Yehova-Yire #3.

<< uliopita

ijayo >>

  Siri hiyo ya Kristo.

Ilimpasa Abrahamu ajaribiwe.


William Branham.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Yehova-Yire #3.

Sasa hebu tuweke msingi wa Abrahamu. Kwanza, Mungu alikutana na Abrahamu, pasipo masharti, agano. Yeye alilofanya na Abrahamu. Siyo kitu chochote hata kidogo, Abrahamu hakuwa na chochote cha kufanya isipokuwa kumwamini Mungu. Lile agano kwa neema tu, na pasipo masharti. Siyo, “kama utafanya”. Mungu alisema, “Nimekwisha kufanya!” Na sasa kila mtu...

Kumbukeni, Uzao wote wa Abrahamu uliowahi kuja kwa Mungu, huja kwa njia hiyo hiyo. Hakuna chochote uliweza kufanya! Usingeweza kujiokoa mwenyewe zaidi kuliko ambavyo usingeweza kuchukua kamba za kiatu chako na kurukia mwezini. Huwezi kujiokoa mwenyewe. Hakuna mtu aliyewahi kumtafuta Mungu, ni Mungu anayemtafuta mtu. “Ninyi kamwe hamkunichagua Mimi,” Yesu alisema, “Mimi niliwachagua ninyi.”

----
Usiku uliopita mnakumbuka kuwa wakati Abrahamu, lile agano lilifanyika kwa Abrahamu na Uzao wake baada yake. Sasa, kulikuweko na uzao wa asili wa Abrahamu, kwa njia ya tendo la imani lilizaa huo; lakini ule Uzao halisi wa Abrahamu ulikuwa Kristo, Biblia... ambao ulikuwa Uzao wa kifalme wa Abrahamu. Sasa, tazama. Abrahamu, kabla ya maangamizi ya moto katika siku yake, kulikuweko na ishara iliyofanyika kwa Abrahamu. Kundi lake teule. Na hiyo ilikuwa, Mungu alishuka chini katika umbo la mwanadamu, akigeuzia hema kisogo toka pale Sara alikokuwa, na kusema kile Sara alichokuwa akisema ndani ya hema. Na Yesu alikuja pale na alisema jambo lile lile lingekuweko penye mwisho wa kipindi. Sasa, huyo alikuwa Abrahamu.

Ndipo uzao wake wa asili, Masihi atakapokuja. Na Simoni alimjia Yesu, na Yeye akamwambia jina lake lilikuwa Simoni, na alikuwa mwana wa Yona, alijua siri za moyo wake. Alimwambia Filipo... au Natanaeli, kuwa Filipo alikuwa, “Nilikuona wewe ulipokuwa chini ya mti.” Alimwambia yule mwanamke pale kisimani, “Unao waume watano.” Na yeye akasema, “Bwana natambua Wewe ni nabii.” Unaona, mwisho wa uzao wa kimwili wa Abrahamu ulipata hiyo ishara. Na hilo lilibashiriwa na Mzao wa kifalme Mwenyewe, Kristo, kuwa ule Uzao wa kifalme, mwishoni mwa siku zao, ungelikuwa na kitu kile kile. Sasa ninatumaini tunalipata hili.

Alimbadilisha.... Angalia, Mungu alibadilisha jina la Abrahamu. Ni bora niondoke kwenye hilo. Nitakaporudi kwa ajili ya uamsho mrefu, tutaingia katika hilo. Ilipasa yeye abadili jina lake kutoka kwenye jina lake la kidunia, kwenda kwenye jina alilopewa na Mungu. Unasema, “Jina la mtu ni nini kwetu, chochote?” Loo, ndugu, kama tu ungejua! Mbona, baadhi ya haya majina ya kisasa tuliyo nayo! Sitaki kuyataja hayo, kwa sababu hilo litaumiza hisia zenu. Lakini Mungu anayo majina yanayomaanisha mambo, hilo hubadilisha mwenendo mzima. Ee, unasema, “Upuuzi!”

Vipi juu ya-vipi juu ya Yakobo? Kabla yeye hajafanyika mwana wa mfalme mbele za Mungu, ilimbidi yeye abadilishwe jina lake kutoka Yakobo kuwa Israeli. Je, hilo ni sahihi? Hakika. Paulo; Sauli alimpasa jina lake libadilishwe kuwa Paulo. Ee, ni wangapi tungeweza kuwataja, na kusema kuwa Mungu alibadilisha jina lao! Abramu kuwa Abrahamu, Sarai kuwa Sara, akibadilisha jina lao. Loo, jamani! Ni baraka iliyoje, kuingia katika kanisa fulani dogo likiwa na kundi teule, na kwenda kufundisha hilo, unaona haleluya katika moyo wao, unapoona kile Mungu anachofanya.

Sasa, jioni iliyopita nilikuwa nikieleza juu ya “katikati ya msitari” na “kuthibitisha hilo.” Nataka tu kuligonga hilo tena kabla sijaingia katika somo. Kwamba, Mungu alimbadilisha Abrahamu kutoka mwanamume mzee mwenye makunyanzi, yeye na Sara, kurejea kwenye watu wawili walio vijana, alibadilisha hali yao ya kimwili kabla wao hawajaweza kumpokea yule mwana wa ahadi. Ishara ya mwisho waliyopata ilikuwa udhihirisho wa Mungu katika mwili, aliweza kusoma moyo wa mwanamke nyuma Yake, katika hema. Na jambo lililofuata lilikuwa kwamba miili yao ilibadilishwa. Sasa, jioni iliyopita nilikuwa ninachelewa, na niliweza kuhisi baadhi wakishangaa kuhusu hilo. Nataka bado nililete hilo karibu zaidi kidogo.

Sasa, uthibitisho wa hilo ulikuwa kwamba, wakati wote wawili walipokwenda ile safari ndefu, walikuwa wamebadilishwa kabisa. Na Biblia ilisema, “Wote wawili wamechukuliwa na umri. Na mwili wa Abrahamu ulikuwa kama uliokufa, na tumbo la uzazi la Sara lilikuwa limekufa.” Je, hilo lilikuwa sahihi? Tunajua wao walikuwa wamekufa, lakini Mungu aliwabadilisha. Sasa ili kuwathibitishia hilo, kwamba Yeye alifanya hilo. Kwanza, kwa nini yule Mfilisti (au siyo niniii...) ndiyo, naamini alikuwa mfalme wa Wafilisti, alimpenda Sara, mwanamke mzee? Na Sara alikuwa mzuri wa sura.

Jambo lingine. Isaka alipozaliwa, na Sara na Abrahamu walikuwa na umri mkubwa, wakiwa tayari kufa, ndipo wakaishi, na Isaka akaoa alipokuwa na umri wa miaka arobaini; Sara akafa. Na Abrahamu akaoa mwanamke, Ketura, na alikuwa nao watano, sita wana, naamini ilikuwa hivyo, mbali na mabinti, baada ya hilo; na hapa, miaka sitini iliyopita, yeye alikuwa kama aliyekufa! K-e-t-u-r-a, Ketura. Yeye alimwoa Ketura, miaka hamsini au sitini baada ya hilo, naye alikuwa na wanawe sita mbali na mabinti zake; na miaka sitini hapo kabla, yeye alikuwa kama aliyekufa. Haleluya! Hilo ndilo jambo lenyewe! Ahadi ya Mungu ni hakika. Amina. Loo, nalipenda Hilo!

----
Hilo ndilo jambo lenyewe! Unapokuwa na ahadi, nawe unajua hiyo ni ahadi, dumu nayo! Ilimpasa Abrahamu ajaribiwe. Dumu na ahadi!
Sasa, wao walikuwa na ishara yao ya mwisho. Ndipo mwili wao ukabadilishwa. Na kwa haraka Isaka mdogo alitokea penye sehemu ya tukio, mvulana mzuri mdogo wa Kiyahudi, ningewazia baada ya siku zake nane yeye alitahiriwa. Vipi yule mama kijana, mwenye umri wa miaka mia... Vipi yule Abrahamu, akiwa na umri wa miaka mia; au Sara akiwa na tisini na Abrahamu akiwa na miaka mia; wao wangeweza kuwaje, mnamo miaka ishirini, wakishangilia. Huyu jamaa mdogo, yeye alikuwa mzuri iliyoje...

Na unajua, Mungu alisema, “Sasa katika kuwafanya watu katika siku zijazo (ule Uzao wa Abrahamu) wajue, Uzao wako ujue kuwa Mimi naishikilia ahadi Yangu kwa mtu wangu ambaye atalishikilia Neno Langu, nitampa yeye jaribu.”
Wakati yule mvulana mdogo alipofikia umri wa miaka kumi na nne, nawazia, nywele ndogo zilizokuwa timtim bila mpango mzuri, na macho madogo mazuri. Ee, ni furaha iliyoje kwa hao baba na mama! Mnajua jinsi ninyi wazazi mlivyo na mtoto wenu, mtoto pekee. Ndipo Mungu akamwambia Abrahamu... Sasa, Yeye asingelimwambia Sara hilo, kwa sababu Sara alikuwa chombo kidhaifu zaidi. Na hivyo Yeye alisema, “Abrahamu, nataka umchukue huyu mvulana mdogo niliyekupa, yule ambaye nitakufanya wewe baba wa mataifa kwa yeye, na nataka umpeleke juu ya mlima nitakaokuonyesha jioni hii, katika ono, na ndipo umwue yeye.” Kuangamia kwa tumaini pekee lililokuwepo kwake kuwa baba wa mataifa, ili Mungu atimize Neno Lake; Mungu alisema, “Nitakufanya kuwa baba wa mataifa.” Sasa Abrahamu alikuwa amesubiri miaka yote hii, hadi akawa na umri wa miaka mia, umri wa miaka mia na kumi na nne. “Na hapa kuna huyu mvulana mdogo sasa, na ushahidi pekee ulio nao kwamba Mimi nitashikilia Neno Langu, uende kule juu na ukauangamize huo. Bado Mimi nitakufanya baba wa mataifa kwa njia ya huyu mtoto.”

----
Sasa Mungu alisema, “Mchukue yule jamaa mdogo, mpeleke juu kule penye kilele cha mlima.”
Sasa mnataka kujua kama Abrahamu alikuwa mwanamume kijana au la? Yeye alikwenda safari ya siku tatu pamoja na mtoto, akiwa na kuni, pamoja na mtumishi, na punda. Sasa mwanamume yeyote, mwanamume wa kawaida... Mimi nilikuwa zamani nikifanya doria njia za umeme, nilikuwa zamani nikitembea nikiwa mkuu wa hifadhi ya wanyama pori; na niliweza kutembea, kwa urahisi, maili thelathini kwa siku. Na tulikuwa na miguu ya mafuta ya gari, tunaliita hilo. Lakini wale watu, usafiri wao pekee ni kwa mguu, au kupanda punda. Nao walikuwa hapa pamoja na punda mdogo anayetembea pole pole; na tunaweza kutembea zaidi yake. Na yeye alikuwa hapa, safari ya siku tatu, na ndipo akainua kichwa chake na akauona mlima kwa mbali bado. Lazima yeye alikuwa kama maili mia mbali na ustaarabu nyuma kule jangwani. Sasa sikilizeni na mwone.

Ndipo yeye akachukua zile kuni na kuziweka mgongoni mwa Isaka; msalaba, Mwana wa Mungu miaka kadha baadaye. Na Isaka alibeba zile kuni hadi juu ya kilima, kile yeye alichokuwa anakwenda kulala juu yake kwa ajili ya dhabihu. Kutangulia kwa kivuli.
Kama Mungu alitanguliza kivuli cha hilo hadi kufuatilia kwa makini; mke wa Lutu, je usigeuke na kutazama nyuma kuelekea mambo ya ulimwengu. Mifano hiyo yote na vivuli ni vikamilifu. Unaona? Mkumbukeni Hawa. Mkumbukeni mke wa Lutu. Mkumbukeni Lutu mwenyewe, wewe mwanamume. Kumbukeni, Adamu alijitolea kwa mke wake; Lutu, vivyo hivyo. Uwe mwangalifu. Mimi nawaambia tu, kama ndugu. Muda umeendelea kuliko unavyofikiri.
Mtazame Isaka mdogo akikwea kilima. Naye akapata mashaka. Na yeye akatazama huko na huko, akasema, “Baba yangu?”
Naye akasema, “Mimi hapa, mwanangu.”
Isaka akasema, “Hapa kuna kuni. Na hapa kuna vyote, kila kitu, moto. Lakini yuko wapi kondoo wa sadaka ya kuteketeza?”
Msikilize yule baba mzee, pasipo na kutetemeka katika sauti yake, yeye alisema, “Mwanangu, Mungu atajipatia Mwenyewe hiyo dhabihu.” Mwanawe pekee akienda kwenye machinjio, lakini bado ule moyo mwaminifu wa kale ulikuwa umejua kuwa Mungu hawezi kusema uongo...
Huo ndio Uzao wa Abrahamu leo! “Inawezekanaje, Ndugu Branham?” Mungu atajipatia Mwenyewe! “Yeye atafanyaje?” Mimi sijui. Lakini Yeye ni Yehova-Yire!

Akafika kwenye kilele cha kilima, wakiliviringisha lile jiwe hadi juu. Akaweka kuni juu ya yale mawe, na kuziwasha hizo moto. Akasema, “Isaka, mwanangu, geukia kule.” Akachukua kamba kuizingira kiunoni mwake, na kumfunga mikono yake na miguu yake. Isaka, akiwa mtiifu, kama Kristo alivyokuwa, hadi mauti. Akamlaza pale juu ya pande la jiwe. Akaingiza mkono wake kufikilia katika ala na kuvuta kisu kikubwa; akakinoa kwa mara kadha, akiwa anatazama kuelekea angani.

“Yeye hakuyumba penye ahadi ya Mungu kwa kutokuamini, bali alikuwa imara, akijua kwamba yeye alikuwa amempokea mtoto akiwa kama aliyetoka kwa wafu; alishawishika kikamilifu kuwa kama Mungu alisema hivyo, kuwa yeye afanye hilo, Yeye Mungu angeweza kumfufua kutoka kwa wafu.” Huyo ni Abrahamu, na huo ni Uzao wake baada yake. Kama huo ulikuwa uzao wa asili, ule Uzao wa kifalme unapaswa uweje? Hakuna kuyumba! Kile Mungu alichosema, Mungu atakifanya. Akijua hilo, yeye alishawishika kikamilifu; kwamba kile Mungu alichokwishaahidi, Mungu alikuwa anaweza kufanya.

Alinoa kisu; macho madogo meusi ya Isaka mdogo yakiwa yanatazama ubapa mkali wa kisu kilipokuwa kinanolewa juu ya lile jiwe. Akarudi nyuma; akarudisha nyuma nywele zilizokunjamana kutoka usoni pake, akavuta nyuma kidevu chake kidogo. Akainuka, na machozi yakiwa yanatiririka usoni mwake namna ile. Akijua, na yeye hakuyumba penye ile ahadi ya Mungu! Akainua kichwa chake ili kuzamisha kile kisu katika koo la mwana wake mwenyewe.
Naye alipofanya hivyo, sauti ya Mungu iliita, na kumshika mkono wake, ikasema, “Abrahamu! Abrahamu, zuia mkono wako! Sasa najua kwamba unanipenda.” Yeye Bwana alikuwa anafanya nini? Akitoa ushuhuda kwa Uzao wa Abrahamu, baada yake. “Zuia mkono wako, usimdhuru huyu mtoto! Najua kuwa unanipenda.”

Na karibu wakati ule, Abrahamu alisikia kitu fulani nyuma yake. Naye akatazama, na kulikuweko na kondoo dume (huyo ni kondoo dume) aliyenaswa pembe zake katika magugu na vichaka. Na Abrahamu akaenda na kumchukua yule kondoo dume na kumwua, badala ya mwanawe.

Yule kondoo dume alitokea wapi? Yeye yuko maili mamia mbali na ustaarabu. Mbona, wanyama pori wangeliweza kumwua kama yeye angelikuwa nyuma kule. Hakika, yeye ni-yeye ni mnyama wa kufugwa. Yeye alitokea wapi? Na, mbali na hilo, ni mbali kule juu ya mlima, kule ambako hakuna majani wala maji. Na Abrahamu aliokota mawe kote huko, pale huyo kondoo dume alikokuwa, ili kutengeneza madhabahu. Yeye alitokea wapi? Hilo halikuwa ono; yeye alitokwa na damu. Ono huwa halitokwi na damu. Haleluya! Yehova-Yire alikuwa amejipatia dhabihu Mwenyewe.

Mungu anapochukuliwa kwenye Neno Lake, Yeye anaweza kutoa chochote kile anachotaka. Mungu, Yehova-Yire, bado ni Yehova-Yire jioni hii! Yeye amekwishajipatia Dhabihu. Yeye amekwishajipatia Kanisa. Yeye amekwishajipatia Mjumbe, Roho Mtakatifu. Yeye yupo hapa sasa, Yehova-Yire! Bwana amejipatia Mwenyewe Biblia, Roho, Ujumbe, Mjumbe. Na ile saa iko hapa sasa kwa ajili ya kunyakuliwa kwa Kanisa na kupelekwa nyumbani. Yehova-Yire atatoa njia ya kuliondoa hilo Kanisa kutoka kwenye huu ulimwengu, kwa kubadilishwa kutoka kwenye hii miili yetu iliyo midhaifu, na kuipeleka juu Utukufuni. Yehova-Yire! Hilo litatukia vipi katika siku ya kisasa kama tunayoishi, kuwa haya mambo yatatokea.

Kusoma kamili ya akaunti katika...
Yehova-Yire #3.


Siri hiyo ya Kristo.

Kiingereza Jarida Tovuti.

Kitabu cha Ufunuo.

 

Mungu na Sayansi.
- Akiolojia.

Unyakuo anakuja.

 

Mafundisho ya kuu ya Ujumbe.

Habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili
ya dhambi zenu.

Ubatizo wa Maji.

 
 

Wingu Supernatural.

Nguzo ya Moto.

Shekina utukufu wa Mungu.

Kaburi ni tupu
Amefu fuka.

Forerunner.

Jina la Mungu.

Mfululizo wa
wakati wa mwisho.

Neno lililo hai
mfululizo.

Mungu, kwa jinsi alielezea.

Dhambi ya asili.
Ilikuwa ni apple?

Nyakati Saba Za Kanisa.

Mihuri Saba.

Uthibitisho Nabii.

Sauti ya ishara.

Mungu na Sayansi.
- Mageuzi.

Mungu na Sayansi.
Myth ya Dinosaurs.

Tetemeko Hukumu.

Kifo. Ni nini basi?

Mungu na Sayansi.
Mikrobiolojia.

Mungu na Sayansi.
Kosmolojia.

Orodha ya Ujumbe.

  Maandiko Anasema...

Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.

Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.

Mwanzo 22:13-14


Bonyeza juu ya picha download PDFs au ukubwa kamili picha.


Acts of the Prophet

(PDFs Kiingereza)

Mungu Akijificha Kwa
Urahisi Halafu
Akajifunua Kwa Jinsi
Hiyo.
(PDF)

William Branham Life
Story.

(PDF Kiingereza)

How the Angel came
to me.

(PDF Kiingereza)


 


Ujumbe kitovu...Chagua lugha yako na kupakua ujumbe huru kutoka Ndugu Branham.