Waefeso wanafanana na Yoshua.

<< uliopita

ijayo >>

  Kuasili mfululizo.

Kuasili #1.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1.

Sasa, Kitabu cha Waefeso, kama nilivyokuwa nikisema tu, mimi... kwa maoni yangu, ni moja ya Vitabu vikuu sana vya Agano Jipya. Kinatuachia, mahali ambapo Ukalvini unaegemea kwenye tawi moja, na Uarmenia unaegemea kwenye tawi lingine, lakini Kitabu cha Waefeso kinayavuta hayo pamoja na kuliweka Kanisa mahali pake.
Sasa, nimekifananisha na Yoshua. Kama mliona, Israeli waliletwa kutoka Misri, na kuna hatua tatu za safari yao. Hatua moja, ilikuwa ni kuondoka Misri. Hatua iliyofuata, ilikuwa ni jangwani. Na hatua iliyofuata, ilikuwa ni Kanaani.

Sasa, Kanaani haiwakilishi ule wakati wa Utawala wa Miaka Elfu. Inawakilisha tu wakati wa mshindi, kipindi cha kushinda, kwa sababu huko Kanaani waliua na kuchoma moto na kuitwaa miji. Na hakutakuwa na mauti katika ule Utawala wa Miaka Elfu.
Lakini jambo lingine ambalo hilo linafanya, linaleta kuhesabiwa haki kwa imani, baada ya wao kumwamini Musa na kuondoka Misri. Utakaso, kule kufuata chini ya ile Nguzo ya Moto na upatanisho wa yule mwana-kondoo wa dhabihu kule jangwani. Na kisha kuingia katika nchi ambayo ilikuwa imeahidiwa.

Sasa, ni nchi gani iliyoahidiwa mwamini wa Agano Jipya? Ahadi ni Roho Mtakatifu. “Kwa kuwa itakuwa katika siku za mwisho,” Yoeli 2:28, “ya kwamba nitamwaga Roho Yangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri. Na juu ya watumishi Wangu na wajakazi wangu nitawamwaga Roho Wangu, nao watatabiri. Nitaonyesha maajabu mbinguni juu. Na katika nchi, nguzo za moto, na moshi, na mvuke.” Naye Petro alisema, kwenye Siku ya Pentekoste, baada ya kuchukua somo lake na kuhubiri, “Tubuni, kila mmoja wenu, mkabatizwe katika Jina la Yesu Kristo mpate ondoleo,” kuondoa, kusamehe, kuondoa makosa yote ya huko nyuma.

Je mliona, Yoshua, kabla wao hawajavuka Yordani, Yoshua alisema, “Piteni katikati ya kambi mkafue nguo zenu na kila mmoja wenu ajitakase, wala mtu ye yote asimkaribie mkewe, kwa maana mnamo siku tatu mtaona Utukufu wa Mungu.” Unaona? Ni mchakato wa kuwa tayari kuirithi ile ahadi. Sasa, ahadi kwa Israeli, ilikuwa, Mungu alimpa Ibrahimu ahadi ya ile nchi, ya Palestina, na ilikuwa iwe milki yao milele. Nao walipaswa daima kudumu katika nchi hii.
Sasa, wao walipitia hatua tatu, wakija kwenye nchi hii ya ahadi. Sasa angalia, jambo hili limeonyeshwa kwa mfano kamili katika Agano Jipya.
Sasa hili, kama nilivyosema, linapingana na baadhi ya mawazo yenu. Baadhi yenu ninyi Wanazarayo wa thamani, Church of God, na kadhalika, msiruhusu liwaudhi, bali liangalieni tu kwa makini na mwangalie mifano yake. Angalieni na mwone kama kila mahali hapatimiliki kikamilifu kabisa.

Kulikuwako na hatua tatu za ile safari, na kuna hatua tatu za safari hii. Kwa kuwa, tunahesabiwa haki kwa imani, tukimwamini Bwana Yesu Kristo, tukiiacha nchi ya Misri, tukatoka. Na kisha tunatakaswa kwa toleo la Damu Yake, tunaoshwa mbali na dhambi zetu, na tunakuwa wasafiri na wageni, tukikiri kwamba tunaitafuta nchi, mji ujao, ama ahadi.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli jangwani, wageni, hawana mahali pa kupumzika, wakisafiri usiku baada ya usiku, wakiifuata ile Nguzo ya Moto, lakini hatimaye wakafikia ile nchi ya ahadi ambamo walikaa.

Hapo ndipo mwamini anakokuja. Anakuja kwanza kwenye kutambua kwamba yeye ni mwenye dhambi; ndipo anatenganishwa na maji, kuoshwa kwa maji, kwa njia ya Damu, na... ama kuoshwa kwa maji kwa kwa njia ya Neno, ndiyo namaanisha, kumwamini Bwana Yesu Kristo. Ndipo, akiisha kuhesabiwa haki kwa imani, anakuwa mshiriki, na kuwa amani na Mungu, kwa kupitia Kristo, aliyebatizwa katika Jina la Yesu Kristo, kumwingiza safarini. Mnalipata? Kuingia safarini! Ndipo anakuwa mgeni na msafiri. Yeye yuko safarini kuelekea wapi? Ahadi ambayo Mungu aliitoa.

Israeli walikuwa bado hawajaipokea ile ahadi, bali walikuwa kwenye safari yao. Na bila kuinua... Tafadhali eleweni. Hapo ndipo ninyi, Wanazarayo na Pilgrim Holiness, na kadhalika, mlipoangukia. Kwa sababu, Israeli, walipofika mahali pale, Kadeshi-Barnea, wakati wale wapelelezi walipovuka kule na kusema, “Nchi hiyo ni nzuri sana,” lakini baadhi yao walirudi na kusema, “Hatuwezi kuitwaa, kwa sababu miji hiyo ina kuta, na kadhalika.” Lakini Yoshua na Kalebu wakajitokeza, na kusema, “Tunaweza kitwaa bilashaka!” Kwa sababu ya matamshi yao ambayo tayari yameandikwa na kutiwa sahihi, wao waliamini katika kazi mbili za neema, kuhesabiwa haki na kutakaswa, na wasingeweza kuendelea mbele zaidi. Na, sikilizeni, kizazi hicho chote kiliangamia jangwani. Lakini wale wawili walioingia kwenye ile nchi ya ahadi na kuleta ushuhuda ya kwamba ilikuwa ni nchi nzuri, “nasi tulikuwa tunaweza kuitwaa bila shaka, kwa sababu ilikuwa ni ahadi ya Mungu.” Ndipo badala ya watu kusonga mbele, kumpokea Roho Mtakatifu, kunena kwa lugha, kupokea nguvu za Mungu, ubatizo wa Roho Mtakatifu, ishara, maajabu, miujiza, walijisikia ya kwamba lingeyavunja mapokeo yao ya mafundisho. Na ilikuwaje kwa hilo? Waliangamia nchini! Hiyo ni kweli.

Lakini walio waamini, hao akina Kalebu na Yoshua, ambao walikuwa wakiendeea ile ahadi, walisongambele kuingia kweye hiyo nchi, wakaitwaa hiyo nchi, na kukaa katika hiyo nchi, kama milki. Nasi kamwe hatukomei kwenye kuhesabiwa haki, kutakaswa. Hebu tuendelee hadi kwenye ubatizo wa Roho Mtakatifu. Hebu tusiishie kwenye kumwamini Bwana Yesu, kubatizwa. Hebu tusikome kwa sababu Yeye alitusafisha na maisha ya dhambi. Lakini sasa tulisonga mbele kufikia mahali fulani, kufikia ahadi ya ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kwa maana Petro alisema, kwenye Siku ya Pentekoste, “Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa hao walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

Kwa hiyo, Waefeso hapa inatuweka kama Yoshua, mahali petu. Unaona, Yoshua, baada ya kuvuka hiyo nchi, na kuitwaa hiyo nchi, ndipo akaigawanya ile nchi. “Efraimu hapa, Manase hapa, na huyu hapa, Gadi hapa, Benyamini hapa.” Aliigawanya hiyo nchi.
Na tazama! Loo, hili linachoma tu mioyo yetu! Kila mmoja wa hao mama wa Kiebrania, wakizaa hao watoto, alitaja hasa mahali pale, katika utungu wake wa kuzaa, ambapo wao wangewekwa katika hiyo nchi ya ahadi. Loo, ni somo kuu! Laiti tungeliliingilia kindani, jambo ambalo lingechukua masaa kadha wa kadha. Siku moja tutakapomaliza kanisa letu, ningetaka tu kuja na kuchukua mwezi mmoja ama miwili, nikae tu moja kwa moja katika yake. Angalia wakati wao, kila mmoja wa hao akina mama, wakati alipoita kwa sauti, “Efraimu,” wakati alipokuwa katika utungu wa kuzaa, alimweka mahali pake ambapo miguu yake ilikuwa imewekwa kwenye mafuta. Mahali hasa alipokuwa kila moja wao!
Naye Yoshua, bila kujua jambo hili, bali kwa uvuvio, akiongozwa na Roho Mtakatifu, baada ya kuwa katika nchi ya ahadi, alimpa kila mtu ahadi yake, kile hasa Roho Mtakatifu alichoahidi kupitia kule kuzaliwa kule nyuma.

Jinsi ambavyo Mungu amewaweka wengine kanisani, kupitia utungu wa kuzaa! Loo, wanakuwa wa kutisha sana wakati mwingine. Wakati kanisa linapougua chini ya mateso ya ulimwengu wa nje, likimwamini Bwana Yesu, ya kwamba ile ahadi ya Roho Mtakatifu ni halisi tu kwetu kama ilivyokuwa kwa Pentekoste, jinsi wanavyougua na kulia kwa utungu wa kuzaa! Lakini wakati wanapozaliwa, na kuzaliwa mahali pao katika Ufalme wa Mungu, ndipo Roho Mtakatifu ameweka kanisani, wengine mitume, wengine manabii, wengine waalimu, wengine wachungaji, wengine wainjilisti. Ndipo Yeye anawapa mle ndani, kunena kwa lugha, kufasiri lugha, maarifa, hekima, karama za uponyaji, kila aina za miujiza.

Mahali lilipo kanisa... Sasa hili ndilo kusudi langu la kufanya jambo hili. Kanisa daima linajaribu kuchukua kisehemu cha mtu mwingine. Lakini usifanye hivyo. Kamwe huwezi kulima mahindi katika kisehemu cha Efraimu, kama wewe ni Manase. Huna budi kuchukua mahali pako katika Kristo, chukua mahali pako. Loo, linakuwa la kilindi na kukolea tunapoingia hapa, jinsi ambavyo Mungu humweka mmoja kanisani kunena kwa lugha, mwingine... Sasa, tumefundishwa mara nyingi, “inatubidi sote kunena kwa lugha.” Hilo ni kosa. “Sote hatuna budi kufanya hivyo.” La, hatupaswi. Wote hawakufanya jambo lile lile. Kila mmoja alikuwa...

Kila mmoja, ardhi ilitolewa na kugawanywa kwa uvuvio. Na, kila mmoja, ningeweza kuchukua Maandiko na kuwaonyesha jambo hilo kikamilifu, ya kwamba yeye aliwaweka mahali walipopaswa kuwa, mahali pao, jinsi ambavyo hayo makabila hiyo nusu ya makabila yalipaswa kuishi upande ule mwingine wa mto, jinsi ambavyo mama zao walipaza sauti wakisema jambo hilo katika kuzaliwa kwao, na jinsi ambavyo kila mahali palipaswa kuwa.
Na sasa baada ya wewe kuingia, hilo halimaanishi kwamba uko huru na vita. Bado inakubidi kupigania kila inchi ya ardhi unayokanyaga. Kwa hiyo, unaona, Kanaani haikuwakilisha Mbingu kuu, kwa sababu ni vita na shida na mauaji na mapigano, na kadhalika. Lakini iliwakilisha jambo hili, kwamba lazima iwe ni kutembea kukamilifu.

Hapo ndipo kanisa linaposhindwa leo, kwenye kutembea huko. Je! Unajua ya kwamba hata tabia yako mwenyewe inaweza kumtupa mtu mwingine asipate kuponywa? Tabia zenu mbaya, za dhambi zenu ninyi waamini ambazo hazikutubiwa, zinaweza kusababisha kanisa hili lishindwe vibaya. Na kwenye Siku ya Hukumu utawajibika kwa kila sehemu yake. “Loo,” unasema, “sasa, ngoja kidogo, Ndugu Branham.” Vema, hiyo ni Kweli. Wazia jambo hilo!

Yoshua, baada ya kuvuka akaingia katika ile nchi, Mungu alimpa ahadi kwamba... Hebu wazia tu, kupigana vita hivyo vyote bila ya kupoteza mtu, bila hata kupata mkwaruzo, bila kuhitaji kuwa na nesi, ama huduma ya kwanza ama bendeji. Amina. Mungu alisema, “Hiyo nchi ni yenu, nendeni mkapigane.” Wazieni, juu ya kupigana vita, na hakuna Msalaba Mwekundu kokote, hakuna mtu atakayeumia!

Nao wakawaua Waamori na Wahiti, bali hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa miongoni mwao hadi dhambi ikaingia kambini. Na wakati Akani alipotwaa lile vazi la Babeli na ile kabari ya dhahabu, na kuvificha chini ya kambi yake, ndipo kesho yake wakapoteza watu kumi na sita. Yoshua alisema, “Simameni! Simameni! Ngojeni kidogo, kuna kasoro fulani! Kuna kasoro hapa. Tutaitisha siku saba za kufunga. Mungu alitupa ahadi, 'Hakuna kitu kitakachotudhuru.' Adui zetu wataanguka miguuni petu. Na kuna kasoro fulani hapa. Kitu jambo fulani limeenda kombo mahali fulani, maana tuna maiti za watu kumi na sita zilizolala hapa. Wao ni ndugu zetu Waisraeli, nao wamekufa.”

Kwa nini wamekufa, watu wasio na hatia? Kwa sababu mtu mmoja alitoka nje ya mstari. Mnaona ni kwa nini jambo hili linapasa kufundishwa? Kanisa likijiwela sawa, likijiweka sawa na Neno la Mungu, likijiweka sawa na Mungu na kujiweka sawa mmoja kwa mwingine, wakitembea kikamilifu, kwa kiasi, mbele za watu wote, wakimcha Mungu. Kwa sababu mtu mmoja aliiba vazi, na kufanya jambo ambalo hakupaswa kufanya, watu kumi na sita wakauawa! Nafikiri ilikuwa kumi na sita, labda wengi zaidi. Naamini ilikuwa ni watu kumi na sita waliokuwa wamekufa.
Yoshua akapaza sauti, akasema, “Kuna kasoro fulani! Mungu alitoa ahadi, na kuna kasoro.”
Tunapowaleta wagonjwa mbele zetu, nao wanashindwa kuponywa, tunahitaji kuitisha kufunga kwa uchaji, tuitishe kusanyiko. Kuna kasoro mahali fulani. Mungu alitoa ahadi, Mungu hana budi kushikilia ahadi hiyo, Naye ataitekeleza hiyo.

-----
Paulo, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu (waliotakaswa) walioko Efeso, na kwa wanaomwamini Yesu Kristo; (Waefeso 1:1)

Angalia jinsi yeye anavyoandika hili. Hili si kwa wasioamini. Hili ni kwa kanisa. Hili linaagiziwa wale walioitwa, hao waliotakaswa na kuitwa walio katika Kristo Yesu.

Sasa, kama unataka kujua jinsi tunavyoingia katika Kristo Yesu, kama utafungua Wakorintho wa Kwanza 12, ilisema, “Kwa maana kwa Roho mmoja sote tumebatizwa kuwa Mwili mmoja.” Vipi? Kubatizwa kwa nini? Roho Mtakatifu. Si kwa ubatizo wa maji, ninyi watu wa Kanisa la Kristo, bali kwa R-o-h-o mmoja wa herufi kubwa, kwa Roho mmoja. Si kwa kupeana mkono kumoja, kwa barua moja, si kwa kunyunyiziwa kumoja. Bali, “Kwa Roho mmoja sisi sote tumebatizwa kuwa Mwili mmoja,” milki yetu, ile Nchi ambayo Mungu alitupa tupate kuishi ndani yake, Roho Mtakatifu. Kama tu vile alivyowapa Wayahudi Kanaani, Yeye ametupa Roho Mtakatifu. “Kwa Roho mmoja sote tumebatizwa kuwa Mwili mmoja.” Mnalipata?

Sasa, yeye anawazungumzia Wakanaani wa kiroho, Israeli, Israeli wa kiroho ambao wameimiliki ile nchi. Loo, hivi wewe huna furaha kwamba umetoka kwenye vitunguu saumu vya Misri? Hivi hamna furaha kuwa umetoka jangwani? Isitoshe, kumbukeni, iliwabidi kula mana, chakula cha Malaika kilichotoka Mbinguni, mpaka walipovuka wakaingia kwenye hiyo nchi. Nao walipovuka wakaingia kwenye hiyo nchi, hiyo mana ikaacha kuanguka. Walikuwa wamekomaa kabisa wakati huo, nao wakala mahindi ya zamani ya hiyo nchi. Sasa, sasa kwa kuwa ninyi si watoto wachanga tena, sasa kwa kuwa hamtamani maziwa ya akili ya Injili, kwamba si lazima mbembelezwe kitoto, na kupigwapigwa mgongoni, na kushawishiwa kuja kanisani, sasa kwa kuwa ninyi ni Wakristo waliokomaa kikamilifu, mko tayari kula nyama ngumu sasa. “Mko tayari kufikia kitu fulani,” yeye akasema. Mko tayari kufahamu kitu fulani chenye kilindi na kinono. Loo, tutakifikia hicho moja kwa moja. Na, loo, kimefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Yeye alisema, “Sasa kwa kuwa mmefikia jambo hili, ninawaandikia ninyi haya.” Si kwa wale ambao ndiyo kwanza watoke Misri, si kwa wale wangali safarini bado, bali kwa wale walio katika nchi ya ahadi, ambao wamepokea ahadi.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #1.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

  Maandiko Anasema...

Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.

Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.

Yoshua 1:6-7


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.