Mbegu ya Hitilafu.

<< uliopita

ijayo >>

  Mfululizo wa wakati wa mwisho.

Kwa matunda yao wanajulikana.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mbegu ya Hitilafu.

Nilikuwa nikiomba kwenye pango ambapo ningeenda kuomba. Kulikuwa na mavumbi pangoni, na alasiri moja nilitoka, nikaweka Biblia yangu juu ya gogo, na upepo ukaifungua katika Waebrania, mlango wa 6. Ambapo ilisema, ya kwamba katika siku za mwisho, jinsi ingekuwa kama tukianguka kutoka katika Kweli na kujifanya upya tena hata tukatubu, hakukuwako na dhabihu ya dhambi tena, na jinsi ambavyo miiba na michongoma, ambayo mwisho wake ni kukataliwa, ambayo mwisho wake ni kuteketezwa; lakini mvua huinyea nchi, mara nyingi, kuitia maji, kuilima; lakini miiba na michongoma ingekataliwa, bali ngano ingekusanywa. Nami nikawaza, “Vema, ni upepo tu ulitokea ukafungua huo.” Vema, niliiweka tu Biblia chini tena. Ndipo nikawaza, “Vema, sasa nitaninii tu...” Na hapa ukaja upepo na kuifungua. Hilo lilitukia mara tatu. Nami nikawaza, “Vema, sasa, hilo ni jambo la ajabu.”

Halafu nilipokuwa nikiinuka, nikawazia, “Bwana, mbona umenifungulia Biblia hiyo nisome jambo hilo, mimi... nilipofikia mahali hapo, ambapo 'miiba na magugu, ambayo huwa karibu na kukataliwa, ambayo mwisho wake ni kuteketezwa'?” Nikawazia, “Mbona, ungetaka kunifungulia jambo hilo pale?” Na wakati nikiangalia huko nje...

Sasa, maono haya halisi huja bila kuingiza gia yoyote. Huyo ni Mungu tu. Mnaona? Nikaangalia na nikaona dunia iliyokuwa ikigeuka mbele yangu, nami nikaona yote imelimwa. Kulikuwako na mtu aliyevaa nguo nyeupe, alizunguka-zunguka akipanda ngano. Kulikuwa kuna mtu aliyevaa nguo nyeupe, aliyetoka akaenda akipanda ngano. Na baada ya yeye kwenda kwenye mpindiko wa dunia; akatokea mtu fulani, alionekana wa kuchukiza, naye alikuwa amevaa vazi jeusi, naye alikuwa akitupa mbegu za magugu juu yake kila mahali. Wote wawili wanakuja pamoja. Zote ziliota pamoja. Na zilipoota, zote zilishikwa na kiu, kwa maana mvua ilihitajika. Na kila moja ya hizo ilionekana kana kwamba inaomba, huku imeinamisha kichwa chake kidogo, “Bwana, tupe mvua, tupe mvua.” Ndipo hayo mawingu makubwa yakatokea, na mvua ikanyeshea zote mbili. Wakati ilipofanya hivyo, ile ngano ndogo iliruka juu na kuanza kusema, “Bwana asifiwe! Bwana asifiwe!” Ndipo maskini magugu hayo yakaruka moja kwa moja upande ule ule, na kusema, “Bwana asifiwe! Bwana asifiwe!”

Na ndipo lile ono likatafsiriwa. Mvua huwanyeshea wenye haki na wasio haki. Roho yule yule anaweza kushuka mkutanoni, na kila mtu akafurahi katika jambo hilo: wanafiki, Wakristo, na wote pamoja. Sawa kabisa. Lakini ni kitu gani? Kwa matunda yao wanajulikana. Mnaona? Hiyo ndiyo njia pekee inayoweza kujulikana.

Ndipo unaona jambo hilo sasa, kwa kuwa shayiri mwitu, ama ngano mwitu na nafaka mara nyingi huiga nafaka halisi, ya kienyeji, zinafanana sana hata ingewapoteza walio Wateule. Nafikiri tunaishi katika wakati wenyewe, wakati mambo haya yanapaswa kuhubiriwa na kuzungumziwa.

Angalia katika kifungu cha 41, hizo mbili pia zinafanana sana, zinafanana sana katika siku za mwisho hata Yeye hakufanya jambo hilo... Yeye asingeweza kutegemea kanisa fulani kuwatenganisha, tuseme, Methodisti ama Baptisti, wala Wapentekoste kuwatenganisha. Yeye alisema, “Yeye huwatuma malaika Wake kuwatenganisha.” Malaika anakuja kuleta utengano, ubaguzi kati ya mema na mabaya. Na hakuna mtu anayeweza kufanya jambo hilo ila Malaika wa Bwana. Yeye Ndiye atakayewaambia ni lipi ni kweli na lipi ni baya. Mungu alisema atawatuma malaika Wake katika nyakati za mwisho. Si malaika kupitia hapa, bali malaika wakati wa mwisho, nao wangekusanyika pamoja. Tunajua ya kwamba huu ni wakati wa mavuno unaokuja sasa. Sasa, malaika kweli anafasiriwa “mjumbe.” Na tunaona ya kwamba kuna malaika saba wa yale makanisa saba, na sasa... la, katika nyakati za kanisa.

Angalia Yeye alisema ya kwamba wapanzi walikuwa ni nani, na pia ile mbegu ilikuwa ni nani. Mmoja, mpanzi alikuwa ni Yeye, Mwana wa Mungu, ambaye alitoka akaenda akipanda Mbegu. Ndipo adui akaja nyuma Yake, ambaye alikuwa ni ibilisi, na akapanda mbegu ya hitilafu, nyuma ya kupanda Mbegu iliyo sahihi. Sasa, enyi marafiki, hilo limetukia katika kila wakati tangu tumekuwa na ulimwengu. Kweli kabisa. Kote tangu mwanzo, lilianza jambo lile lile.

----
Tunaona ya kwamba mpanzi wa kwanza wa mbegu ya hitilafu aliitwa “ibilisi,” nasi tunajua ilikuwa hivyo, katika Mwanzo 1. Sasa tunaona, na hapa katika Kitabu cha Mathayo, mlango wa 13, Yesu angali anataja hitilafu yo yote kwenye Neno Lake kuwa ni “ibilisi.” Na mwaka huu wa 1956, kitu cho chote kinachopanda hitilafu, kinyume cha Neno lililoandikwa la Mungu, ama kuweka tafsiri yo yote ya kibinafsi Kwake, ni mbegu ya hitilafu. Mungu hataiheshimu. Hawezi. Haitachanganyikana. Hakika halitachanganyikana. Ni kama mbegu ya haradali; haitachanganyikana na kitu kingine chochote, huwezi kuichanganya, haina budi kuwa ndiyo kitu halisi. Mbegu ya hitilafu!

Sasa tunaona, wakati Mungu alipopanda Mbegu Yake katika bustani ya Edeni, tunaona ya kwamba ilimzaa Habili. Lakini wakati Shetani alipopanda mbegu yake ya hitilafu, ilimzaa Kaini. Mmoja alimzaa mwenye haki; mmoja alizaa asiye haki. Kwa sababu Hawa alilisikiliza neno la hitilafu, kinyume na Neno la Mungu, nalo lilianzisha mpira wa dhambi unaotikisika papo hapo, na umevingirishwa tangu wakati huo. Na kamwe hatutaliondoa lote mpaka malaika watakapokuja na kutenganisha kitu hicho, ndipo Mungu awapeleke watoto Wake kwenye Ufalme, na magugu yatateketezwa. Angalia hiyo mizabibu miwili.

Angalia, mbegu zao zilikua pamoja kama tu vile Mungu alivyosema hapa pia katika mlango wa 13, wa somo letu usiku wa leo, wa Mathayo, “Zikuze pamoja.” Sasa, Kaini alienda kwenye nchi ya Nodi, akajitafutia mke, na kuoa; na Habili aliuawa, na Mungu akamwinua Sethi apachukua mahali pake. Na vizazi vikaanza kusonga mbele, kati ya mema na mabaya. Sasa, tunaona walikusanyika, kila mmoja wao, wakati baada ya wakati, na Mungu ilimbidi... Ilikuwa wovu sana hata ikambidi Mungu kuiangamiza.

Lakini hatimaye walitokea mpaka mbegu hizo mbili, mbegu ya hitilafu na Mbegu ya Mungu, zikatokeza vichwa vyao halisi, na jambo hilo likakamilishwa katika Yuda Iskariote na katika Yesu Kristo. Kwa kuwa, Yeye alikuwa ni Uzao wa Mungu, Yeye alikuwa mwanzo wa kuumba kwa Mungu, Yeye hakuwa kitu ila Mungu. Na Yuda Iskariote alizaliwa mwana wa upotevu, alitoka kuzimu, akarudi kuzimuni. Yesu Kristo alikuwa ni Mwana wa Mungu, Neno la Mungu lililodhihirishwa. Yuda Iskariote, katika hitilafu yake, alikuwa ni uzao wa Ibilisi, aliyekuja ulimwenguni, na kwa ajili ya udanganyifu; kama tu alivyokuwa hapo mwanzo, Kaini, baba yake wa zamani.

Yuda alicheza tu kanisani. Yeye hakuwa mwaminifu kabisa. Kwa kweli hakuwa na imani; asingemsaliti Yesu kamwe. Lakini, mnaona, yeye alipanda hiyo mbegu ya hitilafu. Alifikiri ya kwamba angeweza kufanya urafiki na ulimwengu, mali, na pia kuwa na urafiki na Yesu, lakini alikuwa amechelewa sana kufanya jambo lo lote kuhusu jambo hilo. Wakati ile saa ya kufa ilipowadia, wakati alipofanya jambo hili ovu, alivuka mstari wa kutenganisha kati ya kwenda mbele na kurudi. Ilimbidi kuendelea katika njia aliyoiendea, kama mdanganyifu. Yeye alipanda mbegu ya hitilafu, alijaribu kupata kibali kwa hayo madhehebu makubwa ya siku hiyo, na Mafarisayo na Masadukayo. Naye alidhani angejitengenezea kipande cha fedha, na angependwa na watu. Kama hilo halisababisha watu wengi sana kuingia katika hitilafu hiyo, wakijaribu kupata kibali kwa wanadamu! Hebu na tupate kibali kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Lakini hivyo ndivyo Yuda alivyofanya wakati hitilafu hizi zilipoingia ndani yake.

Nasi tunajua ya kwamba Yesu alikuwa Neno, Yohana Mtakatifu 1, ilisema, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili akakaa hapa miongoni mwetu.” Halafu, Neno ni Mbegu, kisha Mbegu ikawa mwili ikakaa kwetu.

Kama Yuda alikuwa ni uzao wa adui na hitilafu, pia ulifanyika mwili na kukaa miongoni mwetu katika nafsi ya Yuda Iskariote. Yeye kamwe hakuwa na imani halisi, halisi. Alikuwa na kile alichodhani ni imani. Kuna kitu kama kuwa na imani; na imani ya kujifanya. Na imani halisi ya Mungu itamwamini Mungu, na Mungu ni Neno, kamwe haitaongeza kitu Kwake. Biblia inatuambia kama tukiongeza neno moja, ama kuondoa Neno moja, sehemu yetu itaondolewa kwenye Kitabu cha Uzima, Ufunuo 22:18, mlango wa mwisho wa kumalizia.

Katika mwanzo wa kwanza, Kitabu cha kwanza cha Biblia, Mungu aliwaambia wasivunje Neno moja la Hilo, “kila Neno halina budi kutunzwa,” hawana budi kuishi kwa Neno hilo. Yesu, katikati ya Kitabu, alikuja na kusema jambo hilo katika wakati Wake, na kusema, “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno ambalo— litokalo katika kinywa cha Mungu.” Na katika wakati wa kumalizia wa Ufunuo, uliotabiriwa kwetu, ya kwamba “Mtu ye yote atakayeondoa Neno moja katika Kitabu, ama kuongeza neno moja Kwake, sehemu yake itaondolewa kwenye Kitabu cha Uzima.”

Kwa hiyo hapawezi kuweko na kitu cho chote kisicho cha hakika, ni Neno tu halisi la Mungu, lisiloghoshiwa! Hao ni wana wa Mungu, binti za Mungu, wasiozaliwa kwa mapenzi ya mwanadamu, wala kwa kupeana mkono, wala aina fulani ya ubatizo; bali wamezaliwa katika Roho wa Mungu, kwa Roho Mtakatifu, na Neno likijidhihirisha lenyewe kupitia kwao. Hiyo ni Mbegu halisi ya Mungu!

Adui hujiunga na kanisa na anakuwa wa kweli sana katika kanuni ya imani ama kitu fulani. Lakini hiyo si... Hiyo ni hitilafu, kitu chochote kinachoingilia aina hiyo ya Ukweli halisi wa Neno la Mungu. Na tunajuaje? Tunasema, “Vema, wao, una haki ya kulifasiri?” La, bwana! Hakuna mtu aliye na haki ya kufasiri Neno la Mungu. Yeye ni mfasiri Wake Mwenyewe. Yeye huliahidi, kisha analitimiza, hiyo ndiyo tafsiri yake. Wakati alipoliahidi, basi Yeye analitimiza, hiyo ndiyo tafsiri Yake. Chochote kinyume cha Neno la Mungu ni hitilafu! Kabisa!

Sasa, kama nilivyosema, Yuda hakuwa na imani halisi. Alikuwa na imani ya kujifanya. Alikuwa na imani ambayo alifikiri ya kwamba huyo alikuwa ni Mwana wa Mungu, bali hakujua huyo alikuwa ni Mwana wa Mungu. Asingefanya hivyo. Na mtu ambaye atapatana juu ya Neno hili la Mungu kuwa ni Kweli, yeye ana imani ya kujifanya. Mtumishi halisi wa Mungu atashikilia Neno hilo.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mbegu ya Hitilafu.



 

Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu;

bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.

Waebrania 6:7-8


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Ndoa Na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.