Neno kwa kanisa.

<< uliopita

ijayo >>

  Neno lililo hai mfululizo.

Neno kwa kanisa.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
  Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa.


William Branham.

Pendaneni ninyi kwa ninyi zaidi ya yote. Pendaneni ninyi kwa ninyi Msi... Haidhuru kile shetani anachojaribu kusema! Sasa ninyi ni kundi moja kubwa tamu sasa, lakini kumbukeni onyo langu, unaona, Shetani hawezi kuachia hilo lidumu namna hiyo.

Hapana, bwana. Atatupia kila kitu mshale, ikiwa yeye angemleta mtu fulani ndani amfanye lengo lake. Atamleta ndani mtu mkosoaji au asiyeamini, na kumketisha chini, na kumfanya yeye kushiriki pamoja nanyi chini ya utulivu na mambo ya aina hiyo na ndipo atamtupia yule mtu aina fulani ya sumu, naye ataanza kuzunguka nayo kanisani. Msikae upande wake. Msiwe na chochote cha kufanya na kitu kingine chochote. Mdumu kupendana na wema na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi. Mwombeeni yule mtu, kwamba aokolewe vile vile, au yule mwanamke, au yeyote yule awaye, waombeeni tu. Na shikamaneni ninyi kwa ninyi
Na dumuni na mchungaji wenu. Unaona, Yeye ni mchunga kondoo, nanyi mpeni heshima. Yeye atawaongoza hadi mwisho na kwa sababu yeye ameamriwa na Mungu kufanya hivyo.

Sasa mnalikumbuka hilo? [Kusanyiko linasema, “Amina.” -Mh] Adui atakuja. Naye anapokuja. mshikamane tu pamoja kwa karibu zaidi. Na yule ambaye shetani anamtumia kama adui ama atatoka nje ama aingie ndani na kuwa mmoja wenu. Ni hilo tu.

Kamwe msifanye ukoo miongoni mwenu, au-au kuongea na kujifanyia mshikamano wa kiukoo. Sisi ni wamoja. Singesema “Mkono wa kushoto nimekukasirikia, nitakuondoa kwa sababu wewe si wa mkono wa kulia.” Yeye ni mkono wangu wa kushoto. Nataka akae pale. hata ncha ndogo ya kidole changu, nataka ikae pale pale tukae kila mmoja na mwingine, kila mmoja akae kabisa na mwingine.

Na sasa mnazo kanda juu ya hilo. Mnazo kanda juu ya kile tunachoamini. Mnazo kanda juu ya nidhamu kanisani, jinsi tunavyoenenda kwa kujiheshimu katika kanisa la Mungu, jinsi itupasavyo kuja hapa pamoja na kukaa pamoja katika makao ya Kimbinguni. Msikae nyumbani. Ikiwa Mungu yuko moyoni mwako huwezi kusubiri milango ifunguliwe pale, ili uingie hapa kushiriki pamoja na ndugu zako. Kama huwezi, hujisikii namna hiyo, ni wakati wa kwenda kwenye kuomba.

Bila shaka tuko katika siku za mwisho, pale Biblia ilipoinuka... au ilitufundisha kuku, “Zaidi tuonapo ile siku ikiwadia” kumpenda mwingine kwa upendo wa Kikristo na upendo wa Kiungu, 'kukusanyika wenyewe pamoja katika sehemu za Kimbinguni na-na Kristo Yesu,“ na pendaneni ninyi kwa ninyi. Kwa hili watu wote wajue ninyi ni wanafunzi Wangu, mtakapopendana ninyi kwa ninyi.” Hilo ni sahihi. Kaeni pamoja kila mmoja na mwingine.

Kama unafikiri ndugu amekosea kidogo, au dada, sema “Bwana usiniache kamwe shina la uchungu likachipuka kwa sababu ita-itamuathiri Yeye na itamtoa Kristo nje kutoka katika maisha yangu”. Ile sumu ya tindikali ya nia ya kudhuru wengine na wivu, na chuki, hayo yatamtoa tu Roho Mtakatifu atoke kwako. Itamwondoa Yeye hapa Hekaluni. itamuua Roho wa Mungu, au itamwondoa Yeye atoke hapa, kumsononesha mchungaji wenu. Itafanya kila kitu. Unaona? Msifanye hilo.

Mzidi zaidi kushikana tu karibu pamoja. Vuteni... Chukueni kishikizo kama ndugu alivyoshuhudia mhudumu hapa usiku ule, kuhusu kuwa na bakoli akiona kwenye ono. Tu... Hiyo inafunga pamoja silaha zote za Mungu. Hiyo inafunga pamoja tu, kaza, jongeeni karibu zaidi kila mmoja kwa mwingine, pendaneni ninyi kwa ninyi, kwa vyovyote... Zungumzeni mema kila mmoja juu ya mwingine. Semeni mambo mema kila mmoja kuhusu mwingine na ndipo Mungu atawabariki.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
  Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa.


  Neno lililo hai mfululizo.

Sheria ya Mungu ya uzazi.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
  Wakati wa Kanisa la Pergamo.


William Branham.

“Haya ndiyo ninayojaribu kuwaambieni. Sheria ya kuzaa ni kwamba kila jamii izae kwa jinsi yake yenyewe, yaani kulingana na Mwanzo 1:11, “Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi: ikawa hivyo.” Uhai wo wote ule uliokuwemo katika mbegu ulijitokeza katika mmea na baadaye katika tunda. Sheria iyo hiyo inatenda kazi kwa kanisa leo. Mbegu yo yote iliyoanzisha kanisa itamea na kuwa kama ile mbegu ya asili kwa sababu ni mbegu ile ile. Katika siku hizi za mwisho Kanisa la Bibi-arusi wa kweli (mzao wa Kristo) litafikia kwenye Jiwe la Kileleni, nalo litakuwa ni kipeo cha kanisa, mzao bora sana, linapomkaribia Yeye. Wao katika Bibi-arusi watakuwa chapa Yake hivi kwamba watafanana Naye kabisa. Hii ni kusudi wapate kuungana Naye. Watakuwa mmoja. Watakuwa dhihirisho lenyewe la Neno la Mungu aliye hai. Madhehebu hayawezi kuleta hili (wao ni uzao mbaya). Wataleta kanuni zao za imani na mafundisho yao ya sharti, yaliyochanganywa na Neno. Mchanganyiko huu huzaa mzao mchanganyiko.

Yule mwana wa kwanza (Adamu) alikuwa ni mzao_Neno lililonenwa na Mungu. Alipewa bibi-arusi kusudi azaliane. Hiyo ndiyo sababu yeye alipewa bibi-arusi, apate kuzaliana, amzae mwana mwingine wa Mungu. Lakini huyo mwanamke alianguka. Alianguka kwa kuchanganya mbegu. Alisababisha mumewe afe.

Mwana wa pili (Yesu), pia Mzao-Neno lililonenwa na Mungu alipewa bibi-arusi kama vile Adamu alivyopewa. Lakini kabla hajaweza kumwoa, yeye pia alikuwa ameshaanguka. Yeye, kama vile mke wa Adamu, alijaribiwa kama angeliamini Neno la Mungu na aishi, au alitilie shaka Neno na afe. Alitilia shaka. Yeye aliliacha Neno. Alikufa.

Toka kwenye kundi dogo la mzao halisi wa Neno, Mungu atamtuza Kristo na bibi-arusi mzuri. Yeye ni bikira wa Neno Lake. Yeye ni bikira kwa sababu hazijui kanuni zo zote za imani zilizobuniwa na wanadamu wala mafundisho ya sharti. Kwa njia ya washirika na kupitia kwa washirika wa bibi-arusi yatatimizwa yale yote yaliyoahidiwa na Mungu kudhihirishwa katika bikira.

Neno la ahadi lilimjia bikira Mariamu. Lakini hilo Neno la ahadi lilikuwa ni Yeye, Mwenyewe, kudhihirishwa. Mungu alidhihirishwa. Yeye, Mwenyewe, alifanya tendo wakati huo na kulitimiza Neno Lake la ahadi katika huyo bikira. Malaika ndiye aliyemletea ujumbe. Lakini ujumbe wa malaika ulikuwa ni Neno la Mungu. Isaya 9:6. Yeye aliyatimiza wakati huo yote yale yaliyoandikiwa Yeye kwa sababu huyo bikira alilikubali Neno Lake alilomletea.

Washiriki wa bibi-arusi bikira watampenda Yeye, nao watakuwa na uweza Wake, kwa maana Yeye ndiye kichwa chao, na nguvu zote ni Zake. Wanamtii Yeye kama vile viungo vya miili yetu vinavyotii vichwa vyetu.

Angalia kupatana kwa Baba na Mwana. Yesu hakufanya lo lote mpaka alipoonyeshwa jambo hilo kwanza na Baba. Yohana 5:19. Kupatana huku kunatakiwa sasa kuwepo kati ya Bwana Arusi na bibiarusi Wake. Yeye humwonyesha Neno Lake la uzima. Naye analipokea. Yeye kamwe hatilii shaka. Kwa hiyo, hakuna kitu kinachoweza kumdhuru, wala hata mauti. Kwa kuwa kama mbegu imepandwa, maji yataifufua tena. Siri ya jambo hili ndiyo hii: Neno liko ndani ya bibi-arusi (kama ilivyokuwa katika Mariamu). Bibi-arusi ana nia ya Kristo kwa kuwa anajua kile anachotaka kifanyike kwa Neno. Anatekeleza maagizo ya Neno katika jina Lake kwa kuwa yeye anayo “Bwana asema hivi.” Ndipo Neno linahuishwa na Roho nalo linatimia. Kama vile mbegu ambayo imepandwa na kumwagiwa maji, inafikia mavuno kamili, ikitimiza kusudi lake.

Wale walio katika bibi-arusi hufanya mapenzi Yake tu. Hakuna mtu anayeweza kuwafanya wafanye vinginevyo. Wao wana 'hivi asema Bwana' ama wanatulia. Wanajua ya kwamba hapana budi iwe ni Mungu ndani yao anayefanya hizo kazi, akilitimiza Neno Lake Mwenyewe. Yeye hakumaliza kazi Zake zote alipokuwa katika huduma Yake ya duniani kwa hivyo sasa Yeye hutenda kazi katika na kwa kupitia kwa bibi-arusi.

Bibi-arusi ajua hayo, kwa sababu wakati Wake wa kufanya mambo fulani ambayo hana budi kuyafanya sasa haukuwa umewadia. Lakini sasa Yeye atatimiza kupitia kwa bibi-arusi kazi ile aliyoiacha ili ifanywe kwa wakati huu uliokusudiwa.

Sasa hebu na tusimame kama Yoshua na Kalebu. Nchi yetu ya ahadi imeanza kuonekana kama vile yao ilivyoanza kuonekana. Sasa Yoshua maana yake ni “Yehova-Mwokozi,” naye anamwakilisha kiongozi wa wakati wa mwisho ambaye atakuja kwa kanisa kama vile Paulo alivyokuja kama kiongozi wa kwanza. Kalebu anawakilisha wale waliodumu waaminifu kwa Yoshua

Kusoma kamili ya akaunti katika...
  Wakati wa Kanisa la Pergamo.


  Maandiko Anasema...

Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.

Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.

Isaya 60:1-2



Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Mtangulizi.

Jina la Mungu.

Kutembea kwa
Kikristo mfululizo.

Mungu na Historia
mfululizo. Danieli.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni matofaa?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

 

Krismasi mfululizo.

 

Safina ya Nuhu.

 

Babeli ya Siri.
Mama na Mwana.

Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)
 

Kristo Ni Siri Ya
Mungu Iliyofunuliwa.

(PDF)

Kabla...

Baada ya...

Hadithi ya Maisha
Yangu
William Branham.

(PDF)

How the Angel came
to me.
(PDF Kiingereza)