Mnasema huyu eti kuwa ni nani?
<< uliopita
ijayo >>
William Branham.Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mnasema huyu eti kuwa ni nani?Mathayo 21:10-11,
10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.Sasa tunajua wakati umewadia, na wengi wenu mnajua Maandiko ya sura hii fulani. Ni kwenye... kweli siku ile Kristo alipokuja Yerusalemu, akimpanda huyu punda mdogo. Nasi tunaninii... Kuna hadithi inayosema ya kwamba “alikuwa ni punda mweupe.” Ningewazia, katika mfano wa utangulizi wa kuja Kwake mara juu ya farasi wa vita. Wakati huo, nabii alisema, ya kwamba “Yeye angempanda... Mfalme wako anakuja amepanda mwana-punda, na ni mnyenyekevu na mpole.” Hivyo ndivyo alivyokuja na... juu ya mwana punda, masikini mbeba mizigo. Lakini wakati mwingine atakapokuja kutoka Utukufuni (katika sura ya 19 ya Ufunuo), Yeye anakuja kama Mshindi Mwenye Nguvu. Vazi lake limelowekwa katika damu, akiketi juu ya farasi mweupe, na jeshi lote la Mbinguni linamfuata juu ya farasi weupe. Na hadithi hiyo (si ya Kimaandiko wala ya kihistoria)... Lakini hadithi inaamini ya kwamba Yeye alikuwa amepanda punda mdogo mweupe wakati akiingia Yerusalemu.
Sasa hiyo... Nimelichagua hili... bado lingali... kwa sababu tuko katika vivuli vya... ama katika wakati wa msimu wa sikukuu ya Krismasi, na wa Mwaka Mpya; kumalizika kwa mwaka uliopita, na mwanzoni mwa mwaka mpya. Siku chache kutoka sasa, watu wengi watakuwa wakifungua kurasa mpya na kufanya mambo mapya na kufanya nadhiri mpya; na ni mwanzo wa Mwaka Mpya. Na kwangu kamwe haionekani sana kama Krismasi. Sijui ni kwa nini, daima napenda kuiita “Siku ya Baba Krismasi.” Mnaona? Kwa sababu hakuna mengi sana...
Isingekuwa siku ya kuzaliwa kwa Kristo. Kamwe isingewezekana kuwa. Angepaswa azaliwe Marchi ama Aprili, maana Yeye alikuwa ni Mwana-Kondoo. Naye alikuwa mwana-kondoo dume na alizaliwa chini ya kondoo dume, Mapacha. Ilibidi iwe hivyo, mnaona. Na kondoo hawazaliwi Desemba hata hivyo. Kondoo huzaliwa katika majira ya Kuchipua. Na halafu jambo lingine, vilima vya Yuda sasa, kuna futi ishirini za theluji juu yake. Wachungaji wangewezaje kuwa huko nje?
Kwa hiyo kweli inatokana na hadithi za kubuni za Kirumi, ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa mungu jua. Jua linapopita, siku hurefuka na kuzidi kuwa ndefu, na usiku unakuwa mfupi. Na katikati ya Desemba 20 na 25 ni sikukuu ya kuzaliwa kwa mungu jua, chini ya ninii za Kirumi— hadithi za kufikirika za Kirumi. Na halafu miungu yao... Na ndipo wakaadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mungu jua. Naye Konstantino, na—na kuandikwa kwa katiba ya kanisa na taifa na kadhalika. Yeye alisema, “Tutaibadilisha” (bila kujua siku hiyo ilikuwa nini) “na kuiweka kwenye siku ya kuzaliwa kwa mungu jua, na kuifanya: Siku ya kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu.” Mnaona? Ambayo... Lakini hatujui ilikuwa ni siku gani.
Lakini sasa, yao, wameondoa mengi sana ya Kristo, hata imekuwa ni kila kitu... wengine tena walirudisha hadithi za kiumbe fulani kilichoishi, ilivyodhaniwa, kinachoitwa Mtakatifu Nikolas ama Kriss Kringle, hadithi fulani za Kijerumani. Na yote ni hadithi tu, na Kristo hayumo ndani yake hata kidogo. Na watu wamegeukia kwenye kununua wiski, na kucheza kamari, na mitindo. Na mtu ambaye... mfanyabiashara anayeweza kuuza bidhaa zake wakati wa Krismasi anaweza kuishi mwaka mzima, karibu mwaka mzima. Mnaona? Ni likizo kubwa sana, ya kibiashara. Na maskini watoto wadogo mtaani; ambao wazazi wao hawawezi kuwatembelea na zawadi, kama ile inayotoka kwa Baba Krismasi, basi wanatembea mtaani, huku maskini mikono yao ni michafu na macho yao ni mekundu. Ninachukia kuona jambo hilo likija. Inapaswa kuwa ni siku yenye uchaji ya kumwabudu Mungu, badala ya kuugua moyo na kuumwa na kichwa na hayo mambo yanayotendeka. Hakuna kitu kwa Kristo juu ya jambo hilo. Lakini sisi tuko moja kwa moja katikati ya haya yote sasa.
Tunajikuta wenyewe, kitu kama walivyokuwa wakati huo. Mnaona, kuingia tu sasa kwenye karamu kuu. Yesu alikuwa akija kwenye Sikukuu ya Pasaka. Naye alikuwa ameingia Yerusalemu... ama akiingia Yerusalemu. Na unabii wa kila kitu alichofanya hauna budi kutimizwa. Kila kitu katika Biblia kina maana. Kila jina lina maana. Hakuna kitu kilichoandikwa katika Maandiko ila kilicho na maana kubwa sana.
Nilihubiri hivi majuzi usiku huko Tucson, juu ya “Kwa Nini Ilibidi Iwe Ni Wachungaji Badala Ya Mwanateolojia?” Yeye alizaliwa moja kwa moja upande wa kanisa. Naye Roho Mtakatifu akienda moja kwa moja nyikani na kuchukua, si wanatheolojia, bali wachungaji. Ilibidi iwe hivyo. Wanatheolojia wasingeamini Ujumbe kama huo. Kwa hiyo wao... ilibidi iwe ni wachungaji.
Nilihubiri hapa, miaka michache iliyopita, miaka miwili iliyopita, “Kwa Nini Ilikuwa, Ilikuwa Ni Bethlehemu Mdogo?” Bwana akipenda, Krismasi ijayo, ninataka sisi kuhubiri juu ya, “Kwa Nini Ilibidi Iwe Ni Mamajusi?” Hizi “Kwa Nini?”— zina majibu yake, na yako mumu humu katika Biblia. Nasi tunaishi katika wakati wa ajabu, wakati mkuu sana wa nyakati zote. Tunaishi kufikia kwenye wakati, wakati wowote ambapo utaninii... wakati unaweza kukoma na Umilele unaweza kuchanganyika moja kwa moja pamoja na wakati na kuendelea. Nyakati za manabii wote na wenye hekima, walitazamia. Tunapaswa kuwa macho kila saa, tukikesha kuja Kwake.
Tunajikuta wenyewe, kwenye Krismasi hii, kama tu vile walivyofanya Krismasi ya kwanza hata hivyo. Ulimwengu uko karibu kuporomoka. Kama nilivyohubiri wakati mmoja, mahali fulani, kuhusu ujumbe wa Krismasi, Ulimwengu Unaporomoka. Na ulimwengu tena uko karibu kuporomoka. Angalia matetemeko ya nchi hapa California. Ninabashiri, kabla ya kuja kwa Bwana Yesu, ya kwamba Mungu atapazamisha mahali hapo. Ninaamini ya kwamba Hollywood na Los Angeles, na sehemu hizo chafu kule, ya kwamba Mungu Mwenyezi atazizamisha. Yataenda chini ya kilindi cha bahari. Na kuna dhambi nyingi sana, unaona, ni kile kizuizi.
Ustaarabu umesafiri pamoja na jua, kutoka... na ulianza Mashariki, ukielekea magharibi. Na sasa uko kwenye Pwani ya Magharibi. Kama ukienda mbali zaidi, utarudi Mashariki tena. Kwa hiyo hicho ndicho kizuizi. Nayo dhambi imesafiri pamoja na ustaarabu, na umekuwa ni shimo la maji machafu ya nyakati zote. Mambo wanayofanya ambayo wanadamu katika wakati mwingine wowote wasingeweza kuwazia jambo kama hilo. Wanawake wamejitupa kwenye takataka nyingi sana, hata hakuna mwanamke katika wakati wowote angaliweza kufikiria jambo kama tunalofanya siku hizi. Na halafu bado tunajiita Wakristo. Ni aibu iliyoje!
-----
Mungu alitoa... anajibu jibu la maombi yako. Umeomba, nawe utapokea. Na hiyo ni... Ningeweza kusimama hapa kwa saa nyingi, juu ya wanaume na wanawake, Wakristo hata, kuomba kwa ajili ya kitu fulani; na Mungu hutoa jibu na hata hawalitambui.Na sasa, Mungu aliwapa jibu. Wao wanataka Masihi. Walijua ya kwamba walikwisha kuwa na Makaisari, nao walikwisha kuwa— walikwisha kuwa na akina Daudi, walikwisha kuwa na akina Sulemani (yule mtu mwenye hekima), walikuwa na akina Daudi (mashujaa wakuu wa vita), wao— walikwisha kuwa na kila namna, bali walijua iliwabidi kupata msaada kutoka Mbinguni nao... Mungu alikuwa amewaahidi Masihi. Naye akawatumia huyo Masihi, katika jibu la maombi yao, bali hawakumtaka.
Nashangaa, leo, kama maombi yetu... Unawasikia wakisema, “Ombeni kwa ajili ya ufufuo mkuu. Omba kwa ajili ya jambo hili. Ombeni kwa ajili ya ushindi. Ombeni kwa ajili ya umoja.” Nashangaa, kama Mungu angetuma mpango kama huo, kama tungaliukubali. Nashangaa tu kama tungekubali yale anayotutumia. Mnaona, Yeye... Sababu ya sisi kuombea vitu hivi, ni kwa sababu tunajua vinahitajika. Lakini wakati Mungu anapolituma jinsi anavyotaka, basi si kulingana na ladha yetu, na kwa hiyo hatutalipokea. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa katika siku hiyo. Kama Yeye hakuwa katika ladha ya imani yao na... Wao wasingempokea tena, leo. Hiyo ndiyo sababu waliuliza swali hili, “Ni nani huyu? Jamaa huyu anayekuja ni nani?” Mnaona, ulikuwa ni wakati— mzuri sana. Loo, kila mtu alikuwa... wasiwasi. Kitu fulani kilikuwa karibu kutukia.
Na hebu uangalie ulimwengu leo, ni wasiwasi wa namna gani ulimwengu mzima unaoishi nao. Unashuka kwenda barabarani... Hata— si salama kuendesha gari. Si salama kuwa katika barabara kuu yenye njia nne. Kila mtu yuko kwenye wasiwasi, anapiga kelele na... Kuna nini? Tulia. Unaenda wapi? Hilo ndilo linalofanya hospitali za wenda wazimu kujaa. Hilo ndilo limeliletea kanisa machafuko kama hayo. Wao wana— wana kichwa kigumu sana juu ya jambo fulani. Hawatasimama na kutafakari Neno la Mungu, na saa tunayoishi; wote wamelemewa na uchovu, wasiwasi.
Na sasa, tunajua. Tunafahamu. Dunia ndiyo kwanza ipitie maumivu makali sana ya kuzaa. Na kanisa linapitia katika utungu wa kuzaa. Ilibidi lipitie utungu wa kuzaa kabla ya kutoa... Kila mmoja wa manabii, walipokuja ulimwenguni, ilikuwa ni uchungu wa kuzaa kwa kanisa. Ulimwengu umepitia kwenye Vita vya Kwanza vya Dunia, Vita vya Pili vya Dunia, na sasa uko tayari kwa Vita vya Tatu vya Dunia. Na iko katika utungu wa kuzaa tena. Lakini kuna kitu kimoja tu kinachoweza kuleta amani, na hicho ni Kristo.
Mifumo yetu yote, na mawazo yetu, na makanisa yetu yanajenga, na siasa zetu zote, na sayansi yetu yote na kila kitu, imethibitishwa ya kwamba ni upuuzi. Na halafu tunamwomba Mungu atusaidie, aingilie kati, “Njoo utufanyie jambo fulani.” Na basi anapofanya jambo hilo, sijui kama tungeweza kufahamu jambo Hilo; kama tungeweza kulipokea; ama hata tungaliweza kulifikiria?
Sasa hilo ndilo lililofanywa huko nyuma katika siku hizo. Walikuwa wakiomba, waliisha kuwa na kila namna ya viongozi wakuu, waliishakuwa chini ya serikali mbalimbali, waliishakuwa chini ya ufalme, waliishakuwa chini ya kila kitu, waamuzi. Lakini walijua ya kwamba kuna kitu kimoja tu ambacho kingeweza kuwaokoa, hicho kilikuwa ni kuja kwa Masihi. Na Masihi maana yake ni “aliyetiwa mafuta.” Mwanadamu aliyetiwa mafuta. Ndipo mwanadamu, aliyetiwa mafuta na Neno. Neno lililofanyika mwili miongoni mwetu. Na wakati alipokuja, hakuwa na ladha ya jinsi vile walivyomtaka hasa awe; si ladha waliyokuwa nayo... ambayo anapaswa kuja nayo. Kwa hiyo basi wao wanalia, “Ni nani jamaa huyu? Ghasia yote hii ni ya nini?” Kundi la wakulima wadogo pale langoni, wakivunja mitende na...
Naye akasema, “Mbona, hebu wanyamazishe. Wanatukera, jinsi wanavyoshangilia, na kupiga vifijo, na kufanya ghasia.”
Yeye akasema, “Wakinyamaza, miamba hii mara moja itapaza sauti.”Loo, wakati ulikuwa ukifunuliwa! Unabii ulikuwa ukitimizwa. Si ajabu! “Simba ananguruma, ni nani hatahofu? Na Mungu amenena. Ni nani atakayejizuia kutabiri?”
“La, kama hakuwa katika ladha yetu wenyewe hasa... Kama asingalikuwa jinsi tu tulivyomtaka, jinsi ambavyo tulidhani angalipaswa kuja, tusingalimpokea.” Basi, kanuni zao za imani ndizo zilizowatoa kwenye Neno lililoandikwa. Walikuwa wameliacha kwa mbali sana, walishindwa kumtambua Yeye waliyekuwa wameomba aje. Makanisa yao yalikuwa yamewapeleka mbali sana, mpaka jambo lile lile walilokuwa wameliomba, lilikuwa papo hapo pamoja nao, na halikuwa katika ladha yao, na kwa hiyo wao hawakuweza kuliamini. Ilibidi wajiepushe Nalo. Ilibidi wajiepushe Nalo. Walilitupilia mbali. Wao... Kuna jambo moja tu unaloweza kufanya wakati unapokutana na Kristo. Hiyo ni ama kumkubali Yeye ama kumkataa. Huwezi kuondoka ukiwa pande zote mbili. Huwezi kufanya hivyo. Si kazi yako kufanya hivyo. Ni hivyo tu.Hebu angalia tu, jinsi wachache walivyomtambua kuwa Neno Lililotiwa Mafuta, la siku ile. Mnaona, Mungu hapo mwanzo, akiwa asiye na kikomo, na aliyejua mambo yote tangu mwanzo... Na jambo pekee ambapo vitu hivi vilivyo ni kwamba ni onyesho la sifa Zake. Sifa... Una sifa. Ni wazo lako. Unawazia jambo fulani, kisha unalinena, halafu unalichukua. Huyo ni Mungu. Yeye, hapo mwanzo... Kama wewe ni... Kama uliwahi kuwa au utapata kuwa Mbinguni, hapo mwanzo ulikuwa Mbinguni. Wewe ni sehemu ya Mungu. Wewe ulikuwa wazo Lake. Yeye alijua jina lako. Yeye alijua wewe ulikuwa nani kabla hakujapata kuwa na molekuli, kabla hakujakuwako na nuru. Kabla hakujakuwako na cho chote, Yeye alikujua wewe na jina lako. Na kuliweka kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, kabla ulimwengu haujapata kuumbwa. Mnaona, wewe ulikuwa ni wazo Lake. Na halafu ninii... Ndipo unakuwa Neno. Na neno ni wazo lililotamkwa. Ndipo unadhihirishwa.
Hivyo ndivyo alivyokuwa. Hapo mwanzo alikuwa peke Yake. Mungu aliishi peke yake na mawazo Yake. Kamwe hatafanya hivyo tena maana mawazo Yake yanadhihirishwa. Na hiyo ndiyo sababu tuko papa hapa, siku hii... ni Mungu akishirikiana na mawazo Yake, akidhihirishwa. Mnaona? Tuko hapo. Kwa hiyo, wewe, kwa kuwazia, huwezi kuongeza mkono mmoja kwenye kimo chako. Huwezi kufanya hivi, vile, ama vinginevyo. Ni Mungu anayeonyesha rehema. Ni Mungu. “Wote alionipa Baba watakuja Kwangu, wala hakuna mtu awezaye kuja asipovutwa na Baba Yangu.” Hilo latosha.
Kusoma kamili ya akaunti katika...
Mnasema huyu eti kuwa ni nani?