Kwa nini ilipaswa kuwa ni Wachungaji.
<< uliopita
ijayo >>
Kwa nini Wachungaji.
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kwa nini ilipaswa kuwa ni Wachungaji.Luka 2:8-16,
8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.
9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
10 Yule malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa, tazama, nawaletea habari njema ya furaha kuu, ambayo itakuwa kwa watu wote.
11 Kwa maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi, ambaye ni Kristo Bwana.
12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.
13 Mara walikuwapo nanii... Mara waliku-... pamoja na huyo malaika, wingi wa...jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,
14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.
15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
16 Wakaenda upesi, wakamkuta Mariamu, na Yusufu, na mtoto mchanga amelala horini.Sasa, ni ninii... Kwa nini tukio hili kubwa lilifunuliwa kwa wachungaji? Hilo lingekuwa ni jambo la kushangaza kwetu. Nina baadhi ya Maandiko yaliyoandikwa hapa, na maandishi machache ambayo nitajaribu kuyasoma, kuwaelezea kwa nini kadiri niwezavyo. Na labda basi baada ya jambo hili, kwamba Bwana kwa neema Yake, usiku wa leo, ataondoa hizi ni kwa nini kutoka kwetu. Lakini alifanya ... Karibu sisi sote, nadhani, wakati mmoja ama mwingine, tumeshangaa ni kwa nini tukio hili kubwa kuliko yote lilifunuliwa kwa wachungaji. Kwa nini lilifunuliwa kwa wachungaji na si kwa wanatheolojia wa siku hiyo? Hao ndio waliofunzwa kulisikia. Na ni kwa nini lilikuja na kuwapita matajiri, na kuwajia maskini? Pia, kwa nini liliwapita waliosoma na wenye hekima, na kuwajia wanyenyekevu na wasio na elimu? Kuna maswali machache ya kwa nini katika jambo hili.
Na sababu nyingine ninayoweza kusema, angalia, mtoto huyo mchanga alizaliwa Bethlehemu. Ambayo Bethlehemu katika tafsiri ya Kiebrania, kama tulivyokuwa nayo miaka michache iliyopita hapa, Bethlehemu maana yake ni “nyumba ya mkate wa Mungu.” Nasi tulithibitisha katika Maandiko, Yeye asingeweza kuja mahali pengine popote. Bethlehemu ilianzishwa na Rahabu na nanii wake- mume wake. Rahabu alikuwa ni kahaba ambaye jemadari alimpenda, kutoka kwa- kwa jeshi la Israeli, baada ya kuiteka Yeriko. Na kwa imani aliamini Ujumbe wa Mungu, katika hali yake, naye akaokolewa. Na kutoka hapo, wakati Yoshua alipogawanya nchi ambapo kila mmoja angekuwa,...
Na kuna somo kuu ambalo wakati mwingine natumaini kuwa na uwezo wa kuleta huko Tucson, kuhusu hao mama wa Kiebrania wanaowazaa watoto hao. Wakati alipougua katika utungu wa kuzaa mtoto mchanga, aliita jina la mtoto huyo mchanga na hiyo ikamweka mahali pake katika nchi ya ahadi, kabila lake. Jambo kubwa, Neno lote la Mungu huafikiana moja kwa moja. Lisipoafikiana, Neno la Mungu silo lisiloafikiana, mawazo yako ndiyo ambayo hayaafikiani na Neno. Yote yanalingana.
Kwa hiyo, basi, Yeye alikuwa Mkate wa Uzima, kama tulivyofundisha juma lililopita huko Phoenix, ama juma lililotangulia. Na kwa kuwa yeye ni Mkate wa Uzima, asingeweza kuja mahali pengine ila “nyumba ya mkate wa Mungu.” Na hiyo ndiyo iliyokuwa ile ni kwa nini. Sasa, hapa, Yesu amezaliwa Bethlehemu, na Bethlehemu kulikuwako na sinagogi, viongozi wakuu wa kidini waliishi Bethlehemu. Daudi mfalmemchungaji mkuu alizaliwa Bethlehemu, baba yake Yese alizaliwa Bethlehemu, babu yake Obedi alizaliwa Bethlehemu. Pia, huko nyuma kabisa, yeye alitoka Bethlehemu.
Na hapa, Yesu Mwana wa Daudi amezaliwa Bethlehemu, moja kwa moja chini ya vivuli vya makanisa makuu. Basi kama watu hao wamefunzwa, na wamekuwa wakimtazamia Masihi kwa miaka hii yote; miaka elfu nne, Masihi alikuwa ametabiriwa kuja. Na basi kama Masihi akizaliwa katika kivuli cha kanisa kuu, kwa nini iliwabidi kurudi moja kwa moja wakaingia milimani kwa kundi la wachungaji wasio na elimu na wasiofunzwa, kuleta Ujumbe huu mkuu, Ujumbe wa kwanza? Nao wakawaagiza wachungaji! Si wenye hekima na waliofunzwa, bali ni wachungaji. Ni jambo la ajabu, sivyo? Lakini hapana budi kuwe na sababu fulani mahali fulani... Kuna sababu, sasa hapana budi kuwe na jibu kwa nini! Na hakuna mtu ajuaye jibu ila Mungu. Yeye Ndiye anayejua jibu.
Sasa, kumbukeni, Masihi alikuwa tayari mjini, alizaliwa mjini, katika hori; moja kwa moja karibu na makanisa makuu ambapo kuhani mkuu... na makuhani wakuu, na wanatheolojia, na wenye hekima, na waliofunzwa, wote walikuwa pale wakimngojea Masihi. Naye alikuwa pale, moja kwa moja katikati yao! Lakini kwa nini basi walienda kwenye... huko kwenye milima ya Yuda kwa wasio na elimu, wasio na mafundisho, wasio na elimu, maskini kuliko wote? Alionekana kama mtu asiyefaa sana kwa kazi hiyo, kufunua Ujumbe na kuwatuma nje kuuleta Ujumbe.
Mnajua maoni yangu? Huenda yasifae kitu, bali nataka kutoa maoni yangu: ninaamini ni kwa sababu ya hekima ya Mungu, kwamba Yeye alijua wasingeupokea Ujumbe kama huo jinsi ulivyokuja. Haikuwa katika ladha ya elimu yao. Ilikuwa ni tofauti. Haikuwa vile walivyofunzwa kuamini Yeye angekuwa. Ilikuwa ni kinyume cha ufahamu wao wa kitheolojia. Mafunzo yao yote, elimu yao yote ilipitwa, ikawa bure. Ninaamini ni hekima ya Mungu iliyojua ya kwamba wasingeupokea Ujumbe kama huo.
Kwa hiyo Masihi alikuwa hapa, na hapana budi kuwe na mtu anayemtambua. Naye alijua wale ambao hawakuwa wamechanganyikiwa katika upuuzi kama huo. Angekuwa anaweza hata na zaidi kuupeleka ujumbe Wake kwa kundi lisilo na elimu, kuliko vile angaliweza kwa kundi lililochanganyikiwa ambalo lilikuwa limeshika njia za mwelekeo mkali hata hakuna kitu kingaliweza kuwageuza, si hata Neno la Mungu.
Na sasa, rafiki Mkristo, hebu niulize swali hili, kwa unyofu wote na upendo. Nashangaa tu kama Yeye angetenda tendo lile lile usiku wa leo, na kututumia sisi katika kizazi hiki Neno la ahadi lililoahidiwa kwa ajili ya kizazi hiki, nashangaa kama wanatheolojia wetu, na walimu, na wenye hekima, wasingeukataa Ujumbe huo kama vile tu walivyofanya wakati huo? Mwanadamu habadiliki, wala Neno la Mungu halibadiliki. Yeye ni Mungu asiyebadilika, Yeye habadiliki!
Angalia, Malaika wakija na... Malaika wakija na kutoa Ujumbe wao kwa watu wa hali ya chini sana, wakati kulikuwako na watu pale zaidi (wazo la kidunia la) wenye sifa kuliko hawa wachungaji maskini, wasiojua kusoma. Mchungaji alikuwa mtu asiye na elimu kuliko mtu yeyote, hakuhitaji kujua kitu ila kuhusu kondoo wake tu. Hakuhitaji kujua hisabati. Hakuhitaji kujua jinsi ya kugawanya atomi. Hakuhitaji usomi wowote. Ilimbidi tu kuwajua kondoo wake, hayo tu ndiyo aliyohitaji kujua. Na Mungu, Hekima kuu, na Chemchemi na rasilimali ya hekima yote, angemchagua mtu kama huyo (watu, hasa, kama huyo), na kuwapita wasomi wote waliofunzwa vizuri waliofunzwa kujua Hilo. Inaonyesha jambo moja, ya kwamba walifunzwa katika fani isiyofaa. Akiwapita watu wote mashuhuri wa nchi hiyo; kulikuwa na watu wa maana, walimu mashuhuri, akina kuhani mkuu Kayafa, watu wengine wengi mashuhuri, Waisraeli wote wenye elimu nyingi, madhehebu yote, na wanatheolojia wote wenye kujigamba, Mungu alimpita kila mmoja wao! Sasa, hiyo ni hekima ya Mungu.
Angalia, Mbingu za Juu sana zikiharakisha kuwaheshimu walio wanyenyekevu sana na wasio na elimu. Aliye Juu Sana wa Mbinguni alishuka kujitambulisha kwa walio duni sana wa dunia, akiwapita wote walio katikati apate kujitambulisha kwa wachungaji wa kawaida; akija kuwapa hawa wachungaji wa kawaida Ujumbe ulio mkuu sana wa nyakati zote. Kulikuwa na wajumbe wengi mashuhuri. Tungewazia juu ya siku ya Nuhu, na hao manabii, na makuhani adhimu, na kadhalika, walikuwako katika siku zilizopita. Watu mashuhuri walio na elimu, wafalme, viongozi wakuu, watawala, bali Huyu hapa anakuja akiwa na Ujumbe mkuu kuliko jumbe zingine zote. Ujumbe ulikuwa ni nini? “Masihi yupo hapa sasa!” Mnaona? Na kulijulisha hilo, Yeye aliwapita wote waliofunzwa, kuwajulisha wachungaji wanyenyekevu.
Wazia jambo hilo: makasisi wote, watu wote wa kanisa, walimu wote, mafundisho yote ya theolojia, fedha zote zilizokuwa zimetumiwa, makanisa yote, na mafundisho, na madhehebu, yote yalipitwa! Elimu yote waliyokuwa wametumia juu ya wamishenari wo- wote, na ushawishi wote wa kubadili dini, uanachama wote, na kila kitu walichokuwa wamewazia wamefanya kumheshimu Mungu, hata hivyo Ujumbe ulio muhimu sana kuliko zote uliwapita. Ajabu! Kwa nini? Mnaona?
Angalia, Mbingu za Juu sana zikiharakisha kuwaheshimu walio wanyenyekevu sana na wasio na elimu. Aliye Juu Sana wa Mbinguni alishuka kujitambulisha kwa walio duni sana wa dunia, akiwapita wote walio katikati apate kujitambulisha kwa wachungaji wa kawaida; akija kuwapa hawa wachungaji wa kawaida Ujumbe ulio mkuu sana wa nyakati zote. Kulikuwa na wajumbe wengi mashuhuri. Tungewazia juu ya siku ya Nuhu, na hao manabii, na makuhani adhimu, na kadhalika, walikuwako katika siku zilizopita. Watu mashuhuri walio na elimu, wafalme, viongozi wakuu, watawala, bali Huyu hapa anakuja akiwa na Ujumbe mkuu kuliko jumbe zingine zote. Ujumbe ulikuwa ni nini? “Masihi yupo hapa sasa!” Mnaona? Na kulijulisha hilo, Yeye aliwapita wote waliofunzwa, kuwajulisha wachungaji wanyenyekevu.
Wazia jambo hilo: makasisi wote, watu wote wa kanisa, walimu wote, mafundisho yote ya theolojia, fedha zote zilizokuwa zimetumiwa, makanisa yote, na mafundisho, na madhehebu, yote yalipitwa! Elimu yote waliyokuwa wametumia juu ya wamishenari wo- wote, na ushawishi wote wa kubadili dini, uanachama wote, na kila kitu walichokuwa wamewazia wamefanya kumheshimu Mungu, hata hivyo Ujumbe ulio muhimu sana kuliko zote uliwapita. Ajabu! Kwa nini? Mnaona?
Na angalia, si hayo tu, bali mahali pasipotarajiwa kabisa kwa tukio kama hilo. Wachungaji, sasa, ndio walioupokea Ujumbe. Na sasa angalia mahali Ujumbe ulipokuwa: katika mahali pasipotarajiwa kabisa ambapo mtu yeyote angeutarajia kuja. Nami nashangaa, usiku wa leo, kama tulikuwa tukiutazamia Ujumbe wa kweli wa Bwana Yesu, sijui kama ungekuwa katika kundi lisilotarajiwa, mahali ambapo palikuwa ...ambapo ulimwengu mkuu, wenye utamaduni wa hali ya juu na kanisa siku hizi wangefikiri lilikuwa ni kundi la, loo, wazushi? Nashangaa kama hilo halingekuwa mahali ambapo tungempata? Mahali pasipotarajiwa, na kwa wasemaji wasio na sifa. Wachungaji hawakujua kitu juu ya kunena, ila tu kuwaita kondoo; vema, labda hiyo ndiyo sababu Huo ukaja.
Lakini kulikuwako na Neno lililoahidiwa. Angalia, ingewezekana hilo litendeke tena. Uliwapita watu wote walio bora wa nchi. Uliwapita watu wote walio bora, na ukafunuliwa kwa watu wasi kitu. Watu wote walio bora waliokuwa wametunukiwa nishani za- za daktari wa uungu na- na saikolojia, na- na elimu ya hali ya juu, na makanisa makuu na kadhalika, vyote vilipitwa na kufunuliwa kwa watu wa hali ya chini. Ile hekima, hekima isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu ilifanya jambo hilo, kuwajulisha Ujumbe ulio mkuu sana uliowahi kutokea, “Masihi sasa yuko duniani.” Ni hekima iliyoje! Ingeweza tu kutoka kwa Mungu anayejua hekima! Hekima yote na elimu yote, na kila kitu, sasa vilitupiliwa mbali na kupitwa na hekima kuu ya Mungu. Ninaendelea kurudia hayo kwa sababu ninataka yaingie ndani kabisa. Yote yameharibiwa, haikuwa na faida yoyote. Yote yalipitwa kusudi hekima ya Mungu ionekane wazi, ya kwamba Mungu huchukua wasio chochote na kuwafanya watu mashuhuri.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kwa nini ilipaswa kuwa ni Wachungaji.