Chujio la mtu mwenye busara.

<< uliopita

ijayo >>

  Kutembea kwa Kikristo mfululizo.

Chujio la ulimwengu wa kidini.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Chujio la mtu mwenye busara.

Hesabu 19:9,
Na mtu aliye msafi atayakusanya majivu ya huyo ndama, na kuyaweka nje ya marago mahali safi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya kusanyiko... (angalia sasa) kwa ajili ya kusanyiko la wana wa Israeli kwa ajili ya maji ya kutenganisha: ni utakaso wa dhambi.

Somo ambalo ninatumia kwa ajili ya usiku wa leo ni: Chujio la Mtu Mwenye Busara. Hilo linasikika ni la kimapinduzi kwa somo, kwa mhudumu ambaye anapinga sana kuvuta sigara, angechukua somo kama hilo, Chujio la Mtu Mwenye Busara. Ilitimia, ya kwamba, hivi majuzi asubuhi nilipokuwa nimeenda kuwinda kindi.

Kama ninyi watu huko nje kwenye- huko nje kwenye redio, hewani, ama kwenye wimbi la simu, mngeweza kuona sura ya kusanyiko hili wakati nilipotangaza somo langu, mngeliweza kutoa kicheko kutokana na hilo. Chujio la Mtu Mwenye Busara.

Vema, yote yalitokea ambapo Malaika wa Bwana walinitokea asubuhi moja, na hao kindi walinena wakawa. Ninyi nyote mnakumbuka wakati jambo hilo lilipotukia. Na, pia, kwenye kilele cha kilima nilichokuwa nimesimama, ndipo ambapo... kabla tu ya kuhubiri Nyakati Saba za Kanisa, nikienda kuwinda asubuhi moja kabla ya mapambazuko. Pale walisimama... Nilifikiri jua lilikuwa linachomoza, yapata saa nne asubuhi. Jambo lisilo la kawaida; Niliona Nuru hiyo, nami nikageuka, na pale palisimama Vinara vya Taa Saba vya Dhahabu vikisimama pale juu ya kilima, na kama upinde wa mvua ulikuwa ukija kupitia kwenye mabomba na kulisha.

Mara baada ya hayo, Bwana Yesu alitutokea. Na papo hapo nikasikia Sauti iliyosema, “Yehova wa Agano la Kale ni Yesu wa lile Jipya.” Naye alikuwa hapo, baada ya kitambo kidogo, akafunuliwa baada ya vile Vinara vya Taa Saba vya Dhahabu. Basi angalia jambo hilo. Ni wangapi wanaolikumbuka somo hilo? Nililiandika nyuma ya-la sanduku la-la magurudumu niliyokuwa nayo mfukoni mwangu. “Yehova wa Agano la Kale ni Yesu wa lile Jipya.” Mungu Mbinguni anajua ya kwamba hilo lilikuwa ni kweli.

----
Nilikuwa nimesoma katika Kitabu cha... cha Danieli, ambapo alimjia “Mzee wa Siku, Ambaye nywele Zake zilikuwa nyeupe kama sufu.” Ndipo nikamwona yule Mzee wa Siku. Yeye alikuwa ni yule Mzee wa Siku, yeye yule jana, leo, na hata milele. Unaona, ilikuwa ni mfano, wakati huo. Kwa nini sufu nyeupe? Na halafu mimi... Roho Mtakatifu alionekana akinena nami juu ya picha niliyoona wakati mmoja, ya hakimu wa kale. Ndipo nikaenda kwenye historia; Nilirudi katika historia ya Biblia na yote, kujua. Nao mahakimu wa kale, kama vile kuhani mkuu katika Israeli, ilimbidi kuwa na hizo nywele nyeupe, nywele na ndevu zenye mvi, kwa sababu zile nyeupe juu yake zilionyesha kwamba yeye alikuwa ndiye mamlaka kuu ya mahakimu katika Israeli.

Na hata katika siku hizi, na hadi miaka mia chache iliyopita, labda miaka mia kadha iliyopita, ama labda si hivyo, baadaye kuliko hapo. Majaji wote wa Kiingereza, haidhuru walikuwa ni vijana vipi au walikuwa na umri gani, walipoingia kwa ajili ya hukumu, walivaa wigi nyeupe; na kuonyesha ya kwamba hakuna mamlaka mengine, katika ufalme huo, juu ya neno lao. Neno lao ndilo la mwisho la huo ufalme. Kile wanachosema, ni hicho tu. Na sasa, basi, niliona jambo hilo. Huyo hapo alikuwa amesimama pale, bado ni Kijana, lakini amevaa wigi nyeupe. Yeye alikuwa ndiye Mamlaka yote, kamilifu. Yeye alikuwa Neno. Naye anafanya hivyo, amevaa wigi nyeupe.

Halafu, baadaye tulipomaliza, na mahubiri, na tukaenda magharibi, na wakati Malaika wa Bwana walipojitokeza kule nje kwa ajili ya ile Mihuri Saba, nayo ikaenda hewani (ambayo tuna picha yake hapa, na kila mahali nchini), huyo hapo alikuwa amesimama pale, angali amevalia wig pamoja na mamlaka hayo makuu. Yeye ni Kichwa cha Kanisa. Yeye ni Kichwa cha Mwili. Hakuna kitu kama Yeye, mahali popote. “Yeye aliumba vitu vyote kwa nafsi Yake. Yeye aliumba vitu vyote kwa ajili Yake, na pasipo Yeye hakukuwa na kitu kilichoumbwa.” “Yeye ana mamlaka yote Mbinguni na duniani,” na kila kitu ni mali Yake. “Na katika Yeye unakaa utimilifu wa Uungu kwa jinsi ya mwili.” “Naye Neno alikuwa Mungu, naye amefanyika mwili miongoni mwetu.” Naye alikuwa Ndiye aliyefunua siri yote ya mpango wote wa wokovu, ambao manabii wote na watu wenye hekima walikuwa wamenena habari zake. Yeye pekee ndiye aliyekuwa na wigi na mamlaka kuu.

Sasa, nilikuwa nimesimama, huko juu kilimani asubuhi nyingine, ilionekana kana kwamba kulikuwa na kindi waliokuwa wakikata kule juu. Nami nikaanza kuketi. Nami nimekuwa tu pale kwa muda mfupi, wakati, vichaka vilipigwa na mimi, na jamaa fulani mkubwa sana mwenye namna ya bunduki yenye mitutu miwili akaja akitembea vichakani kule, na kama kwamba alinitisha kiasi cha kufa. Nikaenda kule, nikainama chini; Niliogopa kusogea, nilihofu angenipiga risasi. Na vichaka vikitembea, kwa hiyo nilikaa kimya kabisa.

Kindi akaanza kupanda juu ya kilima, naye akafyatua risasi kwa mitutu yake mwili. Na kwa hiyo akamkosa, na kwa hiyo kindi akashuka juu ya kilima. Nikawaza, “Sasa nitaondoka; kelele yote hiyo inatoa mwangi. Alikuwa na bunduki yake ikiwa haina risasi.”

Nami nikaanza kushuka kilimani, na jamaa huyo akapiga risasi moja kwa moja mbele yangu. Ilinigeuza nyuma namna hii. Nami nikaanza kuja hapa, kushuka kwenda upande mwingine, na bunduki ya ishirini na mbili ikaanza kupiga risasi, na risasi zikivuma juu yangu. Nikasema, “Aisee, niko mahali pabaya sana.”

Kwa hiyo nikageuka nikaenda karibu na mto. Nami nikawaza, “Nitashuka niende hapa chini na kujificha mpaka watakapomaliza, kusudi niweze kutoka.” Na nilipokuwa nikishuka chini, ilitokea kuvuta... Usikivu wangu ulivutwa kuangalia upande wangu wa kulia. Na, kama nilivyofanya, kulikuwako na pakiti tupu ya sigara ambapo mmoja wao alikuwa ameitupa chini, katika mbio zote za... wakati kindi walipokuwa wakipita vichakani.

Niliitazama hapo chini. Sikuikokota, maana sipendi harufu ya vitu hivyo, kwa kuanzia. Nami nikaangalia kule chini, na ni kampuni fulani ya tumbaku ambayo nadhani sipaswi kutaja jina lao, bali mtajua. Ilisema pale, “Chujio la mtu mwenye busara na ladha ya mtu anayevuta sigara.” Nikaangalia kitu hicho, na nikawaza, “Chujio la mtu mwenye busara?” Nikawaza, “Kama mtu huyo angeweza kuwazia hata kidogo, asingevuta sigara hata kidogo. Ingewezaje kuwa 'chujio la mtu mwenye busara'? Mtu mwenye busara hangevuta sigara hata kidogo.” Vema.

----
Nilitazama kitu hicho, na nikawaza, “Ni kitu kama madhehebu ya siku hizi, makanisa tuliyo nayo.” Kila mmoja wao ana chujio lake; wana aina yao ya chujio. Yanaachilia tu kile yanachotaka kiingia, na kile kisichoingia; yale yanayoyachuja kuingia na yanayochuja yasiingie , kwa chujio la aina yao yenyewe. Yanaacha tu kiasi fulani cha ulimwengu kuingia kuwaridhisha wasioamini walio mle ndani. Yatawaingiza ndani haidhuru wao ni akina nani, kama wana pesa. Yatawaingiza ndani haidhuru wao ni nani, kama wanapendwa na watu. Lakini kuna jambo moja juu yake, huwezi kuingia katika Kanisa la Mungu namna hiyo; si madhehebu sasa, ninamaanisha Kanisa halisi, kanisa halisi la Mungu.

----
Watu, wanajua wanachotaka. Kwa hiyo kama itawabidi kupata wanachotaka, basi itawabidi kuwa na chujio la namna fulani, na ulimwengu wa kutosha kuzungumza, kuridhisha ladha yao ya kilimwengu. “Chujio la mtu mwenye busara, ladha ya mtu anayevuta sigara.” Chujio la ulimwengu wa kidini, na ladha ya mtu wa kilimwengu.

Wanataka kuwa wa kidini. Wanafikiri hawana budi kuwa wa kidini, kwa sababu wana nafsi. Tulipokuja kwa mara ya kwanza nchini humu, mlikuta Wahindi wakiabudu jua na kadhalika, kwa sababu (kwa nini?) Yeye ni mwanadamu. Tunarudi kwenye misitu ya mbali ya Afrika, tunawakuta wenyeji wakiabudu kitu fulani. Kwa nini? Wao ni wanadamu, nao wanataka, hawana budi kuabudu.

Kwa hiyo mwanadamu, haijalishi ameanguka namna gani, angali anajua kuna kitu fulani mahali fulani. Lakini yeye ana ladha hiyo ya ulimwengu, hata hawezi kuchukua chujio sahihi. Hana budi kuwa na chujio alilojitengenezea mwenyewe. Kila mmoja akifanya chujio la aina yake.

Kila kampuni ya sigara inajivunia yao, yale wanayoweza kufanya, “Chujio halisi! Hii ndiyo chujio bora zaidi! Wote wako mbele!” na wote namna hiyo. Kasema, “Ladha huja,” ama kitu fulani, “kutoka mbele.” Loo, kwa ajili ya wema. “Mbele”? Kuna nini nyuma yake, hata hivyo? Hakika si mwanamume mwenye busara wala mwanamke mwenye busara. Lakini hivyo ndivyo wanavyosema, kuwadanganya tu watu.

----
Angalia katika Hesabu 19, nawatakeni msome mnapoenda nyumbani, mtakapokuwa na wakati zaidi. Angalia, wakati Israeli walipokuwa wamefanya dhambi, kwanza walimchukua ndama mwekundu ambaye kamwe hakuwa amewekwa nira shingoni mwake. Hiyo inamaanisha kamwe hakufungwa nira na chochote.

Naye ilimbidi awe mwekundu. Rangi nyekundu ni-ni rangi ya upatanisho. Unajua, sayansi inajua ya kwamba kama ukichukua nyekundu na kuangalia kupitia nyekundu, kwa nyekundu, ni nyeupe. Angalia kupitia kwenye nyekundu, kwenye nyekundu, ni nyeupe. Yeye huangalia kupitia Damu nyekundu ya Bwana Yesu, na dhambi zetu nyekundu zinakuwa nyeupe kama theluji; nyekundu kupitia nyekundu. Na huyo ndama aliuawa wakati wa jioni, na kusanyiko lote la Israeli. Na pale paliwekwa milia saba kwa damu yake mlangoni ambapo kusanyiko lote lilipaswa kuingia; mfano wa zile Nyakati Saba za Kanisa, kwa Damu.

Na ndipo mwili wake ukachukuliwa na kuteketezwa kwa moto. Iliteketezwa kwa moto pamoja na kwato, pamoja na ngozi, pamoja na matumbo, pamoja na mavi. Kila kitu kiliteketezwa kwa moto, pamoja. Na ilibidi achukuliwe na mtu msafi, na ilibidi kuwekwa mahali safi nje ya kusanyiko. Kwa hiyo, kama Israeli wangaliona tu mfano! Neno hili la Mungu halipaswi kubebwa na mikono michafu ya kutokuamini. Haina budi kuwa ni mtu msafi. Na kama yeye ni msafi, ilimbidi kupitia kwenye Chujio la Mungu.

Mtu safi, mikono safi, na ilibidi kuwekwa mahali safi; si mahali ambapo akina Yezebeli, na Rickies, na kila kitu wanashiriki; kula ushirika na kadhalika, wakati wanapokuwa wakizurura na wake, na waume, na kila namna ya uchafu; wakienda kwenye dansi na karamu, na kuwa na nywele zilizokatwa, na kaptura, na kila kitu kingine, na kujiita Wakristo. Linapaswa kuwekwa mahali safi, na kushughulikiwa kwa mikono safi. Na ndipo Israeli walipotenda dhambi, na kutambua ya kwamba walikuwa wametenda kosa, basi walinyunyiziwa majivu ya ndama huyu, juu yao. Na hayo yalikuwa maji ya utengano, utakaso wa dhambi.

Angalia. Hili hapa! Na wakati Israeli, kabla hawajaingia katika ushirika katika ibada, iliwabidi kwanza kupitia kwenye maji ya utengano. “Kuhesabiwa haki kwa imani; huja kwa kusikia, kusikia Neno.” Ndipo wakaingia katika kusanyiko chini ya hiyo milia saba, ile damu, kuonyesha ya kwamba kitu fulani kilikufa na kutangulia mbele yao, kwa ajili ya dhambi zao. Walitengwa kwa kulisikia Neno, maji ya utengano, kisha wakaingia katika ushirika.

Mahali pekee ambapo Mungu alikutana na mwanadamu palikuwa nyuma ya utaratibu huo. Asingekutana naye mahali pengine popote. Ilimbidi kuja nyuma ya utaratibu huo. Mungu alikutana na Israeli mahali pamoja tu. Na Mungu anakutana nawe leo mahali pamoja, na hapo ni katika Yesu Kristo; Naye ni Neno, maji ya utengano. Na Damu Yake ilimwagwa kwa ajili ya Nyakati zote Saba za Kanisa. Halafu basi, kwa Roho Mtakatifu, tunaingia katika ushirika huo, ambao hutolewa tu kwa Kanisa. Loo, jinsi Yeye alivyo mkuu!

Pia, sasa, tunataka kuangalia Waefeso 5:26, ilisema, “Ni kuoshwa kwa maji kwa Neno,” maji ya utengano. Hufanya nini? Halafu, Chujio la Mungu ni Neno. Maji ya utengano, “kuoshwa kwa maji, ya utengano, kwa Neno,” Chujio la Mungu.

Basi, huwezi kuingia katika Kristo kupitia chujio la kanisa. Huwezi kuja kwa chujio la kimadhehebu au chujio la kanuni za imani. Kuna Chujio moja tu, ambapo unaweza kuingia katika mahali pale patakatifu, hiyo ni kwa “kuoshwa kwa maji kwa Neno.” Neno la Mungu ni Chujio la mtu mwenye busara.

Kanisa litakuhukumu hapa kama wewe ni mshiriki mzuri, ama la. Watakupa mazishi mazuri, na nusu mlingoti wa bendera wakati wa kufa kwako, watatuma mashada makubwa ya maua na kukufanyia kila kitu. Lakini inapofikia kwenye nafsi yako inayomkabili Mungu, haina budi kuwa na Uzima wa Milele. Na kama ni Uzima wa Milele, ni sehemu ya Neno. Na kwa kuwa neno langu mwenyewe haliwezi kukana... Mkono wangu mwenyewe hauwezi kuukana mkono wangu. Macho yangu mwenyewe hayawezi kuukana mkono wangu, wala mguu wangu, wala kidole changu cha mguu, wala sehemu yoyote yangu. Haviwezi kuukana.

Na wala mwanamume ambaye ni sehemu ya Neno la Mungu, ama mwanamke, hawezi kukana sehemu moja ya Neno la Mungu. Halafu, enyi wanawake, mnapofikiri mnaweza kukata nywele na kuja katika Uwepo wa Mungu, mmekosea. Mnaona jambo hilo? Umekosea; huwezi kuja kupitia kwenye Chujio la Mungu ambapo unaoshwa na maji ya Neno. Ndipo unaingia katika ushirika. Unafikiri uko hivyo, bali huwezi kuwa mpaka utakapopitia kwenye Neno, na kila sehemu ndogo, kila Neno dogo la Mungu. “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno.” Haina budi kupitia kwenye huo mchujo, likipita moja kwa moja. Na hiyo inatoa ladha ya mtu mwenye haki, maana hiyo ndiyo anayoitafuta, akitafuta kitu fulani cha kumsafisha.

Neno, Neno la Mungu ni Chujio la mtu mwenye busara, na Hufanya ladha ya mtu mwenye haki. Tunajua hilo ni kweli; huchuja dhambi zote za kutokuamini. Hakuna kutokuamini tena unapopitia kwenye Chujio, kwa sababu ni ladha ya mwaminio wa kweli.

Mwamini wa kweli anataka kuwa sahihi, haidhuru. Hataki tu kusema, “Vema, mimi ni mmoja wa tabaka bora la kijamii. Mimi ni mfuasi wa kanisa, kanisa kubwa kuliko yote mjini.” Sijali kama ni misheni fulani kule pembeni, kama ni mkutano wa nje, mahali fulani, mtu mwenye busara anajua ya kwamba hana budi kukutana na Mungu. Na haidhuru kanisa linasema nini, ama mtu mwingine ye yote asemaye, hana budi kuja kulingana na masharti ya Mungu. Na masharti ya Mungu ni Neno la Mungu.
“Vema,” wao wanasema, “'Neno la Mungu.'”
Hakika, wote wanaamini ni Neno la Mungu, lakini unaweza kuchuja kupitia Hilo? Utamwachaje mwanamke aliyekata nywele zake apitie Pale? Utafanyaje jambo hilo? Utamwachaje mwanaume apitie Huko ambaye hatashikilia Fundisho hili? Mnaona?
Si ladha ya mtu mwenye busara. La. Mtu mwenye busara atafikiri, mtu mwenye busara atafikiri mara mbili kabla ya kurukia kitu kama hicho.

Angalia, Neno hilo haliwezi kujikana Lenyewe. Halafu limeridhika, ama ni shauku. Ni shauku ya nini? Ni kitu gani kilichokufanya na shauku hiyo, kwanza? Kwa sababu chini katika nafsi yako kulikuwako na mbegu iliyochaguliwa tangu zamani ambayo ilikuwa ni Uzima wa Milele, daima ikikaa mle ndani, daima ilikuwa mle ndani. “Wote alionipa Baba watakuja Kwangu. Hakuna hata mmoja wao atakayepotea.”

Ladha ya mtu mwenye busara, wakati mtu mwenye busara anapolisikia Neno la Mungu, “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu, mgeni hawatamfuata,” kwa maana ndani humo kuna Uzima, na Uzima unaungana na Uzima. Dhambi huungana na dhambi, na dhambi ni ya unafiki sana hata inadhani ya kwamba imeokolewa wakati haijaokoka. Ni katika kilindi kabisa cha unafiki.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Chujio la mtu mwenye busara.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;

apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Waefeso 5:25-27


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Chapter 11
- The Cloud.

(PDF Kiingereza)
 

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.