Muhuri Wa Pili.
<< uliopita
ijayo >>
Farasi nyekundu mpanda farasi.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Pili.Na sasa, usiku huu, tunajifunza Muhuri huu wa Pili. Na katika hii Mihuri minne ya kwanza kuna wapanda farasi wanne. Nami nawaambieni, leo jambo fulani lilitukia tena. Na, mimimimi, jambo fulani ambalo mimi... Ninakwenda na kuchukua maandishi ya zamani niliyokuwa nayo, niliyoyahubiri, siku nyingi zilizopita, na nikaketi tu chini pale. Nami nikawazia, “Vema, ni-nilijitahidi sana nilivyoweza.” Na waandishi wengi na mambo, basi nikawazia, “Vema, nitasoma kidogo, kisha nichunguze na nione jambo hili na lile.” Ndipo muda si muda wajua, mara jambo fulani linatendeka, na ni kitu tofauti kabisa. Linatokea tu vinginevyo. Ndipo ninanyakua penseli upesi sana, na kuanza kuandika haraka niwezavyo, wakati Yeye akiwa angalipo.
-----
Sasa , jana jioni, kama daima tunavyopendelea, katika kufundisha juu ya-juu ya ile Mihuri, tunaifundisha kwa njia ile ile mnayofanya juu ya-juu ya zile nyakati za kanisa. Na wakati tulipomaliza kufundisha juu ya wakati wa kanisa, wakati wa mwisho nilipozichora hapa mi-mimbarani, ubaoni, ni wangapi wanaokumbuka yaliyotukia? Yeye alishuka moja kwa moja, akaenda moja kwa moja kule nyuma ukutani, katika Nuru, na kuzichora, Yeye Mwenyewe, pale pale ukutani, mbele yetu sote.Malaika wa Bwana alisimama papa hapa mbele ya watu mia kadha. Na sasa Yeye-Yeye anafanya jambo fulani la kimbinguni kweli kweli sasa, pia, na kwa hiyo tunatarajia tu mambo makuu. Hatujui...Unapenda kungojea tu hayo-hayo matarajio makuu, hatujui tu litakalotukia tena, unajua, unaninii tu-unaongeaje tu. Sasa, jinsi Mungu alivyo mkuu kwetu, na jinsi alivyo wa ajabu! Tunamfurahia sana!
Sasa, aya ya 1 na ya 2, nitaisoma, kuweka msingi kidogo kwa namna fulani. Kisha tutachukua aya ya 3 na ya 4, kwa ajili ya Muhuri wa Pili. Halafu aya ya 5 na ya 6 ni Muhuri wa Tatu. Na ya 7 na ya 8 ni ile... Aya mbili kwa kila mpanda farasi. Na sasa nawatakeni mwangalie jinsi jamaa hawa... Kuhusu farasi huyu wa kijivu, labda... Huyu hapa anakuja, anaendelea tu kubadilika anapoendelea mbele.
Na ndipo ule Muhuri mkuu, Muhuri wa mwisho kufunguliwa, Mungu akipenda, Jumapili ijayo usiku! Ambapo, jambo hilo lilipotukia, kulikuwa tu na ninii, jambo pekee lililotukia, “ilikuwa ni kimya Mbinguni kwa muda wa nusu saa.” Mungu atusaidie. Sasa nitasoma aya ya ya 3 sasa.
Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo uone! Akatoka farasi mwingine,... (aya ya 4) ...mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi... ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Sasa, jambo la siri sasa, wakati yu-yule Mwenye Uhai alipomwambia Yohana, “Hebu njoo tu uone.” Naye hakuona ilikuwa ni kitu gani. Aliona mfano tu. Na mfano huo, sababu ya huo mfano... Alisema, “Njoo uone,” lakini aliona mfano, ambao alikuwa auonyeshe kwa kanisa, katika njia ambayo wao wangengoja; mpaka itakapofikia kwenye wakati wa mwisho, na ndipo Muhuri huo ungefunguliwa.
Sasa, kila mtu anaelewa na hilo sasa, mnaona, ile Mihuri itafunguliwa. Basi hivi ninyi hamna furaha kuishi katika siku hii? [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Hilo, mnaona, si hilo tu, enyi wapendwa, lakini daima kumbukeni sasa, Jumapili iliyopita asubuhi, pale ambapo jambo hilo lote liliwekewa msingi, urahisi! Mnaona? Rahisi, nyenyekevu, linatendeka kwa njia ambayo watu wanalipita tu na hata hawajui Hilo linatukia. Na, kumbukeni, tunakutazamia kule Kuja kwa Bwana, wakati wowote. Na wakati sisi... Nilitoa tamshi, ya kwamba labda mimi Kunyakuliwa kutakuwa jinsi hiyo hiyo. Kutapita, kupite, na hakuna mtu atakayejua habari zake. Kutatukia tu namna hiyo. Mnaona? Na kwa kawaida... Rudi tu nyuma upitie kwenye Biblia uangalie jinsi linavyotukia namna hiyo. Mnaona?
Hata jambo kuu kama kule kuja kwa Bwana Yesu, hakuna mtu aliyejua lolote juu yake. Wao walidhani, “Huyo mwenda wazimu, mtu fulani.” Makanisa yalisema, “Ni mshupavu tu wa dini. Sisi...Yeye kweli ana kichaa.” Yasema “Yeye ni mwenda wazimu.” “Tunajua wewe ni mwenda wazimu.” Mwenda wazimu maana yake ni “kichaa.” “Tunajua una pepo, na amekutia kichaa. Nawe ati unajaribu kutufundisha sisi? Wakati, Wewe ulizaliwa huko, isivyo halali. Sisi... Wewe ulizaliwa katika uasherati. Ati unajaribu kuwafundisha watu kama sisi, makuhani, na kadhalika, hekalu?” Vema, jamani, huko kulikuwa ni kuwatukana.
Yohana alipokuja, alikuwa amenenwa habari zake, kote kote katika miaka mingi iliyopita, tangu Isaya mpaka Malaki. Hiyo ni miaka elfu moja mia mbili... ama miaka mia saba na kumi na miwili, aliyokuwa ameishaonwa na manabii, akija. Kila mtu alikuwa akimtazamia aje, akilitarajia jambo hilo wakati wowote. Lakini jinsi alivyokuja, yeye alihubiri na kutimiza huduma yake, kisha akaenda Utukufuni.
Wala hata mitume hawakujua jambo hilo, kwa maana wao walimwuliza Yeye. Walisema, “Sasa, kama-kama Mwana adamu anakwenda Yerusalemu, mambo haya yote, ya Yeye kutolewa dhabihu,” wakasema, “mbona Maandiko husema ya kwamba ‘Eliya hana budi kuja kwanza’?” Yesu akasema, “Amekwisha kuja tayari, wala hamkutambua hilo. Naye alifanya sawasawa na Maandiko yalivyosema atafanya. Nao walimfanyia sawasawa na yale aliyoandikiwa.” Unaona? Nao walimfanyia sawasawa na yale aliyoandikiwa.” Nao hawakuweza kufahamu hayo. Yeye akasema, “Iikuwa ni Yohana.”
Na, ndipo, “Loo!” Unaona, wao-wao wakazinduka, katika jambo hilo. Wao... Na wakati, hata, hatimaye, baada ya mambo yote Yeye- Yeye aliyokuwa amefanya, na ishara alizowaonyesha, na hata alikuwa amewaita. Kasema, “Ni nani kati yenu awezaye kunihukumu Mimi nina dhambi, kutokuamini? Kama sijafanya sawasawa kabisa na yale Maandiko yalivyosema kwamba huduma yangu itafanya nitakapokuja duniani, basi nionyesheni mahali ambapo nimetenda dhambi. Unaona? Ndipo nitanitawaonyesha kile mnachopaswa kuwa, na hebu tuone kama mnaamini jambo hilo, au la.” Mnaona? Angalirudi moja kwa moja na kusema, “Mlipaswa kuniamini Mimi nilipokuja.” Hawakumwamini, mnaona, kwa hiyo walitahadhari kumtegea, kwenye jambo hilo. Lakini Yeye alisema, “Ni nani kati yenu anayeweza kunihukumu Mimi juu ya kutokuamini? Mnaona? Je! Mimi sikufanya jinsi vile ilivyotakiwa?”
-----
Sasa, kwanza yeye aliitwa mpinga-Kristo. Hatua ya pili, aliitwa nabii wa uongo, kwa maana roho huyo miongoni mwa watu alifanyika mwili. Mnakumbuka, yule mpanda farasi mweupe sasa hakuwa na taji wakati alipoanza, lakini baadaye yeye angeninii... alipewa taji. Kwa nini? Alikuwa ni roho ya Unikolai, kwanza; na baadaye akafanyika mwili katika mwanadamu; na halafu akavikwa taji, na akapokea kiti cha enzi na kuvikwa taji. Na ndipo akatumika namna hiyo kwa muda mrefu, kama tutakavyoona tunaponinii... Mihuri inapovunjwa. Na halafu tunaona, baada ya muda huo mrefu, Shetani alifukuzwa kutoka Mbinguni. Naye akashuka, kulingana na Maandiko, na kujitawaza mwenyewe. Wazia tu, akajifanyia kiti cha enzi mwenyewe katika mtu huyo, ndipo akawa mnyama. Naye alikuwa na mamlaka, mamlaka kuu sana, kama vile alivyofanya, miujiza yote na kila kitu, ambayo-ambayo, ama mauaji na vita vya umwagaji damu na kila kitu ambachoambacho Rumi ingeweza kutunga.-----
Sasa huu hapa ufunuo wangu wa jambo hili. Huyu ni Shetani, tena. Ni Ibilisi, tena, katika umbo lingine. Sasa, tunajua ya kwamba-ya kwamba Mihuri ilihusu... kama nilivyosema juzi usiku. Na baragumu zinahusiana na vi-vi-vita vya wenyewe kwa wenyewe, unaona, miongoni mwa watu, miongoni mwa mataifa. Lakini unaona, hapa, ya kwamba mtu huyu ana upanga, kwa hiyo anahusiana na kanisa, vita vya kisiasa. Sasa huenda usifikiri hivyo, lakini angalia tu jambo hilo kwa dakika moja, dakika chache tu.Angalia badilisho la rangi la farasi hawa. Mpanda farasi yule yule; badiliko la rangi ya farasi. Na farasi ni mnyama. Na mnyama, katika Biblia, chini ya mfano fulani, anawakilisha nguvu. Ni utaratibu ule ule ukipanda farasi wa rangi nyingine, nguvu, kutoka nyeupe isiyo na hatia mpaka aliye mwekundu kama damu. Unaona? Mwangalieni sasa, jinsi anavyokuja.
Wakati alipoanza mara ya kwanza, yeye alikuwa ninii tu, vema, alikuwa ni fundisho dogo tu katika-katika, miongoni mwao, lililoitwa Unikolai. Bila shaka, haungeweza kuua chochote. Hiyo ni Ufunuo 2:6, kama mkitaka kuliandika. Yeye hangeua chochote. Ni fundisho tu, ni roho fulani tu miongoni mwa watu. Sasa, yeye hangeua chochote. Loo, alikuwa asiye na hatia kabisa, akimpanda farasi huyu mweupe. “Vema, unajua, tunaweza kuwa na kanisa kubwa la ulimwenguni kote. Tungeweza kuliita kanisa la ulimwengu mzima.” Wangali wanaliita hivyo. Vema. Unaona? Sasa, “Tungeweza kuwa na ninii...” Loo, halina hatia kabisa. Na, loo, halina hatia kabisa. “Ni kundi tu la watu. Tutaungana sote kwa ajili ya ushirika.” Unaona, hana hatia kabisa; ni mweupe, alikuwa ni farasi mweupe. Unaona?
-----
Tazama. Angalia. Wakati Shetani... Sasa, kila mtu, ambaye, anatambua ya kwamba Shetani anatawala nguvu zote za siasa za ulimwengu. [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Yeye alisema hivyo. Mathayo mlango wa 4, mtalipata, na kifungu cha 8. Falme zote ni zake. Hiyo ndiyo sababu wanapigana, wanapigana vita, wanauana. Sasa kumbuka. Je! jambo hilo si ni la ajabu? Walipewa upanga huu, wapate kuuana. Loo, loo, loo, jamani! Angalia sasa. Sasa, wakati alipofanya jambo hilo, hakuwa na nguvu za kidini bado. Lakini alianza na pepo la mafundisho ya uongo. Na mafundisho hayo yakawa kanuni. Kanuni hiyo ikafanyika mwili katika nabii wa uongo. Na basi akaenda moja kwa moja mahali penyewe kabisa. Hakwenda Israeli, sasa. Alikwenda Rumi; Nikea, Rumi.Walifanya baraza, nao wakachagua askofu mkuu. Na ndipo, kwa kufanya jambo hili, waliunganisha kanisa na taifa pamoja. Ndipo, akaangusha uta wake. Akashuka kwenye farasi wake mweupe. Akampanda farasi wake mwekundu, kwa maana anaweza kuua mtu yeyote asiyekubaliana naye. Huo hapo Muhuri wako. Jamaa yule yule! Mwangalie akipanda akielekea huko Umilele, pamoja naye, unaona, anaunganisha nguvu zake mbili pamoja.
-----
Sasa, sasa kumbukeni, yeye ana upanga. Anatoka kwenda mbele, upanga mkononi; amepanda, farasi mwekundu, akikanyaga na kupita katika damu ya kila mtu asiyekubaliana naye. Sasa mnafahamu jambo hilo? [Kusanyiko, “Amina.”-Mh.] Ni wangapi wanaofahamu Muhuri huo ni nini sasa? [“Amina.”] Vema. Sasa, Yesu alisema nini? “Waushikao upanga wataangamia kwa upanga.” Hiyo ni kweli? Vema. Vema. Mpanda farasi huyu na raia wote wa ufalme wake wanaoua katika ule wakati wote mzima, ambao wamemwaga damu hii yote ya wafia imani ya watakatifu, wataua kwa Upanga wa Yesu Kristo hapo atakapokuja. “Hao waushikao upanga watauawa kwa upanga.” Waliuchukua upanga wa fundisho la sharti na la mpinga-Kristo, na kuwaua waabudu halisi, wa kweli, kote kote katika nyakati, kwa mamilioni. Na wakati Kristo atakapokuja na ule Upanga, kwa maana ni Neno Lake linalotoka katika kinywa Chake, Yeye atamwua kila adui aliyeko mbele Zake. Mnaamini jambo hilo?Kusoma kamili ya akaunti katika...
Muhuri Wa Pili.