Ishara.

<< uliopita

ijayo >>

  Kutembea kwa Kikristo mfululizo.

Ishara inayotakiwa ya Yehova.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ishara.

Kutoka 12:12-13.
12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huu, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa wanadamu na wa wanyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu. Lisiwapige pigo to lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.

Sasa ni nini, kwanza, ishara? Ni neno ambalo linatumiwa sana miongoni mwetu watu wanaozungumza Kiingereza, hasa hapa Marekani. Ishara ni... Kwa kweli, kamusi inasema ishara ni dalili, ni dalili ya nauli, gharama iliyolipwa, mwaona, ya kwamba nauli, ama gharama, gharama inayohitajika ambayo imekwisha lipwa. Kama vile nauli kwenye reli ama nauli kwenye basi. Unaondoka unaenda unalipa nauli yako, kisha wanakupa tikiti, na hiyo tikiti haiwezi kutumika kwa cho chote kingine, ila gari la moshi. Na ni ishara, kwa kampuni ya reli, ya kwamba umelipa nauli yako. Ni ishara, wala huwezi kuitumia kwa kitu kingine chochote. Haifanyi kazi kwenye mstari mwingine wowote. Inafanya kazi tu kwenye mstari huo tu. Na ni ishara.

Sasa hapa chini, tunayonena habari zake, ambapo tunaanzia, ni Mungu akiwaambia Israeli, “Damu ya mwana-kondoo ni ishara kwenu.” Mwana-kondoo wa Israeli, aliyechinjwa, alikuwa ndiye ishara inayotakiwa ya Yehova. Haina budi kuwa ni damu. Mungu alifanya ishara na kuwapa Israeli. Na hakuna ishara nyingine itakayofanya kazi, mnaona, haiwezi kutambuliwa.

Kwa ulimwengu, ni furushi la upuuzi. Lakini, kwa Mungu, ndiyo njia pekee. Kitu pekee anachohitaji ni ile Ishara. Haina budi kuwepo. Nawe huwezi kuwa na Ishara mpaka nauli itakapolipwa, basi wewe ni mmiliki wa ile Ishara inayokupa upendeleo wa kupita bure. “Nitakapoiona ile Damu, nitapita juu yenu.” Ni wakati ulioje, huo, ni majaliwa yaliyoje, kujua ya kwamba umebeba, ndani yako, ile Pasi. “Nitakapoiona ile Damu, nitapita juu yenu.” Ndicho kitu pekee ambacho Yeye atatambua. Si kitu kingine chochote kinachoweza kuchukua mahali Pake; hakuna kibadala, hakuna dhehebu, hakuna kitu kingine. Inahitajika Hiyo. Mungu alisema, “Hiyo pekee ndilo nitayoiona.”

Haidhuru walikuwa wenye haki iliyoje, walikuwa wazuri iliyoje, walivyokuwa na elimu nyingi, jinsi walivyovaa, ishara ndiyo kitu pekee. “Nitakapoiona ishara, nitapita juu yenu.” Ile damu ilikuwa ni ishara ya kwamba matakwa ya Yehova yalikuwa yametimizwa, ya kwamba yalikuwa yametimizwa. Ile damu ilisimama kwaajili ya ishara. Ile damu ndiyo iliyokuwa ishara. Mnaona?

Mungu alikuwa amesema ya kwamba, “Siku utakayokula, siku hiyo utakufa.” Na kulikuwako na uhai wa kibadala uliochukuliwa kwa ajili ya uhai wa mwaminio. Mungu, katika rehema, alikubali kibadala cha maisha ya mtu aliyetiwa unajisi. Wakati mtoto Wake alipojitia unajisi kwa dhambi, ya kutokuamini Neno, ndipo Mungu, mwingi wa rehema, akafanya kibadala; na, hiyo ilikuwa, kitu fulani kilipaswa kufa mahali pake. Hakuna kitu kingine kingeweza kufanya kazi.

Hiyo ndiyo sababu matofaa na mapichi ya Kaini, na kadhalika, hayakufanya kazi. Ilibidi iwe ni uhai uliokuwa na damu ndani yake, na uhai huo ulikuwa umeondoka kwenye dhabihu, na sasa ile damu ilikuwa ni ishara ya kwamba agizo la Mungu lilikuwa limetekelezwa. Sasa, Mungu alihitaji nini? Uhai; na damu ilionesha ya kwamba ilibidi kuwe na uhai uliokwisha. Kwa hiyo damu ilikuwa ndiyo ishara ya kwamba uhai ulikuwa umetolewa, ya kwamba kitu fulani kilikuwa kimekufa, mahitaji ya Mungu; ya kwamba uhai ulikuwa umetolewa, na damu ilikuwa imemwagwa. Na damu ilisimama kwa ishara, ya kwamba uhai ulikuwa umeondoka. Uhai wa mnyama ambao Mungu alikuwa ameagiza utolewe, ilikuwa ile damu iliyowakilisha ile ishara.

Mwabudu aliyeamini alitambulishwa pamoja na sadaka yake, kwa ile ishara. Sitaki kuchukua muda mrefu sana katika matamshi haya madogo; bali, ambapo waweza kuchukua ibada nzima kwa moja ya haya, bali nataka kukomea hapa kwa muda mdogo kusisitiza hayo. Mwamini alipaswa kujitambulisha kwa sadaka yake. Mnaona? Kama ni sadaka tu na ilifanyiwa mahali fulani kule nje, aliitoa; bali alipaswa kujitambulisha katika hiyo. Kwa kweli, ilimbidi kuweka mikono yake juu yake, kwanza, kujitambulisha na sadaka yake. Na ndipo damu ikawekwa mahali ambapo angeweza kusimama chini ya damu. Damu haina budi kuwa juu yake. Na hiyo ilikuwa ni ishara ya kwamba alikuwa amejitambulisha mwenyewe, mwenye hatia, na alikuwa amethibitisha ya kwamba kibadala kisicho na hatia kimechukua mahali pake.

Ni picha nzuri jinsi gani! Loo, aliyekombolewa! Mnaona, haki ilikuwa imetimizwa, na matakwa ya haki takatifu ya Mungu yalikuwa yametimizwa. Naye Mungu alisema, “Sasa nahitaji uhai wako,” kisha ule uhai ulikuwa umetenda dhambi. Ndipo kibadala kisicho na hatia kikachukua mahali pake. Naye alikuwa ni mnyama mwenye damu; si tofaa, pichi. Hilo linapaswa kufanya uzao wa nyoka dhahiri sana kwa kila mtu, kwamba ilikuwa ni damu. Na damu hii, ambayo haingeweza kutoka kwenye tunda, ilitoka kwa kibadala kisicho na hatia. Na uhai ulikuwa umetoka, pia, mahali pake, na ile damu ilikuwa ni mfano kwamba mnyama alikuwa amekufa na damu ilikuwa imetoka.

Naye mwabudu akijipaka damu juu ya nafsi yake, alionesha ya kwamba alitambulishwa katika ukombozi, kwa sababu amejitambulisha na ninii... kwenye ile dhabihu, alijiunganisha na ile dhabihu, na damu ilisimama kwa ajili ya ishara. Jinsi- ni ajabu iliyoje! Ni picha iliyoje! Ni mfano mkamilifu wa Kristo, hasa kabisa, mwaminio leo amesimama chini ya Damu iliyomwagika, akitambulishwa na ile Sadaka. Ni kamilifu tu kama linavyoweza kuwa! Na jinsi Kristo, kwa kuwa hakuwa mnyama... Mnaona, yule mnyama alikufa, bali ilikuwa...

Jambo lisilo na hatia sana tulilo nalo, nadhani, lingekuwa, yule mnyama, mwana-kondoo. Wakati Mungu alipotaka kumtambulisha Yesu Kristo, Yeye alimtambulisha kama Mwana-Kondoo. Na wakati alipotaka kujitambulisha Mwenyewe, Yeye alijitambulisha kama ndege, Hua. Na hua ndiye asiye na hatia na msafi kuliko ndege wote, na mwana-kondoo ndiye asiye na hatia na msafi kuliko wanyama wote.

Kwa hiyo mnaona wakati ninii... Yesu alibatizwa na Yohana, na Biblia ilisema, “Naye akaona Roho wa Mungu, kama hua, akishuka juu Yake.” Kwa hiyo kama ingalikuwa... Kama ingalikuwa ni mbwa mwitu, ama kama ingalikuwa mnyama mwingine ye yote, maumbile ya hua yasingeweza kuchanganyikana na maumbile ya mbwa mwitu, wala tabia ya hua haingechanganyikana na mnyama mwingine yeyote ila mwana-kondoo. Nazo hizo tabia mbili zikapatana, ndipo zingekubaliana moja kwa nyingine.

Sasa mnaona kuchaguliwa tangu asili? Alikuwa mwana-kondoo alipokuja pale. Mnaona? Mnaona? Ninii ...Alikuwa mwana-kondoo wakati alipoletwa. Alikuwa ni mwana-kondoo. Alizaliwa mwana-kondoo. Alilelewa, mwana-kondoo. Mnaona? Na, kwa hiyo, huyo ndiye aina pekee ya Roho wa kweli anayeweza kupokea Neno, anayeweza kumpokea Kristo. Zingine zitajaribu, walijaribu kulipata, wakaweka Roho wa Mungu juu ya mbwa mwitu, mnaona, mwenye hasira, mwovu, duni. Hatadumu mle. Roho Mtakatifu huruka mara moja. Hatafanya hivyo.

Vipi kama huyo Hua alikuwa ameshuka, na, badala ya Yeye kuwa Mwana-Kondoo, kungekuwako na mnyama mwingine? Angaliruka upesi na kurudi. Mnaona? Bali alipotaka ile tabia ambayo ingepatana naye, wakawa tu Mmoja. Ndiposa yule Hua akamwongoza yule Mwana-Kondoo, na, tazama, alimwongoza yule Mwana-kondoo hata machinjioni. Sasa, Mwana-Kondoo alikuwa mtiifu kwa Hua. Mnaona? Haidhuru alikoongozwa, alikuwa tayari kwenda.

Nashangaa, leo, Mungu anapotuongoza kwenye maisha ya kujitolea kabisa kwa utumishi Wake, nashangaa iwapo roho zetu wakati mwingine haziasi, hiyo ikionyesha dhahiri ya kwamba, nashangaa iwapo sisi ni wana-kondoo? Mnaona? Mnaona? Mwana-kondoo ni mtiifu. Mwana-kondoo hujitolea kuwa sadaka mwenyewe. Yeye hachukui, hadai vilivyo vyake. Unaweza kumlaza chini na kumkata manyoya. Hicho ndicho kitu pekee alicho nacho. Kamwe haisemi chochote juu yake; hujitolea tu kila kitu alicho nacho. Huyo ni mwana-kondoo. Anatoa kila kitu kwa ninii yake... anatoa kila kitu, mwenyewe na yote aliyo nayo. Na hivyo ndivyo Mkristo halisi alivyo, kama wana... kujitolea wenyewe, hawajali chochote kwa ulimwengu huu, bali wanatoa yote waliyo nayo kwa Mungu.

Na sasa huyu alikuwa ndiye Mwana-Kondoo mkamilifu, Kristo alikuwa hivyo. Kisha kupitia kwa ile iliyomwagika ya mwana-kondoo huyu, yule mwana-kondoo wa kawaida kule Misri, damu ilipakwa, kisha, ilipopakwa iliwakilisha ishara, basi, Damu ya huyu Mwana-Kondoo ingewakilisha nini? Mnaona? Ile Ishara ya kwamba tumekufa kwa nafsi zetu na kutambulishwa na Dhabihu yetu. Mnaona? Ndipo, Mwana-Kondoo na ile Damu na mtu huyo hutambulishwa pamoja, Dhabihu na mwaminio. Mnaona, unatambulishwa maishani mwako, kwa Sadaka yako. Hilo linakufanya jinsi ulivyo.

Ndipo damu ilikuwa ni ishara, ama kitambulisho. Ile damu ilitambulisha ya kwamba mwabuduo alikuwa amemchinja mwana-kondoo, na kumkubali mwana-kondoo, na kujipaka ishara yeye mwenyewe, ya kwamba hakuona haya. Hakujali ni nani aliyeiona. Alitaka kila mtu aione, na iliwekwa mahali ambapo kila mtu anayepita angeweza kuona ishara hiyo. Mnaona, watu wengi wanataka kuwa Wakristo, nao wanataka kufanya hivyo kwa siri kusudi mtu ye yote asipate kujua ya kwamba wao ni Wakristo. Ama, wale wao wanaotembea pamoja nao, wengine wao wanafikiria, “Vema, tazama sasa, na nataka kuwa Mkristo, bali sitaki Fulani ajue hayo.” Mnaona? Vema, sasa, mnaona, huo si Ukristo. Ukristo hauna budi kuonesha Ishara yake, mnaona, hadharani, katika maisha ya hadharani, ofisini, barabarani, wakati kuna shida, cho chote kile, kanisani, kila mahali pengine. Ile Damu ndiyo Ishara, na Ishara haina budi kupakwa, mnaona, au (sivyo) hata agano halitumiki.

Ile damu ilikuwa ni ishara, ama kitambulisho, kumtambulisha mtu huyu kuwa amekombolewa. Sasa, vema, angalia, wao walikuwa, walikuwa wamekombolewa kabla ya jambo lolote kuwahi kutokea. Kwa imani waliipaka hiyo damu. Mnaona, kabla halijatukia kweli, damu ilipakwa kwa imani, wakiamini ya kwamba itatukia. Mnaona? Kabla hiyo hasira ya Mungu kupita nchini, ilibidi damu ipakwe, kwanza. Ilikuwa imechelewa sana baada ya ghadhabu kushuka. Sasa tuna somo pale ambalo tungeweza kweli, labda kulileta kwenye wazo lako, kwa muda kidogo tu. Angalia, kabla halijatukia, kwa maana unakuja wakati ambapo hautaweza kupakwa Damu yo yote.

Mwana-kondoo aliuawa wakati wa jioni, baada ya kuwekwa siku kumi na nne. Na halafu mwanakondoo akauawa na damu ikapakwa wakati wa jioni. Mnalipata? Ile ishara kamwe haikuwepo mpaka wakati wa jioni.

Na huu ndio wakati wa jioni wa wakati tunaoishi. Huu ni wakati wa jioni kwa Kanisa. Huu ni wakati wa jioni kwangu. Huu ni wakati wa jioni wa Ujumbe wangu. Ninakufa. Ninaenda. Ninaondoka, katika wakati wa jioni wa Injili. Nasi tumepitia kwenye kuhesabiwa haki, na kadhalika, lakini huu ndio wakati ambapo Ishara haina budi kupakwa. Niliwaambia Jumapili iliyopita nilikuwa na jambo ninalotaka kuzungumza nanyi; hili ndilo. Wakati ambapo wewe- huwezi tu kucheza Nalo. Haina budi kufanywa. Kama litatendeka, halina budi kufanywa sasa. Kwa sababu, tunaweza kuona ya kwamba hasira iko karibu kupita nchini, na kila kitu kutoka chini ya hiyo Ishara kitaangamia. Ile Damu, inakutambulisha.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ishara.



Kutembea kwa Kikristo mfululizo.
Itaendelea kwenye ukurasa unaofuata.
(Ubatizo wa Maji.)


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

1 Yohana 2:2


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Chapter 9
- The Third Pull

(PDF Kiingereza)

Kabla...

Baada ya...

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.