Ndoa Na Talaka.

<< uliopita

ijayo >>

  Kutembea kwa Kikristo mfululizo.

Tangu mwanzo haikuwa hivi.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ndoa Na Talaka.

Mathayo 19:8,
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

Andiko hili, swali hili, lilimkabili Yesu mwanzoni kabisa mwa huduma Yake. Nalo lilimkabili Musa mwanzoni kabisa mwa huduma yake. Ni swali muhimu sana mioyoni mwa waaminio. Mwenye dhambi hajali. Lakini ni kwa ajili ya waamini, kwa sababu mwamini anajaribu kutenda yote ambayo anajua jinsi ya kutenda kuishi sawa mbele za Mungu. Kwa hiyo, swali lolote linakuja juu ya dini, ndipo kesi ya Ndoa na Talaka inakuja, (kwa nini?) kwa sababu ni chanzo cha dhambi ya asili. Hapo ndipo dhambi ilipoanzia. Na hiyo ndiyo sababu linaletwa kila wakati, kwa sababu ni mwanzo kabisa wa dhambi.

Sasa sitakuwa na wakati wa kuelezea mambo haya yote, bali nitafurahi kujibu barua yenu ama cho chote niwezacho. Ama, tuna vitabu vilivyoandikwa juu yake, na maswali mengi, na hata kato za magazeti na kadhalika hapa, kuthibitisha jambo hili, tunajua kwamba ilikuwa Hawa (Tofaa ambalo alidhaniwa alikula, ambapo hata si Kimaandiko, sasa wanadai ilikuwa embe dodo; haikuwa mojawapo ya hayo.), Alizini, hilo lilimleta mtoto wa kwanza, ambaye alikuwa Kaini, mwana wa Shetani, kwani ndani yake mlikaa uovu. Haukuja kwa Habili. Haukupitia kwa Habili. Mwana wa Shetani alikuwa Kaini.

----
Na kama nilivyosema, kama nilitaka kwenda mashariki asubuhi hii; na kwa yote ambayo nimejua hili, ilinibidi kutafuta kitu fulani shambani, na kilikuwa moja kwa moja mashariki, nami nilikwenda mashariki. Mtu fulani alisema, “Ndugu Branham, hii ni mashariki.” Ni mashariki, kwa uwezekano, bali ni kaskazini mashariki. Ningepita kitu kile kile nilichokuwa nikitafuta; Ningerudi, nikijua nilikosea. Halafu basi kama mtu fulani alisema, “Ndugu Branham, nenda huku, upande wako wa kulia.” Sasa, hiyo ni uwezekano wa mashariki, pia, lakini ni kusini mashariki. Ningepoteza kitu nilichokuwa nikitafuta, kwa sababu nilivuka mipaka ya njia kamilifu na ya moja kwa moja.

Tuna mawazo mawili juu ya Ndoa na Talaka. Na hiyo ni kusema, mmoja wao anasema, ya kwamba, “Mtu anaweza kuoa mara moja tu, isipokuwa mkewe amekufa.” Na hilo ni moja ya hayo maswali, lakini, ukiifuata hiyo, utakosa kiasi. Na halafu nyingine husema, “Loo, kama mke au mume, mmoja wao, amezini, mmoja wao anaweza kuachwa na afunge ndoa tena.” Unajikuta umekosa kiasi kwa jambo hilo.

Kwa hiyo, mnaona, si kusini mashariki wala kaskazini mashariki; tunataka moja kwa moja mashariki. Ungekosa Maandiko unapoenda huku, unakosa Maandiko unapoenda upande ule. Tunataka kujua mahali Maandiko yanapokutana na Maandiko, na kujua Ukweli wake ni nini. Kila mmoja anachukua njia tofauti, na anashindwa kuleta jibu sahihi, lakini bado lazima kuwe na jibu.

Ni kama tu, leo, kuna itikadi mbili maarufu za mafundisho katika kanisa; moja yao ni Ukalvini, nyingine ni Uaminia. Mmoja wao ni mshika sheria, huyo mwingine ni neema. Nasi tunakuja kuona ya kwamba watu wanaoamini katika neema, Wakalvini, wanasema, “Mungu atukuzwe, hainidhuru kuvuta sigara. Hainidhuru kunywa pombe. Ninaweza kufanya mambo haya, nina usalama wa Milele.” Halafu tunaona ule upande mwingine, wa mshika sheria, kasema, “Loo, ningetaka kumkaripia kwelikweli, ningetaka ajue ninavyosikia, lakini, mimi ni Mkristo, yanipasa ninyamaze.” Mnaona, unajikuta katika barabara mbili tofauti, wala hakuna moja ya hizo zilizo sahihi. Sasa, hilo ni vigumu kusema jambo hilo, bali ni kweli. Tunajikuta katika barabara mbili mbalimbali; moja iendayo upande mmoja, nyingine upande mwingine. Sasa hebu tuone Kweli ni nini.

----
Pia tuna mawazo mawili ya hii Ndoa na Talaka. Sasa, kwamba, Bwana wetu ametufungulia siri ya Mihuri Saba ya Neno Lake, katika siku hizi za mwisho. Sasa, wengi wenu, hii huenda ikawa ni Kiyunani kwenu, bali kanisa langu linafahamu. Kwa kitu gani? Nawe umesikia habari za maono na yale yaliyotukia. Na swali hilo ni swali la Biblia, tumekaribishwa hapa kuamini lazima kuwepo na jibu la kweli kwa siri yote nzima iliyofichwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Na Biblia inatabiri na kusema ya kwamba katika siku hii siri hizi zingefunuliwa. Ufunuo 10, “Na malaika wa saba atakapopiga baragumu, mjumbe wa Laodikia, siri za Mungu zingefunuliwa.” Na huu ndio wakati wa mwisho, ambao ni Laodikia.

----
Yesu, katika somo letu, anatualika kurudi nyuma mwanzoni, kwa jibu la kweli la Kimaandiko. Sasa, wakati alipokabiliwa na jambo hili, kulikuwa na mambo mawili yaliyoonekana. Makuhani walimwambia, “Je, mwanamume anaweza kumwacha mkewe, aoe mwingine, kwa sababu yoyote?” Naye Yesu akasema, “Haikuwa hivyo tangu mwanzo.” Ndipo wao wakasema, “Musa alituruhusu kumpa hati ya talaka na kumwacha kwa lo lote walilotaka.” Yeye akasema, “Kwamba, Musa alifanya hivyo kwa sababu,” ninaachilia hilo lishike kidogo, “kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu; lakini tangu, au mwanzoni haikuwa hivyo.” Swali!

Kama Yesu alisema, “Rudini hapo mwanzo,” kulikuwako na jozi moja tu ya cho chote duniani. Kulikuwako na Adamu mmoja, Hawa mmoja, waliunganishwa na Mungu peke yake. Farasi mmoja jike, mmoja dume; kasuku mmoja wa jike, mmoja wa kiume. “Hapo mwanzo,” kama alivyotuambia turudi, kulikuwa na jozi moja tu ya chochote. Hiyo ni kweli? Basi, tunaona sasa kwamba kila kitu hapo “mwanzo” kilikuwa kikienda katika kanuni timilifu na upatano na Mungu, hakuna kitu kilichokuwa nje ya mpangilio. Kila kitu mbinguni bado kiko katika utaratibu; nyota zote, jamii ya nyota, mfumo wa jua, kila kitu kiko katika utaratibu kikamilifu. Moja yao ikisogea, itakatiza mpango wote.

Sasa sikilizeni. Mnaona? Katizo moja huharibu mpango wote! Sasa, wakati wanadamu walipokuwa wakiendelea na mwendo pamoja na Mungu, pamoja na mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, mwanamke huyu alitenda dhambi na hilo lilitupilia mbali mpango wote wa duniani kwa mwendelezo pamoja na Mungu. Kwa hiyo, neno moja lililoongezwa kwenye Kitabu hiki, ama Neno moja lililoondolewa Kwake, linamtupa Mkristo nje ya mwendelezo pamoja na Mungu, linatupa kanisa nje ya mwendelezo pamoja na Mungu, linatupa familia nje ya mwendelezo pamoja na Mungu. Kila mwamini anaweza kutupwa nje, kwa kutokukubali kila Neno la Mungu.

----
Sasa, wakati huo mwanamume alifanywa kumtawala mwanamke, kwa Neno la Mungu. Hakuwa sawa naye tena. Alikuwa sawa katika maumbile, mwajua; lakini, wakati alipolivunja Neno la Mungu, Mungu alimfanya mwanamume awe mtawala juu yake. Mwanzo 3:16, ukitaka kuliandika. Hakuwa sawa tena na mwanamume. Yeye alikuwa mvunjaji wa Neno la Mungu. Hivi hamwoni, “mwanamke,” yeye, kanisa hapa chini? Mvunjaji wa Neno la Mungu, hilo lilimtupa nje kabisa katika mwendelezo. Na hivyo ndivyo kanisa limefanya, na kutupa mauti ya kiroho juu ya kitu hicho chote. Sasa mtaelewa ni kwa nini ninayagongolea mambo haya kama ninavyofanya. Ni Kweli! Huu ni ukweli wa Biblia.

Angalia, kwa nini alifanya jambo kama hili; mwanamke huyo wa kupendeza, mrembo, mkamilifu angewezaje? Niliona picha wakati mmoja, ninaamini ilikuwa huko Ugiriki, ya msanii aliyechora picha ya Hawa. Alikuwa kitu cha kutisha sana ulichowahi kuona. Hiyo inaonyesha kile mtu wa kimwili awezacho kuangalia. Lakini, yeye hakuwa; alikuwa mrembo, maana alikuwa ni mwanamke mkamilifu, mwanamke wote.

Angalia, kwa nini alifanya jambo hilo, akiwa katika hali hiyo ya hali ya juu? Alikuwa sawa na mwanamume, sawa naye. Lakini sote tunajua sasa ya kwamba alipoteza usawa wake na mwanamume, wakati alipotenda dhambi, na Mungu akasema, “Mwanadamu atakuwa mtawala wako tangu hapa na kuendelea.” Sasa, hayo ni Maandiko. Kama mkitaka, tungeweza kulisoma. Ninawapa Maandiko, kwa hiyo kuokoa wakati kwa ajili ya mawasiliano haya makubwa kote nchini, mpate kuyasoma wenyewe.

Angalia sababu ya yeye kufanya hivyo. Shetani alimpataje? Je! Ulijua Shetani alikuwa sawa na Mungu siku moja? Hakika alikuwa, kila kitu isipokuwa muumba; Yeye alikuwa kila kitu, alisimama kwenye mkono wa kuume wa Mungu, Mbinguni, yule Kerubi mkuu aliyeongoza. Angalia sababu ya yeye kufanya jambo hili, yeye hakuwa katika uumbaji wa asili. Yeye hayuko katika uumbaji wa asili wa Mungu; yeye ni kitu kingine. Kwa hiyo, “hapo mwanzo,” kama Yesu alivyorejea kwake, yeye hakuwa kiumbe asili cha uumbaji wa Mungu. Yeye ametoka kwa mwanamume, wakati Yesu aliporejea kwa hilo “hapo mwanzo.”

-----
Sasa juu ya Ndoa Na Talaka, mnaona, haina budi kufunuliwa. Mpaka itakapofunuliwa, huijui. Lakini Yeye aliahidi katika siku hizi za mwisho, katika wakati huu, ya kwamba kila siri iliyofichwa katika Biblia ingefunuliwa. Ni wangapi wanaojua jambo hilo? Ufunuo, mlango wa 10! Yesu aliahidi jambo hilo, ya kwamba siri hizi zote zilizofichwa juu ya—juu ya Ndoa na Talaka, siri hizi zingine zote zilizofichwa, zingefunuliwa katika wakati wa mwisho. Sasa mnakumbuka, ile Sauti ilisema, “Nenda Tucson.” Kumbukeni ile Nuru ya kisiri angani; yule Malaika wa saba amesimama pale; kurudi, na kule kufunguliwa kwa ile Mihuri Saba? Angalia kilichotukia. Hiyo ni kweli.

-----
Hili ni jambo zito mno, sikujua jinsi ya kulieleza. Nitafanya nini, na huku nina wanaume na wanawake wanaoketi kwenye kusanyiko langu, baadhi yao wameolewa na kuoa mara mbili au mara tatu? Wanaume wazuri na wanawake wazuri, wote wamechanganyikiwa! Ni kitu gani kilichofanya jambo hilo? Mafundisho ya uongo, bila shaka, bila ya kumngojea Bwana.

“Aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.” Sio aliowaunganisha mwanadamu; aliowaunganisha “Mungu”! Unapopata ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu, huyo ni mkeo, na jambo lile lile, huyo ni wako maishani mwako mwote. Mnaona? Lakini aliowaunganisha mwanadamu, mtu ye yote anaweza kuwatenganisha. Lakini aliowaunganisha Mungu, mwanadamu ye yote asithubutu kuwagusa. “Kila anaowaunganisha Mungu,” Yeye alisema, “mwanadamu asiwatenganishe.” Sio wale waliounganishwa na hakimu fulani aliyelewa nusu au na kitu kingine, au mchungaji fulani aliyerudi nyuma akiwa na tita la kanuni za imani katika kitabu, ambaye angewaruhusu kufanya kitu cho chote ulimwenguni, na Neno la Mungu likiwa limekaa pale pale. Mnaona? Ninazungumza juu ya kile Mungu alichounganisha pamoja.

-----
Juzijuzi, nikijua kwamba ninapowaambia kitu cho chote, lazima kije BWANA ASEMA HIVI, basi nilikuwa na Maandiko kama Yeye alivyonifunulia. Lakini, “Bwana Mungu, naweza kuliambia kusanyiko hilo nini? Nitasababisha watu kuachana. Wanaume watakuwa wameketi sebuleni na nje uwanjani, na kila mahali penginepo, 'Nimwache?' Wanawake, 'Nimwache mume wangu?' 'Nifanye nini?'” Nikasema, “Bwana, nifanye nini?”
Kitu fulani kiliniambia, “Nenda kule mlimani, nami nitazungumza nawe.”

Na wakati nilipokuwa kule juu mlimani, bila kujua ya kwamba kule chini Tucson walikuwa wanaiona hiyo. Lakini hata waalimu waliwaita watoto toka...msichana wangu mdogo na wengineo, toka darasani, kasema, “Angalieni kule mlimani! Kuna Wingu la moto lenye sura ya kaharabu linapaa angani na kushuka chini, linapaa juu angani na kushuka chini.”

Bibi Evans, uko hapa? Ronnie, wewe uko hapa? Nikashuka nikarudi kwenye kile kituo, huyu mvulana kwenye kituo cha mafuta, kituo cha mafuta cha Evans pale. Na kabla sijajua ambacho yule mvulana anataka kusema, alinishangaza, akasema, “Ndugu Branaham, ulikuwa kule mlimani, sivyo?”
Nikasema, “Unamaanisha nini, Ronnie? La,” unaona, kuona atafanya nini. Mara nyingi vitu hutukia, mimi siwambii, huwaambii watu. Ikawa ... Jambo ni kwamba, unaona mengi sana yakitukia, inakuwa ni jambo la kawaida kwako. Mnaona? Siwaambii tu watu. Nikasema, “Ronnie, ulikuwa nini...”
Akasema, “Ninaweza kukuonyesha mahali ulipokuwa.” Kasema, “Nilimwita mama, nasi tukasimama hapa na kuangalia Wingu hilo likining'inia kule juu, likipanda juu na kushuka. Nikasema, 'Haina budi kuwa ni Ndugu Branham anayeketi kule juu mahali fulani. Huyo ni Mungu akinena naye.'”
Na mji mzima, watu, waliliangalia. Katika siku yenye kung'aa bila mawingu mahali po pote hata kidogo, huku Wingu hili kubwa la kaharabu likining'inia pale; likishuka chini kama mfereji, na kurudi na kuenea.

-----
Sasa tunakutwa katika mchafuko huu kwa sababu ya theolojia iliyofafanuliwa vibaya. Hiyo ni kweli? Hiyo ndiyo sababu ninyi wanawake mmeolewa mara ya pili, nanyi wanaume, kwa sababu ya theolojia iliyofafanuliwa vibaya. Sasa nataka kuwaonyesha jambo fulani ambalo Yeye aliniambia. Na kama Mungu, Muumba wetu, aliulizwa hilo swali alipokuwepo hapa duniani, Yesu Kristo; na wakati nabii wake wa kukomboa alipokuja, Musa, huko chini Misri, kuwatoa wale wana kutoka Misri, kuwaweka kwenye nchi ya ahadi; na Yesu alisema hapa kwamba Musa aliwaona watu katika hali hii, naye akawapa hati ya talaka, kwa sababu hali ilikuwa vile alivyokuwa. Musa aliyakuta hayo, kama, “Na amwache...” Mungu alimruhusu Musa, Yule nabii aliyetumwa kwa hao watu, kuwapa hii hati ya talaka.

Na katika Wakorintho wa Kwanza, mlango wa 7, kifungu cha 12 na 15, katika nabii wa Agano Jipya, Paulo, ambaye alikutana na jambo lile lile kanisani, na kunena jambo hili, “Huyu ni Mimi, si Bwana.” Hiyo ni kweli? Kwa sababu ya hali za talaka.
“Haikuwa hivyo tangu mwanzo.” Lakini Musa aliruhusia, naye Mungu akalitambua kuwa ni haki. Na Paulo pia alikuwa na haki, wakati alipolipata kanisa lake katika hali hiyo.

Sasa mnaamini Hili kuwa ni kweli, na mnaamini linatoka kwa Mungu! Na kwa udhihirisho wa Wingu Lake na Ujumbe Wake ambao umenifikisha umbali huu, je, Mungu huko mlimani asingeniruhusu mimi kutenda jambo lile lile, kuwaruhusu ninyi mwendelee jinsi mlivyo, na msitende jambo hilo tena! Nendeni na wake zenu mkaishi kwa amani, kwa maana wakati umechelewa. Kuja kwa Bwana kumekaribia. Hatuna wakati wa kuvunja mambo haya. Usithubutu kujaribu kufanya jambo hilo tena! Ninazungumza na kusanyiko langu tu. Lakini kama umeoa... Na Mungu alinishuhudia kuhusu jambo hilo, kule mlimani, kwamba ningeweza kunena jambo Hili, ufunuo wa kiroho, kwa sababu ya kule kufunguliwa kwa zile Muhuri Saba, na hili ni swali katika Neno la Mungu. “Waacheni waendelee jinsi walivyo, wasitende dhambi tena!”

“Haikuwa hivyo tangu mwanzo.” Hiyo ni kweli, haikuwa hivyo, na haitakuwa mwishoni. Lakini katika hali za kisasa, kama mtumishi wa Mungu... Sitajiita mwenyewe nabii Wake; lakini ninaamini pengine, kama nisingepelekwa kwa ajili ya jambo hilo, ninaweka msingi kwa ajili yake huyo ajapo. Kwa hiyo chini ya hali za kisasa, ninakuamuru uende nyumbani kwako, pamoja na mke wako sasa. Kama una furaha naye, ishi naye, walele watoto wako katika maonyo ya Mungu. Lakini Mungu na akurehemu kama ukifanya hivyo tena! Wafundisheni watoto wenu wasije wakafanya jambo kama hilo, waleeni katika maonyo ya Mungu. Na sasa kwa kuwa mko jinsi mlivyo, hebu twendeni sasa, katika majira ya jioni yaliyochelewa ambamo tunaishi, na “tukaze mwendo tuifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu katika Kristo,” ambapo mambo yote yatawezekana.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Ndoa Na Talaka.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

   Maandiko Anasema...

akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

Mathayo 19:5-6



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Sirs, is this the time?

(PDF) Mlima Sunset.
Ambapo wingu ilionekana.

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)

Chapter 11
- The Cloud.

(PDF Kiingereza)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)