Kuasili.
<< uliopita
ijayo >>
Kuasili #4.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #4.Sasa yeye alisema, “Alitujulisha lile fumbo.” Upate Roho Mtakatifu wakati fulani, na uanze kuendeleza Hilo na uangalie tu jinsi inavyoenda. Alasiri ya leo nilikuwa na, loo, kama dakika thelathini za kusoma, kupitia tu somo hili; labda sivyo, ningesema nusu ya hizo, kama kwenye dakika kumi na tano katikati ya nyakati. Nami nikaanza kulifuatilia, nikawaza, “Lile fumbo, ni ya kimafumbo iliyoje!” Na Maandiko yalinirudisha katika Agano la Kale, kisha yakanirudisha kwenye Agano Jipya; yakafumanganisha mambo fulani pamoja, kuona lile fumbo la Kuja Kwake, fumbo la mapenzi Yake, lile fumbo la sisi kuketi pamoja. Kumbuka, haiwezi kufundishwa katika seminari yoyote. Ni fumbo. Huwezi kulijua kwa njia ya elimu, kwa njia ya theolojia. Ni fumbo lililofichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, likingojea kudhihirishwa kwa wana wa Mungu.
Niambie, ndugu yangu, niambie, dada yangu, ni wakati gani ambapo wana wa Mungu walipaswa kudhihirishwa nje ya wakati huu sasa? Ni lini kuliwahi kuwako na wakati katika historia, walipodhihirishwa katika wakati wa kuyakomboa viumbe vyote? Viumbe, viumbe vyenyewe vinaugua, vikingojea ule wakati wa kudhihirishwa. Mbona, kabla ya ule upatanisho kufanywa, kabla ya Roho Mtakatifu kumwagwa, kabla ya Agano la Kale lote, na kuendelea huko kote, hakungaliweza kuwa na kudhihirishwa. Kulipaswa kungoje mpaka wakati huu. Sasa mambo yote yamekwishaletwa, yakija, yakielekea kwenye jiwe la kichwani, kufikia kule kudhihihirishwa kwa wana wa Mungu, na Roho wa Mungu akiingia ndani ya hawa watu, kikamilifu sana, hata huduma yao itafanana sana na ya Kristo hata itamuunganisha Yeye na Kanisa Lake pamoja.
----
Kama ulikuwa umechaguliwa tangu zamani kwa ajili ya Uzima wa Milele, Mungu atakuita kwa njia fulani, kwa namna fulani, kwa njia fulani ama nyingine. Hakika atakuita. “Wote alionipa Baba watakuja Kwangu.” Haidhuru wewe ni wa kanisa gani, hilo halina uhusiano wowote nalo. Lakini dhehebu kamwe halitakusaidia kwa lolote, bali huenda likakuzuia sana kuambatana na Mungu, bali halitafanya jambo lingine kamwe. Linakusanya pamoja na kundi la waaminio na wasioamini. Bila shaka, unakutana na hilo kila mahali uendako, na hata walikuwa na jambo hilo Mbinguni. Kwa hiyo, ni sawa, bali unategemea dhehebu lako. Mtegemee Yesu, Yeye Ndiye wa kutegemewa.----
Sasa, tazama, basi kule Kuja kwa Bwana Yesu kumekaribia sana hata Roho kutoka kwenye kina cha ndani kabisa humu... kufikia tu kuhesabiwa haki, kutakaswa, ubatizo wa Roho Mtakatifu, na sasa kufikia wakati wa kuja kwa lile Jiwe la Kuweka Juu. Kanisa halina budi kufanana kikamilifu kabisa na Kristo hadi Kristo na Kanisa waweze kuungana pamoja, Roho yule yule. Na kama Roho wa Kristo yumo ndani yako, anakufanya uishi maisha ya Kristo, kutenda maisha ya Kristo, kufanya kazi za Kristo. “Yeye aniaminiye Mimi, kazi nizifanyazo Mimi yeye naye atazifanya.” Yesu alisema hayo. Unaona? Sasa tutakuwa na, tuna huduma inayokuja ambayo inafanana kabisa na maisha ya Kristo. Huduma hiyo inatambulisha nini? Kuja kwa Bwana.Liangalie hilo ulimwenguni leo, na uone yale Khrushchev anayosema, mambo haya mengine yote makuu, na mizozo mikubwa ulimwenguni kote ilnavyokaribia, wakati wo wote, ingeweza kuwa unga sekunde yoyote. Hiyo ni kweli. Na kama ndivyo, tunajua ya kwamba hilo linakaribia. Mtu ye yote mwenye akili anaweza kusoma katika gazeti ama kusikiliza redio, na kujua kwamba jambo hilo limekaribia. Vema, kumbukeni, Kristo anakuja kwa ajili ya Kanisa Lake kabla jambo hilo halijatukia. Kwa hiyo Kuja kwa Bwana Yesu kumekaribia namna gani? Labda kabla mkutano huu haujaisha usiku huu. Tuko katika wakati wa mwisho. Ni kweli hakika.
Angalia jinsi kanisa limekuja, linavyosonga mbele. Hebu liwazieni katika nia zenu, ninyi wanahistoria mnaosoma historia. Angalia kanisa la Kiluteri chini ya kuhesabiwa haki, likitoka tu katika Ukatoliki likiwa jipya, liangalieni likisonga mbele. Kisha mwangalieni Wesley akikaribia kidogo, katika utakaso, akipitia katika Maandiko. Angaliani papo hapo katikati, yule Wesley. Ndipo kitu kilichofuata kilikuwa ni wakati wa Kipentekoste. Na wakati wa Pentekoste ukiwa ni kurejeshwa kwa karama, karama za kiroho. Sasa, angalieni ule wakati unaokuja sasa hadi kwenye lile Jiwe la Kuweka Juu. Mnaona ninalomaanisha? Kuja kwa Bwana, kufunuliwa. Mungu pamoja na viumbe vyote anangojea kanisa lipate mahali pake.
----
Baada ya kanisa kuchukua mahali pake, tunaitwa tupate kufanywa wana wenye mamlaka, kwa njia ya Roho Mtakatifu. Na wakati kila mtu anapochukua mahali pake, kile Mungu amemwitia kufanya, na kusimama kwenye mwisho wa safari, akiwafuatilia waliopotea.Kwanza, Paulo anaondoa woga wote kutoka kwenye hilo, kwa hiyo sasa, “Kama umeitwa, iwapo wewe husukumwi na namna fulani ya theolojia, kama kweli umezaliwa na Roho, basi Mungu alikuchagua tangu zamani kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, akaliandika jina lako kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, na sasa tunakusanyika pamoja kuketi katika maeneo ya Kimbinguni katika Kristo Yesu. Watu watakatifu, taifa takatifu, watu wa kipekee, ukuhani wa kifalme, tukitoa dhabihu za kiroho kwa Mungu, yaani, matunda ya midomo yetu ikilisifu Jina Lake.”
Watu huingia na kusema, “Hao watu wana kichaa.” Hakika ni vichaa; hekima ya Mungu ni upumbavu kwa mwanadamu, na hekima ya mwanadamu ni upumbavu kwa Mungu. Zinahitilafiana, moja kwa nyingine.Lakini kanisa halisi lililojazwa na Roho, lililojaa nguvu za Mungu, likiketi pamoja katika meneo ya Kimbinguni, likitoa dhabihu za kiroho, sifa za Mungu, Roho Mtakatifu akitenda kazi miongoni mwao, akizitambua dhambi na kutangaza mambo yaliyo mabaya miongoni mwao, akiyanyoosha na kuyalainisha yawe usawa. Kwa sababu nini? Daima Uweponi mwa Mungu kuna ile Dhabihu iliyotapakaa damu.
Sasa kumbukeni, tuliyapitia hayo asubuhi ya leo. Hukuokolewa kwa Damu, unahifadhiwa uliyeokolewa kwa njia ya Damu. Bali uliokolewa kwa njia ya neema, kupitia imani, ukiiamini Hiyo. Mungu alibisha hodi moyoni mwako kwa sababu alikuchagua tangu zamani. Uliinua macho yako juu na ukaiamini, ukaikubali. Sasa Damu inafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zako. Kumbukeni, nilisema, “Mungu hamhukumu mwenye dhambi kwa ajili ya kufanya dhambi.” Yeye kwanza ni mwenye dhambi. Yeye humhukumu Mkristo kwa kutenda dhambi. Halafu basi kwa sababu amemhukumu, Kristo alichukua hukumu yetu. Kwa hiyo hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, wanaoenenda si kwa kuufuata mwili, bali kwa jinsi ya Roho. Na kama ukifanya jambo lo lote baya, si kwa makusudi. Hutendi dhambi makusudi. Mtu anayetenda dhambi makusudi, anatoka na kutenda dhambi makusudi, bado hajaingia katika huo Mwili. Lakini mara mtu anapoingia mle, amekufa, na uhai wake umefichwa katika Mungu, kwa njia ya Kristo, akatiwa muhuri nakw anjia ya Roho Mtakatifu, na Ibilisi hata hawezi kumpata, yuko kule nyuma kabisa. Itambidi atoke mle kabla Ibilisi hajampata. “Kwa maana umekufa!”
----
Na kumbukeni jambo hilo, tulilipitia tu hivi punde. Waefeso, sura ya 1, aya ya 10.
Yaani kuleta madaraka ya wakati mkamilifu...
Sasa, tulijifunza kwamba madaraka ya wakati mkamilifu ni kungojea nini? Utimilifu wa wakati wote, wakati ambapo dhambi itakoma, wakati ambapo mauti yatakoma, wakati ambapo magonjwa yatakoma, wakati ambapo dhambi itakoma, wakati ambapo upotovu wote (mambo hayo mapotovu, ambayo ibilisi ameyapotosa), yatakwisha, wakati majira yenyewe yatakwisha. Angalia.
Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumuisha... vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia; Naam, katika yeye huyo:“Kuvijumuisha vitu vyote kwa njia ya Kristo.” Kama nilivyosema asubuhi ya leo, vito vyote vidogo tunavyoona, mambo haya madogo yaliyo muhimu, unaweza kuyafafanua katika Mwanzo, unaweza kuyafafanua katika Kutoka, unaweza kuyafafanua katika Mambo ya Walawi, na kuyaleta kote, na katika Ufunuo yataishia kuwa Yesu. Mchukue Yusufu, mchukue Ibrahimu, mchukue Isaka, mchukue Yakobo, mchukue Daudi, kichukue chochote kimoja cha vito hivyo, hao watu wa Mungu, na uone kama humwoni Yesu Kristo akionyeshwa katika kila mmoja wao. “Apate kuvijumuisha vitu vyote katika Mtu moja, Kristo Yesu.”
Sasa, mbele kidogo sasa, sasa hiyo aya ya 11.
Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi,...
Loo, “urithi.” Mtu fulani hana budi kukuachia kitu fulani, upate kukirithi. Je, hilo ni kweli? Urithi! Tuna urithi gani? Mimi nilikuwa na urithi gani? Sikuwa na wowote. Lakini Mungu aliniachia urithi wakati alipoliweka jina langu katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.Loo, unasema, “Sasa, ngoja kidogo, ndugu, Yesu alifanya hivyo wakati alipokufa kwa ajili yako.” La, Yeye kamwe hakufanya hivyo. Yesu alikuja kununua huo urithi kwa ajili yangu. Soma ile inayofuata... inayofuata papo hapo.
Na ndani yake sisi nasi tulifanywa kama... tumefanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake;Mungu, kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kama tulivyolieleza kote katika somo, ninyi watu, jinsi tulivyoona kwamba Mungu aliishi peke Yake, jinsi ambavyo katika Yeye mlikuwemo na upendo. Ndani Yake mlikuwwemo kuwa Mungu; hakukuweko na kitu cha kumwabudu. Ndani Yake mlikuwemo kuwa Baba; kulikuwako... Yeye alikuwa peke Yake. Ndani Yake mlikuwemo kuwa Mwokozi; hakukuwa na kilichopotea. Ndani Yake mlikuwemo kuwa Mponyaji. Hizo ni sifa Zake. Hapakuwepo na kitu hapo. Kwa hiyo Yeye Mwenyewe, shauri la mapenzi Yake Mwenyewe lilitoa mambo haya, ili kwamba katika Mtu huyu mmoja, Kristo Yesu, avikusanye vitu vyote pamoja tena. Loo! “Jicho halijaona, sikio halija...” Si ajabu ni jambo la ajabu!
Angalia, “ametuchagua tangu awali tupate huu urithi.” Kama mimi nina haki ya kurithi kitu fulani, kama Mungu anabisha hodi moyoni mwangu na kusema, “William Branham, nilikuita muda mrefu uliopita, kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kuihubiri Injili,” ninao urithi, urithi wa Uzima wa Milele. Sasa, Mungu alimtuma Yesu kuufanya urithi huo kuwa halisi kwangu, kwa sababu hakuna kitu ningeweza kufanya ili kuurithi. Uikuwa mtupu, ulikuwa halali, nisingewe kufanya lolote. Lakini katika utimilifu wa wakati Mungu alimtuma, katika wakati Wake Mwenyewe uliofaa, Yesu aliye Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Damu Yake ilimwagika kusudi nipate kwenda kwenye urithi wangu. Kuwa nini, urithi gani? Uana, kuwa mwana wa Mungu.
Na sasa Hii linaweza kuwasonga roho nusura mfe. Lakini je! Mlijua ya kwamba watu ambao ni wana wa Mungu ni miungu wadogo? Ni wangapi waliopata kujua jambo hilo? Ni wangapi wanaojua ya kwamba Yesu alisema hivyo? Biblia, Yesu alisema, “Je! Torati yenu haikusema, yenyewe, ya kwamba ninyi ni 'miungu'? Na kama mkiwaita miungu...” Ambapo, Mungu alisema katika Mwanzo 2 kwamba wao walikuwa ni miungu, kwa sababu walikuwa hivyo, walikuwa na utawala mkamilifu juu ya milki ya ulimwengu. Alimpa utawala juu ya vitu vyote. Naye akapoteza uungu wake, akapoteza uwana wake, akapoteza milki yake, na Shetani akaichukua. Lakini, ndugu, tunangojea madhihirisho ya wana wa Mungu watakaorudi na kuimiliki tena. Tunangojea utimilifu wa wakati, wakati piramidi itakapofikia kileleni, wakati utimilifu wa wana wa Mungu utadhihirishwa, wakati nguvu za Mungu zitakapotembea (haleluya) na kumnyang'anya Shetani kila nguvu aliyo nayo. Naam, bwana, ni mali yake.
Yeye ni Logos iliyotoka kwa Mungu, hiyo ni kweli, iliyokuwa Mwana wa Mungu. Kisha akamfanya mtu mungu aliye mdogo. Naye akasema, “Kama waliwaita hao waliojiliwa na Neno la Mungu liliwajia, hao manabii, kama waliwaita 'miungu' hao waliojiliwa na Neno la Mungu ...” Na Mungu alisema hivyo, Yeye Mwenyewe, kwamba walikuwa miungu. Yeye alimwambia Musa, “Nilikufanya wewe mungu, na kumfanya Haruni nabii wako.” Amina. Whiu! Huenda nikafanya kama kichaa wa kidini, bali sivyo nilivyo. Loo, wakati macho yako yanapoweza kufunguka na kuona mambo hayo. Vema. Yeye alimfanya mwanadamu mungu, mungu katika milki yake. Na milki yake inaenea kutoka bahari hata bahari, kutoka pwani hadi pwani; yeye ana mamlaka juu yake.
Na wakati Yesu alipokuja, akiwa ndiye yule Mungu Mmoja asiye na dhambi, Yeye alilithibitisha jambo hilo. Pepo zilipovuma, Yeye alisema, “Amani, tulia!” Amina. Na wakati mti, Yeye alisema, “Mtu asile kutoka kwako.”
“Amin, nawaambia, ninyi mlio miungu midogo, mkiuambia mlima huu, 'ng'oka,' na msitilie shaka mioyoni mwenu, bali mwamini ya kwamba yale mliyosema yatatimia, mnaweza kupata yale mliyosema.”Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #4.