Kitabu hiki cha Mihuri Saba.

<< uliopita

ijayo >>

  Mihuri Saba mfululizo.

Kitabu hiki cha Ukombozi.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Pengo kati ya Nyakati Saba za Kanisa na Ile Mihuri Saba.

Na kwa hiyo nilipokuwa nikiomba [Sabino]; jambo la ajabu lilitukia. Na-na nataka kuwa mwaminifu. Sasa, ingewezekana kwamba nililala usingizi. Huenda ilikuwa ni kitu kama njozi, ama ingeweza kuwa ilikuwa ni o-o-ono. Zaidi sana ninaegemea kwenye kuamini kwamba lilikuwa ni ono. Kwamba, nilikuwa nimeinua mikono yangu juu, nikisema, “Bwana, mlipuko huu unamaanisha nini? Na Malaika hawa saba katika kundi la-la piramidi, kunitwaa mimi juu toka ardhini na wakaelekea mashariki, inamaanisha nini?”

Nilikuwa nimesimama pale, nikiwa katika maombi , ndipo jambo fulani likatukia. Na, sasa, kitu fulani kilianguka kwenye mkono wangu. Nami najua, kama wewe hufahamu mambo ya kiroho, huenda likaonekana ni la ajabu sana. Lakini kitu fulani kilianguka kwenye mkono wangu. Na, wakati nilipoangalia, ilikuwa ni upanga. Na mpini wake ulikuwa wa lulu, lulu nzuri kuliko zote nilizopata kuona. Na ile ki-kinga, mwajua, ambapo.... Nadhani ni ya kuzuia mikono yako isichomwe, mwajua, wakati unapo... wa-watu wakipigana; ilikuwa ni ya dhahabu. Na ubaba wa kitara chake haukuwa mrefu sana, lakini ulikuwa tu ni mkali kama wembe; na ulikuwa wa fedha inayomeremeta. Nao ulikuwa ni kitu cha kuvutia kuliko vitu vyote nilivyowahi kuona. Ulinienea mkononi mwangu sawasawa kabisa. Nami nilikuwa nimeushika. Nikasema, “Jinsi ulivyo mzuri!” Nikauangalia. Nami nikawaza, “Lakini, unajua, siku zote ninaogopa upanga.” Kwa namna filani nilifurahi ya kwamba sikuishi katika siku walipozitumia, kwa maana ni-ninaogopa kisu. Na hivyo ni-nikawazia, “Ningefanya kitu gani na huo?” Na wakati nilipokuwa nimeushika mkononi mwangu, Sauti kutoka mahali fulani ikasema, “Huo ni Upanga wa Mfalme.” Na kisha ukaondoka.

-----
Kwa hiyo, mambo hayo tu-tunayadhania tu, kwa maana, bila elimu, mimi hufundisha kwa mifano, ninaangalia na kuona mambo yalivyo, ama jinsi yalivyokuwa katika Agano la Kale, ambalo ni mfano ama kivuli cha lile Jipya, ndipo ninapata wazo fulani lile Jipya lilivyo. Mnaona? Kama vile...Nuhu aliingia safinani kabla ya ile dhiki haijaanza, mfano, lakini hata kabla ya Nuhu, mnaona, kuingia safinani, Henoko alinyakuliwa, unaona, kabla halijatukia jambo lolote. Naye Lutu aliitwa atoke Sodoma kabla chembe moja ya dhiki kuanza, ya maangamizi; lakini Ibrahimu alikuwa, wakati huo wote, nje ya jambo hilo. Unaona, mifano.

Lakini sasa tutasoma aya ya1, Nitasoma aya za kwanza mbili ama tatu Zake.

1 Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.
2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?
3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
(Sasa, unanena kuhusu kutostahili? “Hata kustahili kukitazama; hapana mtu, mahali popote.”)
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.

Tutasimama hapo kwa muda kidogo, katika kusoma Ufunuo sura ya 5, kuendelea hata kufikia aya ya 7.

Kitabu hiki cha Mihuri Saba kinafunuliwa wakati wa zile Ngurumo Saba za Ufunuo 10.

-----
Sasa, angalia, siri ya Kitabu hiki cha Mihuri Saba itafunuliwa wakati wa kupiga baragumu ya Ujumbe wa malaika wa kanisa la saba. Unaona? “Malaika wa saba anaanza kupiga baragumu,” na ndizo hizo hapo Jumbe zilizoandikwa humo, nasi tunazo kwa jinsi ya kanda na vitabu. Sasa, “Mwanzoni mwa kutangazwa kwa Ujumbe huo, siri ya Mungu itamalizika, unaona, wakati huo.” Sasa tutaona. Kile Kitabu, cha siri ya Mungu, hakifunuliwi mpaka Ujumbe wa malaika wa saba utakapotangazwa. Sasa, mambo haya yatakuwa ni muhimu katika ile Mihuri, nina hakika, maana hakina budi, kwa kila sehemu, kushikamana.

Sasa, kumeandikwa kimafumbo, kwa sababu hakuna mtu, mahali popote , anayekijua. Mungu peke Yake, Yesu Kristo, unaona. Sasa, lakini ni ....Ni Kitabu, Kitabu cha kimafumbo. Ni Kitabu cha Ukombozi. Tutaingilia jambo hilo, hivi punde. Na sasa tunajua ya kwamba Kitabu hiki cha Ukombozi hakitafahamika vizuri kabisa; kimechunguzwa, katika nyakati sita za kanisa. Lakini mwishoni, wakati malaika wa saba atakapoanza kutangaza siri yake, anamalizia sehemu zote zilizoachhwa ambazo jamaa hawa walichunguza. Nazo hizo siri zinashuka kutoka kwa Mungu, kama Neno la Mungu, na kufunua ufunuo wote mzima wa Mungu, ndipo Uungu na chochote kile kinakamilishwa. Mafumbo yote, uzao wa nyoka, na chochote kile, zitafunuliwa.

-----
Mihuri saba kwenye Kitabu hicho, zime... Kile Kitabu kimefungwa kwa Mihuri hii Saba. Mnaona? Kitabu kimefungwa kabisa. Mnaliona jambo hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.”-Mh.] Kitabu kilichofungwa kabisa mpaka ile Mihuri Saba itakapovunjwa. Kimefungwa kwa Mihuri Saba. Sasa, hiyo ni yofauti na zile Ngurumo Saba. Unaona? Hizi ni Mihuri Saba kwenye kile Kitabu. Nacho Kitabu hakitaninii, Mihuri haitaachiliwa mpaka kwenye ule Ujumbe wa malaika wa saba. Unaona? Kwa hiyo tuna-tunadhania; lakini Ufunuo halisi wa Mungu utakamilishwa katika kule kutangazwa, kwa ile kweli iliyothibitishwa. Sasa, hivyo ndivyo Neno linavyosema hasa, “Ile siri itatimizwa katika wakati huo.” Na Kitabu hiki cha Mihuri Saba, kumbuka, kilikuwa kimefungwa hapa, katika Ufunuo sura ya 5, na katika Ufunuo sura ya 10 kimefunguliwa.

Na sasa tutaona vile Kitabu hiki kinavyosema kuhusu jinsi kilivyofunguliwa. Na hakijulikani mpaka Mwanakondoo anapokitwaa kile Kitabu, na kuivunja ile Mihuri, na kukifungua Kitabu. Mnaona? Mwanakondoo hana budi kukitwaa kile Kitabu.

Kimefichwa. Sasa kumbukeni, “Hakuna mtu Mbinguni, hakuna mtu duniani,” papa, askofu, kadinali, mzee wa jimbo, ama yeyote yule, “anayeweza kuivunja hiyo Mihuri, wala kukifunua kile Kitabu, ila Mwanakondoo.” Nasi tumetafuta, na kubahatisha, na kujikwakwaa, na kushangaa, na-na hiyo ndiyo sababu sote tuko katika mchafuko kama huu.

Lakini tukiwa katika ahadi ya Kiungu ya kwamba Kitabu hiki cha Ukombozi kitafunguliwa kikamilifu na Mwanakondoo, na Mihuri yake itafunguliwa na Mwanakondoo, katika siku za mwisho tunazoishi sasa. Na hakitajulikana mpaka Mwanakondoo atakapokitwaa Kitabu hicho na kuivunja ile Mihuri. Kwa sababu, kumbukeni, kile Kitabu kilikuwa kimeshikiliwa katika mikono ya Yeye aliyeketi juu ya Kiti cha Enzi. “Naye Mwanakondoo anamjia Yeye aliyeketi juu ya Kiti cha Enzi na kukitwaa kile Kitabu kutoka katika mkono Wake wa kuume.” Anakitwaa kile Kitabu! Loo, hilo ni la kilindi. Tutajaribu kulitatua kama tukiweza, kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Sasa tunamtegemea Yeye. Nasi tutaona, baadaye, ni kwenye wakati wa mwisho, “Hapo wakati utakapokuwa umekwisha.” Hakuna madhehebu yaliyo na haki ya kukifasiri Kitabu hiki. Hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kukifasiri. Mwanakondoo ndiye anayefasiri. Na Mwanakondoo ndiye anayekinena, naye Mwanakondoo anafanya Neno lijulikane, kwa kulithibitisha na kulihuhisha Neno. Unaona? Kweli kabisa!

-----
Lakini sheria Mungu ilipokea kibadala. Sasa, vipi kama Mungu hakuwa amejitolea kutoa kibadala? Lakini Upendo ulimshurutisha kufanya jambo hilo. Kwamba, mwanadamu hakuwa na njia ya kurudia, na hakuna njia kwake ya kurudi. Alikuwa amepotea. Lakini neema ya Mungu ilikukutana na huyu Mkombozi aliye wa Jamaa wa Karibu katika Utu wa Yesu Kristo. Sheria ilihitaji jambo hilo. Neema ikatimiza masharti yake. Loo, neema ya ajabu , jinsi inavyosikika tamu! Sheria ya Mungu ilihitaji kibadala kisicho na hatia. Na ni nani ambaye hakuwa na hatia? Kila mtu alikuwa amezaliwa kwa kujuana kimwili, kwa kujuana kimwili, kila mmoja. Na yule pekee asiyekuwa hivyo, alikuwa amepoteza haki za Uzima wa Milele na yeye kuwa mfalme duniani.

Loo, ninapowazia Andiko hilo, “Kwa kuwa umetukomboa kuturudisha kwa Mungu, na tupate kutawala na kuwa wafalme na makuhani juu ya nchi.” Loo, jamani! Ni nini? Mkombozi aliye wa Jamaa wa Karibu! Loo, ni habari ya namna gani tungeisimulia hapa! Angalia, sheria ilihitaji Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu ili kukomboa kitu kilichopotea. Neema ilitimiza sharti hili katika Utu wa Yesu Kristo. Jamaa wa Karibu hana budi kuzaliwa kwa jamii ya wanadamu.

Sasa, tungewezaje kuwa huyo, wakati kila mtu aliyezaliwa hana budi kuninii...Na mtu yeyote asiyeweza kuona ilikuwa ni tendo la kujuana kimwili pale, vema, yeye ni kipofu kabisa, unaona, maana kila mtu aliyepata kuzaliwa alizaliwa na mwanamke. Na Mungu alihitaji Mkombozi aliye ya Jamaa wa Karibu, naye hana budi kuwa ni mwanadamu. Loo! jamani! Mtafanya nini sasa? Sheria ilitaka Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu. Sasa, Yeye asingeweza kuchukua Malaika. Ilibidi amchukue mwanadamu, maana sisi si wa ukoo wa Malaika. Sisi ni ndugu sisi kwa sisi. Malaika hakuanguka kamwe. Yeye ni kiumbe cha namna nyingine, ana mwili tofauti. Yeye hakufanya dhambi wala chochote kile. Yeye ni tofauti. Lakini sheria ilitaka Mkombozi aliye Jamaa ya Katibu. Na kila mtu duniani alizaliwa kwa kujuana kimwili. Sasa, je, hamwoni, hapo ndipo hilo lilipochimbuka. Hapo ndipo dhambi ilipoanzia. Kwa hiyo unaona mahali jambo hilo lilipo sasa? Huyo hapo anakuja, uzao wenu wa nyoka, unapoingia. Unaona?

Sasa, angalia, alihitaji Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu. Na Mkombozi, Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu , hana budi kuzaliwa na jamii ya mwanadamu. Hapa, hiyo itatuacha mahali pa hatari. Lakini hebu niwapigie Baragumu. Ule uzazi wa kibikira ulimleta yule-yule mzao. Amina. Uzazi wa kibikira ilimzaa Mkombozi aliye wa Jamaa yetu wa Karibu. Si mwingine bali ni Mwenyenzi Mungu aliyefanyika Imanueli, mmoja wetu. Imanueli! Yule “Mkombozi aliye Jamaa wa Karibu” alipatikana. Unaona jinsi Mungu anavyotoa masharti fulani, na hakuna jambo tunaloweza kufanya. Lakini basi neema inaingia na kuzidi hiyo sheria, na kuleta ule uzao. Amina!

-----
Kitabu cha Ruthu kinatoa picha nzuri ya jambo hili, jinsi Boazi... na Naomi walivyokuwa wamepoteza shamba. Ninyi, mnajua. Mlinisikia nikihubiri juu ya jambo hilo, sivyo? Inueni mikono yenu juu kama mlinisikia nikihubiri juu ya jambo hilo. Kwa hiyo, mnafahamu, mnaona. Ilimbidi Boazi awe mkombozi. Naye ndiye tu ambaye angeliweza kuwa mkombozi. Ilibidi awe jamaa, jamaa wa karibu. Na, katika kumkomboa Naomi, alimpata Ruthu. Huyo alikuwa ni Yesu, Boazi akiwa ni mfano wa Kristo. Na alipowakomboa Israeli, alimpata Bibiarusi Mmataifa. Kwa hiyo basi, mnaona, ni zuri mno! Tunalo katika kanda, nina hakika, hapa mahali fulani, mkitaka kulipata.

-----
Huyo ndiye aliyetimiza lile sharti. Neema ilileta Utu wa Yesu Kristo. Nasi tunaona, Kitabu hiki sasa...Mungu alitandaza hema Yake, iliyotoka kwa Mungu, akifanyika mwanadamu. Alibadili hali Yake kutoka kuwa Mwenyenzi, akawa mwanadamu; kuchukua umbo la mwanadamu, apate kufa, ili amkomboe mwanadamu. Ngojeni mpaka tutakapomwona, wakati hakuna mtu yeyote anayestahili. Unaona? Vema.

Katika Biblia, katika Kitabu cha Ruthu, unaposoma, utaona kwamba, mtu kama huyo aliitwa “goel,” Aliitwa g-o-e-l. Aliitwa goel, ama, alikuwa ni mtu fulani ambaye angeweza kutimiza masharti hayo. Na goel hana budi kuwa angeweza kufanya jambo hilo, hana budi kuwa tayari kufanya jambo hilo, na hana budi kuwa jamaa, jamaa aliye wa karibu, ili kufanya jambo hilo. Na Mungu, yule Muumba, wa Roho, akafanyika jamaa yetu wa karibu hapo Yeye alipofanyika mtu, kusudi kwamba Yeye aweze kujitwika dhambi yetu, na kulipa gharama, na kutukomboa kurudi kwa Mungu tena. Hivyo ndivyo ilivyo. Huyo hapo yule Mkombozi. Kristo ametukomboa sasa. Sasa sisi tumekombolewa. Lakini bado hajadai mali Yake. Sasa, unaweza kutokubaliana na jambo hilo, lakini ngoja tu kidogo, unaona.

Tutaona. Unaona? Hajadai. Unaona? Kama alikitwaa kile Kitabu cha Ukombozi, kila kitu ambacho Adamu alikuwa nacho na kila kitu ambacho alipoteza, Kristo anakikomboa na kukirudisha. Naye tayari ametukomboa. Lakini bado hajachukua mamlaka; hawezi mpaka wakati ulioamriwa. Na ndipo utakuja ufufuo, na halafu dunia itafanywa upya tena. Na ndipo atamiliki, mali Yake aliyopata hapo alipotukomboa sisi, lakini atafanya hivyo katika wakati ulioamriwa. Loo, jamani! Jambo hili limeelezwa katika Kitabu hiki cha Muhuri Saba tunachonena habari zake sasa. Vema. Kitau cha Ukombozi, yote yameelezwa hapa ndani. Yote yale ambayo Kristo atafanya wakati wa mwisho yatafunuliwa kwetu juma hili, katika ile Mihuri Saba kama Mungu ataruhusu. Unaona?...

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Pengo kati ya Nyakati Saba za Kanisa na Ile Mihuri Saba.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.

Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.

Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.

Ufunuo 10:1-3


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDF Kiingereza)

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)
Ambapo upanga ulionekana.

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)

Kitabu hiki
cha Mihuri Saba
kinafunuliwa
wakati wa zile
Ngurumo Saba
za Ufunuo 10.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.