Kudhihirika mwana wa Mungu.
<< uliopita
ijayo >>
Kuasili #2.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2.Tunaamini? Sijui ningefanya nini kama sikuwa Mkristo. Nisingetaka kuishi zaidi. Hakuna kitu cha kuishia, ila kuwafanya wengine waokolewe, ndilo jambo bora sana nijualo.
Sasa, usiku wa leo tunataka tu kuanzisha msingi mdogo wa somo letu lililopita. Nami nitajaribu kusoma, kwa sababu, ile sura nzima, kama nataweza usiku wa leo. Kwa hiyo Jumapili asubuhi itanibidi labda kuingiza ndani Jumapili asubuhi na usiku, kama hilo ni sawa, kujaribu kupata katika taratibu hii ya yale ninayotaka kanisa lione. Loo, ni jambo tukufu sana kuona mahali pako! Na hakuna mtu anayeweza kufanya jambo lo lote isipokuwa ujue vizuri unalofanya.Vipi kama ulikuwa unakwenda kuwa... kufanyiwa upasuaji, na kulikuwako na daktari kijana ambaye ndiyo kwanza atoke shuleni ambaye ange... hakuwahi kufanyiwa upasuaji hapo awali. Hata hivyo, yeye alikuwa kijana na mwenye sura nzuri, na nywele zake zimechanwa zikalazwa maridadi kisasa, naye alikuwa amevalia vizuri sana, kavalia kimaridadi sana, na kila kitu. Naye akasema, “Nimenoa visu, na nimechemsha vyombo vyote na kadhalika.” Lakini ungekuwa na wasiwasi kidogo juu ya jambo hilo. Afadhali nipate daktari mzee ambaye alikuwa amefanya upasuaji huo mara nyingi huko nyuma, kabla sijakubali kukatwa. Ni- nataka kumjua mtu fulani si yule aliyetoka shuleni hivi karibuni, nataka mtu aliye na ujuzi fulani. Na Yule aliye na ujuzi kuliko wote ninayemjua, kumwita usiku wa leo, ni Roho Mtakatifu. Yeye ni Tabibu mkuu na Mwalimu mkuu wa Mungu.
-----
Sasa, usiku wa leo, Maandiko yetu yanagawanya Kitabu cha Waefeso, ndicho Kitabu cha Yoshua cha Agano Jipya. Kinawagawia na kuwaweka katika utaratibu “wale walioshinda.” Sasa, ni msingi tu kwa dakika chache, kupata mahali kabla hatujaanza kusoma, tukianzia na ile aya ya 3. Sasa, tunaona Jumapili iliyopita usiku ya kwamba... Mungu katika Agano la Kale alikuwa amewaahidi Israeli nchi ya pumziko, kwa sababu walikuwa wamekuwa wasafiri na wenye kutangatanga. Nao walikuwa katika nchi ambayo si yao, na Mungu alikuwa ameahidi kupitia kwa Ibrahimu ya kwamba angeishi ugenini, uzao wake ungekaa ugenini kwa muda wa miaka mia nne kati ya watu wa wageni, na kutendwa mabaya, lakini kwa mkono wenye nguvu Yeye angewatoa huko akawaingize katika nchi nzuri iliyojaa maziwa na asali.Na, sasa, wakati wa ile ahadi ulipokaribia, Mungu alimwinua mtu fulani awapeleke kwenye nchi hiyo. Ni wangapi darasani usiku wa leo huyo alikuwa nani... wanaojua huyo alikuwa ni nani? Musa. Angalia, mfano halisi kabisa wa Yule wetu aliyetolewa kutuleta kwenye Nchi ya ahadi, Kristo. Sasa tunayo ahadi, maana ahadi yetu ni Pumziko la kiroho, ambapo, lao lilikuwa ni pumziko la kimwili. Na kwa hiyo wao walikuwa wakija kwenye nchi ambayo wangeweza kusema, “Hii ndiyo nchi yetu, sisi si wenye kutangatanga tena tumetulia, hii ni nchi yetu, na hapa tuna pumziko. Tutapanda mahindi yetu, mashamba yetu ya mizabibu, na tutakula kutoka kwenye mashamba yetu ya mizabibu. Na kisha tutakapoaga dunia, tutawaachia watoto wetu.”
-----
Lakini sasa, tusonge mbele. Basi je! Ulimwona Musa, yule mtenda miujiza mashuhuri aliyewaleta Israeli kupitia ile nchi, na kuwaleta hata kwenye nchi ya ahadi, lakini yeye hakuwapa urithi wao? Yeye hakuwapa urithi wao; aliwaongoza hadi kwenye ile nchi, lakini Yoshua ndiye aliyewagawia hao watu ile nchi. Sivyo? Naye Kristo alilileta kanisa kufikia mahali ambapo waliandaliwa milki yao, walipewa, ikisalia tu kuvuka Yordani, bali Roho Mtakatifu Ndiye anayeliweka kanisa katika utaratibu. Yoshua wa leo hii analiweka kanisa katika utaratibu wake, akimpa kila mmoja, karama, mahali, cheo. Naye ndiye Sauti ya Mungu ikinena kupitia kwa yule mtu wa ndani ambaye Kristo amemwokoa, Roho Mtakatifu. Sasa mnafahamu umbali huo? Sasa tunaingia katika Kitabu cha Waefeso. Sasa, vivyo hivyo, Yeye anaweka kanisa mahali pao. Sasa, Yoshua aliwaweka katika nchi ya kawaida. Sasa Roho Mtakatifu analiweka kanisa, mahali pake, katika nchi, ili kwamba wao, katika mahali ambapo ni pao, urithi wao.Sasa, jambo la kwanza analoanza nalo hapa, anaandika barua yake, “Paulo.” Ambalo, tutaona baada ya kitambo kidogo kwamba fumbo hili lote lilifunuliwa kwake, si katika seminari, si kwa njia ya mwanatheolojia ye yote, bali ilikuwa ni ufunuo wa Kiungu wa Roho Mtakatifu ambao Mungu alimpa Paulo. Tukijua kwamba fumbo la Mungu, yeye alisema, ambalo liliyokuwa limefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, lilikuwa limefunuliwa kwake na Roho Mtakatifu. Na Roho Mtakatifu miongoni mwa watu alikuwa akimweka kila mmoja katika utaratibu, akiliweka kanisa mahali pake.
-----
Lakini mtu aliye nje ya Kanaani hajui kitu juu yake, angali anatangatanga. Si kusema ya kwamba yeye si mtu mzuri, sisemi hivyo. Sisemi mtu aliye Misri si mtu mzuri, bali yeye, hadi awe ameingia kwenye milki hii. Na hiyo milki, ambayo, ile ahadi iliyotolewa kwa kanisa si nchi ya kawaida, bali ni nchi ya kiroho, kwa kuwa sisi ni ukuhani wa kifalme, taifa takatifu. Ndipo katika ukuhani huu wa kifalme, taifa takatifu, watu wa kipekee, walioitwa watoke, waliochaguliwa, wakatengwa, waliotengwa, ndipo ulimwengu wote umekufa upande wa nje. Nasi tunaongozwa na Roho. Wana na binti za Mungu wanaongozwa na Roho wa Mungu; si na mwanadamu, bali kwa Roho.-----
Kwa matarajio ya dhati, viumbe vyote vinatazamia huo udhihirisho. Unaona, huo udhihirisho! Udhihirisho ni nini? Kufanya wajulikane!
Ulimwengu mzima. Waislamu kule, wanakutazamia. Pande zote, kila mahali, wanakutazamia. “Wako hawa wako wapi?” Tumekuwa na ninii... Tumekuwa na upepo wenye nguvu unaovuma ukienda kasi, tumekuwa na ngurumo na umeme, tumekuwa na mafuta na damu, tumekuwa na mambo ya kila namna; lakini tulishindwa kuisikia ile Sauti ndogo ya utulivu iliyomvutia yule nabii, ambaye alijifunika joho na kutoka, kasema, “Mimi hapa, Bwana.” Unaona?-----
Tunapokuwa katika Kristo, tuna baraka ya kiroho. Nje ya Kristo, tuna mihemuko. Katika Kristo tuna baraka halisi. Si kuamini kwa kujifanya, si kujisingizia, si kuigiza. Lakini mradi tu unajaribu kusema kwamba uko katika Nchi ya ahadi, nawe hauko, dhambi zako zitakufichua. Na, muda si muda unajua, utajikuta mwenyewe unatatanika na-na kadhalika, kama tunavyokuita ulimwenguni, umevurugikiwa. Utaona ya kwamba huna kile unachozungumzia. Lakini unapokuwa katika Kristo Yesu, Yeye amekuahidi amani ya Kimbinguni, baraka za Kimbinguni, Roho wa Kimbinguni, kila kitu ni chako. Wewe uko katika Nchi ya ahadi na umemiliki kabisa kila kitu. Amina. Linapendeza iliyoje! Loo, hebu na tujisome.
Kama vile alivyotuchagua...
Sasa, hapa ndipo kanisa linapojikwaa vibaya sana.
Kama vile alivyotuchagua katika yeye...
(Katika Nani?) Kristo.-----
Sasa, hivi majuzi usiku, ama asubuhi ya hivi majuzi, kwenye saa moja, wakati Roho Mtakatifu, kwa wema Wake na neema Yake, alinitwaa kutoka kwenye mwili huu, naamini, naamini. Ndiyo au la, sisemi mimi, na nikaingia katika nchi hiyo na kuwaona watu hao, nao wote walikuwa vijana. Nami nikawaona watu wenye sura nzuri sana niliopata kuwaona maishani mwangu. Naye akaniambia, “Baadhi yao walikuwa na umri wa miaka tisini. Hao ni waongofu wako. Si ajabu wanapaza sauti, 'Ndugu yangu! Ndugu yangu!'”
[Unaona: Kifo. Ni nini basi?]-----
Tulipataje hili? Tunalijuaje? Mungu, kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, alituchagua tangu zamani! Akina nani? Wale walio katika Nchi ya ahadi.
...alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo... sawasawa na uradhi wa mapenzi yake,
Na usifiwe utukufu Wake...
Ili tupate kumsifu Yeye kama alivyosema. Hivyo ndivyo alivyokuwa, Mungu. Tunataka kumsifu Yeye.
...usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametufanyia tukubalike katika huyo mpendwa.
Katika Kristo tumekubalika.
Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa d-a-m-b-i....Inanibidi kurudi kwenye kufanywa wana wenye mamlaka, lakini ninataka kukomea kwenye “dhambi” hapa kwa dakika moja. “Dhambi,” mliona hilo? Unajua Mungu hamhukumu mwenye dhambi kwa kutenda dhambi? Yeye humhukumu kwa kule kuwa mwenye dhambi. Kama mwenye dhambi akivuta sigara, Yeye hamhukumu kwa jambo hilo; yeye ni mwenye dhambi, hata hivyo. Unaona? Unaona? Yeye hana dhambi zozote, mwenye dhambi hana. Yeye ni mwenye dhambi tu, unaona, hana dhambi zozote. Bali ninyi mna dhambi, ninyi ambao ni Wakristo. Unaona hapa anazungumza na Kanisa. Kulinyosha. Unaona? Unaona? “Msamaha wa dhambi,” d-h-a-m-b-i. Tunafanya dhambi. Lakini mwenye dhambi ni mwenye dhambi tu, Mungu hamsamehi.
-----
Kwa hiyo “dhambi,” d-h-a-m-b-i, tuna msamaha wa dhambi zetu kwa (nini?) Damu Yake, Damu ya thamani.
...sawasawa wingi wa...
Tunaisahaunamna gani? Kwa sababu tunastahili, tulifanya jambo fulani kusudi dhambi zetu zisamehewe? Ati nini Yake?
...neema;
Loo, jamani! Sina kitu mikononi mwangu ninacholeta, Bwana. Hakuna kitu ningeweza kufanya, hakuna kitu ningeweza kufanya. Tazama! Yeye alitangulia kunichagua, aliniita, alinichagua. Kamwe mimi sikumchagua Yeye. Yeye alinichagua, alikuchagua wewe, alituchagua sisi sote. Sisi hatukumchagua. Yesu alisema, “Ninyi hamkunichagua Mimi, niliwachagua ninyi.” Yeye alisema, “Hakuna mtu awezaye kuja Kwangu asipovutwa na Baba Yangu kwanza, na wote alionipa Baba watakuja Kwangu. Na hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa mwana wa upotevu, kutimiza Maandiko.” Mnaona? Kasema, “Lakini wote alionipa Baba watakuja Kwangu.”-----
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua ili...
Neno “ili” linamaanisha nini, neno “ili”? Linamaanisha kitu fulani tunachoendea, ili. “Naenda nifike kisimani. Naenda nifikie kile kiti.” Humes, unalipata hilo? “Naenda nifikie kwenye lile dawati.” Sasa, Yeye alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi Yake Mwenyewe,
Ni kiasi gani cha uradhi? Ulikuwa uradhi wa nani, wema wa nani? Wake Mwenyewe. Uradhi Wake wa Mapenzi Yake Mwenyewe!Sasa, “kufanywa wana wenye mamlaka” ni nini? Sasa hebu nipate hili sasa, sijui kama... Sitakuwa na wakati wa kumaliza hili, bali nitaligusia. Ndipo kama kuna swali, mnaweza kuniuliza baadaye kidogo wakati fulani katika ujumbe, kitu fulani. Sikilizeni. Kuasili kwako kuwa mwana mwenye mamlaka si kuzaliwa kwako. Kufanywa kwako mwana mwenye mamlaka ni kuwekwa mahali pako. Wakati ulipozaliwa mara ya pili, Yohana 1:17, naamini, tunapozaliwa kwa Roho wa Mungu, sisi ni wana wa Mungu. Lakini tulichaguliwa tangu zamani. Sasa hapa ndipo ninapojaribu kuwafikisha, kwa ajili ya wana hawa wa siku za mwisho, mnaona. Ku... Unaona? Tulichaguliwa tangu zamani ku- (ili) tufanywe wana wenye mamlaka.
Sasa, sasa hebu tuendelee. Sasa, jambo hili ndilo linalowaudhi Wapentekoste kidogo. Wao wanasema, “Nimezaliwa mara ya pili! Bwana asifiwe, nina Roho Mtakatifu!” Sawa. Wewe ni mwana wa Mungu. Hiyo ni kweli. Lakini hata hivyo hilo silo ninalozungumzia. Unaona, ulichaguliwa tangu zamani upate kufanywa mwana mwenye mamlaka. Kufanywa wana wenye mamlaka, ni kumweka mwana mahali pake.
Ni wangapi wanaojua sheria za kufanywa mwana mwenye mamlaka katika Agano la Kale? Bila shaka, mmeangalia. Mwana alizaliwa. Naamini nilihubiri katika mahubiri fulani. Ni upi huo, Gene, unaukumbuka? Uko kwenye kanda. Loo, ilikuwa nini? Nimeigusia. Loo, naam, nimeupata, Msikieni Yeye. Msikieni Yeye; kufanywa wana wenye mamlaka kwa watoto. Sasa, katika Agano la Kale, wakati mtoto alipozaliwa katika familia, yeye alikuwa mtoto alipozaliwa, kwa sababu alizaliwa na wazazi wake, yeye alikuwa ndiye mwana wa kiume wa hiyo familia na mrithi wa vitu vyote. Sasa, lakini huyu mwana alilelewa na waalimu. Wagalatia, sura ya 5, aya ya 17 hadi ya 25. Vema. Yeye alilelewa na waalimu, walezi, waalimu.
-----
Kuingia katika Nchi hii ya ahadi. Tunaingiaje? Tumechaguliwa tangu zamani kuiingia hiyo. Kanisa, kwa kujua kwa Mungu zamani, limechaguliwa tangu zamani (kwa ajili gani?) Kwa ajili ya heshima Yake, kwa neema Yake, kwa utukufu, na ibada na utukufu wa Mungu. Baba, akiwa ameketi kule nyuma mwanzoni, anayeishi peke Yake, hakuna kitu kilichomzunguka, alitaka kitu fulani cha kuabudu, kwa hiyo Yeye alitangulia kulitenga na kulichagua kanisa tangu zamani, na kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, na kuweka majina yao katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, wakati wao ... aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, wapate kuonekana kwa ajili ya utukufu Wake na kwa sifa Zake mwishoni mwa wakati, wakati Yeye atakapovikusanya vitu vyote katika huyo Mtu mmoja, Kristo Yesu. Whiu! Utukufu! Hivyo ndivyo ilivyo. Hiyo ni ninii tu... Nayo ndivyo hiyo papo hapo, ndugu yangu, dada. Uje kamwe ukatoka kwenye Hilo.Mungu, kwa neema Yake ya kuchagua, alikuita. Mungu, kwa neema Yake ya kuchagua, alikutakasa. Mungu, kwa neema Yake ya kuchagua na nguvu Zake, alikubatiza na kukuweka katika nchi hii ya Pumziko. Wale ambao wameingia katika Pumziko hili wameachana na kupotoka kwao. Wamestarehe wenyewe mbali mbali na kazi zao kama vile Mungu alivyostarehe kutoka kwenye kazi Zake. Wana furaha isiyoneneka, na wamejaa utukufu! Mti wa Uzima unachanua ndani yao. Wao wana uvumilivu, upole, wema, saburi iletwayo na imani, imani, upole, unyenyekevu, na kadhalika. Mti wa Uzima unachanua ndani yao kwa sababu tumaini lao limetiwa nanga katika Kristo Yesu, ushahidi wa Roho Mtakatifu ukishuhudia kwa ishara na maajabu vikiwafuata waaminio. “Ishara hizi zitawafuata hao waaminio.” Wanaposonga mbele, wanawaponya wagonjwa, wanafukuza mapepo, wananena kwa lugha, wanaona maono. Wao... Nao wanatembea pamoja na Mungu, wanazungumza na Mungu. Hakuna ibilisi anayeweza kuwatikisa, wao ni imara, wakitafuta... Wakiyasahau hayo mambo yaliyopita, wanakaza mwendo waifikilie ile mede ya mwito mkuu katika Kristo Yesu. Hao hapo. Hao hapo. Hilo ndilo Kanisa.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2.