Muhuri Wa Tatu.

<< uliopita

ijayo >>

  Mihuri Saba mfululizo.

Mpanda farasi mweusi.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Tatu.

Ee, Mungu tusaidie! Loo! Tutasimamia hapa tu. Lakini, Mungu tusaidie kuona sasa, ombi langu, tunapokuja sasa. Maana, Sitaki kuwakawisha sana. Mungu tusaidie kuona. Ninaamini labda, Roho akiwa juu yetu, ingekuwa ni sasa hivi ambapo angetusaidia kufunua, kufungua Muhuri huu. Hebu na tusome. Tunapoona hali lilimo kanisa, tunaona mahali lilipokuwa, tunaona kile walichofanya, tukaona mahali linapopaswa kufikia, tunaliona pale, na tunaona yale waliyopaswa kufanya. Walifanya jambo hilo hilo. Sasa mnaona mahali tulipo? Wewe toa uamuzi. Mimi siwezi kuamua. Mimi ninawajibika tu na kuleta Neno hili. Jinsi tu ninavyopewa, ndivyo ninaweza kulitoa. Mpaka nilipewe, siwezi kulitoa; hakuna mtu mwingine awezaye.

Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo uone! Nikaona, na tazama, farasi mweusi; na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, lakini usiyadhuru mafuta wala divai.

-----
Sasa, angalia mahali tulipo, usiku wa leo, ule wakati mwingine wa kanisa sasa. Unaona? Tunakuja kwenye wakati wa tatu wa kanisa sasa. Unaona? Tuko katika wakati wa tatu wa kanisa barabara kabisa, ni sawasawa kabisa kama tu yule farasi wa tatu. Unaona? Sasa, wakati wa kwanza wa kanisa, ulikuwa ni nini? Wanikolai walikuwa na fundisho, unaona, wa kwanza tu. Vema. Na basi, muda si muda tunajua, fundisho hili la Wanikolai, liliidhinishwa na likawa sawa, likaanza kutenda kazi. Nao wakamtia taji jamaa huyu. Ndipo, roho hii, mpinga-Kristo, ikafanyika mwili katika mtu fulani. Unaona? Nasi tunaona, baadaye, yeye anakuwa Ibilisi mwilini, pia; pepo anaondoka, na Ibilisi anaingia.

Na kama tu vile kanisa lile ni la namna hiyo, kanisa la mpinga-Kristo, linavyosonga mbele; vivyo hivyo Bibi-arusi amekuja na mambo mbalimbali: kupitia kuhesabiwa haki, kutakaswa, ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kuendelea moja kwa moja, unaona, namna hiyo tu. Ila tu, wao walipata uamsho wao kwanza, nalo Kanisa linaupata wake mwisho. Miaka yao mitatu ya kwanza...hatua za kwanza tatu za hao waliopitia kwenye wakati wa giza; halafu ya tatu, hatua tatu, Kanisa linatoka; kutoka kwenye kuhesabiwa haki, kutakaswa, ubatizo wa Roho Mtakatifu, katika Mungu aliyefanyika mwili akidhihirishwa kati yetu.

Huyu hapa anakuja, kama mpinga-Kristo, kama nabii wa uongo, halafu mnyama, halafu katika wakati wa giza. Na kanisa linatoka katika wakati huo wa giza; kuhesabiwa haki, kutakaswa , ubatizo wa Roho Mtakatifu, Neno lililofanyika mwili, ndio njia sasa. Naye anashuka anaenda. A-ha. Unaona jambo hilo? Yeye anashuka anaenda. Kanisa linapaa juu. Unaona? Ni jambo kamilifu kabisa tu linavyoweza kuwa. Loo! linapendeza. Ninalipenda tu.

Mpanda farasi huyu ni yule yule, lakini hatua nyingine ya huduma yake. Hatua ya kwanza, farasi mweupe, unaona, yeye alikuwa ni mwalimu tu, ni mwalimu mpinga-Kristo tu. Yeye alikuwa kinyume cha Neno la Mungu. Na sasa unawezaje kuwa mpinga- Kristo? Mtu ye yote anayekana ya kwamba kila neno la hii si kweli, na kufundishwa vile vile lilivyo, ni mpinga- Kristo, ‘maana wao wanakana Ne-Ne-Neno. Naye ni Neno.

-----
Sasa, sasa hii hapa siri ya jambo hili. Na sasa, Hiyo, wakati Yenyewe iliponifunulia kwangu alfajiri na mapema leo, kabla hakujapambazuka. Ndipo nikaenda upesi kwenye Maandiko na kuanza kuangalia, kulichunguza. Hiyo hapo. Mitatu kati ya Hiyo, kufikia wakati huu, imefunuliwa dhahiri kimbinguni. Naam. Sasa hii hapa siri ya yule farasi mweusi, kulingana na vile ilivyofunguliwa kwangu.

Yeye alianza kumpanda katika wakati wa nyakati za giza. Hilo ndilo farasi mweusi alilowakilisha, zile nyakati za giza, kwa maana ilikuwa ni wakati wa usiku wa manane kwa waamini wa kweli waliosalia. Angalieni sasa katika wakati ule wa kanisa, wakati huo wa katikati wa kanisa, wakati wa giza wa kanisa. Angali jinsi Yeye anavyosema, “Una nguvu kidogo tu.” Ilikuwa ni usiku wa manane kwao, kwa mwamini wa kweli. Sasa angalia. Karibu kila tumaini lilikuwa limeondolewa katika Kanisa la kweli, kwa maana jamaa huyu alitawala kanisa na taifa pia. Watafanya nini? Unaona, Ukatoliki ulikuwa umetawala, kanisa na taifa pia. Na wote ambao hawakukubaliana na Ukatoliki, waliuawa. Hiyo ndiyo sababu alikuwa amepanda farasi mweusi. Basi angalia jinsi ulivyotenda jambo ovu, unaona, ndipo unaweza kuona. Nawe unaninii tu... Kama unajua historia yako, iangalie, ndipo utaninii... Vema, hata haitakubidi kuijua, ku-kujua jambo Hili. Sasa angalia. Tumaini lote lilikuwa limekwisha. Huyo ndiye farasi wake mweusi. Sasa, yeye alimpanda farasi wake mweupe, ujanja.

Kisha akapewa mamlaka; akaondoa amani, akaua mamilioni. Hivyo ndivyo alivyokuwa anataka kwenda kufanya alipompanda akienda zake. Na angali anafanya jambo hilo. Unaona? Sasa, huyu hapa yuko juu ya farasi wake mweusi sasa, akijitokeza. Wakati wa giza, huu ulikuwa ndio wakati ule. Mnamo wakati tu baada ya kanisa kuimarika, na likapata mamlaka, walinyamazisha kila kitu kinginecho. Na likasafiri moja kwa moja, yapata, mamia na mamia na mamia ya miaka, ndiyo kila msomaji anavyojua kama nyakati za giza. Ni wangapi wanaojua jambo hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Ndiyo, zile nyakati za giza. Huyo hapo farasi wako mweusi, akiwakilisha wakati ule wa giza. Sasa, matumaini yote yalikuwa yamekwisha; hakuna tumaini lo lote. Kila kitu kilionekana ni giza, kwa maskini wale waamini wachache. Sasa, hiyo ndiyo sababu unaitwa, uliwakilishwa na farasi mweusi.

“Mizani zake, ama mizani zake, mkononi mwake,” unaona. Akipaza sauti, “Kibaba cha ngano na nusu rupia, na vipimo vitatu vya shayiri kwa nusu rupia.” Unaona, kwa kweli, hiyo ni kusema, ngano na shayiri ni vitu vya maisha ya kawaida. Hivyo ndivyo vinavyotengeneza mkate na kadhalika. Lakini, unaona, yeye alikuwa akiwatoza pesa kwa ajili ya vitu hivi. Maana yake, ni kwamba, yeye alikuwa akiwatoza pesa raia wake kwa ajili ya tumaini la maisha alilokuwa anawapelekea, kwa kufanya... Yeye alianzia katika wakati huo huo, wa kuwafanya walipie maombi. Waangali wanafanya jambo hilo; maombi ya siku tisa mfululizo.

Maana, yeye alikuwa anafanya nini? Akichukuwa utajiri wa ulimwengu. Ile mizani, akipima, “Kibaba cha ngano kwa nusu rupia; vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia.” Yule mpanda farasi aliyempanda farasi mweusi, unaona, yeye alikuwa akifanya... akiwanyang’anya raia wake pesa zao. Wakati, Biblia inabashiri ya kwamba yeye anashikilia, karibu, utajiri wote wa ulimwengu. Kama tulivyosema jana usiku juu ya Urusi, na yote hayo, ya kwamba wao wanachukuwa pesa zote tu na kunyang’anya watu tu kila walichokuwa nacho, kila kitu. Kwa hiyo, hivyo ndivyo ilivyo.

-----
Angalia. Hii hapa sehemu nzuri sasa. Angalia. ...wala usiiadhuru divai hii na mafuta. “Ni kidogo tu kilichobakia pale, lakini usikiguse Hicho!” Sasa, mafuta ni... yanawakilisha Roho, Roho Mtakatifu. Nitawapa vifunngu vichache mkitaka. Kuna Maandiko mawili. Katika Mambo ya Walawi, 8:12, ambapo Haruni, kabla hajaingia, ilimbidi kutiwa mafuta, mnajua. Na katika Zakaria 4;12, juu ya mafuta yakimiminika kupitia katika mabomba, kisha akasema “Hii ni Roho Yangu, Mafuta.” Jambo lingine, kama ukitaka kuona Mathayo, 14...25, kulikuwako na mwanamwali mjinga, ama 25:3, yule mwanamwali mjinga hakuwa na Mafuta, hana Roho. Na Mathayo 25:4, yule mwanamwali mwerevu alikuwa na Mafuta kwanye taa yake, amejazwa Roho. Roho! Mafuta ni mfano wa Roho. Loo, utukufu! [Ndugu Branham anapiga makofi mara moja-Mh.] Vema. Mnalipata? [Kusanyiko linasema “Amina.’’] Vema.

Sasa, mafuta yanamwakilisha Roho. Na divai inawakilisha changamko la ufunuo. Loo, kaa-karibu nikimbie huku na huko kila mahali. Nashangaa sikuwaamsha majirani, wakati Bwana aliponionyesha jambo hilo, unaona, “changamko la ufunuo.” Unaona? Mafuta na divai, katika Biblia, vinahusiana pamoja, siku zote. Nilichukua itifaki na kuangalia. Kuna mlolongo wa hayo, hiyo-nama hiyo, ambapo divai na mafuta vinaambatana, siku zote. Unaona?

Wakati Kweli ya Neno la Mungu lililoahidiwa imefunuliwa kwa kweli kwa watakatifu Wake ambao wamejazwa na Mafuta, wote wanachangamka. Divai ni mchangamko. Utukufu! Ninalihisi hivi sasa. Kuchangamshwa na furaha, vifijo! Unaona? Na, inapofanyika hivyo, ina matokeo yale yale kwao ambayo-ambayo divai huwa nayo kwa mtu wa kawaida. Kwa sababu, wakati ufunuo umetolewa, wa Kweli ya Mungu, na mwamini wa kweli aliyejazwa na Mafuta, na ufunuo unafunuliwa, kuchangamka kunakuwa kukuu mno mpaka Yeye anamfanya kutenda isivyo kawaida. Kweli. Utukufu! [Kusanyiko linafurahi-Mh.] Unaona, hicho ndicho kinachowatukia basi. Hiyo ni kweli, kunawafanya watende isivyo kawaida.

-----
Wakati nikiona kwamba Mungu aliahidi kufanya jambo fulani katika siku hii, wakati Yeye aliahidi kuvunja Mihuri hii katika siku ya mwisho! Na hamjui hiyo furaha, huo utukufu, wakati nilipomwona Yeye akifunua jambo hili, nikisimama pale na kuliona likitukia! Na kujua ya kwamba nitamchukuwa mtu ye yote, kumwamuru: Yeye kamwe hajawahi kutuambia jambo moja ila lililotukia vile vile. Halafu kuona furaha iliyo moyoni mwangu, nionapo ahadi Yake kwa ajili ya hizi siku za mwisho, kama alivyoahidi kufanya. Na hapa naliona Hilo limethibitishwa na kufanywa kamilifu sana.

Mimi ni niniii tu... Mnasikia nikisema, “Ninajisikia wa kidini.” Sababu yake ni hiyo. Lile changamko ni kubwa sana, karibu ni-ni-niko tu-tu kuanza kukatika vipande vipande, unajua. Changamko, kutokana na ufunuo! Vema. Wao walichangamka sana, kwa u-ufunuo, hata wao walithibitisha,vema, ile ahadi. Sasa, loo, jamani! Hapo ilitokea furaha ya kuchangamka, mpaka watu wakasema, “Wamelewa kwa mvinyo mpya,” wakati Mungu alipofunua ahadi Yake kwao. Na si kwamba tu Yeye alifunua, bali aliithibitisha. Hivyo ndivyo nilivyosema daima. Mtu anaweza kusema jambo lolote, naam, yeye angeweza tu kuwa hodari kusema lolote; lakini wakati Mungu anapokuja kuthibitisha jambo hilo!

Sasa Biblia ilisema, “Kama kuna mtu mmoja kati yenu, anayedai kwamba ni wa kiroho au ni nabii, kama akisema mambo haya na yasitimie, basi msimjali. Msimwogope, hata kidogo. Msimwogope mtu huyo. Lakini akilisema na litimie; huyo ni Mimi, unaona. Mimi, Mimi niko katika jambo hilo. Hilo linathibitisha kwamba ni Mimi vipi.”

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Tatu.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

2 Petro 3:10-11


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)

Nguzo ya Moto -Bega.

 
 

Lilies ya Moto.

 
 
 

Magari ya vita
ya Moto.

Elijah kukamatwa
akiwa up.

Nguzo ya Moto
- Houston 1950

Mwanga juu ya
mwamba piramidi.


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.