Nafasi katika Kristo.

<< uliopita

ijayo >>

  Kuasili mfululizo.

Kuasili #3.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3.

Na sasa kusudi la masomo haya ni kuwatia nanga wale ambao tayari wamevuka na kufika Nchini. Kusudi la somo hili, kule kujifunza Kitabu hiki cha Waefeso, ni kuliweka kanisa mahali pake ambapo linasimama imara katika Kristo. Ni mfano wa Agano la Kale na Kitabu cha Yoshua, ambapo Yoshua aliwagawia. Jumapili iliyopita tulikuwa nalo, ambapo Yoshua aliigawa ile ardhi kwa kila mtu. Naye alifanya hilo kwa uvuvio.

-----
Sasa, huenda ukakosea, na kila unapofanya kosa lo lote utalilipia. Naam, bwana, utavuna unachopanda! Lakini hilo halina uhusiano wo wote na wokovu wako. Unapozaliwa kwa Roho wa Mungu, una Uzima wa Milele na huwezi kufa tena kama Mungu asivyoweza kufa. Wewe ni sehemu ya Mungu, wewe ni mwana wa Mungu.
Nilizaliwa Branham. Huenda ukanitengenezea jina lingine, baadhi ya majina mengine, lakini hutanifanya nisiwe hata kidogo, mimi bado ningali Branham. Nilizaliwa Branham, daima nitakuwa Branham. Huenda nikaharibiwa sura sana siku moja, niambukizwe yabisi kavu, nipate ajali ya gari na nijeruhiwe sana hata nionekane kama mnyama, lakini bado nitakuwa Branham! Kwa nini? Damu ya Branham iko ndani.

Hivyo ndivyo wewe ulivyo. Na mradi tu Mungu amekufanya... Sasa kumbukeni, siwazungumzii hao walio nje ya Kristo. Nawazungumzia hao walio ndani ya Kristo. Unaingiaje katika Kristo? “Kwa Roho mmoja!” Herufi kubwa R-o-h-... ambayo inamaanisha, “Kwa Roho Mtakatifu mmoja sote tumebatizwa kuwa Mwili mmoja.” Sisi tunaingiaje? Kwa ubatizo wa maji? Jinsi nisivyokubaliana na ninyi Wabaptisti na ninyi Kanisa la Kristo. Si kwa ubatizo wa maji, la hasha! Wakorintho wa Kwanza 12, ilisema, “Kwa Roho mmoja, Roho Mtakatifu, tunaingizwa katika Mwili huo.” Nasi tunakuwa salama tu kama vile Mwili huo ulivyo salama. Mungu aliahidi jambo hilo.

Mungu angewezaje kumhukumu tena, na huku Yeye alienda Kalvari? Akipanda kwenda Golgotha, alipigwa, akajeruhiwa, Yeye asingeweza kuponya, hata hangeweza kunena neno, ilikuwa vigumu. Kwa sababu gani? Yeye alikuwa amebeba dhambi za ulimwengu juu Yake. Si kwa sababu Yeye alikuwa mwenye dhambi, bali “Yeye alifanyika dhambi” kwa ajili yangu na kwa ajili yako. Dhambi zote za ulimwengu tangu Adamu mpaka kuja Kwake, zilikuwa juu ya bega Lake. Na Mungu hakuwa anamwadhibu Mwanawe. Alikuwa akiadhibu dhambi. Mnaona jinsi lilivyokuwa la kutisha? Alikuwa akifanya upatanisho. Alikuwa akitengeneza njia ya kuepukia kwa wale wote ambao Mungu, kwa kujua Kwake tangu zamani, alijua wangekuja.

Sasa, basi, unapokuwa “kwa Roho mmoja tumebatizwa katika Mwili huo, Mwili mmoja, ambao ni Kristo,” nasi tuko salama milele.
Sasa, hapo ndipo linapoonekana kama linagusa sana, hasa hao waumini Waarmenia, ya kwamba wao... inawabidi kufanya jambo fulani kusudi wastahili, ama jambo fulani la kustahilisha. Inawezaje kuwa kwa mambo mawili kwa wakati ule ule? Aidha ni kwa neema ama kwa matendo, mojawapo. Haiwezi kuwa kwa jambo lile lile, ni kwa mambo mawili tofauti; haina budi kuwa ni kwa njia moja.

Mimi, jamani, siwezi kuona kitu kingine ila neema ya Mungu. Nimeumbwa hivyo. Daima nimeamini katika neema. Mimi ni neema tu kila mahali, hivyo tu. Si mimi... hata maishani mwangu, nilipokuwa mvulana, nikuweza kuona chochote, neema tu, neema. Wao wanasema, “Ukikuna mgongo wangu nami nitakuna wako.” Vema, huo ni msemo wa kutisha. Lakini sijali kama utaukuna wangu au la, kama wako unahitaji kukunwa, nitakukuna hata hivyo. Unaona, neema. Naam, bwana. Unaona, neema hutenda kazi kwa upendo. Kama unahitajihilo! Haidhuru kama hukufanya kitu cho chote kamwe, sina uhusiano wo wote nawe, kama ukihitaji nitalifanya hilo hata hivyo. Neema! Kwa sababu unaihitaji!

Nilihitaji kuokolewa. Hakukuwa na kitu kingeweza kuniokoa. Hakuna kitu ningeweza kufanya juu yangu mwenyewe, singeweza kujiokoa hata nifanyeje. Lakini nilihitaji kuokolewa, kwa sababu niliamini katika Mungu fulani. Naye Mungu akamtuma Mwanawe, aliyefanywa katika mfano wa mwili wenye dhambi, apate kuteseka mahali pangu, nami nikaokolewa, kwa neema pekee niliokolewa. Singeweza kufanya hata jambo moja, ama wewe ufanyae kujiokoa mwenyewe. Na wale aliotangulia kuwajua tangu zamani kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu....

-----
Kisha ndani Yake mlikuwemo sifa ya kuwa Mwokozi. Mmoja wa hao Viumbe angewezaje, wakati hakukuwemo na dhambi wala mawazo ya dhambi, mmoja wao angewezaje kupotea? Isingewezekana. Kwa hiyo ilibidi kuwe na kitu fulani kilichofanywa ambacho kingeweza kupotea, ili kwamba aweze kuwa Mwokozi. Ndani Yake kulikuwa na Mponyaji. Mnaamini Yeye ni Mwokozi? Mnaamini Yeye ni Mponyaji? Lakini vipi kama hakungekuwako na kitu cha kuokoa au kuponya? Unaona, ilibidi kuwe na kitu kilichofanywa namna hiyo.

Kwa hiyo sasa, Yeye hakulifanya hivyo, bali alimpa mwanadamu uhuru wa kuamua takalo, “Kama ukichukua hii utaishi, kama ukichukua ile unakufa.” Na kila mtu anayekuja ulimwenguni angali amewekwa katika hali ile ile. Mungu, kwa kujua Kwake tangu zamani, alijua ni nani angefanya na ni nani asingefanya.

-----
Kwa hiyo sasa, Mungu huweka. Yeye tayari amejidhihirisha Mwenyewe, Yeye ni Mungu. Yeye tayari amejidhihirisha Mwenyewe kama Mwokozi, mwanadamu alipotea Naye akamwokoa. Yeye tayari amejidhihirisha Mwenyewe kama Mponyaji. Haidhuru watu wanasema Yeye ni nani; Naye ndivyo alivyo, hata hivyo, vile vile. Yeye ni Mponyaji, Yeye ni Mwokozi, Yeye ni Mungu, Yeye ni wa Milele. Naye ana kusudi. Na kusudi Lake lilikuwa, hapo mwanzo, kuwaumba viumbe ambao wangempenda na kumwabudu.

Naye akaumba viumbe, na viumbe vikaanguka. Na kisha Mungu, kwa kutokuwa Kwake na ukomo, aliangalia kupitia mlolongo wa wakati akaona kila mtu ambaye angeokolewa. Kila mtu, Yeye alijua hilo kwa kutangulia... kwa kujua tangu zamani. Kwa hiyo kama Yeye, kwa kujua tangu zamani, alijua ni nani angeokolewa na ni nani hangeokolewa, Yeye angeweza kuchagua tangu zamani. Kwa hiyo, hilo neno hilo si neno baya hata hivyo, sivyo? Yeye angeliweza kuchagua tangu zamani, kwa sababu alijua ni nani angeokoka na ni nani asingeokoka. Kwa hiyo, kusudi apate kuwapata wale ambao wangeokoka, ilimbidi kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zao. Loo, kama tunaweza, tunataka kulifikia jambo hilo, aya chache tu hapa chini. Yeye alitangulia kutuchagua tangu zamani tupate Uzima wa Milele, akijua kwamba wale ambao wangeweka kando kila kitu, na hata ionekane ni gumu vipi kwa watoto wa ulimwengu, haingemaanisha lolote kwao, kwa sababu wao walikuwa watoto wa Mungu. Naye aliwaita.

Naye alimtuma Yesu, ili kwamba Damu Yake ipate kuwa upatanisho, Upatanisho wa Damu, kufanya upatanisho, ama kukubalika, ama utakaso. Utaratibu wa kutakasa ili daima... Si wakati mmoja tu kwenye uamsho mmoja, bali “yu hai daima, akiwaombea,” hivi kwamba Mkristo anawekwa msafi mchana na usiku. Hiyo hapo Damu ya Yesu Kristo inayofanya kukubalika msalabani pale, kwenye... katika Uwepo wa Mungu, ambayo hutusafisha daima, mchana na usiku, mbali na dhambi zote. Nasi tumeingizwa ndani salama. Kuingizwa ndani vipi? Na Roho Mtakatifu, katika Mwili wa Bwana Yesu, na tuko salama. “Yeye ayasikiaye Maneno Yangu na kumwamini Yeye aliyenituma, yuna Uzima wa Milele na hataingia hukumuni kamwe, bali amepita kutoka mautini kuingia Uzimani.” Hakuna hukumu tena! Mkristo kamwe haingii hukumuni. Kristo alikwenda kwa ajili yake. Wakili wangu alisimama mahali pangu. Yeye alinitetea, ya kwamba sikujua. Yeye alimwambia Baba kwamba sikustahili, ya kwamba sikujua kitu. Lakini Yeye alinipenda na akachukua mahali pangu, na akanitetea, na leo niko huru! Naam, bwana. Naye akamwaga Damu Yake, kuitoa paleo kwa ajili ya dhambi zetu.

-----
Kisha kufanywa wana wenye mamlaka, kuwekwa mahali petu. Sasa, wema wa Mungu unapaswa kutenda kazi. Na sasa kama ninaweza kuwaeleza jambo hili, basi tutaanza sasa hivi ile aya ya 5, nataka kuisoma.
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi Yake Mwenyewe.
Mungu hupendezwa kufanya mapenzi Yake, kufanya wana wenye mamlaka, kuwaweka mahali pao. Sasa Yeye anafanya nini? Akiliweka Kanisa Lake mahali pake. Kwanza, Yeye ameliita kanisa Lake, Methodisti, Presbiteri, Lutherani, Baptisti, akiwaita. Kisha Yeye alifanya nini? Akamtuma Roho Mtakatifu na kuwapa ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Nawatakeni ninyi Wapentekoste mwondoe jambo hili mioyoni mwenu. Pentekoste si dhehebu; Pentekoste ni tukio. Ni Roho Mtakatifu. Si shirika la dini. Usingeweza kumfanya Roho Mtakatifu dhehebu. Yeye hatavumilia jambo hilo. Sasa mna dhehebu mnaloliita hivyo, bali Roho Mtakatifu hutoka nje kabisa na kuwaacha mmeketi papo hapo mlipo, na anazidi tu kusonga mbele. Unaona? Pentekoste si dhehebu; Pentekoste ni tukio.

-----
Sasa kumweka mwana mahali pake. Jambo la kwanza baada ya mwana kuingia, akawa mwana, lakini basi tunaona tabia yake ndiyo iliyomfanya afanywe mwana mwenye mamlaka, kama alikuwa na tabia nzuri au la. Na ni kipentekoste... Sasa hebu niwaonyeshe tu kwamba Pentekoste si dhehebu. Ni Wabatisti wangapi humu ndani waliokuwa Wabatisti, waliompokea Roho Mtakatifu, hebu tuone mikono yenu. Unaona? Ni Wamethodisti wangapi walio humu ndani waliompokea Roho Mtakatifu, inueni mikono yenu. Ni Wanazarayo wangapi humu ndani waliompokea Roho Mtakatifu, inueni mikono yenu. Mpresbiteri, mmempokea Roho Mtakatifu? Unaona? Mluteri? Madhehebu mengine, ambayo hayakuwa ya Pentekoste kabisa, yalikuwa tu ya dhehebu fulani, yaliyompokea Roho Mtakatifu, hebu tuone mkono wako. Unaona? Kwa hiyo basi Pentekoste si dhehebu, ni ujuzi.

Sasa, Mungu alikuingiza katika Mwili wa Kristo. Sasa Yeye anafanya nini? Baada ya kujithibitisha mwenyewe, ukajitakasa mwenyewe kwa tabia yako njema, mtiifu kwa Roho Mtakatifu, haidhuru ulimwengu ulisema nini.

-----
Mtaendelea kutumia jina hilo “Baba, Mwana na Roho Mtakatifu” kubatiza, wakati hakuna hata chembe moja ya Andiko kwa ajili ya jambo hilo katika Biblia. Nataka askofu mkuu ama mtu mwingine anionyeshe mahali mtu ye yote katika Biblia aliwahi kubatizwa katika jina la “Baba, Mwana, Roho Mtakatifu.” Ninataka mtu fulani anionyeshe mtu yeyote aliyewahi kubatizwa kwa njia yo yote mbali na Jina la Yesu. Lakini wa Yohana hawakuwa... wamebatizwa, walibatizwa wakiamini kwamba Yeye alikuwa anakuja, bali hawakujua Yeye alikuwa nani. Lakini mara walipotambua jambo hilo, iliwabidi kuja na kubatizwa tena katika Jina la Yesu Kristo. Ninataka mtu fulani a... Nimewauliza Assemblies of God, hao wahubiri wengine, Wabatisti, Wapresbiteri, na kila kitu. Hawataki, hawatazungumza juu ya jambo hilo. Nataka kuyaona hayo Maandiko.

Na kisha ati mimi ni “mshupavu wa dini,” aha, halafu mimi ni “kicha,” nimerukwa na akili, mimi ni “mwenda wazimu,” kwa sababu tu kwamba ninajaribu kuwaambieni ile Kweli? Sasa, hilo ni uaminifu, enyi ndugu. Kama mtu amejitolea kabisa kwa ajili ya Mungu, umejitolea kabisa kabisa, kwa hali na mali. Wewe umewekwa wakfu, wewe ni kiumbe tofauti.

Wengi wameitwa, wachache wamechaguliwa. Naam, watu wengi wameitwa, unapata wito moyoni mwako, “Naam, naamini Mungu ananipenda. Naamini Yeye ananipenda.” Lakini, ndugu, hivi, utapotea kabisa kama hao wengine, kwa sababu watakuja huko siku hiyo, hata wakisema, “Bwana, nimetoa pepo katika Jina Lako. Nimefanya kila kitu kingine katika Jina Lako. Nimekuwa na ibada za uponyaji. Nimehubiri Injili. Nimetoa pepo.” Naye Yesu anasema, “Ondokeni hapa, hata siwajui, wanafiki. Ni Yeye afanyaye mapenzi ya Baba Yangu!” Kwa nini watu hawawezi kuliona jambo hilo? Sasa, najua hilo linaudhi. Nami simaanishi kuwaumiza, sikusudii iwe hivyo.

Inaonekana kwangu kana kwamba tuko katika wakati wa mwisho, na Mungu anawafanya wana wenye mamlaka, akiwaeka katika mahali pao Kanisani, katika Mwili wa Kristo, Wake. Sasa, hakutakuwa na wengi sana ambao Yeye atawaweka mle ndani, nitawaambieni hilo kwanza. Unasema, “Loo, vema, kutakuwa na idadi kubwa sana!” Lakini Yeye amekuwa na miaka elfu sita ya kuwavuta watoke, pia. Kumbukeni, ufufuo unakuja nasi tunanyakuliwa pamoja nao. Wachache wao tu, mnaona. Wewe unatafuta wokovu wako, upesi. Jichunguze mwenyewe na uone ni kitu gani kimeharibika. Unaona? Angalia tu— kuna shida gani. Najua hilo ni gumu, lakini, ndugu, ni Kweli. Ni Kweli ya Mungu. Kufanywa wana wenye mamlaka!

-----
Kufanywa wana wenye mamlaka, kuwekwa mahali pao! Wako wapi? Nionyeshe mahali walipo. Mungu akiwaita watoto Wake kando kwa njia ya udhihirisho. Haiwalazimu kusema neno moja juu yake, unaona jambo fulani limetukea. Akimweka mwanawe mahali pake, akimweka katika taratibu na mambo yale yale hasa. Yeye yuna mamlaka sawa, neno lake ni kama tu la Malaika Mkuu, bora zaidi. Mwana alifanywa mwana mwenye mamlaka, akawekwa mahali pa juu, akaketishwa pale, akabadilisha majoho yake, akabadilisha rangi zake. Baba yake alikuwa na sherehe, kasema, “Huyu ni mwanangu, tangu sasa yeye ndiye liwali. Yeye ndiye mtawala. Yeye yuko juu ya urithi wangu wote. Yote niliyo nayo ni yake.” Hiyo ni kweli.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;

bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

Wagalatia 4:1-3


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Kimo Cha Mtu
Mkamilifu.
(PDF)

Nguzo ya Moto.
- Bega

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.