Mungu wa Wakati huu Mwovu.

<< uliopita

ijayo >>

  Mfululizo wa wakati wa mwisho.

Akimwita Bibi-arusi kwa ajili ya Kristo.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mungu wa Wakati huu Mwovu.

Amina! Hivyo ndivyo Neno linavyosomeka! Sasa, somo langu asubuhi ya leo, ni: Mungu Wa Wakati Huu Mwovu. Kama tulivyosoma katika Maandiko, “mungu wa ulimwengu huu, wakati huu mwovu.” Sasa, Ujumbe huu unaonyesha uovu wa wakati huu mwovu, na unafaa kwa unabii kwa ajili ya wakati huu mwovu.

Na ninaamini kwamba kila… ya kwamba Biblia ina kila jibu kwa kila wakati, tayari limeandikwa katika Biblia, kwa ajili ya mwamini wa wakati huo. Ninaamini ya kwamba kila kitu tunachohitaji kimeandikwa papa Hapa, kinahitaji tu kufasiriwa na Roho Mtakatifu. Siamini ya kwamba mtu ye yote duniani ana haki ya kuweka tafsiri yake mwenyewe kwenye Neno. Mungu hahitaji mtu ye yote kufasiri Neno Lake. Yeye hujifasiria Mwenyewe. Yeye alisema angefanya jambo hilo, Naye hulifanya.

Kama nilivyosema mara nyingi. Yeye alisema, “Bikira atachukua mimba,” Yeye alisema hayo kwa midomo ya nabii, naye akachukua. Hakuna mtu anayepaswa kufasiri jambo hilo. Hapo mwanzo, Yeye alisema, “Iwe nuru,” na ikawa. Hakuna mtu anayepaswa kulifasiri. Yeye alisema, “Katika siku za mwisho, Yeye angemwaga Roho Wake juu ya wote wenye mwili,” Naye akamwaga. Sihitaji mfasiri wa ye yote wa jambo Hilo. Yeye alisema, “Katika siku za mwisho, mambo haya” (ambayo tunaona yakitendeka sasa) “yatakuwa hapa.” Haihitaji tafsiri yo yote. Tayari limefasiriwa. Mnaona?

Sasa, angalia kwa makini sasa tunapojifunza Neno. Mungu wa Wakati Huu Mwovu, tunaoishi sasa. Huenda likaonekana ni la ajabu, jambo la ajabu sana, katika wakati huu wa neema, wakati, “Mungu anawachukua watu kwa ajili ya Jina Lake,” huyo ni Bibi-arusi Wake, katika wakati huu mwovu ambao unapaswa kuitwa wakati wa uovu. Wakati ule ule ambapo “Mungu anawaita watu kwa ajili ya Jina Lake,” kwa neema, kutoka, na unaitwa wakati mwovu. Sasa, tutathibitisha kwa Biblia ya kwamba huu ndio wakati aliokuwa akinena habari zake. Ni jambo la ajabu sana kuwazia hilo, ya kwamba katika wakati mwovu kama huu, ya kwamba Mungu wakati huo angekuwa anamwita Bibi-arusi Wake.

Mnaona, Yeye alisema, “watu,” si “kanisa.” Kwa nini? Hata hivyo, linaitwa Kanisa, bali Yeye angewaita “watu.” Sasa, kanisa ni mkusanyiko wa watu wengi wa namna mbalimbali. Lakini Mungu anamwita mmoja hapa … Yeye hakusema, “Nitaita Methodisti, Baptisti, Pentekoste.” Yeye alisema angewaita watu. Kwa nini? Jina Lake. Mnaona, watu; mmoja kutoka Methodisti, mmoja kutoka Baptisti, mmoja kutoka Lutheran, mmoja kutoka Katoliki. Mnaona?

Lakini Yeye anawaita, si kundi la kanisa, bali “watu kwa ajili ya Jina Lake,” wanaopokea Jina Lake, wanaohusika katika Jina Lake, wanaoenda kwenye arusi kuolewa Naye, wapate kuwa sehemu Yake, mnaona, kwa kuchaguliwa tangu asili. Kama tu vile mwanamume anayechagua mke mzuri maishani, aliyechaguliwa kuwa sehemu ya mwili wake. Kwa hiyo, hiyo ni kusema, Bibi-arusi wa Kristo atakuwa, na sasa, tangu zamani, amechaguliwa na Mungu kuwa sehemu ya Mwili huo. Mnaona? Loo, Maandiko ni tajiri sana, yamejaa asali!

Angalia, si kile mtu fulani amesema, wala mtu fulani alioita; bali ni wale waliochaguliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, naye anawaita watu hawa katika siku za mwisho; si madhehebu. “Watu kwa ajili ya Jina Lake.” Na wakati huu mwovu ni wakati ambapo Yeye anafanya jambo hilo, wakati huu huu wa udanganyifu.

Juma lililopita, katika Mathayo 24, ulikuwa ndio wakati wa udanganyifu sana wa nyakati zote. Nyakati zote za udanganyifu, tangu bustani ya Edeni, kote kote, hapajakuwako na wakati wa udanganyifu kama huu. “Manabii wa uongo watatokea na kuonyesha ishara na maajabu, ikiwezekana kuwadanganya walio Wateule.” Mnaona? Sasa, ni makanisa baridi tu, ya kawaida, yaliyo magumu, na kadhalika, ya theolojia ya kujibunia, hayo hayangeweza; Wateule wasingejali jambo hilo kamwe. Lakini ni kule juu karibu sana na jambo lililo halisi. Kuacha tu Neno moja ndivyo tu unavyopaswa kufanya. Ameahidiwa wakati; wakati mkuu sana! Enyi Wakristo, kila mahali, jihadharini na saa tunayoishi! Andikeni, na msome, na msikilize kwa makini.

Ni kwa nini Mungu angewaita watu kwenye wakati huu mwovu, kwa ajili ya Jina Lake? Sababu yake ni, ni kumjaribu, Bibi-arusi Wake. Ni ku... Wakati Yeye amedhihirishwa, akajaribiwa, kuthibitishwa, akathibitishwa kwa Shetani. Kama vile ilivyokuwa hapo mwanzo, ndivyo itakavyokuwa mwishoni. Wakati mbegu inapoanza ardhini, inachipuka kupitia kwa wabebaji, uhai wake, bali inaishia kwenye mbegu ile ile kama ilivyokuwa wakati ilipoingia ardhini.

Na vivyo hivyo mbegu ya udanganyifu ilipoanguka ardhini, katika Edeni, ndivyo inavyoishia katika siku za mwisho. Kama tu vile Injili ilivyokuwa wakati ilipoangukia kwenye dhehebu huko Nikea, Rumi, inaishia katika dhehebu la hali ya juu. Kama tu vile Mbegu ya Kanisa ilivyoanguka huko nyuma, ikiwa na ishara, maajabu, na Kristo aliye hai miongoni mwao, inaishia katika siku za mwisho chini ya huduma ya Malaki 4, na kuirudisha tena Imani asili iliyotolewa mara moja.

Tunaona sasa, wakati huu mwovu ni kuthibitisha, kwa Shetani, Yeye si kama Hawa, ya kwamba Yeye si mwanamke wa aina hiyo. Naye atajaribiwa kwa Neno Lake, Bibi-arusi, kama vile bibi-arusi wa Adamu alivyojaribiwa kwa Neno. Na bibi-arusi wa Adamu aliamini kila sehemu ya Neno, lote, ila akachanganyikiwa kwenye ahadi moja, ya kwamba, “Ni yeye yule jana, leo, na hata milele,” leo; Lakini akashindwa kwenye ahadi moja, kwa kujaribiwa na adui, uso kwa uso. Na sasa, watu wanaoitwa kwa ajili ya Jina Lake, bila shaka, ni Bibi-arusi Wake. Yeye atakutana tena na jambo lile lile; si kwa kweli tu ya kimadhehebu ama kitu fulani, bali kila Neno!

Kwa kuwa, katika mwanzo wa Biblia, mwanadamu alipewa Neno la Mungu apate kuishi kwalo. Neno moja, likafasiriwa vibaya na mtu aliyeitwa Shetani, katika utu wa mnyama aliyeitwa nyoka. Shetani, katika mtu huyu, angeweza kuzungumza na Hawa, na kumfasiria vibaya Neno, kisha akapotea. Mnaona, halina budi kuwa ni kila Neno.

Katikati ya Biblia, Yesu alikuja na kusema, “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno,” wakati alipojaribiwa na Shetani. Sasa, Mungu akituambia hapa katika siku za mwisho, ya kwamba, “Mungu wa ulimwengu huu atainuka katika siku za mwisho.”
“Na ye yote atakayeongeza neno moja Kwake, ama kuondoa Neno moja Kwake, sehemu yake itaondolewa katika Kitabu cha Uzima.”
Mungu na aturehemu! Na tusitembee kama wenye majivuno, vifua mbele, kichwa juu, wajuvi, kwa maana sisi pia wakati mmoja tulikuwa katika kuasi. Hebu na kwa neema, na rehema, na kujisikia moyoni mwetu kwa Mungu, kwa unyenyekevu tuje kwenye Kiti cha Enzi cha neema.

Ajabu sasa, baada ya yapata miaka elfu moja mia tisa ya kuhubiriwa kwa Injili, na sasa yeye, huo ni mfumo wa ulimwengu, ni mwovu zaidi kuliko katika siku ambazo, wakati Yeye alipokuwa hapa. Mfumo wa ulimwengu ni mwovu zaidi. Ulimwengu unaelekea kwenye kilele kikuu. Mnajua jambo hilo. Bwana anatimiza Neno Lake kwa kila njia.

Ufunuo 18:4-5,
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

----
Ni onyo lililoje! Hilo linalitupa kanisa kabisa kwenye Ufunuo 3:14, kwenye wakati wa Laodikia, uasi; wa kidini halisi, bali ni waasi. “Wewe, kwa sababu unasema ya kwamba, 'Sisi ni matajiri, hatuna haja na kitu,' wala hujui ya kwamba wewe ni uchi, mwenye mashaka, kipofu, wala hujui.” Linganifu kabisa na Maandiko ya wakati huu, si kwa Maandiko ya wakati wa Danieli, si kwa ya wale katika jina la...wakati wa Nuhu, lakini katika wakati huu wa mwisho, mwovu.

Angalia hapa, “U uchi.” Hebu hilo lilowe kabisa kabisa. Ninajua huenda nisiwe na kutokubaliana sana juu ya wazo hili, lakini imefikia mahali ambapo ni vigumu kwa Mkristo kutoka nyumbani mwake na asiletwe mbele ya wakati huu mwovu, na wanawake wasiovalia vya kutosha.

Enyi wanawake, nitasema jambo hili, nami nawatakeni msikilize. Na, wanaume na wanawake, huenda msikubaliane na jambo hili, lakini ninajisikia kuongozwa kulisema. Je! Ulijua, mwanamke ye yote anayejivua nguo hivyo hana akili timamu? Je! mnajua, yeye ni, aamini asiamini, ama hafikirii hivyo, yeye ni kahaba? Ingawa mwanamke huyo anaweza kusimama ameweka mkono wake mbele za Mungu na kuapa ya kwamba yeye hajaguswa na mwanamume mwingine ye yote ila mumewe, na hiyo inaweza kuwa ni kweli kabisa, bali hata hivyo yeye ni kahaba. Yesu alisema, “Kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye.” Na mwanamke huyo anaweza kuwa...

Mnaona, yeye ni “uchi,” Biblia ilisema, “wala hajui.” Roho inayomtia mafuta kufanya mambo kama hayo ni roho mwovu, roho ya kikahaba. Utu wake wa nje, mwili wake, nyama zake, huenda akawa msafi. Huenda asifanye uzinzi wo wote, na angeweza kumwapia Mungu na kuwa kweli, ya kwamba kamwe, bali roho yake ni roho ya kikahaba. Yeye amepofushwa sana na mungu wa ulimwengu huu wa mitindo; alijivalisha kimapenzi na akatoka akaenda kule.

----
Mtu wa nje ni kiumbe chenye mwili ambacho kinatawaliwa na hisi sita ... ama hisi tano, hasa. Mtu wa ndani ni mtu wa roho ambaye anatawaliwa na hisi tano; dhamiri, na upendo, na kadhalika. Mtu wa nje; kuona, kuonja, kugusa, kunusa, kusikia.

Lakini ndani ya roho hiyo ni nafsi, na inatawaliwa na jambo moja, hiari yako. Unaweza kukubali yale ibilisi anayosema ama kukubali yale Mungu asemayo. Na hiyo itaamua ni roho gani iliyo mle ndani. Kama ni Roho wa Mungu, atakula mambo ya Mungu, wala hatakula chochote cha ulimwengu. Yesu alisema, “Ukiipenda dunia au mambo yaliyo katika dunia, ni kwa sababu kumpenda Mungu hata hakujaingia kwenye sehemu hii ya ndani.” Shetani amekudanganya. “Na mwanadamu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”

Angalia sasa, tunaona ya kwamba yeye ni “uchi,” mchafu na uchi. Na ulimwengu unaonekana kuwa katika wakati mwovu sana uliopata kuwa. Kamwe katika wakati wo wote wanawake hawakutenda namna hiyo, kamwe ila kabla tu ya kuangamizwa kwa ulimwengu uliotangulia gharika. Naye Yesu alirejea kwenye jambo hilo. Tutalifikia hilo baada ya kitambo kidogo.

Je! Mungu amepoteza mamlaka, ama anaruhusu tu mamlaka nyingine itawale? Nashangaa. Jibu la kweli la swali hili ni, kwa maoni yangu, kuna roho mbili zinazopingana ulimwenguni leo, zinazotenda kazi. Sasa, hakuwezi kuwa na zaidi ya viwili, vichwa viwili. Na mmoja wao ni Roho Mtakatifu akitenda kazi; huyo nyingine ni roho ya ibilisi, na, katika siku hizi za mwisho, katika udanganyifu. Sasa nitaweka msingi wa mawazo yangu papa hapa kwa ajili ya somo lililosalia, yale mengine... Ujumbe wetu.

Zile roho mbili. Mmoja wao, Roho Mtakatifu wa Mungu; huyo mwingine, roho wa Ibilisi, akitenda kazi katika udanganyifu. Watu wa dunia sasa wanafanya chaguo lao. Roho Mtakatifu yupo hapa akimwita Bibi-arusi kwa ajili ya Kristo. Yeye anafanya jambo hilo kwa kuthibitisha Neno Lake la ahadi Kwake, kwa ajili ya wakati huu, akionyesha ya kwamba ni Kristo. Kama kidole kinapaswa kusogea katika wakati huu, kidole kitasogea. Kama mguu unapaswa kusogea katika wakati huu, mguu utasogea. Kama jicho linapaswa kuona katika wakati huu, jicho litaona. Mnaona?

Roho wa Mungu, wakati anapokuwa akafikia kimo kikamilifu cha Mungu, ndio wakati tunaoishi sasa. Roho Mtakatifu yuko hapa akithibitisha Ujumbe wa wakati huu. Naye Roho Mtakatifu anafanya jambo hili, ili kwamba watu wanaomwamini Mungu wataitwa watoke kwenye machafuko haya. Roho mchafu wa Ibilisi yuko hapa akiliita kanisa lake kwa upotovu, kama kawaida, kwa kupotosha Neno la Mungu, kama alivyofanya hapo mwanzo. Angalieni likirudi moja kwa moja kweye wakati ule wa mbegu tena; kutoka Edeni, hii hapa tena. Hii hapa tena.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mungu wa Wakati huu Mwovu.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

Ufunuo 18:1-2


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Mungu Akijificha
Kwa Urahisi...

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)