Kuchaguo Bibi-arusi.

<< uliopita

ijayo >>

  Kutembea kwa Kikristo mfululizo.

Uchaguzi ni jambo kuu.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kuchaguo Bibi-arusi.

Sasa katika ile aya ya 9 ya sura ya 21 ya Ufunuo.
Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.

Katika mambo mengi ya maisha tumepewa uchaguzi. Njia ya maisha, yenyewe, ni uchaguzi. Tunayo haki ya kufanya njia yetu wenyewe, kuchagua njia yetu tunayotaka kuishi. Elimu ni uchaguzi. Tunaweza kuchagua kama tutaelimishwa, ama kama hatutaelimishwa. Huo ni uchaguzi tulio nao. Jema na baya ni uchaguzi. Kila mwanamume, kila mwanamke, mvulana na msichana, hana budi kuchagua kama watajaribu kuishi kwa usahihi ama kutoishi kwa usahihi. Ni uchaguzi. Uchaguzi ni jambo kuu.

Kikomo chako wa Milele ni uchaguzi. Na labda, usiku huu, baadhi yenu mtafanya huo uchaguzi, mahali ambapo mtaishi Umilele, kabla ibada hii haijaisha usiku huu. Kutakuwako na wakati mmoja, ambapo, kama ukimkataa Mungu mara nyingi, kutakuwako na wakati mmoja utakapomkataa mara ya mwisho. Kuna mstari kati ya rehema na hukumu. Na ni jambo la hatari kwa mwanamume ama mwanamke, mvulana ama msichana, kuvuka huo mstari, kwa kuwa hakuna kurudi wakati unapovuka mstari huo wa mwisho. Kwa hiyo, usiku huu, huenda ikawa ndio wakati ambapo wengi watafanya uamuzi wao—wao, pale ambapo wataishi Umilele isiyo na mwisho.

Kuna uchaguzi mwingine tulio nao maishani, huo ni, mwenzi wa maisha. Kijana mwanamume au kijana mwanamume, anayeingilia maisha, amepewa haki ya kuchagua. Mvulana huchagua. Mwanamke kijana ana haki ya kuikubali ama kuikataa. Lakini bado ni uchaguzi, pande zote mbili. Wote wawili mwanamume na mwanamke, wanayo haki ya kuchagua. Pia, unao uchaguzi, kama Mkristo.

Una uchaguzi wa kanisa, hapa Amerika, kufikia sasa, ambalo unaweza kwenda. Hayo ni majaliwa yako ya Kiamerika, kujichagulia kanisa lo lote unalotaka kuwa mshirika wake. Huo ni uchaguzi. Si lazima uhudhurie lolote la hayo, kama hutaki. Lakini kama unataka kubadilisha kutoka Methodisti kuingia Baptisti, au Katoliki kuingia Protestanti, au chochote kile, hakuna mtu anayeweza kukwambia ama kukufanya uhudhurie kwenye kanisa fulani. Huo ndio uhuru wetu. Hivyo ndiyo demokrasia yetu ilicho. Kila mtu anaweza kujichagulia mwenyewe. Uhuru wa dini, na hilo ni jambo kuu. Mungu na atusaidie kulidumisha kadiri tuwezavyo.

Unao uchaguzi pia. Kama… Unapochagua kanisa hili, unaweza kuchagua kama wewe, katika kanisa hili, kama utachagua kanisa litakalokuongoza kwenye kikomo chako cha Milele. Unaweza kuchagua kanisa ambalo lina kanuni fulani ya imani, hata ukawaza kwamba kanuni hizo za imani ndizo kile unachokitaka hasa. Ama, kanisa lingine lililo na kanuni zao za imani. Na kisha kuna Neno la Mungu, una uchaguzi kwake. Huna budi kufanya uchaguzi. Kuna sheria isiyoandikwa miongoni mwetu, ya kuchagua.

Naamini ilikuwa ni Eliya, wakati mmoja, kule juu ya Mlima Karmeli, baada ya lile shindano la kuamua, katika saa kuu ya hatari sana ambayo tunakaribia sasa hivi. Labda, huenda ikawa kwako au kwangu, usiku huu, kwamba tufanye uchaguzi huu, kama lile tukio la Mlima Karmeli. Kusema kweli, nafikiri linaendelea, ulimwenguni kote, sasa. Lakini hivi karibuni kutakuwa na wakati ambapo itakulazimu kufanya uchaguzi.

Na ninyi watu hapa, wa makanisa yenu ya kidhehebu, aminini tu hili, kwamba saa imewadia, mtakapochagua. Ama mtaingia kwenye Baraza la Ulimwengu, au hamtakuwa dhehebu tena. Itawabidi kufanya hivyo, na huo uchaguzi unakuja hivi karibuni. Na ni jambo la hatari kungojea mpaka saa hiyo ya mwisho, pia, kwa sababu huenda ukachukua kitu ambacho kamwe usingeweza kujiondoa kwake. Unajua, kuna wakati ambapo unaweza kuonywa, kisha, kama ukivuka huo mstari wa onyo, basi tayari umetiwa alama upande ule mwingine, kupigwa chapa.

Kumbuka, wakati mwaka wa yubile ulipofika, na kuhani akaondoka akipiga baragumu yake, kwamba kila mtumwa angeweza kuwa huru. Lakini kama walikataa kukubali uhuru wao, ndipo ilimpasa apelekwe hekaluni, penye kizingiti, na kutobolewa sikio kwa uma, kisha akamtumikia bwana wake daima. Ilitiwa kwenye sikio lake kama mfano, wa kusikia. “Imani huja kwa kusikia.” Yeye alisikia hiyo baragumu, bali hakutaka kuisikiliza.

Na mara nyingi, wanaume na wanawake husikia Kweli ya Mungu, na kuiona ikithibitishwa na kuhakikishwa, Kweli, lakini hata hivyo hawataki kuisikia. Kuna sababu nyingine. Kuna uchaguzi mwingine walio nao, kuliko kukabiliana na ile Kweli na kweli za mambo, kwa hiyo masikio yao yanaweza kufungwa yasisikie Injili. Hawataisikia tena kamwe. Ushauri wangu kwenu, Mungu anaponena na moyo wako, tenda mara moja wakati huo.

Eliya aliwapa uchaguzi, ambao wangepaswa kufanya: “Chagueni hivi leo mtakayemtumikia. Mungu akiwa ndiye Mungu, mtumikieni. Lakini ikiwa Baali ni Mungu, mtumikieni.”

Sasa, tunapoona kwamba mambo yote ya kawaida ni mfano wa mambo ya kiroho, kama tulivyopitia katika somo letu asubuhi ya leo, kama jua na tabia zake. Hayo yalikuwa ndiyo Biblia yangu ya kwanza. Kabla sijawahi kusoma hata ukurasa mmoja katika Biblia, nilimjua Mungu. Kwa sababu, Biblia imeandikwa kila mahali katika maumbile, na yanalingana tu na Neno la Mungu: jinsi ambavyo kifo, kuzikwa, kufufuka kwa maumbile; na jua likichomoza, likipita, likitua, likifa, likichomoza tena. Kuna mambo mengi sana ambayo tungeweza kuyafananisha, Mungu katika maumbile, ambayo hatuna budi kuyaruka, kwa ajili ya Ujumbe huu.

Sasa, kama yale ya kiroho, au, yale ya kawaida ni mfano wa yale ya kiroho, basi, kuchaguwa bibiarusi, katika yale ya kawaida, ni mfano wa kuchagua Bibi-arusi, yule Bibi-arusi, katika kiroho. Sasa, ni jambo zito sana tunapoenda kuchagua mke, mwanamume, kwa kuwa nadhiri hapa ni mpaka kifo kitakapotutenganisha. Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuidumisha. Nawe unaweka hiyo nadhiri mbele za Mungu, kwamba mauti pekee yatakayowatenganisha. Nami nafikiri tunapaswa... Mtu mwenye akili timamu, anayepanga maisha yake ya usoni, kwamba anapaswa kumchagua mke huyo kwa uangalifu sana. Uwe mwangalifu kwa yale unayofanya. Na mwanamke anayemchagua mume, ama anayekubali uchaguzi wa mume, anapaswa kuwa mwangalifu sana kwa yale anayofanya, na hasa katika siku hizi. Mwanamume anapaswa kuwaza na kuomba kabla hajamchagua mke.

Nafikiri, leo hii, iliyo na visa vingi sana vya talaka sasa, kwamba tunaongoza ulimwenguni huku Amerika, katika visa vya talaka. Tunaongoza ulimwengu wote. Kuna talaka nyingi hapa kuliko mahali pengine popote, taifa hili, na linasemekana kuwa, na kudhaniwa, kuwa taifa la Kikristo. Ni aibu jinsi gani, mahakama zetu za talaka! Nafikiri, sababu yake, ni kwa sababu wanaume wamemwacha Mungu, na wanawake wamemwacha Mungu.
Nasi tunaona, kwamba, kama mwanamume aliomba na mwanamke akaomba juu ya jambo hilo; si tu kuangalia macho marembo, ama mabega makubwa yenye nguvu, ama vitu kama hivyo, ama mapenzi mengine ya kilimwengu; bali angemtazama Mungu kwanza, na kusema, “Mungu, je! huu ndio mpango Wako?”

-----
Na kama tungechunguza yale tunayofanya wakati tutakapoenda kuoana, tunapomchagua wake zetu, waume wetu, laiti tungeyachunguza kwa makini! Mwanamume anapaswa kuomba kwa bidii, kwa kuwa angeweza kuangamiza maisha yake yote. Kumbukeni, nadhiri ni “mpaka kifo kitakapotutenganisha,” naye angeweza kuyaharibu maisha yake kwa kufanya uchaguzi mbaya. Lakini kama anajua ni nini, anachagua vibaya na anaoa mwanamke asiyefaa kuwa mke wake, naye anafanya hivyo haidhuru, basi ni kosa lake. Kama mwanamke akimchukua mume na anajua ya kwamba yeye hastahili kuwa mume wako, basi hilo ni kosa lako mwenyewe, baada ya kujua yaliyo mema na mabaya. Hivyo, hupaswi kufanya hivyo mpaka uombe kwa bidii kabisa.

Vivyo hivyo katika kuchagua kanisa. Sasa, huna budi kuliombea kanisa unamoshiriki. Kumbuka, makanisa huwa na roho. Sasa, sitaki kuwa mkosoaji. Lakini natambua kwamba mimi ni mzee, nami sina budi kuondoka hapa, mojawapo ya siku hizi. Na inanipasa kuwajibika kwenye Siku ya Hukumu kwa yale ninayosema usiku huu ama wakati mwingine wowote. Nami, kwa hiyo, sina budi kuwa mkweli kabisa na kushawishika kweli.

Lakini, unaingia kanisani, na kama utaangalia tabia ya hilo kanisa, hebu mwangalie tu mchungaji kwa muda kidogo, na mara nyingi utaona ya kwamba kanisa linatenda kama mchungaji wake. Wakati mwingine, nashangaa kama hatupati roho wa mwingine badala ya Roho Mtakatifu. Unafikia mahali ambapo mchungaji ni mtu wa mapinduzi kweli kwlei na kadhalika, utaona kusanyiko liko vivyo hivyo. Nitawaleta kwenye kanisa ambapo nimeona mchungaji akisimama, wakitikisa vichwa vyao huku na huko. Wewe liangalie kusanyiko, wanafanya jambo lile lile. Mchukue mchungaji, anayemeza tu kila kitu kwa pupa, kwa kawaida kanisa litafanya jambo lile lile. Hivyo, kama nilikuwa nachagua kanisa, ningechagua kanisa halisi, la kimsingi, linaloamini Injili Yote, kanisa la Biblia, kama ningelikuwa nachagua moja la kuingiza familia yangu. Chagua.

-----
Tena, aina ya mwanamke ambaye mwanamume angemchagua, itaonyesha matamanio yake na tabia yake. Kama mwanamume akimchagua mwanamke asiyefaa, inaonyesha tabia yake. Na kile anachojifunganisha nacho, kinaonyesha kilicho ndani yake kweli. Mwanamke huonyesha kile kilicho ndani ya mwanamume anapomchagua kuwa mke wake. Inaonyesha kile kilicho ndani yake. Haijalishi analosema huko nje, tazama alichooa.

Naenda kwenye ofisi ya mtu fulani, naye anasema yeye ni Mkristo; picha zimebandikwa kote ukutani, ule muziki wa rumba ukiendelea. Sijali yeye anasema nini. Siamini ushuhuda wake, kwa sababu roho yake inakula vitu hivyo vya ulimwengu. Vipi, tuseme, kama angeoa msichana mwimbaji wa bendi, ama vipi kama angeoa kipusa wa watu, ama mrembo tu, mhuni mamboleo? Inaonyesha. Inaonyesha kile alicho nacho katika nia yake, jinsi nyumba yake ya baadaye itakavyokuwa, kwa sababu amemchukua kusudi akawalee watoto wake kwake. Na chochote alicho mwanamke huyo, hivyo ndivyo atakavyowalea hao watoto. Kwa hiyo, inaonyesha kile kilicho ndani ya mwanamume huyo. Mwanamume anayemchukua mwanamke kama huyo, anaonyesha tu kile anachowazia juu ya siku za usoni.

Ungeweza kuwazia Mkristo akifanya jambo kama hilo? La, bwana. Nisingewaza. Mkristo wa kweli hatawatafuta vipusa kama hao, na wasichana waimbaji wa bendi, na vidosho wa watu. Yeye atatafuta tabia ya Kikristo.

Sasa, basi, tunapogeukia sasa kwa muda mfupi, kwenye upande wa kiroho. Na wakati unapoona kanisa ambalo liko ulimwenguni, likitenda kama ulimwengu, likitazamia ulimwenguni, likishiriki ya ulimwengu, likizihesabia Amri za Mungu kana kwamba kamwe Yeye hakuziandika, ndipo unaweza tu kuwazia kwamba Kristo hataenda kumchukue Bibi-arusi kama huyo. Je, ungeweza kuwazia kuchukuliwa kwa hili kanisa la kisasa leo hii kama Bibi-arusi? Si Bwana wangu. Mimi si... Ni vigumu kwangu kuona hilo. Hapana. Kumbuka, sasa, mwanamume na mkewe ni mmoja. Je! Ungelijiungamanisha mwenyewe na mtu kama huyo? Kama ungelifanya hivyo, bila shaka kwa namna fulani lingelivunja imani yangu kwako.

Na, basi, vipi kuhusu Mungu kujiunganisha na kitu kama hicho, kahaba wa kawaida wa kidhehebu? Mnafikiri angefanya hivyo, “Wenye mfano wa utauwa lakini wakikana nguvu zake”? Yeye hangefanya hivyo kamwe. Hana budi kuwa na tabia Yake ndani yake. Kanisa halisi, la kweli lililozaliwa mara ya pili halina budi kuwa na ile tabia iliyokuwa ndani ya Kristo, kwa sababu mume na mke ni mmoja. Na kama Yesu alifanya tu yale yaliyompendeza Mungu, akalitimiza Neno Lake na kulidhihirisha Neno Lake, itampasa Bibi-arusi Wake kuwa wa tabia ya aina ile ile. Bibi-arusi asingeweza, kwa vyo vyote vile, kuwa dhehebu. Kwa sababu, basi, haidhuru ni kiasi gani unataka kusema, “hapana,” hilo linaongozwa na halmashauri mahali fulani, ambayo huliambia litende nini na lisitende nini, na, mara nyingi, huwa umbali wa maili milioni moja kutoka kwenye Neno la kweli.

Ni vibaya sana kwamba tuliondoka kwa yule Kiongozi halisi ambaye Mungu alituachia kuliongoza Kanisa. Yeye kamwe hakuwatuma wazee wa jimbo. Yeye kamwe hakutuma maaskofu, makadinali, makasisi, mapapa. Yeye alimtuma Roho Mtakatifu kwa ajili ya Kanisa, kuliongoza Kanisa. “Wakati Yeye Roho Mtakatifu atakapokuja, atawaongoza katika Kweli yote, awafunulie mambo haya, ambayo nimewaambia, atawakumbusha, na kuwaonyesha mambo yajayo.” Roho Mtakatifu alikuwa afanye hivyo. Sasa, kanisa la kisasa linamchukia Huyo. Hawamtaki Huyo, kwa hivyo lingewezaje kuwa Bibi-arusi wa Kristo? Watu wa siku hizi wanachagua dhehebu la kisasa. Linachofanya, linaonyesha tu ufahamu wao duni wa Neno.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Kuchaguo Bibi-arusi.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

Kumbukumbu la Torati 30:19


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Ndoa na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu.
(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)

As the Eagle
Stireth her nest.

(PDF Kiingereza)

Chapter 14
- Sabino Canyon

(PDF Kiingereza)


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.