Vita vikuu sana vilivyowahi kupiganwa.

<< uliopita

ijayo >>

  Kutembea kwa Kikristo mfululizo.

Uwanja wa vita. Akili ya mwanadamu.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Vita vikuu sana vilivyowahi kupiganwa.

Naam, kabla ya vita vyo vyote kupangwa, yabidi kwanza wachague mahali pa kukabiliana, au mahali ambapo vita vitapiganiwa, mahali palipochaguliwa. Katika Vita Vikuu vya Kwanza vya dunia, vilipangwa vizuri sana, katika ardhi isiyo ya mtu na mahali ambapo wangepigania, Na yabidi pawepo na mahali palipochaguliwa.

Kama vile wakati Israeli walipopigana vita na Wafilisti, kulikuweko na kilima kila upande walikokusanyika. Na hapo ndipo Goliathi alipotoka na kuyaita majeshi ya Israeli. Hapo ndipo Daudi alipokutana naye, bondeni, wakati alipopita kwenye kijito kidogo kilichopita katikati ya vilima viwili, aliokota mawe.

Hapana budi pawe na mahali palipochaguliwa. Na katika hili, kuna mahali palipokubalika na pande zote, ardhi isiyo ya mtu, nao wanapigana mahali hapa. Wao hawafanyi hivyo, hawapigani vita moja hapa, na moja chini hapa, na mmoja hukimbia huku. Kuna uwanja wa vita ambapo wanakutana na kujaribu nguvu zao, ambapo kila jeshi hujaribu nguvu zake dhidi ya jeshi lingine, mahali pa kukutania. Sasa, (msipate) kukosa hili.

Wakati vita hivi vikubwa vilipoanza duniani, ilibidi kuwe na mahali pa kukutania. Ilibidi pawepo mahali palipochaguliwa pa kuanzia vita, na kwa vita kuwaka moto. Na sehemu hizo za vita zinaanzia katika nia ya mwanadamu. Hapo ndipo vita vinapoanza. Akili ya binadamu ilichaguliwa kuwa uwanja wa vita, ambapo vilipaswa kuanzia, na hiyo ni kwa sababu kwamba maamuzi hufanywa kwenye akili, kichwani. Sasa, kamwe hawakuanzisha jambo hilo kutoka kwenye madhehebu fulani. Kamwe hawakuanzisha jambo hilo kutokana na jambo fulani la kimitambo. Uwanja wa mapambano haukuanza hapo kamwe. Kwa hiyo, madhehebu hayo hayawezi kamwe, hayawezi kamwe kufanya kazi ya Mungu, kwa sababu mahali pa mapambano, ambapo inakubidi kukabiliana na adui wako, ni katika akili. Huna budi kufanya chaguo lako. Vinakukabili.

Maamuzi hufanywa akilini, kichwani. Hapo ndipo Shetani anakabiliana nawe, na maamuzi hutolewa, kwa sababu Mungu alimfanya mtu jinsi hiyo. Sasa, nina (kama ulikuwa ukiangalia kwenye muhtasari wangu hapa) ramani ndogo iliyochorwa. Nilikuwa nayo hapa si muda mrefu uliopita, kwenye... iliyotumiwa kwenye ubao. Mwanadamu ameumbwa tu kama punje ya ngano. Ni mbegu. Na mwanadamu ni mbegu. Kimwili, wewe ni uzao wa baba yako na mama yako; na uhai unatoka kwa baba, nyama ya mwili hutoka kwa mama. Kwa hiyo, hizo mbili, pamoja, yai na ile damu, zinakutana. Na katika chembechembe ya damu kuna uhai. Ma mle ndani huanza, kukua kumfanyiza yule mtoto.

Sasa, mbegu yo yote ina ganda upande wa nje; upande wa ndani ni nyama, na ndani ya nyama ni chembe ya uhai. Vema, hivyo ndivyo tulivyoumbwa. Sisi ni mwili, nafsi, na roho. Sehemu ya nje ya mwili, ganda; ndani ya huo, dhamira na kadhalika, ni nafsi; na ndani ya nafsi, ni roho. Na roho inatawala mengine yote.

Sasa, kama utaketi chini utakapofika nyumbani, na kuchora duara tatu ndogo. Utaona kwamba mwili wa nje una hisi tano ambazo huwasiliana kwazo, na hizo ni kuona, kuonja, kuhisi, kunusa, kusikia. Hizo ndizo hisi tano zinazoongoza mwili wa binadamu. Ndani ya mwili ni nafsi, na hiyo nafsi inaongozwa na mawazo, dhamira, kumbukumbu, hoja, na upendo. Hicho ndicho kitu ambacho huongoza nafsi.

Lakini, roho, ina hisi moja tu. Roho... Loo, hebu na tulipate. Roho ina hisi moja, na hisi hiyo aidha inaongozwa, na imani au shaka. Hiyo ni kweli kabisa. Na kuna njia moja tu kwake, hiyo ni uhuru wa kuchagua. Unaweza kukubali shaka au unaweza kukubali imani, mojawapo unayotaka kufanya kazi nayo. Kwa hiyo, Shetani alianzia sehemu hiyo muhimu, kusababisha roho ya binadamu kushuku Neno la Mungu. Mungu alianzia sehemu hiyo muhimu kuweka Neno Lake katika roho ile. Haya basi. Hilo ndilo linalofanya jambo hilo.

Kama kanisa hili, sasa hivi lingeweza kuwekwa pamoja, na kuunganishwa pamoja kwa kitu kama hicho ili kwamba kila mtu awe katika moyo mmoja, bila ya shaka hata kidogo po pote, pasingekuwa na mtu mnyonge miongoni mwetu, katika dakika zingine tano. Kusingekuwa na mtu ye yote hapa anayehitaji Roho Mtakatifu ila ambaye angempokea Huyo, kama mngeweza tu kutengeneza hilo jambo fulani. Sasa, hapo ndipo vita huanza, moja kwa moja mawazoni mwako, kama ukitaka.

Sasa kumbukeni,si Sayansi ya Kikristo, sasa, akili juu ya maumbile ya asili. Hilo halina... Akili hupokea Uzima, ambao ni Neno La Mungu, na hapo huleta Uzima. Wazo lako tu halifanyi hivyo. Lakini, Neno la Mungu, likiletwa katika mkondo wa wazo lako. Mnaona? Siyo wazo, kama Sayansi ya Kikristo inavyolifanya, akili juu ya maumbile ya asili. La. Hilo silo.

Lakini, akili yako inakubali jambo Hilo. Hulishikilia. Akili yako huongozwa na nini? Roho yako. Na roho yako hulinasa Neno la Mungu, na hicho ndicho kitu kilicho na Uzima ndani Yake. Linaleta Uzima ndani yako. Loo, ndugu! Hilo linapotendeka, wakati Uzima hushuka chini kwenye mkondo ule, kuingia ndani yako, Neno la Mungu linadhihirishwa ndani yako. “Ninyi mkikaa ndani Yangu na maneno Yangu yakikaa ndani yenu, basi ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

Basi hilo linafanya nini? Toka katikati ya moyo, ambayo ni nafsi, tokea hapo huenda, kulisha kila mkondo. Shida yake ni kwamba, tunasimama humu ndani tukiwa na shaka nyingi, tukijaribu kukubali yaliyo huko nje. Huna budi kukomesha jambo hilo; na kushuka kwenye mkondo ule na Neno la kweli la Mungu, na ndipo linatoka, lenyewe, bila ya kushurutishwa. Ni kile kilicho ndani. Hicho ndicho kitu cha maana, ni kile cha ndani. Shetani huanza kutukabili kutokea ndani.

Sasa, unasema, “Mimi siibi. Sinywi pombe. Sifanyi mambo haya.” Hilo halina uhusiano wowote nalo. Mnaona, ni mle ndani. Haidhuru wewe ni mzuri iliyoje, ni uadilifu iliyoje, ni mkweli iliyoje, mambo hayo yanaheshimiwa. Lakini Yesu alisema, “Mtu asipozaliwa mara ya pili.” Mnaona? Hapana budi kuwe na jambo fulani linalotukia ndani. La sivyo, hayo ni mambo ya kuigiza, kwani chini ndani ya moyo wako unatamani kutenda jambo hilo kwa vyo vyote. Hakiwezi kuwa cha bandia. Hakina budi kuwa cha halisi.

Na kuna njia moja tu ambayo hicho chaweza kushukia,na hiyo ni kwa njia ya uhuru wa kuchagua, huja katika nafsi, kwa mawazo yako. “Kama vile mtu afikirivyo moyoni mwake, ndivyo alivyo.” Kama ukivambia mlima huu, 'Ng'oka' na usitie shaka moyoni mwako, bali uamini kwamba ulilosema litatukia; litakuwa lako.“ Mnalipata? Haya basi. Mnaona? Huo ndio uwanja wa vita. Kama ungeanza tu hilo, kwanza.

Tuna shauku sana kuona mambo yakitendeka. Tuna shauku sana ya kumfanyia Mungu jambo fulani. Maskini bibi huyu si... anamtamani sana, bila shaka anatamani kuishi Anataka kuwa mzima. Wengine wako hapa, wanataka kupona. Na tunaposikia kuhusu jambo hilo, kama yule daktari, kufufuliwa kwa wafu, mambo makuu ya uweza ambayo Mungu wetu ametenda, basi tunatamani mno. Na jambo ni kwamba, tunajaribu kwa hisi hizi, kushika jambo fulani hapa, kama dhamiri.

Watu wengi, sana mara nyingi, wamekosa kuelewa vema Neno. Nami nimeeleweka vibaya na jambo hili, kwa kufanya miito ya madhabahuni. Nilisema “sishikilii sana miito ya madhabahuni,” simaanishi kwamba hupaswi kutoa mwito wa madhabahuni. Bali mtu fulani anamshika mtu mkono akasema, “Loo, Ndugu Yohana, unajua nini? Mimi na wewe tumekuwa majirani wakati huu wote. njoo huku madhabahuni, piga magoti.” Yeye anafanya nini? Laiti ningalikuwa na ubao hapa, ningeweza kuwaonesha yale anayofanya. Anajaribu kutenda kazi kwa nafsi yake, katika upendo. Hilo halifai kitu. Hiyo siyo ile njia. Hakika, siyo.

Labda yeye anafanya kazi katika (nini?) Kumbukumbu, kupitia hisi ya nafsi yake. “Loo, Ndugu John, ulikuwa na mama mzuri sana. Alikufa muda mrefu uliopita.” Kumbukumbu! Mnaona? Huwezi kufanya hivyo. Halina budi kuja kwa njia ya uhuru wa kuchagua. Wewe, mwenyewe, ruhusu Neno la Mungu... Huji kwa sababu mama yako alikuwa mwanamke mzuri. Huji kwa sababu wewe ni jirani mwema. Unakuja kwa sababu Mungu anakuita uje, nawe unamkubali juu ya msingi wa Neno Lake. Neno hilo ndilo linalomaanisha kila kitu. Hilo Neno! Kama unaweza kuondoa kila kitu njiani, dhamiri yote, hisi zote, na uache tu Neno liingie, Neno hilo litazaa kabisa.

Hapa, mnaona limefunikwa na kitu gani? Unasema, “Vema, sasa,” unasema, “vema, hizi, dhamiri na hisi, na kadhalika, hazina uhusiano wowote nalo, Ndugu Branham?” Hakika zinahusika! Lakini iwapo utaliruhusu Neno liingie na kulifunika na dhamiri, basi haliwezi kukua, litakuwa neno lemavu. Je! uliwahi kuona punje nzuri ya mahindi iliyopandwa ardhini, na kuachia kijiti kiiangukie? Itakua imepinda. Mzabibu wowote, chochote ambacho hukua kitafanya hivyo, kwa sababu kitu fulani kimekizuia.

Vema, hiyo ndiyo shida ya Imani yetu ya kipentekoste leo. Tumeacha mambo mengi sana yaizuie, Imani ambayo tumefundishwa, Roho Mtakatifu ambaye amekuwa akiishi ndani yetu. Tumeachilia mambo mengi sana, tukimwangalia mtu mwingine. Na ibilisi sikuzote anajaribu kukuonesha kushindwa kwa mtu, lakini anajaribu kukuondoa kwenye ushuhuda halisi ambao ni wa kweli. Yeye atakuelekeza kwa mnafiki, wakati fulani, ambaye alitoka akaenda kuiga kitu fulani. Yeye hakufanikiwa, kwa sababu alikuwa anaigiza. Lakini kama linatoka kwenye chanzo halisi cha Neno la Mungu, “Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Langu haliwezi kupita,” halina budi kukaa pale.

Halina budi lipokewe akilini; kisha linaaminiwa kwa moyo. Ndipo Neno la Mungu linakuwa jambo halisi; ndipo kila hisi za nafsi na mwili zinasuguliwa sana kwa Roho Mtakatifu. Ndipo wewe ni hisi ya Mungu; wewe ni dhamiri ya Mungu; kila kitu kinachomcha Mungu kinatiririka kupitia kwako. Hakuna shaka mahali po pote. Hakuna kitu kinachoweza kujiinua.
Hakuna cho chote kinachoweza kuja kwenye kumbukumbu na kusema, “Vema, ninakumbuka Binti Jones alijaribu kumtumaini Mungu na Bibi Fulani. Bibi Doe alijaribu kumtumaini Mungu kwa ajili ya uponyaji, wakati mmoja, naye akashindwa.” Mnaona?
Lakini kama mkondo ule umefagiliwa na kutakaswa, na kujazwa ndani kwa Roho Mtakatifu, hilo hata halikumbukwi, haidhuru kuhusu Bi Jones na yale aliyofanya. Ni wewe na Mungu, pamoja, na si mtu mwingine ila ninyi wawili. Haya basi. Hivyo hapo vita vyako. Muue papo hapo mwanzoni. Mkomeshe kabisa anapokuja. Si unaweza kuendeleza vita muda gani. Ni kuvikomesha sasa hivi!

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Vita vikuu sana vilivyowahi kupiganwa.



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

   Maandiko Anasema...

Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

Kumbukumbu la Torati 30:19


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Ndoa Na Talaka.

(PDF)

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)