Matukio ya Sasa Yanadhihirishwa na Unabii.

<< uliopita

ijayo >>

  Mfululizo wa Wakati wa Mwisho.

Neno la Bwana huwajia manabii.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Matukio ya Sasa Yanadhihirishwa na Unabii.

Waliwaambia ninyi Wapentekoste, miaka arobaini na mitano, hamsini iliyopita. Mama zenu na baba zenu, wakati walipokuwa wapentekoste halisi, walitoka kwenye madhehebu na wakalaani kitu hicho na wakatoka humo. Basi kama mbwa kwenye matapiko yake, moja kwa moja mkarudi ndani yake tena. Mkafanya jambo lile lile lililoliua kanisa hilo, mlijiua kwa kitu kile kile. Sina kitu dhidi ya watu walio mle ndani, sina kitu dhidi yake, ni mifumo ya kitu hicho ndiyo inayofanya jambo hilo.

Na, angalia, walikosa kuona thibitisho la unabii wa Neno la Mungu likitimizwa. Kama hao makuhani... Walikuwa wameiweka sawa kabisa jinsi Masihi atakavyokuja, walijua kitakachotukia. Mafarisayo walikuwa na wazo lao, Masadukayo, Waherodi, na wote, walikuwa na mawazo yao. Lakini Yeye hakuja... Yeye alikuja kinyume na kila mmoja wao, bali kulingana na Neno kabisa. Yesu alisema jambo lilo hilo lilikuwa lipo hapa: “Kama mngalinijua Mimi, mngaliijua na siku Yangu. Kama ungalijua, ungeninii... Mnasema, 'Vema, Musa! Tunaye Musa.'” Kasema, “Mbona, kama mngalimwamini Musa, mngaliniamini Mimi; kwa sababu, yeye aliandika habari Zangu.”

Lakini, unaona, wakati Mungu alipokuwa akithibitisha yale hasa aliyokuwa ameahidi, walikuwa wamejipangia njia fulani ya heshima ambayo Yesu alipaswa kuja, na ninii... Ninamaanisha Masihi. Ilibidi Masihi aje moja kwa moja kwenye kundi lao la sivyo hakuwa Masihi. Vema, ndivyo ilivyo, ni karibu hivyo, siku hizi, “Kama huoni kupitia kwenye miwani yangu, huangalii hata kidogo.” Mnaona, na kwa hiyo hivyo — hivyo ndivyo ilivyo tu. Sisi... Hiyo ni kweli. Tunachukia kuwazia jambo hilo, bali ni Kweli kabisa.

Katika Waebrania 1:1, Mungu kwa sehemu nyingi aliandika Biblia kwa njia Yake Mwenyewe aliyoichagua. Hakuiandika kamwe kwa wanatheolojia, wala halifasiri kwa wanatheolojia. Kamwe hapajakuwako na wakati ambapo wanatheolojia walipata kuwa na fasiri ya Neno la Mungu. Fasiri huja tu kwa nabii. Na njia pekee tutakayoweza kutoka kwenye mchafuko huu ni Mungu kututumia nabii huyo, kweli kabisa, njia pekee tu litakavyofanywa. Imeaminiwa, imetazamiwa, na kutimizwa.

Mnaona, haikuandikwa na mwanadamu, bali iliandikwa na Mungu. Si kitabu cha mwanadamu, si kitabu cha mwanatheolojia. Ni Kitabu cha Mungu, ambacho ni Kitabu cha unabii kilichoandikwa na manabii na kufasiriwa na manabii. Biblia ilisema, “Neno la Bwana huwajia manabii.” Kweli kabisa!

Namna hilo lilivyooneshwa vizuri, ama, lilidhihirishwa wakati Yesu alipokuja duniani, naye Yohana alikuwa ndiye nabii wa siku ile, na yeye alikuwa akitabiri. Wao wakasema, “Loo, unataka kusema ya kwamba Mungu atayaangamiza mashirika yetu makubwa hapa na vitu hivi vyote? Na kutakuwako na wakati, ambapo letu— hekalu letu halitaabudiwa tena?”

Akasema, “Wakati ulikuwa unakuja ambapo Mungu angetoa dhabihu ya Mwana-Kondoo wa Mungu, mwanadamu.” Naye akasema ya kwamba yeye angemjua wakati atakapokuja. Naye akasema... Alikuwa na hakika sana na ujumbe wake, akasema, “Yeye anasimama moja kwa moja miongoni mwenu sasa na hamjui.” Yeye yuko moja kwa moja miongoni mwenu na hamjui.

Na siku moja wakati Yesu alipotoka, Yohana aliangalia juu na kuona ishara hiyo juu Yake, alisema, “Tazama, Mwana -Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Dakika ile ile Yesu alijua basi ya kwamba Yeye alithibitishwa mbele ya watu. Sasa, Yeye alikuwa ni Neno, tungelitilia shaka jambo hilo? Biblia ilisema Yeye alikuwa Neno, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu.” Naye huyu hapa, ninii... Hili hapa Neno duniani (angalia! Kikamilifu!) Linakuja moja kwa moja majini kwa nabii.

Hiyo ni kweli, Neno daima humjia nabii Wake. Kwa hiyo hatuwezi kulitarajia kuwajia wanatheolojia. Hatuwezi kulitarajia kuja kwenye madhehebu. Halina budi kupitia kwenye njia ya Mungu ambayo alitutabiria, na hivyo ndivyo tu litakavyopata kuja. Litachukiwa, litadharauliwa, litakataliwa. Litakapokuja, litatupwa kando, na kila kitu, bali Mungu atafanya hivyo haidhuru. Lilikataliwa katika Yesu Kristo, lilikataliwa katika Yohana, lilikataliwa na Yeremia, lilikataliwa na Musa. Daima iko hivyo. Lakini Mungu anasonga mbele moja kwa moja katika njia ambayo Yeye aliahidi angefanya jambo hilo. Naam, bwana, Yeye hashindwi kamwe kufanya jambo lile lile.

-----
Angalia katika Biblia, unaona ambapo, ni wakati gani tunaoishi wakati huo, unapoona mambo haya makuu yakidhihirishwa. Wakati Mungu alipoahidi kufanya jambo hilo, Yeye daima hufanya jambo hilo mwishoni mwa kila wakati kanisa linapofikia mahali pa kugeukia, nalo linageuzwa kutoka kwenye Neno linaingia katika dhambi na anasa. Anasa ni dhambi. Biblia ilisema, “Ukiipenda dunia au mambo ya dunia, kumpenda Mungu hata hakumo ndani yako.”

Nikizungumza jana usiku, nilikuwa nikizungumza juu ya dhabihu iliyotolewa, Mwana -Kondoo. Ilikuwa iwe ni siku saba, ikiwakilisha zile nyakati saba za kanisa. Haikupaswa kuwepo na chachu iliyopatikana miongoni mwa watu, hakukuwapo na chachu kwa muda wa siku saba. Hiyo inamaanisha ya kwamba hakuna kitu kilichochanganywa Nayo, haijatiwa chachu, kila kipindi. Wala hatutaki kanuni zozote za imani, chachu na kadhalika kuchanganywa nasi. Hatutaki tuchanganywe na ulimwengu. Haina budi kuwa ni Mkate wa Mungu usiotiwa chachu, Neno la Mungu, Neno la Mungu lisiloghoshiwa, ambalo, “Mtu ataishi kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”

Mifumo yetu ya kimadhehebu, na tofauti na kadhalika, imeweka chachu ndani yetu, na hiki na kile na ulimwengu na mtindo. Na, loo, imefikia mahali ambapo karibu ni Hollywood kila mahali. Hatimaye itakuja mpaka iwe ni kama Uingereza kule, wito wa madhabahuni utaonewa aibu. Jamani! Kama ndugu alivyosema, “Unawezaje kupata samaki katika mtumbwi?” Hiyo ni kweli.

Hatuna budi kuhubiriwa Injili katika utimilifu Wake, kwa nguvu za Mungu kuthibitisha hilo kulingana na ahadi ya wakati huo na kuthibitisha ya kwamba hayo hasa ni mapenzi ya Mungu. Nje ya jambo Hilo wewe ni mfuasi tu wa kanisa, haidhuru unajaribu jinsi gani, unajaribu kumfanyia Mungu kazi. Unaweza kwenda kwenye karamu za anasa, huenda ukawa mwaminifu sana kwa kanisa; bali isipokuwa hiyo chembechembe hai ya Uzima wa Milele iwe ilikuwa imechaguliwa awali ndani yako, kuwa mwana ama binti ya Mungu, utakua ukiwa kitu fulani kilichoumbuka; bali kamwe hutakuwa mwana ama binti halisi, wa kweli, wa Mungu.

-----
Angalia, tunaona leo ya kwamba watu... Kuna watu wengi hawawezi kuliamini, hata watu waliojazwa na Roho. Nitawapa moja itakayokukaba koo. Ubatizo wa Roho Mtakatifu haumaanishi unaingia, hata kidogo, si juu ya jambo hilo, hauna uhusiano wowote na nafsi yako. Huo ndio ubatizo, unaona. Hii hapa nafsi ya ndani, humu ndani, hiyo inabidi itokane na Mungu. Lakini basi upande wa nje una hisi tano, na tano nje...milango ya kuingia kwenye ninii yako... kuwasiliana na nyumba yako ya duniani. Upande wa ndani, una roho, na mle ndani una milango mitano: dhamiri yako, na upendo, na kadhalika, milango mitano ya kuingia kwenye hiyo roho. Kumbuka, katika roho hiyo unaweza kubatizwa kwa Roho halisi wa Mungu na hata hivyo upotee. Ni hiyo nafsi iliyo hai, ndiyo iliyochaguliwa na Mungu.

Hivi Yesu hakusema, “Wengi watakuja Kwangu siku hiyo, na kusema, 'Bwana, sijatoa pepo, nikafanya kazi kubwa, kubwa mno, nikatabiri, zile karama kuu za Mungu?'” Yeye alisema, “Ondokeni Kwangu, ninyi mtendao maovu, hata sikuwajua ninyi kamwe. Wengi watakuja siku hiyo.”

Hivi Kayafa hakutabiri? Yeye alikuwa ni ibilisi. Tunaona hapo... Tunaona hapo...Na hao makuhani, hao watu wakuu, waliodhaniwa kuwa ni watu mashuhuri katika siku hizo, wanyenyekevu na chochote kile, bali wakashindwa kuona Neno la Mungu Lenyewe likidhihirishwa mbele zao. Tungeweza tu kuchukua lundo lao nililoandika hapa. Vipi kuhusu Balaamu? Yeye alikuwa... Unasema, “Mungu hubadilisha nia Yake.” Yeye habadilishi nia Yake!

Wakati Balaamu alipotoka kama nabii, na akashuka akaenda kule, askofu, mhubiri, cho chote unachotaka kumwita, yeye alikuwa ni mtu mashuhuri. Lakini wakati alipomtaka Mungu shauri kuhusu kushuka kwenda kule na kuwalaani Israeli; yeye kwanza hakuwapenda. Kwa hiyo wakati alipoomba kwenda, Mungu alisema, “Usiende!”
Ndipo wakamtuma mheshimiwa mmoja, kundi fulani, baadhi yao labda ni maaskofu ama wazee, ama wowote wale, huko chini, elimu zaidi, kumshawishi. Alirudi na kumwuliza Mungu tena. Haikupasi kumwomba Mungu mara ya pili! Mungu anaposema jambo hilo kwanza, hilo ndilo! Haikubidi kungojea chochote.

Rebeka hakungojea kupata utaratibu wa pili. Walimwuliza, wakasema, “Je! Utaenda?”
“Hebu aseme.”
Akasema, “Nitaenda!” Alikuwa amevuviwa kabisa na Mungu. Akawa mmoja wa malkia wa Biblia kwa kutenda kwa mdundo wa Roho wa Mungu aliyetenda kazi juu yake na kupokea kile kilichokuwa ni kweli kabisa, naye akakiamini.

Sasa tunaona, Balaamu, bila shaka, asingeweza kuona. Yeye alitoka akaenda akawaangalia watu, akasema, “Sasa, hebu kidogo! Sisi ni watu wakuu, mashuhuri sana huku, ninyi ni kundi tu lililotawanyika.” Mnaona? “Na sisi sote tunamwamini Mungu yule yule.”
Hiyo ni kweli. Wote walimwamini Mungu yule yule. Wote wanamwabudu Yehova. Angalia sadaka ya Balaamu: madhabahu saba, namba kamilifu ya Mungu; yale makanisa saba, unaona; kondoo dume saba, zikinena juu ya kuja kwa Bwana. Kimsingi, yeye alikuwa wa kimsingi tu kama Musa alivyokuwa; lakini, unaona, hapakuwapo na thibitisho la Kiungu. Mle ndani, wote wawili walikuwa manabii.

Lakini chini ya huduma ya Musa, kulikuwako na Nguzo ya Moto ya kimbinguni, Nuru iliyoning'inia kambini. Kulikuwako na uponyaji wa Kiungu, kulikuwako na kelele za Mfalme kambini, ishara kuu, uponyaji wa Kiungu, na maajabu na kadhalika yaliyofanywa miongoni mwao. Ilikuwa ni ishara ya Mungu aliye hai miongoni mwa watu Wake.
Kimsingi, wote wawili walikuwa sahihi. Basi Balaamu akajaribu kuwashawishi watu, naye akawaloga akawaingiza katika jambo hilo. Lini? Kabla tu hawajafika kwenye Nchi ya Ahadi. Siku nyingine moja ama mbili, wangekuwa katika Nchi ya Ahadi.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Matukio ya Sasa Yanadhihirishwa na Unabii.


   Maandiko Anasema...

Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

Waebrania 1:1-2



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)
 

Sirs, is this the time?

(PDF Kiingereza)
Mlima Sunset. Ambapo
wingu ilionekana.

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)

Chapter 11
- The Cloud.

(PDF Kiingereza)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)