa, katika upofu wao, wamemwua Masihi wao, na sasa wao walikuwa wakijutia jambo hilo. Walifahamu hilo. Walilitambua, baada yakupita. Walimwona wakati huo, walipokuja mbele ya madhabahu ya Mungu. Lakini sasa neema ya Mungu iko juu yao. Angalieni. Sasa, wao wasingeweza, kwa namna yo yote, kuwa ni watakatifu, maana wao tayari wamepewa nguo ndefu. Lakini hawa hapa sasa, ni “roho chini ya madhabahu, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda waliokuwa nao” tu, kwamba wao ni watu wa Mungu, Wayahudi. Lakini sasa, angalieni, neema ya Mungu inawajilia. Na Yesu anawapa, kila mmoja wao, nguo ndefu nyeupe, (loo! jamani! angalia; moja kwa moja huko ng'ambo, baada ya Kanisa kuondoka), kwa sababu walikuwa waaminifu kwa msimamo wao. Nao walipofushwa, wala hawakujua jambo hilo. Hawakulijua. Walikuwa wakitekeleza kikamilifu sehemu ile ambayo Mungu alikuwa amewakusudia kuitekeleza. Na hapa, hapa, Yohana anaangalia kule ng'ambo na kuona roho chini ya madhabahu. Sasa angalia, yeye anaziona hizo roho. Angalia vile anavyoziita. Zinalia, “Bwana, hata lini?” Angalia! “Muda kidogo tu zaidi.” (Hebu tupate jambo hilo, tunapoendelea mbele, kupitia moja kwa moja katika Maandiko sasa.)

Wao wanafahamu walikuwa wamemwua Masihi wao. Unaona? Wala hawakujua jambo hilo, lakini baadaye walitambua. Wao waka-wao wakauawa, vivyo hivyo,kulipia jambo hilo hapo, kwa kutenda mabaya. Na sasa angalia ni jambo gani walilopaswa kufanya! Unaona, walikuwa na hatia ya kuua, kwahiyo wakauawa. Mnaona? Walipiga makelele, “Damu Yake na iwe juu yetu!” Mnaona? Hiyo ni kweli. Nao walipofushwa. Sasa, kama wao hawangekuwa wamepofushwa; Mungu alisema. “Waacheni. Wao hawastahili.” Lakini kwa kuwa walipofushwa na Mungu, neema Yake iliwashukia. Amina! Nena kuhusu neema ya ajabu! Na kumpa kila mmoja wao nguo ndefu, kwa maana Israeli wote wataokoka, kila mmoja aliyeandikwa jina lake. Hiyo ni kweli.

-----
Sasa angalia Wayahudi hawa. Sina budi kufanya jambo hili, kusudi niwaonyeshe ufunuo wa Muhuri huu; mwone ni kitu gani, roho hizi chini ya madhahabu, na kwamba wao ni akina nani. Sasa angalieni. Katika wakati wa Danieli, sasa, ile sehemu ya pili yalile juma la sabini. Sasa kumbukeni, “Masihi alikuwa akatiliwe mbali katikati.” Yaani katikati. Vema, nusu ya saba ni nini? [Kusanyiko linasema, “Tatu na nusu.-Mh.] Tatu na nusu. Kristo alihubiri muda gani? [”Mitatu na nusu.“] Hiloni sawa. Sasa, ”Lakini kumekusudiwa bado, kwa watu,“ (kitu gani?) ”miaka mingine mitatu na nusu.“

Vema, katika kipindi cha wakati huu, mbona, unaona, yale yanayotukia, ni kwamba, Bibi-arusi Mmataifa anachaguliwa katika nyakati saba za kanisa, na anapaa juu. Na wakati hilo linapotendeka, Wayahudi hawa wote ambao waliuawa kwa ajili ya imani yao kule kwa sababu ya upofu, wakiwa wamepumzika chini ya madhabahu, Mungu anakuja na kusema, “Mnaona ilikuwa ni kitu gani? Sasa nampa kila mmoja wenu nguo ndefu nyeupe.” Wakasema, “Hata lini, Bwana? Je! Tunaingia sasa?” Kasema, “La, la, la, la. Wajoli wenu, Wayahudi, hawana budi kuteseka kidogo, bado. Hawana budi kuuawa kama mlivyouawa. Yule mnyama hana budi kuwatesa wakati atakapovunja agano lake.”

-----
Ni-ni-ninajisikia wa ajabu-ajabu tu kidogo, unaona. Unaona? Angalia, kama wengine wanafikiri... Ninawataka mwelewe na jambo hili sasa, mnaona. Kama wengine wangali wanafikiri ya kwamba Malaki 4, “kuwarejesha” watu, ni jambo lile lile atakalofanya kule kwa Wayahudi, na anafikiri yote ni mamoja, hebu nilinyoshe jambo hilo kwa ajili yenu, dakika moja tu. Unaona, lingekuwa jambo la kutatanisha kidogo. Maana, kumbukeni, katika Malaki 4, inasema, “Kuigeuza Imani ya baba zao...ama watoto iwaelekee baba zao.” Mnaona, kuwarudia baba zao!

Sasa hebu niwaonyeshe tofauti za huduma hiyo. Kama akija kuigeuza Imani ya watoto iwaelekee baba zao, yeye angemkana Kristo. Angerudi kwenye torati. Hiyo ni kweli? Baba walishika torati. Mnafahamu jambo hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Angalia, wakati Elisha, wakati alipokuja kuitimiza huduma yake katika Malaki 4, unaona, kama Malaki 4, Eliya alikuwa peke yake. Lakini anapokuja kuwahudumia Wayahudi, wa Ufunuo 11, ameambatana na Musa. [Ndugu Branham anapiga makofi mara mbili-Mh.] Kwa hiyo, hakuna utata, hata kidogo. Unaona? Mnaelewa jambo hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.”] Wakati Elisha anapokuja, wa Malaki4, yuko peke yake. Eliya atatekeleza; si Eliya na Musa. “Eliya” atatokea.

Lakini upako ule ule, ambao, ulisema Eliya atakuja kwa ajili ya sehemu ya mwisho ya wakati wa kanisa, “kuigeuza Imani ya watoto ielekee kwenye Imani asili ya baba zao,” Imani ya mitume, ambayo mnapaswa kuirudia. Na mpinga-Kristo amewavuta akawatoa wote nje. “Kuigeuza,” kama vile Maandiko mengine yote yalivyopatana. Unaona, yeye anakuja peke yake. Unaona? Lakini atakapokuja kwa Kanisa, Biblia... ama atakapokuja kwa wale mia na arobaini na nne elfu, Biblia inasema dhahiri ya kwamba yeye pamoja na...Wako wawili, si mmoja wao. Wawili!

Na huduma yake ya kwanza haingeweza kuwachukua Wayahudi na kuwarudisha kwenye torati, kwa sababu yeye... maana yeye anakuja, akimhubiri Kristo kwa wale mia na arobaini na nne elfu, amina, “Huyo hapo, yule Masihi aliyekatiliwa mbali.” Amina! Hivyo ndivyo ilivyo, kwa hiyo usilichanganye. Si la utata. Maandiko hayasemi uongo, hata kidogo. Utukufu! Loo! nilipoona jambo hilo, nilikuwa nikiruka! Nikasema, “Asante, Bwana,” nilipokuwa nikiangalia jambo hilo likitukia pale. Nilimwona Eliya akienda zake pale kwa ajili ya ule wakati wa kwanza, akiwa peke yake, naye alikuwa peke yake. Halafu nilipomwona akija tena, huko mbali akielekea mahali pengine, walikuwa ni wawili pale wakati jambo hilo lilipotukia. Kasema, “Hilo hapo. Hilo, hilo latosha, Bwana. Amina! Ninaliona sasa! Haleluya!” Hilo ni kweli kabisa. Kama sikuwa nimelitaja, lingekuwa kidogo linamtatiza mtu. Lakini Yeye-Yeye aliniambia niseme jambo hilo, kwa hiyo nimelisema.

Angalia, watu hawa wamehifadhiwa hai na Mungu, toka katika huduma yao ya kwanza, kwa ajili ya huduma ya siku za usoni; waliitumikia vizuri sana. Unaona? Wazieni tu, roho hiyo ya Eliya inahudumu mara tano; Musa, mara mbili. Ati nini? Wamewekwa hai kwa ajili ya huduma yao ijayo, huduma ijayo. Wala hakuna mmoja wa hao wawili aliyekufa sasa; msiamini jambo hilo. Wote wawili walionekana, wakiwa hai, wakizungumza na Yesu kwenye Mlima wa Kugeuzwa Sura. Lakini, kumbukeni, wao hawana budi kufa.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Tano.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa uzito.

Warumi 11:7


Wao walikuwa,
katika upofu wao,
wamemwua Masihi
wao, na sasa wao
walikuwa wakijutia
jambo hilo.


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)

Mteremko wa mlima na mwaridi katika theluji nchini China.

Chapter 13
- God is Light

(PDF Kiingereza)

Kabla...

Baada ya...


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.