Ujumbe wa machweo.

<< uliopita

ijayo >>

  Mfululizo wa wakati wa mwisho.

Mlima Sunset.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ni nini kinachovutia kule mlimani?

Si muda mrefu uliopita, nikiwa nimesimama kwenye mimbara hii, ilisemwa na Roho Mtakatifu, “Siku itakuja ambapo watapiga kigingi mbele ya nyumba yako; watasogeza lango lako. Kwa hivyo, hayo, hutayajali na usikasirike.” Niliona lango langu limevujiliwa mbali na kutupiliwa kilimani. Niliona kile kilima mbele zangu kimelimwa chote, mbao na vinginevyo vilikuwa kule ambako kitu fulani kilivivunjilia mbali. Yeye alisema...

Nikaangalia, na kulikuwako na Ricky mdogo aliyeenda kule na kuvunja-vunja lile lango, akafanya hili. Nikasema, “Kwa nini hukuniambia?” Alikuwa mwerevu kwangu, nami ilinibidi kumpiga. Na nilipofanya hivyo, nikasema, “Sijafanya hivi tangu nilipokuwa mwanandondi, bali nataka tu kujua,” nami nikampiga konde moja. Na wakati nilipomwangusha chini, nikamchukua tena na kumwangusha chini tena. Nami nikamwinua mara tatu nne, na ndipo nikampiga na kumtupa upande mwingine wa kilima kile. Kwa hiyo basi nikaenda kule, na kusema, “Hiyo si sahihi.” Nami nikamchukua na kumpa mikono, nikasema, “Sina hasira nawe, bali nataka tu ujue huwezi kuzungumza nami namna hiyo.”

Halafu basi nilipogeuka na kurudi, Roho Mtakatifu alikuwa amesimama pale langoni, akasema, “Sasa kwepa hili. Wakati kile kigingi kinapopigiliwa chini, geukia upande wa magharibi.”
Kitabu hiki, ndicho kila kitu ninachohitaji,
Kitabu hiki ni Maelezo mazuri,
Kwa namna ambavyo kinaonyesha jinsi ninavyoweza kuepuka shida yangu.
Amina! Na hicho Kitabu ni Neno, na Neno hilo ni Mungu. Usijali shida zako, kitakwambia utakayofanya.

Miaka mitatu iliyopita nilimsikia rafiki yangu, mpimaji wa jiji, anaishi kwenye upande mwingine wa barabara kutoka kwangu, akipigilia kigingi chini. Nilitoka nikaenda kule na kusema, “Kuna nini, Tope?” Mwana wa Bw. King, rafiki msiri wangu.
Kasema, “Billy, wataipanua barabara hii.”
Nyote mnakumbuka. Nikasema, “Huenda ikawa ndiyo lile daraja.” Nilimwambia Ndugu Woods, nikasema, “Shikilia mali yako. Labda daraja hilo litapitia hapa juu, kitu fulani.” Njia hiyo ilikuwa imeraruliwa; matofali, miamba, ilitupwa juu ya kila kitu. Kwa hiyo akasema ... Nikasema, “Shikilia mali yako.” Ndipo wakati mimi...
Bw. King aliniambia hilo lingetukia. Nikaingia, nikamwambia mke wangu anayeketi pale, “Mpenzi, kuna kitu kilichoandikwa kuhusu jambo hilo. Ni BWANA ASEMA HIVI, mahali fulani.”

Niliingia na kuchukua kitabu changu, nikakichunguza, na kasema, “Itakuwa...” Miaka minane baadaye! Ndipo nilipoliangalia, nikasema, “Wakati umewadia sasa, mpenzi, hatuna budi kuelekea magharibi.” Siku mbili baada ya hapo, nikiwa nimesimama chumbani yapata saa nne asubuhi moja, niliingia katika Roho wa Mungu. Niliona lile kundi la hua likiruka, nikawaangalia hao ndege wadogo. Mnakumbuka jambo hilo. Niliwaona Malaika saba katika umbo la piramidi, wakija kwa haraka wakinijia. Kasema, “Geukeni magharibi, mwende Tucson, mwe maili arobaini kaskazini mashariki. Nawe utakuwa ukijitoa gugu fulani” ama, huitwa kichwa cha fahari “kutoka nguoni mwako.”

Ndugu Fred Sothmann, anayeketi pale akiniangalia sasa hivi, alikuwa pale asubuhi hiyo. Nilikuwa nimesahau jambo hilo. Nikasema, “Mlipuko ulitokea kama tetemeko la ardhi, ambalo lilitikisa karibu kila kitu kilichokuwako nchini. Sioni namna mtu angaliweza kuishi.” Niliogopa. Nilisimama huko Phoenix, ninyi nyote mnaosikiliza usiku wa leo nishuhudieni. Nilihubiri mahubiri, Mabwana, Ni Wakati Gani? “Tuko wapi?” Nilienda Magharibi. Wengi wenu hapa mlipata kanda hiyo, wengi wenu hapa mlisikia ikisemwa, mwaka mmoja au zaidi kabla haijatukia.

Nikaenda Magharibi, nikishangaa kile kitakachotukia. Siku moja nilipata mwito kutoka kwa Bwana. Nilimwambia mke wangu, nikasema, “Mpenzi, mimi... labda kazi yangu imekwisha.” Sikujua. Nikasema, “Mimi... Mungu, labda Mungu amemaliza na mimi sasa nami nitaenda nyumbani. Nenda zako pammoja na Billy, uwachukue watoto. Mungu atakufanyia njia, kwa namna fulani. Nenda zako ukaishi mwaminifu kwa Mungu. Angalieni kwamba watoto wanamaliza shule, ukawalee katika maonyo ya Mungu.”
Yeye akasema, “Bill, hujui-hujui kama hiyo ni kweli.”
Nikasema, “La. Lakini mtu asingeweza kustahimili jambo hilo.”
Na asubuhi moja Bwana aliniamsha, kasema, “Nenda kule juu kwenye Magenge Marefu ya Sabino.” Nilichukua kipande cha karatasi na Biblia yangu.
Mke akasema, “Unaenda wapi?”
Nikasema, “Sijui. Nitakwambia nitakaporudi.”

Nikapanda juu kwenye magenge, nikapanda moja kwa moja ambako tai walikuwa wakiruka huku na huko. Nilikuwa nikimwangalia kulungu fulani amesimama pale. Nikapiga magoti kuomba, nikainua mikono yangu, na Upanga ukauangukia mkono wangu. Nikaangalia kila mahali. Nikawaza, “Ni kitu gani hicho? Sijapatwa na kichaa. Hapa mna ule Upanga mkononi mwangu, mwangavu, unaong'aa, unametameta juani.” Nikasema, “Sasa, hamna watu kwa maili nyingi kutoka hapa nilipo kwenye magenge haya. Huo ungeweza kutoka wapi?”
Nikasikia Sauti, ikasema, “Huo ni ule Upanga wa Mfalme.”
Nikasema, “Mfalme ye yote humpandisha mtu cheo kwa upanga.”
Yeye yule Sauti akarudi, kasema,” “Si upanga wa mfalme, bali 'Ule Upanga wa Mfalme,' Neno la Bwana.” Kasema, “Usiogope. Ni ule Mvuto wa Tatu tu. Ni thibitisho la huduma yako.”

Nilikuwa nikienda kuwinda pamoja na rafiki yangu, bila kujua kitakachotukia. Na mtu fulani akanipigia simu, ambaye alinilaumu kwa ajili ya ile picha ya Malaika wa Bwana, ambayo aliipiga. Ilinilazimu kwenda Houston kwa ajili ya mwanawe, kwa maana alikuwa akielekea kwenye maangamizi naye angekufa katika muda wa siku chache. Naye akakutana nami mle ndani na kunikumbatia, akasema, “Wazia, mtu yule yule niliyemkosoa anakuja kumwokoa mwanangu wa pekee!” Chama cha masilahi ya binadamu kikanitunza nishani inayoitwa Oscar, ama cho chote unachotaka kuiita, kwa ajili ya kuokoa maisha.

Ndipo tukarudi, nikaenda mlimani kuwinda. Na hapo Ndugu Fred na mimi, asubuhi moja nilipoondoka, tayari nilikuwa nimempata javelina wangu, na nikatazama na kuona mahali alipokwenda. Nikasema, “Ndugu Fred, nenda kwenye mlima huo asubuhi na mapema sasa, karibu na mapambazuko, nami nitapanda ule mwingine. Sitampiga risasi yule nguruwe mwitu, sitamuua. Lakini kama wakianza upande huu, kundi hilo, nitawapiga risasi mbele yao na kuwarudisha nyuma.”

Ndugu Fred alitoka akaenda kule wala hakukuwa na nguruwe mwitu. Alinipungia mkono nikaona. Nikatelemka katika yale magenge, mashimo makubwa sana, jua lilikuwa likichomoza. Nikazunguka upande mwingine wa kile kilima, bila kufikiria cho chote juu ya ule unabii. Nikaketi chini, nikingoja, nikipumzika, nikawazia, “Imekuwaje kwa wale nguruwe mwitu?”

Nikachukua... Nikaketi jinsi Wahindi huketi, mwajua, kupitanisha miguu, nami nikaangalia mguu wa ovaroli yangu na ilikuwa na mbegu ya kwekwe. Nikaichukua. Nami nikasema, “Hilo ni jambo la ajabu! Niko hapa, yapata maili arobaini kaskazini mashariki mwa Tucson. Yule mtoto wangu mdogo Joseph ameketi pale akiningojea.” Na mara nilipoanza kutazama, nikaona kundi la nguruwe mwitu yapata yadi elfu moja kutoka kwangu, juu mlimani, nami nikatupa ile mbegu ya kwekwe chini. Nikasema, “Nitawapata. Nitaenda nimwite Ndugu Fred, nami nitatundika kipande cha karatasi kutujulisha tupitie wapi, kwenye mzingile mwambije huu hapa, nasi tutampata Ndugu Fred.”

Nami nikaanza kupanda mlima, nikikimbia sana niwezavyo upande ule mwingine. Kwa ghafla, nilifikiri mtu fulani alinipiga risasi. Sikuwahi kusikia mlipuko kama huo; ulitikisa nchi nzima. Na, ilipotendeka, mbele yangu kulikuwa na Malaika saba katika kundi.

Nilikutana na Ndugu Fred na hao wengine, baadaye kidogo. Kasema, “Ilikuwa ni nini?”
Nikasema, “Hiyo ilikuwa ndiyo.”
“Utafanya nini?”
“Rudi nyumbani. Kwa kuwa, BWANA ASEMA HIVI, zile siri saba ambazo zimefichwa katika Biblia miaka hii yote, madhehebu haya na kila kitu, Mungu atatufungulia hizo siri saba katika zile Muhuri Saba.” Kulikuwako na duara hiyo ikipanda juu kutoka ardhini, kama ukungu unaofanyika. Ulipofanya hivyo, ukapanda moja kwa moja juu ya mlima kabisa, ukaanza kuzungukazunguka pande za magharibi jinsi ulivyokuja. Sayansi iliupata baada ya kitambo kidogo, maili thelathini kwenda juu na maili ishirini na tano kwa upana, katika mzunguko wa piramidi kabisa.

Na hivi majuzi, nilipokuwa nimesimama pale, nikaigeuza ile picha upande wa kulia, Yesu akaonekana mle jinsi alivyokuwa katika zile Nyakati Saba za Kanisa, mwenye kufunikwa nywele nyeupe, ikionyesha Uungu Mkuu. Yeye ni Alfa na Omega; Yeye ni wa Kwanza na wa Mwisho; Yeye ndiye Hakimu Mkuu wa Umilele wote, akisimama pale kuthibitisha Ujumbe wa wakati huu. Na kutakuwako Nuru wakati wa jioni! Je, maana yake yote ni nini? Ilikuwa ni kitu gani?

Nikaenda upande wa magharibi. Juu ya mlima ule ule, nikipita pale pamoja na Banks Wood pale, kasema, “Tupa jiwe hewani. Mwambie Bw.Woods, 'BWANA ASEMA HIVI, utauona Utukufu wa Mungu.'”
Kesho yake, tukisimama pale, upepo wa kisulisuli ulishuka na kulipua milima. Majabali yalikatilia mbali vilele vya miti, yapata futi tatu nne juu ya kichwa changu. Ukasababisha milipuko mitatu mikubwa, na ndugu wakanikimbilia. Kulikuwa na watu kama kumi na watano waliosimama pale, wahubiri na kila kitu kingine. “Ilikuwa ni nini?” Akasema, “Ilikuwa ni nini?”
Nikasema, “Hukumu inaipiga Pwani ya Magharibi.”

Yapata siku mbili baadaye, tetemeko la nchi nusura lizamishe Alaska. Je, hii Nuru juu ya Mlima Sunset katika Msitu wa Coronado wa Arizona ni nini? Je, kitu hiki cha ajabu kilichotokea kule juu, ambacho watu wamekuwa wakisafiriri kuelekea mashariki kutokea magharibi, wakiokota miawe yaliyotawanyika pale Hiyo ilikopiga? Na kila moja yao, kila moja ya majabali hayo, lina ncha tatu, lilizopasua. (Hao watatu ni Mmoja.) Yamewekwa kwenye madawati, yanawekwa juu ya karatasi, kote nchini. Je, ni jambo gani hili la ajabu juu ya Mlima Sunset katika Msitu wa Coronado?

Junior Jackson unasikiza, unakumbuka ile ndoto aliyokuwa nayo ambayo niliifasiri, “kuelekea kwenye machweo ya jua”? Na hili lilitukia kwenye Mlima wa “Sunset”. Ni wakati wa jioni, wakati wa machweo. Ujumbe wa machweo kwa machweo ya historia, machweo ya unabii, hasa, ukitimizwa. Na itakuwa Nuru wakati wa jioni, juu ya Mlima Sunset katika Msitu wa Coronado, maili arobaini kaskazini mwa Tucson. Ingia kwenye ramani uone kama kilele cha Sunset pale. Hapo ndipo hasa ilipotukia. Kamwe sijui jambo hilo mpaka hivi majuzi.

Kila kitu ambacho... Hilo halitakufa kamwe. Inaendelea kujifungua kila wakati. Kutoka kwenye jambo lile lile linalotukia, hadi kwenye picha akiwa Yesu amesimama akituangalia; na sasa hasa kwenye Mlima wa Sunset, na Nuru ya machweo ya jua. Nuru ya jioni imekuja, Mungu akijithibitisha Mwenyewe. Ni kitu gani? Ni ukweli kwamba Mungu na Kristo ni mmoja. Kile “cheupe.” Wangapi wamepata kukiona, zile nywele nyeupe juu Yake, kama tulivyonena katika Ufunuo 1? Mnaona, Uungu Mkuu, Mamlaka Kuu; hakuna sauti nyingine, hakuna mungu mwingine, hakuna kitu kingine! “Katika Yeye unakaa utimilifu wa Uungu kwa jinsi ya mwili.” Malaika Wenyewe walikuwa ni wigi Yake. Amina.

Nini kimetukia juu ya Mlima Sunset? Mungu akithibitisha Neno Lake. Hiyo ndiyo sababu ya kelele hizi zote. Tazama, ni Mungu akitimiza Neno Lake lililoahidiwa tena, la Ufunuo 10:1 hata 7, “Na katika siku za kupigwa baragumu ya Ujumbe wa malaika wa saba, hapo ndipo siri ya Mungu inapaswa kutimizwa.” Siri iliyofichwa ya Ufunuo 10:1 hadi 7, Ujumbe wa mwisho kwa wakati wa mwisho wa kanisa. Inatimiza kabisa, katika wakati huu, Luka Mtakatifu 17:30, “Siku atakapofunuliwa Mwana wa Adamu.”
“Na watatokea manabii wa uongo na Makristo wa uongo, wataonyesha ishara kuu na maajabu, hata ingewapoteza walio Wateule kama yamkini.” Watu wangali wana mashaka. Na, kama kawaida, kanisa linashangaa vile vile.

Na sayansi kote katika Tucson, wangali wanaandika makala madogo madogo na kuyaweka magazetini. Kule nyuma mbali sana juu ya Mlima Lemmon, zile kamera kubwa hazikuiona ikiinuka kutoka mahali tulipokuwa tumesimama; ikipeperukia upande wa magharibi, ikionyesha ya kwamba wakati umekwisha. Haiwezi kusonga tena isipokuwa mahali padogo sana, iko kwenye Pwani ya Magharibi. Hukumu ilitokea tu jinsi ilivyoenda. Ikaenda juu kule kupita Phoenix na kuvuka ng'ambo moja kwa moja, hata Prescott na kuvuka milimani hata Pwani ya Magharibi, moja kwa moja hata... Walikuwa wakienda wapi? Kule juu mpaka Alaska, na inanguruma, ikielekea kule.

Na vituo vya uchunguzi wa angani na wengine wote kule Tucson wangali wanauliza, watafiti wa sayansi wanajaribu kuchunguza ni nini. Ilikuwa juu sana ambamo hakuwezi kupata ukungu, umande, ama cho chote kule. “Ilisababishwa na nini? Iko wapi?” Wao wametatanishwa vile vile na ile duara ya mbinguni inayoning'inia kule juu mbinguni kama walivyokuwa wale mamajusi walipokuja wakiifuata nyota, wakisema, “Yuko wapi aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi?” Ilikuwa ni kitu gani? Mungu akitimiza Neno Lake, “Na nyota itatoka katika Yakobo.”

Naye Mungu wa Mbinguni aliahidi wakati wa jioni utakuwa na Nuru za jioni. Miaka mitatu iliyopita siri hii ilikuwa ni unabii, “Ni wakati gani, Bwana?” Lakini sasa ni historia. Imepita. Ahadi imetimizwa. Ni saa ngapi, bwana, na mvuto huu ni nini? Mungu akitimiza Neno Lake! Ni yeye yule jana, leo, na hata milele.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ni nini kinachovutia kule mlimani?


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi;

lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na Bwana; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru.

Zekaria 14:6-7


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Mungu Akijificha
Kwa Urahisi...
(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.